MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...

Latest Post

Yanga ni ushindi tu

Written By CCMdijitali on Sunday, February 14, 2016 | February 14, 2016

Kikosi cha Yanga  1-0  Cercle de Joachim ya Mauritius
 
WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga wameanza vizuri michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius katika mechi iliyochezwa jana.

Bao pekee la Yanga katika mchezo huo wa hatua ya awali lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa raia wa Zimbabwe Donald Ngoma dakika ya 17 akiunganisha krosi ya Juma Abdul.

Ushindi huo wa ugenini unaifanya Yanga kuwa na kazi nyepesi katika mchezo wa marudiano ambao unatarajiwa kuchezwa wiki mbili zijazo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Awali kabla ya kuanza kwa pambano hilo kulikuwa na hofu kwamba huenda lingesogezwa mbele kutokana na mvua kubwa kunyesha na maji kujaa uwanjani lakini baada ya muda mambo yalikaa sawa na mchezo huo kuendelea.

Pamoja na mvua kuharibu ladha ya mchezo kwa wachezaji kuteleza mara kwa mara lakini Yanga walionesha soka safi na kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la wenyeji wao Cercle de Joachim, ambao safu yao ya ulinzi ilifanya kazi kubwa ya kuwadhibiti washambuliaji wa wageni wao.

Wenyeji Cercle de Joachim, pamoja na kufungwa bao la mapema lakini walionekana ni timu nzuri kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha na kuwasumbua Yanga, na kipa Ally Mustaph ‘Barthez’ kufanya kazi kubwa ya kuokoa mashambulizi hayo.

Mshambuliaji Amissi Tambwe, atalazimika kujilaumu kwa kushindwa kuipa ushindi mnono timu yake baada ya kupoteza nafasi mbili za wazi katika mchezo huo ambao kama angezipata timu yake ingepunguza presha katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa wiki mbili zijazo jijini Dar es Salaam.

Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm, na msaidizi wake Juma Mwambusi, walionekana wakali kutokana na kusimama mara kwa mara kutoa maelekezo kwa wachezaji wao ili kulinda bao hilo lisirudi kutokana na kasi waliyokuwa nayo wapinzani wao.

Kipindi cha pili Yanga ilionekana kucheza kwa kujihami zaidi wakilinda bao lao huku wakifanya mashambulizi ya kustukiza ambayo mara kadhaa yalikuwa na madhara makubwa kwa we nyeji wao Cercle de Joachim, lakini hata hivyo waliyahimili.

Katika dakika ya 56 beki Abdul aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake ilichukuliwa na Patto Ngonyani ambaye aliweza kuumudu mchezo huo ingawa ulikuwa mchezo wake wa kwanza wa kimataifa tangu atue Yanga. Ushindi huo unaifanya Yanga kuhitaji anagalau sare katika mchezo wa marudiano ili waweze kusonga mbele raundi ya kwanza ambapo mechi zake zitapigwa kuanzia Machi mwaka huu.

Kikosi kamili cha Yanga kinachokwenda kambini Pemba :

Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benedicto Tinocco.

Mabeki; Juma Abdul, Mbuyu Twite (DRC), Oscar Joshua, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Vincent Bossou (Togo) na Pato Ngonyani.

Viungo ni; Said Juma ‘Makapu’, Salum Telela, Thabani Kamusoko (Zimbabwe), Haruna Niyonzima (Rwanda), Simon Msuva, Issoufou Boubacar (Niger), Godfrey Mwashiuya na Deus Kaseke.

Washambuliaji ni; Malimi Busungu, Paul Nonga, Amissi Tambwe (Burundi) na Donald Ngoma (Zimbabwe).

BENCHI LA UFUNDI; Kocha Mkuu; Hans van der Pluijm (Uholanzi), Kocha Msaidizi; Juma Mwambusi, Kocha wa Makipa; Juma Pondamali

Daktari; Nassor Matuzya, Meneja; Hafidh Saleh, Mchua Misuli; Jacob Onyango na Mtunza Vifaa; Mohammed Mpogolo.

Balozi Seif Ali Iddi amaliza ziara ya Siku Tatu Kisiwani Pemba.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichani hapo uwanja wa ndege wa Pemba kabla ya kurejea Unguja baada ya kumaliza ziara ya Siku Tatu Kisiwani Pemba.

Kulia ya Balozi Seif ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Nd. Vuai Ali Vuai na Kushoto ya Balozi Seif ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Panadu Ameir Kificho.
Balozi Seif akijibu baadhi ya maswali ya Waandishi wa Habari alipokutana nao  uwanja wa ndege wa Pemba baada ya kukamilisha ziara yake ya siku Tatu Kisiwani humo.

Kushoto ya Balozi Seif ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuma Majid na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Dr. Maua  Daftari.

Picha na – OMPR – ZNZ.

                                      Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwa vile Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeshatangaza Tarehe ya Kurejewa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar  yeye binafsi haoni umuhimu wa kurejewa kwa mazungumzo kati ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein .

Alisema mazungumzo hayo kwa sasa hayana tija yoyote kwa vile Wananchi katika kipindi hichi wameanza kujiweka tayari wakijiandaa kupiga kura kufuatia  Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar { ZEC } kufuta matokeo ya uchaguzi Tarehe 28 Oktoba mwaka 2015.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Uwanja wa ndege wa Pemba akijiandaa kurejea Kisiwani Unguja baada ya kumaliza ziara yake ya siku Tatu Kisiwani Pemba kukagua shughuli mbali mbali za Maendeleo akiwa Mtendaji Mkuu wa Serikali Balozi Seif Ali Iddi alisema iwapo yapo malalamiko yoyote muhusika wake ana wajibu wa kwenda Mahakamani kwa hivi sasa.

Balozi Seif alisema mazungumzo ya pamoja kati ya Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi {CUF } Maalim Seif Sharif Hamad  kuhusu kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu yalifanyika kwa maombi ya Maalim Seif ambae yeye binafsi ndie aliyeamua kujiondoka kwenye maendeleo ya vikao vya mazungumzo hayo.

Alisema kinacholikabili Taifa kwa wakati huu ni suala la marejeo ya uchaguzi na kuwaomba watu walioamua kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio ni vyema wakabakia nyumbani ili kutoa fursa kwa wenzao waliokubali kushiriki watumie haki yao ya Kidemokrasia kuwachaguwa Viongozi wanaowataka.

Balozi Seif alifahamisha kwamba hata yeye anaheshimu maamuzi ya Tume ya Uchaguzi  ya Z anzibar ambayo haiwezi kuingiliwa na chombo chochote licha ya kwamba Tayari alikuwa ameshashinda na kupewa cheti kinachothibitisha kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda.

“ Tupo tuliokwishashinda kwenye chaguzi zetu za Majimbo na kupewa vyeti vinavyothibisha ushindi huo lakini baadhi yetu kwa nini tuendelee kushutumu maamuzi ya tume ambayo kutokana na sababu za msingi ilizoeleza  za kujitokeza kwa dosari kadhaa kwenye zoezi zima ikalazimika kufuta matokeo na uchaguzi wote ? ”. Aliuliza Balozi Seif.

Akizungumzia uvumi uliojitokeza  wa kuwepo kikundi cha Vijana wanaopiga watu katika badhi ya maeneo maarufu Mazombi Balozi Seif alisema hana taarifa yoyote iliyomfikia akiwa kama Kiongozi wa Juu wa Serikali kuhusu shutma hizo.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa agizo kwa vyombo vya Ulinzi kufanya uchunguzi dhidi ya shutuma hizo na pale itakapobainika kuwepo kwa shutma hizo vifanye juhudi ya kuwakamata wahusika hao na kuwafikisha mbele ya Doli ili sheria ichukuwe mkondo wake.

Balozi Seif alieleza kwamba nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Ile ya Jamuhuri ya Mauungano wa Tanzania ni kuiona nchi inaendelea  kubakia katika hali ya amani na utulivu wakati wote kabla na baada ya uchaguzi.

Aliwaasa na kuwaomba Wananchi wa maeneo mbali mbali Kisiwani Pemba kuendelea kuishi kwa amani na upendo na kushirikiana katika mambo yao bila ya kuendekeza zaidi itikadi zao za Kisiasa ambazo tayari zimeshaonyesha muelekeo mbaya.

Alieleza kwamba matokeo ya sasa yaliyojichomoza katika hujuma za moto sambamba na baadhi ya watu kuanza kuashiria vitisho dhidi ya wananchi wenzao walioamua kushiriki uchaguzi wa marejeo kwa kuwatilia X nyumba zao yanaonyesha safari ya hatari katika maisha miongoni mwa jamii.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
14/2/2016.
Pemba

Kairuki awageuzia kibao Tasaf

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki.
Kwa ufupi
Pia ameagiza kufanyika ukaguzi maalumu wa fedha za Serikali.
Akizungumza katika Makao Makuu ya Tasaf jijini hapa juzi, Angela alisema anataka ukaguzi wa kina ufanyike kupitia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).



By Vicky Kimaro, Mwananchi vkimaro@mwananchi.co.tz


Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki ametoa siku 30 kwa uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) kujitathmini na kutoa ufumbuzi wa haraka ili kuboresha mradi wa awamu ya tatu unaoendelea kwa kaya maskini nchini.

Pia ameagiza kufanyika ukaguzi maalumu wa fedha za Serikali.

Akizungumza katika Makao Makuu ya Tasaf jijini hapa juzi, Angela alisema anataka ukaguzi wa kina ufanyike kupitia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Katika masuala ya fedha nitakuja sana kukagua zilikuwaje, zimetokaje, kapewa nani, kiasi gani na kama zimemfikia mlengwa,” alisema.

Alisema kwamba haiwezekani kutumia mabilioni ya fedha na ikatokea zikatumika kinyume na malengo kisha taarifa kutolewa vinginevyo.

“Hii siyo sawa ni lazima tuhakiki namna matumizi yalivyo katika ngazi ya kata na watendaji vijijini kama wanatekeleza majukumu yao ipasavyo,” alisema.

Waziri alisema lengo la Serikali ni kuona kila senti ya umma inafanya kazi inayostahili na kwamba, hakutakuwa na msamaha kwa watakaozitumia tofauti.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga alisema mafanikio ya mradi huo yanakwamisha ukusanyaji wa taarifa kutokana na wakusanya takwimu kutoka katika vijiji vya wanufaika.

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AZUNGUMZA NA WAZEE WA DAR ES SALAAM, ASKOFU GWAJIMA NDANI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee tayari kwa kuongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amehudhuria katika mkutano huo ambapo alionekana mtu mwenye kufurahia hotuba hiyo, Kamera ya Fullshangwe ilimnasa askofu huyo maarufu kwa matamshi yake ya "Wakale Malimao" akiwa na tabasam kubwa akionekana kufurahia kuhudhuria kwake katika mkutano huo.

Mwanzo wakati alipofika ukumbini hapo alikuta ratiba inaendelea hivyo ilibidi akae viti vya nyuma lakini Shekh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim alimpigia simu na kumwambia aende mbele akakae pamoja na viongozi wenzake wa dini na ndipo alipoenda kukaa eneo hilo.
(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo wakati alipoongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es salaam mzee Hemed Mkali kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Mh. Raymond Mushi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam 
Ndugu Ramadhan Madabida.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es salaam wa zamani Mzee Idd Simba, 
Kulia ni mfanyabiashara Abdullah Mohamed.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa na Mke wa Rais Mama Janet Magufuli wakiwa meza kuu pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam.
 Baadhi ya mawaziri wa wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya tano wakiwa katika mkutano huo.
 Baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo na ya Kiislamu wanaounda kamati ya Amani wakiwa katika mkutano huo
 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hakubaki nyuma na yeye amehudhuria katika mkutano huo na hapa akionekana mwenye furaha na bashasha kama alivyonaswa na kamera yetu.
 Baadhi ya wazee wa Dar es salaam wakitambulishwa katika mkutano huo.
 Baadhi ya mawaziri waliohudhuria katika mkutano huo kutoka kulia ni Mh. Profesa Sospeter Muhongo, Dk. Abdallah Posi, Nape Nnauye, Januari Makamba na Ummy Mwalimu.
 Baadhi ya wazee wakifuatilia kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia mkutano huo.


 Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimia wazee katika mkutano huo.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimia wazee katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es alaam Mzee Hemed Mkali akihutubia katika mkutano huo na kumkaribisha Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kuwahutubia wazee hao. 

Rais Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee February 13, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru Wazee
wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wazee
wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.


MUFTI MKUU WA TANZANIA ABUBAKARY ZUBEIRY BIN ALLY ARUHUSIWA TOKA HOSPITALINI





Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kwa niaba ya Serikali akizungumza na waandishi wa habari na viongozi wa kidini waliofika katika Hopisitali ya Taifa Muhimbili kumjulia hali Mufti baada ya kupata ruhusa kutoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCT)
Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry bin Ally, akizungumza na waandishi wa habari 
(hawapo pichani ) na
Baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo na ya Kiislamu wanaounda kamati ya Amani walipofika katika Hopisitali ya Taifa Muhimbili kumjulia baada ya kupata ruhusa kutoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCT) ambapo alianza kwa kumshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimwagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu afikishe salamu hizo na kwa Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa na pamoja na wote waliofika kumjulia hali na mungu awaongoze na 
Rais awaangalie madaktari kwa jicho la tatu na awaongezee uwezo, hayo yalizungumzwa na mufti wakati waziri huyo alizipofika kwa niaba ya Serikali na kuahidi salamu hizo zitamfikia Rais Magufuli. mwisho mufti aliwashukuru waandishi wa habari kwa wao kufika mara kwa mara kumjulia hali .(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)





 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCT) akimkaribisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kwa niaba ya Serikali kwa kuzungumza na waandishi wa habari na viongozi wa kidini.
 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (katikati) akiwa na wenzake waliofika katika Hopisitali ya Taifa Muhimbili kumjulia  hali Mufti  baada ya kupata ruhusa kutoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCT)
 Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila akisoma maelezo kwa niaba ya familia ya Mufti,katika Hopisitali ya Taifa Muhimbili kumjulia hali Mufti baada ya kupata ruhusa kutoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCT)





Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (katikati) akiwa na wenzake waliofika katika Hopisitali ya Taifa Muhimbili kumjulia hali Mufti baada ya kupata ruhusa kutoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCT)

UCHAMBUZI: SIKU 100 ZA JPM, Kigwangalla: Kasi ya Magufuli inalenga mabadiliko ya kweli

Written By CCMdijitali on Saturday, February 13, 2016 | February 13, 2016

Dk Hamisi Kigwangalla akiapishwa na Rais John Magufuli kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Kwa ufupi

Ni Naibu Waziri ambaye alianza kazi saa chache baada ya kuapishwa na Rais kushika wadhifa huo, kwa kufanya ziara za ghafla hospitali za Mwananyamala na Amana

"Jana Dk John Magufuli alitimiza siku ya 100 tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndani ya siku hizo amefanya mambo mengi yaliyopongezwa na kukosolewa na watu wa kada"


By Fidelis Butahe, Mwananchi fbutahe@mwananchi.co.tz


Jana Dk John Magufuli alitimiza siku ya 100 tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndani ya siku hizo amefanya mambo mengi yaliyopongezwa na kukosolewa na watu wa kada mbalimbali.

Baada ya kuingia madarakani Novemba 5, mwaka jana, Rais Magufuli alitangaza hatua kadhaa za kubana matumizi yasiyo ya lazima, ikiwamo kufuta safari za nje na kupiga marufuku vikao vya kazi vya taasisi na mashirika ya umma kufanyika mahotelini.

Achana na kubana matumizi, rungu lake pia liliwasomba watu zaidi ya 70, wakiwamo watumishi na wajumbe wa bodi za mashirika au taasisi husika wakidaiwa ama kushindwa kuwajibika au kusimamia maeneo yao.

Walioangukiwa na ‘rungu’ hilo ni watumishi na viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Wizara ya Uchukuzi.

Rais Magufuli ambaye kwa sasa ameteka sehemu kubwa ya mjadala nchini na nje ya nchi kutokana na kasi yake, alihutubia Bunge na kuahidi kutumbua majipu yote sugu, akimaanisha kushughulikia kuziba mianya ya ufisadi, urasimu na rushwa inazofanywa na watumishi wa Serikali wasiokuwa waaminifu wanaoshirikiana na wafanyabiashara kuhujumu mapato ya nchi.

Akizungumzia utendaji kazi wa Rais Magufuli, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla anasema kasi hiyo inalenga kurejesha uwajibikaji, kuondoa mazoea kazini, kuwataka Watanzania kukubali maumivu ili kuendana na kasi hiyo ya kuliletea taifa mabadiliko.

Yafuatayo ni mahojiano kati ya Dk Kigwangalla na mwandishi wa gazeti hili.


Swali: Unauzungumziaje utendaji kazi wa Rais Magufuli, watu wanasema kuwa ni nguvu ya soda, unasemaje kuhusu madai hayo?

Jibu: Kasi yake si nguvu ya soda maana kazi anayoifanya inaonekana. Wapinzani wanalalamika kwa sababu Serikali imebadilika na inafanya kazi kwa mtindo tofauti ambao unapendwa na wananchi.

Hapa namaanisha rais, Waziri Mkuu na mawaziri kuwa watendaji zaidi kunawafurahisha wananchi. Kitu kinachoifanya nchi kuwa bora ni wananchi kuamini kuwa kesho itakuwa bora zaidi kuliko jana.

Wananchi wakipoteza matumaini wanakosa uvumilivu, wanaweza kufanya chochote.

Chini ya Serikali ya Rais Magufuli watu wanaamini maisha yao yatakuwa bora kuliko leo wala jana. Jukumu la kuwafanya watanzania kuwa na matumaini ni la Serikali. Tunaonyesha watu mikakati yetu na wanatuamini. Tunasema jambo kwa kumaanisha na tunaaminiwa.

Swali: Unazungumziaje watumishi wa umma kufukuzwa au kusimamishwa kazi, je ni sahihi na ni kweli taratibu zinafuatwa?

Jibu: Huo ndio mwanzo wa kuwaamsha Watanzania. Anachokifanya rais na watendaji wake ni kubadilisha muundo wa kifikra wa Watanzania. Mabadiliko yoyote huanzia kwenye fikra za watu.

Siku hizi watu wanafunga biashara zao mapema kwa sababu ya kuhamasika na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu. Mfano mimi nilifunga getu pale wizara ya afya baada ya kubaini wafanyakazi wanachelewa, tangu wakati huo mpaka sasa watu wanawahi kazini.

Anachokifanya rais na mawaziri wake ni kuchukua hatua ya moja kwa moja kwa watu watakaobainika kuwa si waadilifu au kushindwa kazi na kuweka wengine watakaofanya kazi kwa mtindo utakaoleta tija kwa wananchi.

Baadhi ya watu wanalalamikia utendaji kazi huu kwa sababu majibu yanayotumbuliwa ni ya rafiki zao, wao wenyewe au ndugu. Rais aendelee kutumbua majibu ili watu watoke katika usingizi. Watu wanapaswa kutambua kuwa zama hizi ni tofauti, yaani ukikosea asubuhi unafukuzwa jioni. Watu waheshimu kazi katika ofisi za umma.

Si kwamba wote wanafukuzwa, wapo wanaosimamishwa kazi au kuwekwa pembeni na kufikishwa mahakamani. Hakuna aliyeonewa wala kusingiziwa.

Mfano Wizara ya Afya tulimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Taasisi ya Ocean Road baada ya kubaini kuwa naye ana hospitali inayotoa huduma kama za taasisi hii. Huu ni mgongano wa kimaslahi maana unaweza kukuta hospitali yake ina dawa kuliko zilizopo Ocean Road.

Hatuwezi kumfukuza kazi tutachunguza kwanza. Mkibaini mnaweza kumuweka kando kwa maana ya kutokuwa kiongozi tena, ila kazi ataendelea nayo kama kawaida na mshahara wake utakuwa ule ule.

Swali: Kuna madai kuwa Baraza la Mawaziri la Rais Magufuli limepunguza gharama za Serikali una maoni gani?

Jibu: Gharama zimepungua kwa asilimia kama 40 hivi. Serikali iliyopita ilianza na mawaziri kama 60 hivi ila Rais Magufuli kaanza na mawaziri 34 tu. Najua atakuwa na changamoto ya kulaumiwa na marafiki na jamaa kutokana na kutowateua katika Serikali yake. Ninachokiona ameteua watu wachache watakaofanya kazi, ameunganisha wizara ili kupunguza gharama na itifaki katika mawizara.

Watu wana tazama hizi gharama kwa mitindo mingi, wapo wanaohoji idadi ya makatibu wakuu ambao binafsi naona wamepungua.

Mimi ninachofahamu, ukiwa na mawaziri na naibu mawaziri wengi maana yake umeongeza gharama. Kama ukiunganisha wizara na ngazi ya chini ukawaacha wataalamu kufanya kazi zao utapunguza gharama.

Mfano wizara ya Afya, kuna waziri wawili na Katibu Mkuu wa Afya na wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Makatibu hawa wawili hawana manaibu na kwa kufanya hivyo unakuwa tayari umepunguza gharama.

Kwa mtindo uliokuwa zamani, maana yake Wizara ya Afya ingekuwa na waziri na naibu waziri na ile ya Maendeleo ya Jamii nayo ingekuwa na mawaziri wawili na makatibu wakuu wawili.

Kitendo cha Wizara ya Afya kuunganishwa na ile ya Maendeleo ya Jamii maana yake Rais Magufuli kapunguza idadi ya mawaziri wawili na makatibu wakuu wawili, hapo maana yake hata magari yaliyopaswa kutumiwa na watu hao nayo hayatatumika tena.

Hakutakuwa na gharama za matengenezo ya magari jambo ambalo wakati nikiwa mbunge nilikuwa nikilisema sana. Kuunganisha wizara hizi kumepunguza posho walizopaswa kulipwa madereva wa mawaziri na wasaidizi wao maofisini.

Wapo wanaosema kuwa na makatibu wakuu hakujapunguza gharama! Napingana na mtizamo huo kwa sababu itifaki ya kumhudumia katibu mkuu si kama ya kumhudumia waziri maana Katibu Mkuu hana msaidizi, mlinzi, msaidizi wa ofisini, wahudumu wa ofisini na nyumbani.

Swali: Nini faida kwa Rais Magufuli kudhibiti safari za nje na nini hasara?

Jibu: Kudhibiti safari za nje ni jambo zuri ninaliunga mkono. Tunapunguza matumizi kwa kiasi kikubwa maana tumejifunza katika Serikali iliyomaliza muda wake, ambayo safari za viongozi zilikuwa nyingi na kuitia hasara Serikali. Hata faida yake hatukuiona.

Rais Magufuli anataka kudhibiti safari za viongozi na watumishi wa umma. Anachuja na kushauriwa na watu wake wa karibu kutokana na umuhimu wa safari husika. Hii inasaidia kuleta uwajibikaji kwenye serikalini, binafsi napenda uwajibikaji na ndio maana nilifunga mageti pale wizarani.

Naamini hatuwezi kupata ustawi bila kuwajibika. Hatuwezi kusonga kutoka hapa tulipo kwenda mbele bila kuwajibika na katika hilo lazima tuumie.

Safari za nje ni nzuri lakini kama hazina tija kwanini ziwe nyingi kiasi hicho. Lazima kuwe na udhibiti na tujifunge mkanda ili tuweze kupata ustawi. Udhibiti ukianzia ngazi za juu hata sisi wa chini tutafuata nyayo za rais.

Serikali inafanya kazi kwa vitendo, kufika kwa wananchi ili waone kazi tunazozifanya. Siku za hivi karibuni ilikuwa ukienda wizarani unasota hata wiki mbili bila kuhudumiwa lakini kwa sasa watumishi wanaheshimu ofisi na wanawahudumia wananchi.

Huo ndiyo wajibu wa kazi. Ukitizama kwa makini utabaini kuwa Serikali imekuja na mfumo tofauti hivyo lazima watu wabadilike, wabanwe na wadhibitiwe. Tutaumia mwanzoni tu. Hivi sasa ni vigumu kwa mfanyakazi wa Serikali kuingia ofisini saa tatu asubuhi.

SIKU 100 ZA JPM: Magufuli amuacha mbali Lowassa




Kwa ufupiMagufuli alishinda mbio za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, akipata asilimia chache kuliko wagombea wengine kutoka CCM, lakini amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akichukua tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015.




By Goodluck Eliona, Mwananchi geliona@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa mapema mwezi huu yanaonyesha kuwa umaarufu wa Rais John Magufuli umeongezeka kufikia asilimia 74.5, akimuacha mbali mpinzani wake wa karibu kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa.

Magufuli alishinda mbio za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, akipata asilimia chache kuliko wagombea wengine kutoka CCM, lakini amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akichukua tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015.

Katika uchaguzi huo, Dk Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47, akifuatiwa na Lowassa aliyepata kura milioni 6.07, sawa na asilimia 39.97.

Lakini utafiti huo uliofanywa na taasisi ya Ms Infotrak Researc and Consultant na Ms Midas Touche East Africa kwa kuwahoji watu 1,200 wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika kanda sita na mikoa 15, unaonyesha kuwa Magufuli ameongeza umaarufu kwa takriban asilimia 20, huku Lowassa akishuka kwa asilimia 20 pia.

Katika utafiti huo, Lowassa anaonekana kushuka hadi asilimia 20.1.

Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Anna Mghwira aliyepata asilimia 1.1, Hashimu Rungwe (0.4), Fahmi Dovutwa (0.2), Lutalosa Yemba (0.1), Janken Kasambala (0.1) na Machmillan Lyimo aliyepata asilimia 0.0. Asilimia 3.5 ya walioulizwa swali hilo walikataa kujibu.

Vilevile, wananchi walipouliza iwapo Uchaguzi Mkuu ukifanyika leo wangemchagua nani kati ya makada waliojitokea kugombea urais mwaka jana, wengi wamemtaja Magufuli.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba wanawake wengi ndiyo wanamuunga mkono Magufuli ikilinganishwa na wanaume. Asilimia 77.9 ya wanawake wanasema wapo tayari kumchagua tena kuwa Rais iwapo kutakuwa na uchaguzi mpya, wakati wanaume wanaosema hivyo ni asilimia 71.5 pekee.

Kinyume na ilivyo kwa Magufuli, utafiti umebaini kwamba Lowassa anapendwa zaidi na wanaume huku asilimia 22.6 wakisema wapo tayari kumchagua kuwa rais. Ni asilimia 17.4 ndiyo wametoa maoni kama hayo kwa Magufuli.

Kwa upande wa kanda; Kanda ya Zanzibar ndiyo inayoongoza kwa ‘kumkubali’ Magufuli ikiwa na asilimia 91.6, ikifuatiwa na Kanda ya Kati yenye asilimia 81.6, Kanda ya Kaskazini (77%), Kanda ya Pwani (72.7) na Kanda ya Ziwa asilimia 67.6.

Alipoulizwa kuhusu matokeo ya utafiti huo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbuso alisema kuongezeka kwa umaarufu wa Rais Magufuli kunatokana na utendaji wake kugusa kero za wanyonge.

Alisema Watanzania wengi hata wale waliokuwa wakiunga mkono vyama vya upinzani, wameanza kukubaliana na Magufuli kutokana na namna alivyoweza kufanya mambo makubwa na yenye umuhimu kwa Taifa ndani ya muda mfupi.

“Hakuna Rais aliyefanya mambo makubwa namna hii ndani ya siku 100 ndiyo maana wanyonge wameonekana kumkubali kwa sababu amegusa na kuonyesha wazi nia ya kumaliza changamoto zao,” alisema.

“Hata ikitokea uchaguzi ukafanyika sasa nina uhakika Magufuli atashinda kwa sababu wananchi wamebaini wazi kuwa anachokizungumza ndicho anachomaanisha. Si siasa kama ambavyo imezoeleka kwa wanasiasa wengine.”

Maoni yake yanalingana na ya naibu katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Hezron Kaaya aliyesema kasi aliyoanza nayo inaridhisha kiasi cha kuwatia moyo wafanyakazi kuwa huenda kero na changamoto zao zinaelekea kutatuliwa.

“Tucta tulishapigia kelele muda mrefu mambo mengi ambayo Magufuli anayatumbua kwa sasa, mfano suala la ukwepaji kodi na wizi bandarini. Tulishikilia kidete tukiamini kwamba ni mianya ya kulikosesha taifa mapato,” alisema Kaaya.

Kaaya alisisitiza kuwa Magufuli akiendelea na kasi hiyo ni wazi kuwa taifa litasonga mbele na kupata maendeleo ndani ya kipindi kifupi.

Kauli hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wa Tanzania Labour Party na mbunge wa zamani wa Vunjo, Augustine Mrema aliyesema kuwa Watanzania walifanya uchaguzi sahihi kumuweka Magufuli madarakani.

Alisema katika kipindi cha siku 100 kiongozi huyo amefanya miujiza ambayo hakuna Mtanzania ambaye alifikiria kuwa ingeweza kufanyika.

“Kwa kazi na makubwa aliyofanya namvulia kofia. Anaonekana wazi ana nia ya kutuondoa kwenye umaskini na dalili tumeshaziona tusubiri makubwa zaidi,” alisema Mrema.

Maoni ya wadau yameandikwa na Elizabeth Edward,Mwananchi eedward@mwananchi.co.tz

Kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa Acacia North Mara kutathminiwa kwa siku 30


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Nyakungulu wilayani Tarime ambaye alikuwa akiwasilisha kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara wakati Profesa Muhongo alipofanya ziara ya kikazi wilayani Tarime.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika kikao na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Mkuu wa wilaya Tarime na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (wa pili kushoto) kilicholenga kutatua kero wanazokumbana nazo wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia NorthMara pamoja na Mgodi husika. Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga. 
Wa kwanza kulia Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi, Mhandisi Juma Sementa, Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Leseni,John Nayopa.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (kushoto) wakijadiliana jambo mara baada ya kumaliza kikao kilicholenga kutatua kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia NorthMara pamoja na Mgodi husika.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia) akitembelea maeneo yanayolalamikiwa na wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia NorthMara wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani Tarime. Kulia kwa Waziri ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, na kulia kwa Mbunge ni Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga.


Na Teresia Mhagama, Tarime

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameipa siku 30 Kamati aliyoiunda ya kutathmini kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara ambapo Kamati hiyo inatakiwa kutoa ripoti tarehe 23 Machi 2016.


Kamati hiyo itakuwa na makundi mawili yatakayofanya kazi sambamba kwa kuzunguka katika vitongoji tofauti vinavyozunguka mgodi kuanzia tarehe 22 Februari, 2016.
Timu hiyo itaundwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Sehemu ya Leseni, Mazingira, Ukaguzi wa Migodi na Idara ya Sheria. 


“Wataalam wengine watakaounda Kamati hii ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Watathmini kutoka Wizara ya Ardhi, Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira ( NEMC) na Wizara ya Maji na Umwagiliaji,” alisema Profesa Muhongo.


Aliongeza kuwa Wajumbe wengine ni Wenyeviti wa Vitongoji vitakavyozungukiwa na Kamati, Wawakilishi wa Mbunge wa Tarime Vijijini, 

Mgodi wa Acacia North Mara na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Alisema kuwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Tarime na Vyombo vya Usalama wilayani humo havitashiriki katika Kamati husika kwani baadhi ya tuhuma za wananchi zimeelekezwa katika Ofisi hizo.


Kila upande unaohusika na zoezi hilo umetakiwa kuwasilisha majina ya wajumbe wa Kamati kwa Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, siku ya Jumanne tarehe 16 Februari, 2016.
Alieleza kuwa Mwenyekiti na Makamu wa Kamati hiyo watatoka Wizara ya Nishati na Madini na kwamba kamati itafanya kazi katika siku zilizopangwa na si vinginevyo na mwenendo wa Kazi wa Kamati husika utakuwa ukifuatiliwa katika kila wiki.

Baada ya zoezi la upangaji wa Kamati hiyo kukamilika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, alimshukuru Waziri wa Nishati na Madini na serikali kwa ujumla kwa kulipa uzito jambo hilo ambalo halijatafutiwa ufumbuzi kwa miaka kadhaa na kuitakia kamati kila la heri katika utendaji kazi ili kila mtu apate haki yake anayostahili.


Naye Meneja Uendelezaji, Mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara, Abel Yiga kwa niaba ya Mgodi huo amemshukuru Profesa Sospeter Muhongo kwa kufika wilayani Tarime ili kutatua changamoto kati ya Mgodi na wananchi kwani wamekuwa wakiwasilisha changamoto zao katika ngazi mbalimbali za uamuzi lakini utatuzi bado haujapatikana. 


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga pia ametoa pongezi kwa Profesa Muhongo kwa kutoa muongozo utakaopelekea kupata suluhisho la kero zinazowapata wananchi wanaozunguka mgodi pamoja na kero ambazo mgodi unazipata katika 

utekelezaji wa majukumu yake.

Alitoa wito kwa wananchi wilayani Tarime kuwa na imani na Kamati hiyo na kila upande ukubaliane na taarifa itakayotolewa na Kamati husika.


Baadhi ya kero zitakazofanyiwa kazi na kamati hiyo ni pamoja na suala la fidia kwa wananchi waliopisha Mgodi, utegeshaji wa nyumba ndani ya eneo la Mgodi, athari za mitetemo inayotokana na upasuaji wa miamba, ajira kwa watanzania ndani ya mgodi, utoaji wa huduma katika mgodi na masuala mengine yatakayojitokeza wakati zoezi la tathmini litakapoanza.

DKT. KIGWANGALLA ASEMA WATAENDELEA KUMSAIDIA RAIS KUTUMBUA MAJIPU

Written By CCMdijitali on Friday, February 12, 2016 | February 12, 2016

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla,(kulia) akiwa kati,ka ibada maalum ya maadhimisho ya 24 ya kuwaombea wagonjwa duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo mkoani humo, katika wilaya hiyo.Kulia niMkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludovick Mwananzila na Kwanza mbele Naibu Askofu wa Jimbo Kuu la Kanisa la Katoliki la Tabora .
 Baadhi ya wananchi wakiwa katika tukio hilo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla (aliyekaa) akiwa katika ibada maalum ya kuombea wagonjwa duniani iliyofanyika leo katika Hospitali ya Ndala,Nzega Mkoani Tabora. Wengine kulia ni Rudrovic Mwananzila na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Jacqueline Liana.

Dk. Kigwangalla akitoa zawadi kwa mmoja wa akina mama waliokuwa kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali ya Ndala, iliyopo Kata ya Ndala, Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora.

 (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Nzega.)



 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link