Comoro kushirikiana na Tanzania katika sekta za kimkakati asema Rais Azali Anena
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazumgumzo na Rai...
Latest Post
July 30, 2017
WAFANYA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA BILA TAARIFA ZA ROBO YA 3 NA YA 4 KWA KUGOMEA VIKAO HIVYO KWA LENGO LA KUIKOMOA SERIKALI.
Msuguano mkali kati ya madiwani na serikali kuu unazidi kupamba moto ambapo Madiwani wa Jiji la Arusha wamelazimika kufanya baraza la kufunga mwaka mnamo 29 Julai 2017 huku kukiwa hakuna mihutasari wala taarifa za:
1. Baraza la robo ya I lilivunjika baada ya wajumbe wengi kutoka ukumbini na kukimbilia mahakamani kusikiliza kesi ya mbunge.
2. Baraza maalum lilivunjika baada ya diwani mmoja kumporomoshea matusi mkurugenzi wa jiji ambapo ilibaki kidogo zipigwe kavukavu na madiwani wengi waliposimama kama ishara ya kumvamia mkurugenzi ndipo mkurugenzi huyo akalazimika kukimbia ukumbini kukwepa kipigo hata hivyo ilibidi kikao kirudiwe chini ya usimamizi wa katibu tawala wa mkoa yeye mwenyewe mhe Richard Kwitega ambapo kiliisha kwa mbinde na mkurugenzi siku hiyo hakuhudhuria aliwakilishwa na mhandisi wa jiji.
3. Kamati ya mipango miji ilivunjwa na mbunge akidai mpaka RC atakapoacha kuingilia masuala ya hospitali inayojengwa na ya wafadili ajenda ambayo haikuwa na uhusiano na kikao hicho.
4. Kamati ya fedha robo ya 3 wajumbe walitoka ukumbini na kwenda polisi kufuatilia dhamana ya meya aliyekuwa anashikiliwa na jeshi hilo kwa kosa la kufanya mkusanyiko usiokubalika katika shule ya luck vicent akidai anapeleka rambirambi.
5. Kamati ya fedha ya robo ya 4 walikataa mjadala wakidai wanataka kwanza wakae cha robo ya 3 ambacho wanasahau kwamba walikigomea.
Vikao vyote hivyo 5 vilivunjika bila sababu inayokubalika kikanuni.
SWALI: JE MEYA WA JIJI LA ARUSHA ANA HAKI YA KUJIITA MEYA BORA KWA VURUGU HIZI ZA MADIWANI MEYA, NA MBUNGE?
Licha ya kuvunjika vikao hivi hata ambavyo vimemalizika bado kumekuwa na mivutano mikali kati ya madiwan kwa upande mmojai na mkurugenzi na wakuu wake wa idara kwa upande mwingine..
Mvutano huu ulisababisha ofisi ya rais TAMISEMI kuunda tume kuchunguza na kisha kutoa maelekezo kwa meya na mkurugenzi ambao ni viongozi wa pande zinazovutana lakini haikusaidia kwa kuwa meya hana ubavu wa kumpinga mbunge.
BREAKING NEWS: MADIWANI WA JIJI LA ARUSHA WAWEKA REKODI YA KUGOMEA VIKAO
Written By CCMdijitali on Sunday, July 30, 2017 | July 30, 2017
KWA
MWAKA WA FEDHA WA 2016/2017 PEKEE VIMEAHIRISHWA VIKAO 5 KUTOKANA NA MADIWANI.
KUGOMA KWA MADAI YA KUINGILIWA NA KUBURUZWA NA SERIKALI KUPITIA MKURUGENZI WA
JIJI.
WAFANYA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA BILA TAARIFA ZA ROBO YA 3 NA YA 4 KWA KUGOMEA VIKAO HIVYO KWA LENGO LA KUIKOMOA SERIKALI.
Msuguano mkali kati ya madiwani na serikali kuu unazidi kupamba moto ambapo Madiwani wa Jiji la Arusha wamelazimika kufanya baraza la kufunga mwaka mnamo 29 Julai 2017 huku kukiwa hakuna mihutasari wala taarifa za:
- ·Robo ya 3 (Januari hadi Machi 2017)
- ·Robo ya 4 (April hadi Juni 2017) za kamati nyeti ya fedha na utawala.
- ·Vilevile vikao viwili vya baraza vilivunjika cha robo ya kwanza na kingine cha baraza maalum vyote kutokana na vurugu na kushutumiana kati ya Wajumbe na Mkurugenzi wa Jiji Athumani Kihamia kwa tuhuma za kutoheshimiana hasa katika maamuzi wanayoyatoa wakidai kinachotekelezwa kwa kiasi kikubwa ni maamuzi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro badala ya maamuzi ya madiwani ambapo ilibaki kidogo ngumi zichapwe katika baraza maalum.
- ·Pia kikao cha robo ya 2 ya kamati ya mipango miji kilivujika kwa madai ya kuingiliwa kiutendaji na ofisi ya RC tuhuma hizi zilitolewa na mbunge Godbless Lema.
1. Baraza la robo ya I lilivunjika baada ya wajumbe wengi kutoka ukumbini na kukimbilia mahakamani kusikiliza kesi ya mbunge.
2. Baraza maalum lilivunjika baada ya diwani mmoja kumporomoshea matusi mkurugenzi wa jiji ambapo ilibaki kidogo zipigwe kavukavu na madiwani wengi waliposimama kama ishara ya kumvamia mkurugenzi ndipo mkurugenzi huyo akalazimika kukimbia ukumbini kukwepa kipigo hata hivyo ilibidi kikao kirudiwe chini ya usimamizi wa katibu tawala wa mkoa yeye mwenyewe mhe Richard Kwitega ambapo kiliisha kwa mbinde na mkurugenzi siku hiyo hakuhudhuria aliwakilishwa na mhandisi wa jiji.
3. Kamati ya mipango miji ilivunjwa na mbunge akidai mpaka RC atakapoacha kuingilia masuala ya hospitali inayojengwa na ya wafadili ajenda ambayo haikuwa na uhusiano na kikao hicho.
4. Kamati ya fedha robo ya 3 wajumbe walitoka ukumbini na kwenda polisi kufuatilia dhamana ya meya aliyekuwa anashikiliwa na jeshi hilo kwa kosa la kufanya mkusanyiko usiokubalika katika shule ya luck vicent akidai anapeleka rambirambi.
5. Kamati ya fedha ya robo ya 4 walikataa mjadala wakidai wanataka kwanza wakae cha robo ya 3 ambacho wanasahau kwamba walikigomea.
Vikao vyote hivyo 5 vilivunjika bila sababu inayokubalika kikanuni.
SWALI: JE MEYA WA JIJI LA ARUSHA ANA HAKI YA KUJIITA MEYA BORA KWA VURUGU HIZI ZA MADIWANI MEYA, NA MBUNGE?
Licha ya kuvunjika vikao hivi hata ambavyo vimemalizika bado kumekuwa na mivutano mikali kati ya madiwan kwa upande mmojai na mkurugenzi na wakuu wake wa idara kwa upande mwingine..
Mvutano huu ulisababisha ofisi ya rais TAMISEMI kuunda tume kuchunguza na kisha kutoa maelekezo kwa meya na mkurugenzi ambao ni viongozi wa pande zinazovutana lakini haikusaidia kwa kuwa meya hana ubavu wa kumpinga mbunge.
Labels:
KITAIFA
July 23, 2017
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ahitimisha kilele cha maadhimisho ya siku ya Mwani ya Kongano Bunifu la Mwani Zanzibar
Written By CCMdijitali on Sunday, July 23, 2017 | July 23, 2017
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea maandamano ya Wazalishaji wa zao la Mwani katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mwani Duniani zilizofanyika Uwanja wa Malindi Mjini Zanzibar.
Akina Mama wazalishaji wa zao la Mwani wakionyesha bidhaa zao kwenye maandamano ya Siku ya Mwani Duniani zilizofanyika Malindi ambapo Mgeni Rasmi ni Balozi Seif Ali Iddi.
Bibi Maryam Pandu Kweleza wa Kikundi cha ushirika cha Kazi Moto Bwejuu akimfahamisha Balozi Seif jinsi ya ukulima wa zao la mwani unavyoendeshwa kwenye maonyesha ya bidhaa zinazozalishwa na zao hilo hapo Malindi.
Balozi Seif na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed wakiangalia Mwani uliopea tayari kwa ajili ya kutengenezwa mali ghafi ya bidhaa mbali mbali.
Nyuma ya Mh. Hamad Rashid ni Mwenyeketi na Muwezeshaji wa Kongano la Ubunifu wa Mwani Dr. Flower Msuya akishuhudia kitendo hicho huku Bibi Marya Kweleza akiendelea kutoa maelezo.
Balozi Seif akiridhika na bidhaa safi za vyakula na Juisi zilizotengenezwa na wazalishaji wa mwani kutoka vikundi mbali vya akina mama wakati akikagua maonyesho ya bidhaa hizo.
Balozi Seif akiangalia sabuni ya maji iliyotengenezwa na Kikundi cha akina Mama wa Kijiji cha Makangale Micheweni Pemba ambayo imetumia Mali ghafi ya Mwani.
Press Release:-

Picha na – OMPR – ZNZ.
Serikali inaendelea kuwaunga Mkono Wananchi kwa
kuwajengea uwezo ikiwemo fursa za mikopo pamoja na kuongeza kasi katika
kutafuta masoko mapya ili kuona
Wakulima wa kilimo cha Mwani wanaongeza
kiwango cha uzalishaji na uwezo wa ubunifu.
Hatua hiyo italeta tija zaidi kwa Wakulima wa Kilimo hicho kilichoanza kulimwa Nchini
takriban kwa karibu Miaka 30 sasa na
kushirikisha vijiji zaidi ya 50 ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuongeza
fursa kwa Taifa katika kukuza mapato yake .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali
Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa kilele
cha maadhimisho ya siku ya Mwani ya Kongano Bunifu la Mwani Zanzibar
yaliyofanyika katika viwanja vya Michezo vya Malindi Mjini Zanzibar.
Balozi Seif
alisema mwenendo wa mapato kwa Wananchi unaonekana kuongezeka siku hadi
siku na kuonyesha haja kwa Serikali
kuendelea kutilia mkazo uzalishaji wa zao Mwani kwa vile ni sekta ya tatu kwa
kuleta tija kwa Taifa ikitanguliwa na Utalii na Karafuu na ni zao la pili kwa
kusafirishwa nje ya Nchi likitanguliwa na Karafuu.
Alisema Sekta hiyo tayari imeshatoa ajira za kudumu
kwa zaidi ya Wakulima 23,000 na kuna ajira nyingi ambazo hutokea kipindi cha
msimu wa kupanda, kuvuna na kusarifu Mwani.
Alieleza kwamba faida imeanza kuonekana kupitia zao
la Mwani Kiuchumi ambapo Wananchi kutoka Vijiji mbali mbali vya Zanzibar na hata baadhi ya Wilaya za Tanzania Bara
walijishughulisha na zao hilo ambapo asilimia kubwa ya Wakulima wake ni
Akinamama.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inazungumza na wadau mbali mbali wa ndani na nje ya Nchi ili waanzishe Viwanda
vodogo vidogo vya kuweza kulifanyia kazi zao hilo hapa nchini pamoja na kuimarisha soko na bei yake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali
inafahamisha kuwa pamoja na faida inayopatikana katika uzalishaji wa zao la
Mwani lakini bado Sekta hiyo imekumbwa na changamoto kubwa ikiwemo kutofahamika
kwa bei yake pamoja na utaratibu wa leseni kwa Wafanyabiashara wa Mwani.
Alisema katika kutatua changamoto za Masoko, Kongano
la Mwani kwa kushirikiana na Shirika la Milele Zanzibar Foundation waliamua
kuweka Siku ya Mwani ili kutoa nafasi kwa Jamii kujua matumizi halisi ya zao
hilo na kulifanya litumike zaidi Nchini na kupunguza utegemezi mkubwa wa soko
la nje.
Balozi Seif alitoa rai ya kuchukuliwa hatua za
makusudi katika kuvitumia vyombo vya Habari Nchini na Nje ya Nchi kuutangaza
Mwani kwa upana zaidi ili Wananchi
wapate mwamko juu ya zao la Mwani na sio kusubiri Makongano kwa ajili ya
kujitangaza.
Amempongeza Mwenyekiti na Mwezeshaji wa Kongano la
Mwani Dr. Flower Msuya kwa uwamuzi wake
wa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Zanzibar pamoja na Shirika la Milele
Foundation Zanzibar kuwa bega kwa bega na Wakulima katika kuzitambua changamoto
zao na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaahidi wadau
wa zao la Mwani kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesikia kilio chao
kinachotokana na kodi kubwa la Bidhaa hizo wanazotozwa.
Alisema juhudi zitachukuliwa katika kuona kodi hizo
zinapunguzwa au kuondoshwa kabisa ili kuwapa fursa ya kuweza kuliendeleza kwa
vile limeshonyesha muelekeo wa kuongeza mapato yao.
Mapema Mwenyekiti na Mwezeshaji wa Kongano la Ubunifu
wa Mwani Dr. Flower Msuya alisema bidhaa za mwani hivi sasa zimefikia 50 ikilinganishwa na bidhaa moja tuu iliyokuwa
ikizalishwa na Kikundi cha Tusife Moyo cha Kijiji cha Kidoti mnamo Mwaka 2006.
Dr. Flower alisema mipango ya baadae ya ya Taasisi
hiyo ni kuendelea kutengeneza bidhaa zinazotokana na zao la Mwani baada ya kufanyiwa utafiti
uliothibitisha kwamba bidhaa hiyo ina matumizi mengi mchanganyiko ikiwemo
chakula.
Akitoa salamu za Taasisi ya Milele Zanzibar
Foundation iliyoratibu hafla hiyo ya siku ya Mwani Duniani, Mwakilishi wa
Milele Zanzibar bibi Khadija Sharifu
alisema Taasisi yake inakusudia kuwaleta Wataalamu wa kigeni kwa ajili ya kuwapatia
mafunzo wazalishaji wa mwani.
Bibi Khadija alisema Wataalamu wa Milele wamegundua
kwamba Sekta ya Mwani inaweza kuwakomboa
wananchi walio wengi kwa kutoa ajira kubwa ambapo kwa sasa tayari imetoa ajira
ya watu zaidi ya 23,000 tokea kuanza kwa sekta hii nchini Tanzania.
Akimkaribisha mgeni rasmi kwenye siku hiyo ya Mwani
Duniani Waziri wa Kilimo, Mali asili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mheshimwa Hamad Rasid
Mohamed alisema jamii inapaswa kubadilika katika utaratibu wao wa nlishe na kupoenda
kutumia mazao ya Mwani kwa lengo la kujenga afya zao.
Waziri Rashid alisema zao la Mwani kwa utafiti wa
kitalaamu linaonyesha kukinga maradhi mbali mbali ikiwemo ukanda wa jeshi, Mshtuko wa Moyo pamoja na maradhi
yanayodhoofisha upungufu wa Damu kutokana na ulaji ovyo wa vyakula vya makopo.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif alipokea maandamano ya wazalishaji wa zao la mwani kutoka wilaya mbali
mbali za Unguja na Pemba na baadaye kukagua bidhaa zao wanazozalisha kutokana
na mali ghafi hiyo ya Mwani.
Wakulima hao walimueleza Balozi Changamoto
wanazopambana nazo katika harakati zao za kulima zao hilo kukausha hadi
kukamilika kwa ajili ya soko ambapo walisema
kodi ya bidhaa iwanayotozwa kuhusiana na bidhaa ya zao hilo imekuwa
ikiwakatisha tamaa.
Walieleza pia upo upungufu wa ukosefu wa mashine ya
kukaushia mwani ambayo kwa sasa inapatikana
Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja pamoja na bei ndogo ya zao hiyo
isiyolingana na gharama za uzalishaji wake.
Kongano Bunifu la Mwani Zanzibar lilianzishwa Mwaka
2006 kwa kupitia Mpango wa Makongano Bunifu Afrika unaosimamiwa na Tume ya
Sayansi Teknolojia Tanzania {COSTECH} ili kuunga mkono juhudi zinazochukiwa na
Serikali.
Mpango huo wa Makongano Bunifu ulianza na Makongano
Manane kwa Tanzania Bara na Kongano Moja tu la Mwani kwa Zanzibar
Tokea kubuniwa kwake ambapo kwa sasa tayari yapo Makongano 70 kwa Bara
na Manane kwa Zanzibar.
Zao Mwani limekuwa likitumika kwa kutengeneza
Sabuni, Mafuta ya kujipaka, shampuu na vyakula vya kama Juisi keki, jam,
kachumbari na kupikwa kama mboga sambamba na utengenezaji wa dawa za
Binaaadamu, vipodozi na chakula cha mifugo.
Ujumbe wa Mwaka huu wa Siku ya Mwani Duniani
unaeleza Mwani kwa afya, Mwani kwa kipato na Mwani kwa uwezeshaji.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
23/7/2017.
Labels:
KITAIFA
July 21, 2017
BREAKING NEWS : KIKAO CHA KAMATI YA FEDHA JIJINI ARUSHA CHAVUNJIKA TENA LEO.
Written By CCMdijitali on Friday, July 21, 2017 | July 21, 2017
MBUNGE LEMA NA NAIBU MEYA WAMUONYA MKURUGENZI.
Kwa mara nyingine madiwani wa kamati ya fedha jijini Arusha leo wamegomea kuendelea na kikao cha robo ya nne cha kamati hiyo kwa madai kuwa hadi wafanye kikao cha robo ya tatu kwanza ambacho pia walikigomea mwezi April mwaka huu. Wajumbe hao wakiongozwa na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema walisema wapo tayari kwa lolote litakalowatokea lakini hawapo tayari kuendelea na kikao. Walisema kikao cha robo ya tatu kiligomewa na wajumbe kwa kuwa serikali ilimkamata meya wao Kalisti Lazaro akitoa rambirambi kwa kukusanya watu bila kibali.
Hata hivyo meya huyo hakuwepo katika kikao hicho cha leo na haikufahamika alipo tangu alipovuliwa madaraka ya ukatibu wa chadema mkoa wa Arusha wiki iliyopita. Mkurugenzi wa jiji la Arusha Bw. Athumani Kihamia pamoja na wakuu wa idara wote walishangazwa na mgomo huo wa madiwani kwa kuwa vikao vya kamati hiyo vya miezi ya April na mei vimefanyika kama kawaida. Diwani wa viti maalum katika kamati hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Sabina amemdokeza mtoa habari hizi kuwa watafanya hivyo hadi mkurugenzi huyu atakapoondolewa au posho zetu alizozikata kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya zitakaporejeshwa na hayo ni maagizo maalum ya mbunge na viongozi wa chama. " Katika baraza la madiwani la mwezi huu mei tutamkataa mkurugenzi huyu ili watafute pa kumpeleka , tangu afike hali imekuwa mbaya kwa watumishi na madiwani.
Tumemjulisha Katibu mkuu ofisi ya raisi tawala za mikoa na selikali za mitaa mara kadhaa tunaamini atatuelewa. Wampeleke wanapotaka ni dikteta sana hata Kaliua waliwahi kumkataa. Anamsikiliza DC na RC sisi anatuona kama watu wasiokuwa na maana, Safari hii tumemchoka na mbunge Lema ameapa kutorudi nyuma kwenye hili" alisikika naibu meya akilalama muda mfupi baada ya kikao kuvunjika. Alipotafutwa Mkurugenzi aelezee hili jambo hakupatikana ingawa mkuu wa kitengo kimojawapo katika jiji la Arusha amedokeza kwamba mvutano huu hautakwisha kwa kuwa madiwani hawa wa Chadema hawayatambui mamlaka na majukumu ya DC na RC kuhusu usimamizi wa jiji na mkurugenzi huyu hapendi kupelekwa pelekwa yeye anacheza na kanuni tu. Hadi sasa hakuna shughuli yoyote ya jiji iliyowahi kusimama licha ya madiwani hawa kumgomea mkurugenzi huyu mara kwa mara karibu vikao 5 sasa kwa nyakati tofauti vimevunjika.
NI KUSUBIRI NA KUONA NINI KITATOKEA TAREHE 28 MEI SIKU YA BARAZA LA MADIWANI
Labels:
ARUSHA
July 13, 2017
DC wa zamani, mbunge wakabana koo uenyekiti CCM Shinyanga
Written By CCMdijitali on Thursday, July 13, 2017 | July 13, 2017
Mbunge wa Shinyanga Mjini,. Ezekiel Maige.
WANACHAMA 26 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza kuwania uenyekiti wa chama hicho mkoani Shinyanga akiwamo aliyewahi kushikilia wadhifa huo na mkuu wa wilaya wa zamani, Charles Gishuli, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige pamoja na wanawake wawili.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Haula Kachwamba alisema jana kwamba wagombea wote waliochukua fomu wamerudisha kwa wakati. Alieleza kuwa katika nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wapo wanachama 12, wajumbe wa NEC Taifa Tanzania Bara wapo 12 na sita wanataka kuwa Katibu wa Siasa na Uenezi.
Kachwamba alisema wanawake wawili ambao ni Angela Joseph na Juliana Billu wamejitokeza kuwania nafasi ya Uenyekiti pamoja na Gishuli na wagombea wengine ambao ni Michael Bundala, Khalfani Mandwa, Sendema Luhende, Nassoro Waryoba, Charles Simon, Bathromeo Mwanansia, Joseph Raulent na Justine Sheka.
Pia wamo Maxmine Mazulla, Erasto Theonest, Shija Malisha, Luhende Richard, Emmanuel Mlimandago, Mabala Mlolwa, Jonh Makune, Salumu Simba, Swetbert Nkuba, Cornel Ngudungi, Ally Manzi, Festo Kang’ombe, Nuhu Mnoni, Ezekiel Maige na Thomas Chuma.
Aliwataja wanaotaka NEC Taifa ni Richard Luhende, Sweetbert Nkuba, Mola Zabroni, Mussa Jonas, Abed Aljabri, Gerad Mwanzia, Peter Daniel, Gasper Kileo, Margaye Makune, Bernard Shigella, Joyce Masunga na Solomoni Matoba.
Kwa upande wa NEC Tanzania Bara, waliojiotokeza ni James Masunga, Gikula Madulu, Donald Tilusasila, Hassan Mwendapole, Khalfan Mashimba, Awadhi Aboud, Abeid Aljabri, Emmanuel Luhende, Erasto Lushekya, Mussa Ngangalla, Saleh Sizya na Meshack Mashigalla. Aliwataja waliojitokeza nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi ni Msanii Masele, Margaye Makune, Maxmine Mazulla, Emmanuel Mlimandago, Jacqueline Brayi na Mussa Ngangalla.
Labels:
KITAIFA
July 13, 2017
Everton watwaa ubingwa ardhi ya Tanzania
Mshabiki wa Man U avamia uwanja kumkubatia Wayne Rooney wakati Everton ikiifunga Gor Mahia 2-1
EVERTON ya Ligi Kuu England imetwaa kombe la SportPesa katika ardhi ya Tanzania baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya 2-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Alhamisi.
Pamoja na ubingwa huo, nyota wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, ndiye aliyekuwa gumzo ndani na nje ya dimba baada ya kufunga goli kwa mkwaju wa mbali katika dakika ya 34 ya mchezo baada ya kubanwa vilivyo kwa muda mrefu na walinzi wa Gor Mahia.
Hata hivyo goli hilo lilidumu dakika tatu tu kwani dakika ya 37, Jacques Tuyisende aliisawazishia Gor Mahia kwa kichwa baada ya mabeki wa Everton kushindwa kuokoa kona na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu hiyo ya England ikitaka bao la pili kwa udi na uvumba lakini mashutu yao yaligonga mwamba huku mengine yakiokolewa na mabeki wa Gor Mahia.
Hata hivyo, Dowel Davies aliiandikia Everton goli la pili katika dakika ya 81 baada ya kufunga mkwaju mkali uliomshinda golikipa wa Gor Mahia na kuifanya timu hiyo ya EPL kuweka historia ya kuchukua kombe hilo hapa nchini.
Labels:
MICHEZO NA BURUDANI