MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...

Latest Post

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Hemed S. Abdulla afungua kongamano la Vijana Pemba

Written By CCMdijitali on Saturday, August 3, 2024 | August 03, 2024

Published from Blogger Prime Android App


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu. Hemed Suleiman Abdulla amesema kufanyika kwa makongamano ya kitaaluma ndani ya chama ni uimarishaji wa chama na kuunga mkono jitihada za viongozi wa Chama na Serikali katika kutekeleza majukumu yao ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.

 Ameyasema hayo wakati Akifungua Kongamano la Vijana la kuonesha mafanikio, fursa na maendeleo ndani ya miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt Hussen Ali Mwinyi lililofanyika katika Ukumbi wa Umoja ni Nguvu Mkoani Pemba.

 Mhe. Hemed amesema Jeshi la CCM ni Vijana ambao wanahitaji kupewa taaluma na kuelimishwa juu ya kazi mbali mbali zinazofanywa na Chama na Serikali ili nao wakawe mabalozi wazuri wa kuyatangaza mazuri yanayofanywa na viongozi wa nchi.

 Mhe. Hemed ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka Viongozi wa chama na Serikali kuungana na kufanya kazi ya kukitumikia chama cha Mapinduzi kwa pamoja, kutangaza fursa kwa vijana zinazopatikana ndani ya Chama na Serikalini jambo ambalo litaendelea kuipa heshima CCM ya kuongoza Nchi awamu kwa awamu.

 Sambamba na hayo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amekemea tabia ya baadhi wa wanachama kuanza kutangaza nia ya kugombea nafasi mbali mbali wakijua muda muafaka wa kugombea haujafika hivyo amewataka wanachama kushirikiana na viongozi waliopo madarakani katika kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi .

 Aidha Mhe Hemed amemuagiza mwenyekiti wa UVCCM Taifa kuwachukulia hatua za nidhamu wale wote ambao wanaenda kinyume na Katiba na sheria za chama jambo ambalo linakiletea sifa mbaya chama cha mapinduzi na jumuiya zake, pamoja na kusisitiza kuwa Serikali iko tayari kutoa kila aina ya msaada ili kuhakikisha malengo ya vijana yanatimia hasa katika kukipigania chama cha Mapinduzi.

 Nae Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Mohammed Ali Kawaida amesema kufanyika kwa kongamano hilo kutatoa fursa kwa vijana wa Mikoa miwili ya Pemba ya kuona  fursa zilizomo ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kutambua namna ya kuzifikia fursa hizo kwa maslahi yao binafsi na taifa kwa ujumla.

 Kawaida amesema Serikali zote mbili zimetenga fedha nyingi kwa ajili ya kuwawezesha vijana hasa wa CCM ili kuhakikisha wanawekeza katika shuhuli mbali mbali za kimaendelo zitakazowakwamua  kiuchumi.

 Mapema  Mbunge wa Vijana Mkoa wa kusini Pemba Mhe. Munira Mohammed Mustafa ambae pia ndie muandaaji wa Kongamano hilo amesema lengo la kuandaa kongamano hilo ni kuwaweka pamoja vijana wa CCM wa mikoa miwili ya Pemba ili kupatiwa mafunzo yatakayowasaidi kuzitambua fursa na namna ya kuzitumia fursa hizo zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Mhe. Munira amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetenga zaidi ya Bilioni 16 kwa ajili ya vijana kujiendeleza kiuchumi, pamoja na kujenga vyuo vya mafunzo ya amali katika wilaya  za Zanzibar ambavyo vinatoa fursa  kwa vijana kujiendeleza kiufundi na kupata ujuzi utakaowasaidi kupiga hatua kimaendeleo.

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

 

Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR)
03.08.2024.

Picha Uzinduzi wa Treni mpya ya kisasa SGR 2024 Tanzania 

Written By CCMdijitali on Friday, August 2, 2024 | August 02, 2024


Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App

















Published from Blogger Prime Android App

WAZIRI KOMBO AMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE UAPISHO WA RAIS WA IRAN



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Masoud Pezeshkian wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Tehran


·      Afanya mazungumzo na Rais huyo

·      Mikakati ya kukukuza zaidi uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi yawekwa

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo alimwakilisha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za uapisho wa 14 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Masoud Pezeshkian iliyofanyika katika viwanja vya Bunge vya Nchi hiyo jijini Tehran, tarehe 30 Julai, 2024.

 

Waziri Kombo aliwasili nchini humo alfajiri ya tarehe 30 Julai 2024 ambapo baada ya kushiriki katika sherehe hizo za uapisho aliendelea kujumuika na maelfu ya Wanadiplomasia na Viongozi wa Nchi na Serikali kutoka sehemu mbalimbali duniani kushiriki katika dhifa iliyofanyika katika Ikulu jijini Tehran. 

 

Waziri Kombo, alimpongeza Mhe. Pezeshkian kwa ushindi wake katika uchaguzi  wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliofanyika hivi karibuni, na kuongeza kusema kuwa Iran na Tanzania zina uhusiano wa karibu wa kiutamaduni na kihistoria ambao ulianza miaka mingi iliyopita wakati kundi la Wairani kutoka Mji wa Shiraz lilipohamia Zanzibar na kueneza utamaduni wa Iran na lugha ya Kiajemi.

 

Mbali na kushiriki katika sherehe za uapisho huo, Waziri Kombo alifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Masoud Pezeshkian yaliyofanyika Ikulu jijini Tehran tarehe 31 Julai, 2024, akiwa ni Waziri wa Mambo ya Nje wa kwanza na pekee aliyepata fursa ya kuzungumza na Rais huyo muda mfupi baada ya kuapishwa kwake.

 

Mazungumzo hayo yalijikita kujadili kuhusu masuala mbalimbali ya kudumisha na kukuza zaidi ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo siasa, kijamii, utamaduni na uchumi kati ya nchi hizo mbili. 

 

Kwa upande wake Rais wa Iran Mhe. Pezeshkian katika mazungumzo yaliyofanyika kwa takriban dakika 25 huku pande zote mbili zikionesha furaha, shauku na umakini, alielezea furaha yake na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuma ujumbe uliowasilisha salam za pongezi na kushikiri katika sherehe za uapisho wake.  

 

Mhe. Pezeshkian aliendelea kueleza kuwa Tanzania na Iran kwa muda mrefu zimekuwa zikishirikiana katika nyanja mbalimbali, hivyo katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha uhusiano huo unaedelea kukua zaidi na maeneo mengine mapya ya ushirikiano yanafunguliwa kwa maslahi ya pande zote mbili.

 

“Kwa muda mrefu tumekuwa na ushikiano mzuri kati yetu katika maeneo mbalimbali, nitoe raia kuwa sasa niwakati muafaka ufanyike mkutano wa mashauriano wa tume ya uchumi ili iandae rasimu ya Hati za Makubaliano ya Ushirikiano ya pande zote mbili” alisema Rais Mhe. Pezeshkian

 

Kwa upande wake Waziri Kombo alieleza baadhi ya mikakati na hatua mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa na Tanzania katika kudumisha na kukuza zaidi ushirikiano na Iran ikiwemo mandalizi ya kufanyika kwa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC), Kongamano la biashara kati ya Tanzania na Iran, kubadilishana ziara za viongozi kufanya mapitio ya suala la Visa rejea (referral visa). 

 

Vilivile, Waziri Kombo alifanya mazungumzo na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Ali Bagheri ambapo walijadili na kukubaliana utekelezaji masuala mbalimbali muhimu katika kukuza ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Masoud Pezeshkian walipokutana kwa mazungumzo katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Tehran, tarehe 30 Julai, 2024, alipokwenda kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akiagana na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Masoud Pezeshkian mara baada ya hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais wa Iran kwa ajili ya wageni wake.

TANZANIA-COMORO ZASAINI HATI NNE ZA MAKUBALIANO



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro anayeshughulikia Nchi za Kiarabu, Nchi zinazozungumza Kifaransa, Diaspora na Mtangamano wa Afrika Mhe. Mohamed Mbae wakitia saini Hati za Makubaliano

Tanzania na Visiwa vya Comoro zimesaini Hati nne za Makubaliano kwenye kilele cha Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Comoro uliofanyika tarehe 24 Julai,2024 jijini Dar es Salaam. 

 

Hati zilizosainiwa katika kikao hicho zinazojumuisha nyanja za; Ushirikiano wa Kidiplomasia, Afya, Biashara na Viwanda na Teknolojia ya Habari.  Utiaji saini hati hizo umeshuhudiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro anayeshughulikia Nchi za Kiarabu, Nchi zinazozungumza Kifaransa, Diaspora na Mtangamano wa Afrika Mhe. Mohamed Mbae.

 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa kihistoria, Waziri Tax ameelezea umuhimu wa kusainiwa kwa hati hizo kuwa itawezesha pande hizo mbili kuwa na ushirikiano ulio katika mpangilio mzuri katika nyanja husika na hivyo kuleta tija zaidi.

 

Pamoja na kutia saini Hati za Makubaliano pia tumekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo mengine mengi ikiwemo miondombinu, nishati, ulinzi na usalama, uchumi wa buluu, utalii, utamaduni, sanaa na michezo na Maendeleo ya vijana. Ameeleza Dkt. Tax
 

Naye Mhe. Mbae ameeleza kufurahishwa kwake na kufanyika kwa mkutano huo wa JPC na kuongeza kuwa mkutano huo ni kiungo muhimu katika kuendelea kukuza na kuimarisha uhusiano na kati ya Tanzania na Comoro.

 

Ameipongeza Tanzania kwa kuandaa mkutano huo na hivyo kuonesha dhamira ya dhati ya Tanzania katika kuendelea kushirikiana na Comoro.

 

Mbali na kusainiwa kwa Hati hizo Mawaziri hao wameridhishwa na kupongeza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa makubaliano na maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa kwa pamoja kati ya pande hizo mbili tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Jumla wa Ushirikinao mwaka 2009. 

 

Vilevile mkutano huo umejadili na kuweka mikakati ya namna ya kuendelea kukuza biashara baina ya pande hizo mbili. Mikakati hiyo pamoja na mambo mengine italenga kuwahimiza sekta binafsi kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili na kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo na zile zinazotokana na Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) na Eneo Huria la Biashara la SADC.

 

Akizungumzi kuhusu mkutano huo Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu ameeleza kuwa, Comoro ni mshirika muhimu wa Tanzania katika biashara, ambapo kwa mwaka 2023 Tanzania iliuza nchini humo bidhaa zenye thamani ya shilingi bilioni 148. 

 

Ameongeza kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano huo sio tu yataongeza ushirikiano wa kidiplomasia bali yanatarajiwa kuongeza kiasi cha bidhaa ambazo Tanzania inaingiza nchini humo. 

 

Katika mkutano huo ujumbe wa Tanzania umejumuisha wataalamu na watendaji kutoka sekta mbalimbali na umeongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax, ambaye pia aliongoza mkutano huo kwa kushirikiana na mwenyekiti mwenza Waziri Mbae wa Comoro. 


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro anayeshughulikia Nchi za Kiarabu, Nchi zinazozungumza Kifaransa, Diaspora na Mtangamano wa Afrika Mhe. Mohamed Mbae wakionesha moja ya Hati za Makubaliano.



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro anayeshughulikia Nchi za Kiarabu, Nchi zinazozungumza Kifaransa, Diaspora na Mtangamano wa Afrika Mhe. Mohamed Mbae wakitia saini Hati za Makubaliano



Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro anayeshughulikia Nchi za Kiarabu, Nchi zinazozungumza Kifaransa, Diaspora na Mtangamano wa Afrika Mhe. Mohamed Mbae akizungumza kwenye Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Comoro uliofanyika jijini Dar es Salaam



Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Comoro uliofanyika tarehe 24 Julai,2024 ukiendelea jijini Dar es Salaam.



Wanaojiandikisha kuwa wapiga kura zaidi ya mara moja kutumikia kifungo jela

 


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 25 Julai, 2024 mkoani Geita. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Bw. Kailima Ramadhan na kushoto ni Mjumbe wa Tume, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omar.


Na. Mwandishi Wetu, Geita

Wananchi watakaofanya udanganyifu ili wajiandikishe zaidi ya mara moja wanatenda kosa na wakibainika wanaweza kufungwa jela kifungo kisichopungua miezi sita na kulipa faini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele leo tarehe 25 Julai, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Geita.  

“Ningependa kusisitiza kuhusu suala la kujiandikisha kuwa mpiga kura zaidi ya mara moja, jambo hili ni kosa la kisheria kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 114(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na.1 ya Mwaka 2024,” amesema.

Jaji Mwambegele amefafanua kuwa kifungu hicho kinasema mtu yeyote atakayeomba kuandikishwa zaidi ya mara moja atakuwa ametenda kosa la kisheria na akitiwa hatiani adhabu yake ni faini isiyopungua kiasi cha shilingi laki moja (100,000/=) na isiyozidi shilingi laki tatu (300,000/=) au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miezi sita na kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja.  

Katika hatua nyingine, Jaji Mwambegele amesisitiza kuwa hakuna uwezekano wa mtu kujiandikisha  mara mbili na taarifa zake kusalia kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kuwa kabla ya kutoa nakala ya mwisho, Tume hulisafisha Daftari kwa kuwaondoa wapiga kura waliojiandikisha zaidi ya mara moja.

“Mara baada ya uandikishwaji wa wapiga kura kukamilishwa, taarifa zote huingizwa kwenye mfumo wa AFIS (Automated Finger Print Identification System) ambao huwaonesha wote waliojiandikisha kwenye Daftari zaidi ya mara moja. Wapiga kura wa aina hii hufutwa moja kwa moja kwenye vituo vyote na kuwabakisha kwenye kituo alichojiandisha mara ya mwisho,” amesema.

Ameongeza kuwa orodha ya waliojiandikisha zaidi ya mara moja hupelekwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya hatua za kisheria na kwamba Tume imefanya hivyo katika chaguzi za nyuma ambapo katika uandikishaji uliofanyika mwaka 2015, Tume ilibaini jumla ya wapiga kura 52,078 waliojiandikisha zaidi ya mara moja ambapo orodha yao ilikabidhiwa kwa Jeshi la Polisi tarehe 27 Agosti, 2015 kwa ajili ya hatua za kisheria.

“Katika uboreshaji wa Daftari wa mwaka 2020, Tume ilibaini majina ya watu 42,301 ambao walijiandikisha zaidi ya mara moja na orodha hiyo ilikabidhiwa kwa vyombo vinavyohusika na makosa ya kijinai,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameeleza kuwa baada ya kukamilika kwa uchakataji wa Daftari, Tume huchapisha na kuweka wazi Daftari hilo chini ya kifungu cha 24 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya mwaka 2024 ambapo wananchi hulikagua.

“Baada ya kukamilika kwa uchapishaji wa mwisho wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, vyama vya siasa hupewa nakala tepe (soft copy), haijawahi kutokea jina likajitokeza zaidi ya mara moja. Hivyo, hakuna uwezekano wa mtu kuandikishwa zaidi ya mara moja na kuweza kutumia nafasi hiyo kuwa kwenye vituo zaidi ya kimoja siku ya kupiga kura,” amesema Jaji Mwambegele.

Mwisho.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AKAGUA UJENZI WA BUSTANI YA MWANAMASHUNGI - CHAKECHAKE

Written By CCMdijitali on Thursday, August 1, 2024 | August 01, 2024

Published from Blogger Prime Android App


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba kuhakikisha ujenzi wa eneo la Bustani ya Mwanamashungi unakamilika ndani ya wiki mbili zijazo ili kutoa nafasi kwa wananchi kulitumia eneo hilo.


Akikagua maendeleo ya ujenzi wa Bustani hio Makamu wa Pili wa Rais amesema kumekuwa na changamoto ya uhaba wa maeneo ya kupumzukia kwa wakaazi wa maeneo hayo na maeneo jirani ya mji wa chake chake  hivyo Baraza la Manispaa wanalazimika kuchukua jitihada za ziada kuhakikisha mkandarasi anamaliza ujenzi huo kwa wakati na viwango vinavyotakiwa ili wananchi waweze kunufaika na bustani hio.

 

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar amesema kukamili kwa bustani hio itawanufaisha wananchi hasa wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuweza kufanya biashara zao maeneo hayo kwa lengo la kujipatia kipato kwa mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa Taifa.

 

Aaidha makamu wa Pili wa Rais ameagiza kuzungushiwa uzio eneo lote linalozunguka bustani hio kwa ajili ya usalama wa wananchi watakaofika katika bustani hio  wao na mali zao.

 

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais amekagua ujenzi wa maegesho ya magari pamoja na ujenzi wa nyumba za makaazi na maduka zinazojengwa na Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC)katika eneo la Mabatini chake chake ambapo  amesema miradi yote inayojengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina maslahi makubwa kwa wananchi kwani kukamilika kwa ujenzi wa nyumba hizo kutapunguza changamoto ya makazi kwa wananchi na wafanyabiasha watafanya biashara zao katika maeneo rasmi.

 

Pia ameawataka wafanya biashara  kuacha tabia ya kufanya biashara pembezoni mwa barabara jambo linaloleta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hizo na kuisababishiaa hasara kubwa serikali .

 

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar amesema kituo cha maegesho ya magari kinachojengwa Tibirinzi kitakapokamilika kitatatua kero ya msongamano wa magari ndani ya mji wa chake-chake na kutoa fursa kwa wafanyakazi kuegesha magari yao katika maeneo salama.

 

Nae Naibu waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Salha Mohd Mwinjuma amesema Wizara itasimamia na kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizo uliojumiisha na Nyumba za Makaazi na  Milango ya maduka unakamilika  kwa wakati uliopangwa na kwa kiwango kilicho kusudiwa ili kuwawezesha wananchi kuishi sehemu salama sambamba na wafanya biashara kuweza kuendelea na  biashara zao ndani ya jengo hilo.

 

Aidha Mhe. Salha ameiomba Serikali kuwapatia eneo lililopo pembezoni mwa nyumba hizo ili waweze kuendelea na ujenzi mwengine wa nyumba ili kuhakisha wanaunga mkono jitihada za Mhe.Rais  za kuwaletea wananchi maendeleo ikiwemo kuwajengea nyumba za kisasa za bei nafuu.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chake - Chake Mhe. Ramadhan Suleima Ramadhan amesema kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Bustani ya Mwanamashungi  na miradi mengine inayojengwa na serikali kutaubadilisha muonekano wa mji wa chake na kuwa wa kisasa zaidi na wananchi watapata fursa ya kufanya biashara zao katika eneo hilo.

 

Amesema wananchi wa Jimbo la Chake - Chake wataendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dkt Mwinyi ambe amedhamiria kuifungua Pemba kiuchumi na kimaendeleo na kuahidi mwaka 2025 kumpigia kura nyingi ili aendeleo kuiongoza Zanzibar kwa mafanikio zaidi.

 

Miradi iliyokaguliwa na Mhe. Makamu wa Pili wa Rais ni pamoja na UJENZI WA MAEGESHO YA MAGARI TIBIRINZI, UJENZI WA BUSTANI YA MWANAMASHUNGI, UJENZI WA MRADI WA NYUMBA ZA MAKAAZI NA MADUKA MABATINI, UJENZI WA OFISI ZA WIZARA YA ELIMU PEMBA NA UJENZI WA SKULI YA MSINGI YA MICHAKAINI "B" YA GOROFA (G+2).

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

 

Imetolewa na kitengo cha habari (OMPR)

Leo tarehe 01.08.2024.

DKT. NCHEMBA AZINDUA RIPOTI YA MWENENDO WA UCHUMI WA NCHI-NCHI YAZIDI KUPAA KIUCHUMI


Published from Blogger Prime Android App

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amezindua rasmi Ripoti ya Mapitio ya Hali ya Mwenendo wa Uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2024, iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), yenye kauli mbiu isemayo “Driving Tanzania’s Transformation - The Reform of the Global Financial Architecture”.


Mhe. Dkt. Nchemba, amezindua Ripoti hiyo kwa njia ya mtandao akiwa Abuja nchini Nigeria, ambako anaongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Ripoti hiyo inaonesha kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi na kijamii na kuwa kinara miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki, licha ya changamoto zinazoikabili Dunia ikiwemo athari za UVIKO-19, mabadiliko ya tabianchi na mizozo ya vita inayoendelea maeneo mbalimbali duniani.

Dkt. Nchemba amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha Uchumi wake kupitia Mpango wake wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III), wenye lengo la kujenga uchumi imara, shirikishi na wenye ushindani kupitia sekta za uzalishaji, ikiwemo kilimo, uzalishaji viwandani, kuongeza thamani ya bidhaa, uwekezaji na biashara pamoja na kukuza ajira kwa wananchi hususan vijana.

Amezitaka Taasisi za Fedha za Kimataifa, ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kuweka mazingira ya upatikanaji wa fedha zenye masharti nafuu ili kuziwezesha nchi za Afrika kuwa na uwezo endelevu wa kutekeleza mipango ya maendeleo kwa ajili ya nchi zao.

Dkt. Nchemba alitaja eneo linalokwamisha maendeleo ya nchi hizo za Kiafrika ikiwemo Tanzania kuwa ni pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi ambapo kila mwaka Tanzania inahitaji dola za Marekani bilioni 6.3 za kukabiliana na hali hiyo zikiwemo athari za papo kwa papo zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ripoti hiyo ya Mwenendo wa Uchumi wa Tanzania iliyowasilishwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania umezidi kuimarika na unatarajia kupanda kutoka asilimia 5.1 mwaka 2023, hadi asilimia 5.7 mwaka 2024, na utafika asilimia 6 mwaka 2025.

Tanzania imesifiwa pia kwa kufanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei na kubaki katika wigo wa chini ya asilimia 3.3 kutokana na sera bora za kiuchumi zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Ripoti hiyo imezitaja sekta zilizochangia ukuaji huo wa uchumi kuwa ni pamoja na sekta ya fedha, huduma, kilimo, kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji, biashara, na sekta ya madini.

Benki ya Maendeleo ya Afrika imeishauri Tanzania kuendelea kusimamia vizuri sera zake za fedha na uchumi, kwa kuendelea kuwekeza zaidi kwenye sekta za uzalishaji, kilimo, nishati na kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Uzinduzi huo wa Hali ya Uchumi wa Tanzania, umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Viongozi waandamizi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB, Wachambuzi wa masuala ya uchumi wa ndani na nje ya  nchi pamoja na wawasilisha mada.

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App

MAAFISA ELIMU WATAKIWA KUWA WAADILIFU NA WAFUATILIAJI WA MIRADI YA MAENDELEO


Published from Blogger Prime Android App























Na OR TAMISEMI, Arusha

Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amewataka Watendaji wa Mikoa, Halmashauri na ngazi ya msingi kuwa waadilifu, kujiamini na kufuatilia miradi ya maendeleo ili kuleta ufanisi na kulinda thamani ya fedha za Serikali.

Dkt. Msonde ametoa kauli hiyo leo tarehe 31 Julai, 2024 Chuo Cha Ualimu Patandi Jijini Arusha wakati akifunga mafunzo ya siku 3 kwa Maafisa Elimu Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga, Maafisa TEHAMA na Waratibu wa Mradi ngazi ya Mkoa, Maafisa Elimu Sekondari, Maafisa Manunuzi na Ugavi ngazi ya Halmashauri, Waratibu wa mradi ngazi ya Halmashauri na Wakuu wa Shule kuhusu utekelezaji wa miradi ya shule za sekondari (SEQUIP).

“niwatake wasimamizi na wataalamu wote wa elimu na Idara mwambata katika usimamizi wa Miradi mkaimarishe usimamizi na kuongeza ubunifu katika utatuzi wa changamoto zinazoathiri shughuli za ujenzi wa miundombinu ya shule. Aidha, mkasimamie vema utekelezaji wa maboresho yanayofanyika mara kwa mara katika shughuli za ujenzi kwenye maeneo yenu” alisema Dkt. Msonde.

Dkt. Msonde amewataka Watendaji hao kuhakikisha ujenzi wa miundombinu inakamilika kabla au ifikapo tarehe 1 Novemba, 2024 ili shule zinazojengwa zisajiliwe na kuwekwa katika mpango wa kuwapokea wanafunzi kwa ajili ya kuanza masomo mwaka 2025 na kuzingatia thamani ya fedha na Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata watakaoshindwa kusimamia wataondoshwa kwenye nafasi zao.

Akitoa maelezo ya awali, Mratibu Mradi wa SEQUIP kutoka Idara ya Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Robert Msigwa amesema mafunzo hayo yamehusisha jumla ya washiriki 240 wakiwemo Maafisa Elimu sekondari 32, Maafisa Ugavi wa Halmashauri 35 na Wakuu wa shule 124 kutoka shule za sekondari zilizopokea fedha za awamu ya tatu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu shuleni.

Aidha, Bw. Msigwa amesema, Ofisi ya Rais TAMISEMI     ilibaini uwepo wa changamoto ya usimamizi na uzingatiaji wa miongozo mbalimbali ya usimamizi wa ujenzi na suluhisho likawa kuwajengea uwezo maafisa hao ili kuimarisha usimamizi wa ujenzi wa miundombinu ya Serikali.

Naye Mkuu wa Shule Kwaraa Sekondari kutoka Babati Mji Deogratius Ami amesema mafunzo hayo yatawasaidia kutekeleza miradi ya ujenzi kwa wakati na ufanisi mkubwa na kuzingatia maelekezo ya Serikali ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Maafisa wengine kwa mujibu wa mifumo ya manunuzi na dhana ya ufuatiliaji miradi (Kobo tool).

Mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa hao yamefanyika katika vituo sita ambapo awamu ya kwanza yalifanyika katika vituo vya Chuo cha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Morogoro, Chuo cha Ualimu Mtwara na chuo cha Ualimu Butimba na awamu ya pili tikifanyika Chuo cha Ualimu Patandi, Tabora na Mbeya.

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link