MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Latest Post
November 22, 2023
TANZANIA MWENYEJI WA TAMASHA LA DUNIA LA WATU WENYE USIKIVU HAFIFU
Written By CCMdijitali on Wednesday, November 22, 2023 | November 22, 2023
Na Eleuteri Mangi, WUSM
Tanzania ni mwenyeji wa tamasha la dunia la watu wenye usikivu hafifu (viziwi) likihusisha shindano la kumsaka mrembo, mtanashati pamoja na wanamitindo litakalofanyika Novemba 25, 2023 jijini Dar es salaam.
Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo Novemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi amesema maadalizi yanaendelea vizuri na Tanzania imejipanga kufanikisha tamasha hilo ambalo Tanzania imepewa heshgima ya kuwa mwenyeji kwa miaka miwili mfululizo.
Maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vyema kwa washiriki kujinoa ili kutoa taji la urembo, utanashati pamoja na wanamitindo dunia kwa viziwi ambapo mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya pili mfululizo hapa nchini baada ya kufanyika kwa mara ya kwanza Afrika na Tanzania kwa 2022.
Hadi sasa washiriki zaidi ya 200 wa tamasha hilo wameshawasili tayari nchini wanatoka mataifa ya Afrika Kusini, Australia, Belarus, Brazil, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Guyana, Haiti, Hispania, India, Iran, Italia, Kenya, Kongo DRC, Malasia, Macedonia, Marekani, Mexico, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Pakistan, Poland, Romania, Rwanda, Senegal, Siera Leone, Sudan Kusini, Thailand, Tunisia, Jamhuri ya Czechoslovakia, Ufaransa, Uganda, Ujerumani, Ukraine, Urusi, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.
Labels:
KIMATAIFA,
MICHEZO NA BURUDANI
November 22, 2023
WAZIRI MAKAMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI EAC JIJINI ARUSHA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 22 Novemba 2023.
Mkutano huo ambao ulianza tarehe 18 Novemba 2023 kwa ngazi ya wataalam na kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu umepitia na kujadili mapendekezo yatakayowasilishwa katika Kikao cha Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha tarehe 24 Novemba 2023.
Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri wa EAC pamoja na mambo mengine umejadili masuala kuhusu Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya mkutano cha Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2022 hadi 24 Novemba, 2023; utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya kuhusu Majadiliano ya Ombi la Shirikisho la Jamhuri ya Somalia kujiunga na EAC; juhudi za utafutaji wa Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo; Hali ya Kifedha ya Mfuko wa Akiba wa Jumuiya; majadiliano kuhusu Katiba ya Fungamano la kisiasa la Jumuiya; Tathmini ya miswada iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki; na Utoaji wa Tuzo kwa washindi wa mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri ambao ni Wajumbe kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kenya, Rwanda, Sudan Kusini na Uganda.
Kukamilika kwa Mkutano huo wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutafuatiwa na Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya EAC uliopangwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2023 jijini Arusha.
Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula na Uendelevu wa Mazingira ambao pia utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya EAC.
Mkutano huo unalenga kupata msimamo wa pamoja wa Jumuiya ya EAC kuelekea katika Mkutano wa Kimataifa wa 28 wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) utakaofanyika kuanzia Novemba 28, 2023 nchini UAE.
![]() |
| Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Jumuiya unapigwa kwenye Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha |
![]() |
| Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha |
![]() |
| Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha |
![]() |
| Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukiwa umesimama wakati wimbo wa Jumuiya unapigwa kwenye Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha |
Labels:
KIMATAIFA
November 22, 2023
DKT. BITEKO AKAGUA MAJENGO YA WIZARA YA NISHATI; SERA, URATIBU NA BUNGE
DKT. BITEKO AKAGUA MAJENGO YA WIZARA YA NISHATI; SERA, URATIBU NA BUNGE MJI WA SERIKALI- MTUMBA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Nishati na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali- Mtumba jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko aliambatana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jimmy Yonaz, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu pamoja na Watendaji mbalimbali kutoka Wizara hizo mbili.
Katika Jengo la Wizara ya Nishati, Dkt. Biteko ameshuhudia ujenzi ukiendelea ambapo kwa sasa umefikia asilimia 69 na Mkandarasi anayehusika na ujenzi huo ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Aidha, ujenzi wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu), unaendelea vizuri huku ukiwa umefikia asilimia 74 na Mkandarasi ni SUMA JKT.
Labels:
KITAIFA
November 21, 2023
NAIBU WAZIRI KIKWETE AZINDUA USAMBAZAJI WA MIFUMO KUBORESHA UWAJIBIKAJI KAZINI
Written By CCMdijitali on Tuesday, November 21, 2023 | November 21, 2023
Uzinduzi wa Zoezi la Usambazaji wa mfumo wa kutathmini na kuhakiki utendaji wa kazi wa Watumishi na Taasisi yaani PEPMIS/PIPMIS NA HR Assessment limefanyika mapema tarehe 20 Novemba 2023 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, mjini Iringa.
Akizungumza wakati anazindua mpango huo wa usambazaji wa Mfumo wa PEPMIS/PIPMIS NA HR Assessment katika shughuli ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bibi Halima Dendegu, Katibu Tawala wa Mkoa huo Mwandisi Masanja, na watumishi mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri zote za mkoa huo na waratibu wa TASAF toka makao makuu ya TASAF - Dodoma ambao walifuatana na Naibu Waziri.
Mh. Kikwete aliuelezea mfumo huu kuwa unakwenda kutatua pamoja na changamoto nyinginezo katika utumishi, mapungufu yaliyojitokeza katika mfumo wa OPRAS.
Ndugu Naibu Waziri aliwakumbusha watumishi kujua kuwa mfumo huu imekuja kuleta ufanisi na faida nyingi ikiwemo kutambua mahitaji ya kweli ya kiutumishi
Labels:
KITAIFA
November 21, 2023
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuja na mpango wa muda mrefu utakaoonesha jinsi nchi itakavyoweza kuongeza kiasi cha gesi asilia
Amesema kuwa kufanya hivyo kutawezesha kuwepo kwa hazina ya kutosha ya nishati hiyo inayotumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme, viwandani, majumbani na katika magari.
Dkt. Biteko ameyasema hayo tarehe 21 Novemba, 2023 wakati wa kikao chake na Bodi na Menejimenti ya TPDC ambacho kililenga kufahamiana, kubadilishana mawazo juu ya utendaji kazi na Mhe. Dkt. Doto Biteko kuelekeza matarajio ambayo nchi inayahitaji kutoka TPDC.
Dkt. Biteko pia amewataka TPDC kutokuwa na urasimu katika uchukuaji wa maamuzi mbalimbali ikiwemo kwenye shughuli za utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia ili kutorudisha nyuma sekta hiyo nchini.
Kuhusu maelekezo aliyoyatoa wakati wa ziara yake, katika Kisiwa cha Songosongo mkoani Lindi na Kijiji cha Madimba na Msimbati mkoani Mtwara, Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, maisha ya wananchi katika maeneo hayo ambayo kuna visima na mitambo ya Gesi Asilia lazima yabadilike na wapewe huduma bora ikiwemo maji, umeme, afya na usafiri.
DKT. BITEKO AIAGIZA TPDC KUANDAA MPANGO WA MUDA MREFU WA UPATIKANAJI GESI NCHINI
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuja na mpango wa muda mrefu utakaoonesha jinsi nchi itakavyoweza kuongeza kiasi cha gesi asilia
Amesema kuwa kufanya hivyo kutawezesha kuwepo kwa hazina ya kutosha ya nishati hiyo inayotumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme, viwandani, majumbani na katika magari.
Dkt. Biteko ameyasema hayo tarehe 21 Novemba, 2023 wakati wa kikao chake na Bodi na Menejimenti ya TPDC ambacho kililenga kufahamiana, kubadilishana mawazo juu ya utendaji kazi na Mhe. Dkt. Doto Biteko kuelekeza matarajio ambayo nchi inayahitaji kutoka TPDC.
“TPDC tujiulize, Je uwezo wetu wa kuzalisha Gesi Asilia unaweza kujibu mahitaji yetu ya Gesi ? tujiulize hili na tuchukue hatua. Tutambue kuwa mahitaji ya Gesi Asilia ni makubwa kwa sasa kwani dunia inahama kutoka matumizi ya mafuta na kwenda kwenye Gesi Asilia hivyo lazima tujipange, na pia tukumbuke tumesaini makubaliano ya kusafirisha nishati hii kwenda Uganda, Zambia na Kenya hivyo lazima tuwe na Gesi ya kutosha.” Amesisitiza Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko pia amewataka TPDC kutokuwa na urasimu katika uchukuaji wa maamuzi mbalimbali ikiwemo kwenye shughuli za utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia ili kutorudisha nyuma sekta hiyo nchini.
Kuhusu maelekezo aliyoyatoa wakati wa ziara yake, katika Kisiwa cha Songosongo mkoani Lindi na Kijiji cha Madimba na Msimbati mkoani Mtwara, Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, maisha ya wananchi katika maeneo hayo ambayo kuna visima na mitambo ya Gesi Asilia lazima yabadilike na wapewe huduma bora ikiwemo maji, umeme, afya na usafiri.
“Nashukuru mmeanza kufanyia kazi maagizo niliyoyatoa kwa haraka, ikiwemo ya kuweka taa za barabarani Kijiji cha Msimbati, kupeleka umeme wa uhakika Madimba na Msimbati unaotoka kwenye mitambo ya Gesi Asilia, kupeleka kivuko kisiwa cha Songosongo na malipo ya mafao kwa wastaafu wa Knight Support ambao walikuwa wakilinda mitambo na visima vya Gesi Asilia Songosongo ambao hawakulipwa muda mrefu, watu hawa wanahitaji huduma bora.”
![]() |
| Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko |
Labels:
KITAIFA
November 20, 2023
SHIBUDA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUMTEUA MAKONDA KUWA MWENEZI WA CCM
Written By CCMdijitali on Monday, November 20, 2023 | November 20, 2023
MAGALLE SHIBUDA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUMTEUA MAKONDA KUWA MWENEZI WA CCM KWANI AMEONESHA JUHUDI NA SHABAHA ZA KUUNDA DARAJA RAFIKI KWA KAZI ZA RAIS SAMIA NA WATANZANIA
- Asema Makonda amejenga uhusiano rafiki wa Kanda ya ziwa kwa kutoa Ahsante kwa uwajibikaji wa Serikali ya awamu ya 6 ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan
- Amejenga na kuleta wokovu wa mlango wa kutokea huzuni za ndani zilizounda ugumu wa mioyo katika kufumbua maono ya Ahsante_
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa, MNEC Mstaafu na Mbunge wa (CCM 2005 & CHADEMA 2010) Mstaafu Magalle John Paul Shibuda ametoa barua aliyoandika Manufaa na Faida kwa Chama Cha Mapinduzi kutokana na Ziara ya Mikoa ya Kanda ya ziwa iliyofanywa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda.
Katika Barua hiyo, Mstaafu Shibuda ameandika kuwa Ziara ya Mwenezi Makonda imebainisha wazi kuwa kuna maisha ya Wajibu wa Uzalendo hitajika wa kufaidisha manufaa ya Maslahi mapana kwa Ujenzi wa kuunda Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Uchumi na Taifa.
Mstaafu Shibuda amesema Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anastahili Tuzo za Utu kwa hali na sababu ni Kiongozi Mkwamuaji wa madhila yaundayo Huzuni.
Amesema kwa kuthibitishi hilo, Watanzania warejee kwa uundwaji wa Kamati kadhalika mfano ya Mhe. Jaji Mstaafu Othman Chande ya kuimairsha Haki za Raia.
Mstaafu Shibuda ameendelea kuandika kuwa Ziara ya Mwenezi Makonda imewadhiirishia Umma kuwa Serikali ya awamu ya 6 ina unyenyekevu wa kutumikia Maslahi ya Umma na kusema kuwa Simu zote kwa Mawaziri ni Fursa rafiki kwa Umma nao utambue kwa umakini na ukubali kuwa ni Uwazi na Ukweli pana mipango ya kazi za kutengua kasoro zinazounda sintofahamu kwa yao matumaini na matarajio ya Wananchi.
Pia, Mstaafu Shibuda amesema binafsi yake ameona Mwenezi Makonsa ameunda vema somo la kwamba Serikali ina wajibu wa kukithaminisha chama kinachoongoza Serikali hiyo ambacho ni CCM na vivyo hivyo CCM ina wajibu wa kuisadikisha Tija ya Serikali yake ndani ya Umma dhisi ya Propaganda Hasi za Vyama Kinzani.
Aidha, Mstaafu Shibda amemtaka Mwenezi Makonda kuendelea kusomesha kuhusu yeye anatenda uwajibikaji wake aminifu kwa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.
Kwa kumalizia, Mstaafu Shibuda ametoa rai kwa CCM kuwa macho na kupambanua akili zao dhidi ya mikakati ya wazuaji wa tafsiri ovu ambazo zinataka kuunda hali ya kuchafuana wenyewe kwa wenyewe na kuwataka kutokuwa malighafi au kitoweo cha Propaganda hasi za kujenga kuandika Uongo mtamu dhidi ya umoja na mshikamano wao.
MWISHO.
Labels:
KITAIFA
November 17, 2023
MHE. BITEKO ATOA MAAGIZO KWA MSAJILI WA HAZINA
Written By CCMdijitali on Friday, November 17, 2023 | November 17, 2023
MHE. BITEKO ATOA MAAGIZO KWA MSAJILI WA HAZINA KUELEZA SABABU YA MASHIRIKA YA UMMA KUTOSHIRIKI SHIMMUTA 2023
Na Shamimu Nyaki
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko amemuagiza Msajili wa Hazina kufikia Jumatatu Novemba 20, 2023 awasilishe taarifa kwa nini mashirika mengi ya Serikali hayajatoa kibali kwa watumishi wao kushiriki Mashindano ya Taasisi, Mashirika ya Umma na Binafsi (SHIMMUTA) mwaka 2023 jijini Dodoma.
Mhe. Biteko ametoa maagizo hayo wakati akifungua mashindano hayo Novemba 17, 2023 Uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo amebaini mashirika ya umma yapatayo 248 nchini hayakushiriki mashindano hayo huku mashirika 54 pekee ndio yametoka kibali kwa watumishi wao kushiriki mashindano hayo.
"Naipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuendelea kusimamia vyema michezo, kwa sasa tunashuhudia nchi yetu ikitangazwa vyema na hivi karibuni tumepata uwenyeji wa Mashindano ya AFCON mwaka 2027 kwa kushirikiana na wenzetu wa Kenya na Uganda" Mhe. Doto Biteko.
Mhe. Biteko amewaasa wanamichezo hao kutumia michezo hiyo kubadilishana uzoefu, kupeana mbinu za mafanikio lakini pia kujifunza kuweka alama mahali wanapofanyia kazi pamoja na kutimiza wajibu wa kuhakikisha wanatatua matatizo ya wananchi kupitia sehemu za kazi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amezipongeza Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na Binafsi yaliyotoa ruhusa kwa Watumishi kushiriki mashindano hayo, akisema ni hatua nzuri ya kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza michezo nchini.
"Katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Sita, tumeshuhusia Maendeleo makubwa katika Sekta ga michezo ikiwemo kupata uwenyeji wa Mashindano ya AFCON mwaka 2027, Klabu ya Simba kucheza hadi robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2022/ 23 na Klabu ya Yanga kucheza hadi Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2022/23" amesema Mhe Mwinjuma.
Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndg. Gerson Msigwa amesema lengo la Mashindano hayo ni kuimarisha afya za watumishi na kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, huku akitoa rai kwa makampuni, taasisi za Serikali na binafsi kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kufanya mazoezi na kushiriki mashindano mara kwa mara.
Mashindano hayo yanajumuisha michezo 12 ikiwemo Mpira wa Miguu, Netiboli, Mpira wa Wavu, Riadha, Kivuta Kamba, na mingine ikihusisha wamichezo 3478.
Labels:
MICHEZO
November 16, 2023
RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NCHINI MHE KYLE NUNAS JIJIJINI DAR ES SALAAM LEO
Written By CCMdijitali on Thursday, November 16, 2023 | November 16, 2023
Na Issa Michuzi
Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Wizara ya Afy na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na washirika kadhaa ikiwa ni pamoja na taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), kwa lengo la kuleta wadau muhimu pamoja ili kusambaza, kuthibitisha, na kujifunza mafundisho yanayopatikana kwa vitendo bora na hatua za msingi zinazotokana na ushahidi wa kisayansi ili kuhakikisha utekelezaji bora.
Mkutano huo hutumika kama jukwaa kubwa kwa wataalamu wa afya, watunga sera na wadau kukutana ili kushirikiana maarifa, kutathmini athari za mikakati iliyopo, kushughulikia masuala magumu, kufikiria suluhisho za ubunifu, na hatimaye kuleta mabadiliko chanya.
Moja ya mada kuu ya mkutano huu ilikuwa ni mikakati ya Tanzania kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 (SDG) na malengo ya Mwaka 2025 yanayohusiana na ubora wa huduma za RMNCAH+N.
Tayari Tanzania imeandaa mfululizo wa mipango ya kitaifa muhimu kuboresha ubora wa huduma, ikiwa ni pamoja na Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo (2021-2025), Mpango wa Sekta ya Afya wa Mkakati (HSSP V, 2021), na Mpango Mmoja wa III (2021-2026).
Mipango hii inalenga kuboresha mfumo wa afya, kuongeza upatikanaji wa huduma za RMNCAH, na kupunguza viwango vya vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga. Kufikia malengo haya kunahitaji kuweka kipaumbele katika mikakati ya kuongeza athari na kuanzisha mifumo bora ya kuhakikisha ubora.
Huduma za RMNCAH+N zinaunganishwa katika ngazi mbalimbali za utunzaji, kutoka kwa wafanyakazi wa afya wa jamii hadi watoa huduma za afya katika hospitali za rufaa za kitaifa na hospitali maalum. Ushirikiano wa ufanisi kati ya ngazi hizi, sasisho la miongozo kwa kawaida, na motisha na fidia za kutosha kwa wafanyakazi husababisha kuongezeka
Ushirikiano wa ufanisi kati ya ngazi hizi, sahisisho la miongozo, motisha na fidia za kutosha kwa wafanyakazi husababisha kuongezeka kwa utoaji wa huduma na matokeo bora kwa ujumla. Hata hivyo, kuna masuala kadhaa na uchunguzi unaokwamisha ushirikiano huu.
Ubora wa huduma za RMNCAH+N unatumika kama kipimo cha mfumo wa afya wa Kitaifa. Ushirikiano kati ya wadau mbalimbali, kutoka kwa watoa huduma za afya hadi taasisi za serikali na wafadhili, ni muhimu kuhakikisha ustawi wa akina mama na mtoto. Kutekeleza changamoto na mapendekezo yaliyoainishwa ni muhimu kwa mustakabali bora kwa akina mama na watoto ulimwenguni.
Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) inalenga kubadilisha maisha ya jamii kupitia masuluhisho ya kibunifu na endelevu, wakati leongo lake katika RMNCAH+N ni kufanya kazi kama mwendeshaji ili kuhakikisha hakuna vifo visivyo vya lazima vya akina mama. Misingi yake mikuu ni kubadilisha Maisha watu, kukuza ushirikiano, na kuweka kipaumbele katika matokeo ya pamoja kupitia ushirikiano.
Labels:
KITAIFA
November 14, 2023
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi katika kikao kilichofanyika Jijini The Hague, Uholanzi ambapo amewasisitiza Watanzania hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Taifa lao.
MCHAKATO HADHI MAALUM KWA DIAPSORA KUKAMILIKA MWAKA 2024
Written By CCMdijitali on Tuesday, November 14, 2023 | November 14, 2023
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kukamilisha utaratibu wa kuwapatia Hadhi Maalum Watanzania waishio nje ya nchi, yaani diaspora ifikapo mwaka 2024.
Hayo yamesemwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na diaspora wa Tanzania nchini Uholanzi kwa heshima ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) aliyepo nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 13 - 15 Novemba 2023.
Akifafanua masuala mbalimbali yaliyowasilishwa kupitia risala ya Watanzania iliyosomwa na Mwakilishi wa Umoja wa Watanzania waishio nchini Uholanzi, Bi. Sylvana Lubuva, Mhe. Makamba alisema utekelezaji wa Hadhi Maalumu unategemea kufanyika kwa mapitio ya baadhi ya sheria za nchi kama ile ya ardhi na uhamiaji ili kurahisisha utekelezaji wenye tija kwa walengwa, yaani diaspora na kwamba mchakato huo unatajiwa kukamilika kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
“Miongoni mwa masuala yatakayopewa kipaumbele kwenye Hadhi Maalum ni haki ya kurithi au kurithishwa mali kwa diaspora wa Kitanzania aishiye nje ya nchi. Ili kutekeleza hili kuna maeneo ya sheria yetu lazima yabadilishwe ili watoto wenu wanaoishi huku nje waweze kurithi au kumiliki ardhi” alisema Waziri Makamba.
Sambamba na hilo, ni utaratibu wa kulipa visa pindi diaspora wa Tanzania wanaporudi nyumbani. “Kwenye Hadhi Maalum, mtaruhusiwa kuja nyumbani na kukaa kwa muda mnaotaka bila malipo ya visa. Lakini kwanza ni lazima sheria yetu ya uhamiaji ipitiwe na kurekebishwa, ili kuruhusu kurudi nyumbani bila kulipishwa visa” alisisitiza Waziri Makamba.
Baadhi ya masuala mengine yatakayowanufaisha watumiaji wa Hadhi Maalum ni fursa na motisha mbalimbali za kuwekeza nchini Tanzania kupitia Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC).
Kadhalika, Mheshimiwa Makamba alisisitiza umuhimu wa kujisajili kwenye mfumo wa Diaspora Digital Hub ambapo alisema licha ya kusaidia kuwatambua Watanzania waishio nje ya nchi, pia inarahisisha kwa kiasi kikubwa kuwarejesha nchini pindi majanga makubwa yanapotokea maeneo mbalimbali duniani.
“Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi imara wa Mama Samia Suluhu Hassan, imeelekeza kuokoa Mtanzania au Watanzania popote pale walipo pindi majanga yanapowakuta. Imefanya hivyo kuwaokoa Watanzania waliokua masomoni Ukraine, imewarejesha nyumbani Watanzania waliokuwa Sudan na hivi karibuni Israeli” Mhe. Makamba aliongeza.
Mazoezi haya ya kuwarejesha Watanzania nyumbani hufanyika chini ya uratibu wa Ofisi za Ubalozi zilizopo nchi husika au nchi jirani na hivyo huratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhe. Makamba yupo nchini Uholanzi kwa ziara ya kikazi ambapo siku ya pili ya ziara hiyo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uholanzi.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka katika ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi, jumla ya watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi nchini Uholanzi na maeneo ya karibu.
![]() |
| Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Carilone Chipeta akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Mheshimiwa Waziri na Diaspora uliofanyika Jijini The Hague, Uholanzi. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi katika kikao kilichofanyika Jijini The Hague, Uholanzi ambapo amewasisitiza Watanzania hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Taifa lao.
Labels:
KIMATAIFA
November 13, 2023
SERIKALI KUENDELEA KUWABEBA WATUMISHI
Written By CCMdijitali on Monday, November 13, 2023 | November 13, 2023
SERIKALI KUENDELEA KUWABEBA WATUMISHI WANAOFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU-KIKWETE.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete aliyasema hayo Bungeni wakati Swali ya Mbunge wa Same Mashariki Ndg. Anna Kilango Malecela .
Naibu Waziri alisema, Serikali imeendelea kutoa motisha ya kifedha na isiyo ya kifedha kwa watumishi wote ikiwemo watumishi wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu kwa kuboresha viwango vya posho ya kazi baada ya masaa ya kazi, posho ya kujikimu wakati wa kusafiri, posho ya mawasiliano, kufikisha huduma ya umeme katika maeneo yao, kutoa magodoro, kutoa nyumba za walimu zenye staha na mengine mengi.
Akijibu swali la Ziada, alimuhakikishia Mbunge na Bunge kuwa Serikali inatambua changamoto za Watumishi katika Halmashauri yao na nyengine Nchini kwa kuwa iko timu iliyokwisha zunguka nchi nzima kukagua mazingira ya Watumishi hivyo upatikanaji wa fedha na mipango ya huduma kwa Watumishi itawahakikishia mazingira mazuri ya Watumishi wanaofanya kazi katika mazingira Magumu.
#KaziInaendelea #Bungeni
Labels:
KITAIFA,
Video Category
November 11, 2023
MAJALIWA ASISITIZA NIDHAMU, MAADILI, UBUNIFU KWA WATUMISHI WA UMMA
Written By CCMdijitali on Saturday, November 11, 2023 | November 11, 2023
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wafanye kazi kwa bidii, weledi, nidhamu, uadilifu na ubunifu ili kutimiza maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo Watanzania.
Amesema kila mtumishi anapaswa kutambua kuwa mafanikio katika utekelezaji wa majukumu, mipango na mikakati wanayoisimamia yanahitaji juhudi ya kila mtumishi na nidhamu katika kufanya kazi.
Ametoa wito huo leo Jumamosi Novemba 11, 2023 katika kikao na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF jijini Dodoma.
“Nitoe wito kwa kila mtumishi kuzingatia nidhamu ya kazi na maadili ya utumishi wa umma, Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatekeleza falsafa ya Kazi Iendelee. Kwa msingi huo watumishi wote wa umma mnao wajibu wa kufuata na kutekeleza falsafa hii. ”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza watumishi hao kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao vizuri na kwa weledi. “Kujituma kwenu, ushirikiano na bidii vimewezesha Serikali na hususan Ofisi ya Waziri Mkuu kupata mafanikio makubwa. ”
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa tangu Rais Dkt. Samia aingie madarakani amekuwa anatoa msukumo wa kuboresha mazingira ya watumishi na kusisitiza kushughulikia stahiki mbalimbali za watumishi wa umma ikiwemo ulipaji wa malimbikizo ya mishahara, upandishaji wa madaraja na utoaji wa ajira mpya.
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amelipa madai malimbikizo ya mishahara ya watumishi 121,858 yenye jumla ya shilingi bilioni 207.97, pia amepandisha madaraja watumishi 91,841 na shilingi bilioni 73.4 zimetumika kuwalipa watumishi hao”
Pia, Mheshimiwa Majaliwa aliwakumbusha watumishi hao kusimamia kikamilifu na kwa makini miradi na programu zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ili Ofisi isipoteze fursa ya kuungwa mkono na Taasisi za Kimataifa “Endeleeni kutoa huduma bora za Serikali kwa umma pamoja na kuratibu na kusimamia shughuli za Serikali katika sekta zote kwa ufanisi na tija. ”
Labels:
KITAIFA










































