TARURA RUVUMA YAIDHINISHIWA SHILINGI BILIONI 38.3 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Songea, Ruvuma Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Ruvuma kwa mwaka wa fedha 2024/2025 umeidhinishiwa Shilingi bili...
Latest Post
March 31, 2015
BALOZI WA CHINA NCHINI AKABIDHI MADARASA JIJINI ARUSHA
Written By CCMdijitali on Tuesday, March 31, 2015 | March 31, 2015
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA,WAKIPOKELEWA NA UMATI WA WANAFUNZI MARA ALIPOWASILI KATIKA SHULE YA MSINGI YA MURRIET.
MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE AKITETA JAMBO NA KATIBU TAWALA WAKE NDG DANIEL MACHUNDA .
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA, WAKIZINDUA RASMI MADARASA HAYO.
MENEJA MKUU WA KAMPUNI YA JINGXI GEO -ENGINEERING (GROUP) CORPORATION YA NCHINA CHINA, AKIELEZEA JINSI WALIVYOFIKA NCHINI NA MIRADI WALIYOFANYA JIJINI AARUSHA , KAMPUNU AMBAYO NDIYO ILIYOJENGA MADARASA HAYO.
KATIBU TAWALA OFISI MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDG DANIEL MACHUNDA.AKIONGEA NA WANANCHI ,KATIKA SHULE YA MSINGI YA MURRIET.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing NA KATIBU TAWALA OFISI MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDG DANIEL MACHUNDA.
MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA,AKITAMBULISHA VIONGOZI ALIOFUATANA NAO PAMOJA NA KUMKARIBISHA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing ,MUWAKILISHI WA MAMBO YA UCHUMI NA BIASHARA NCHINI WA JAMHURI YA WATU WA CHINA NDG Lin Zhi Young NA MENEJA MKUU WA KAMPUNI YA JINGXI GEO -ENGINEERING (GROUP) CORPORATION YA NCHINI CHINA, ILIYOJENGA MADARASA HAYO.
BAADHI YA VIONGOZI MEZA KUU
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIONGEA NA UMATI WA WANANCHI WALIOJITOKEZA KATIKA SHEREHE FUPI ZA KUKABIDHI MADARASA MAWILI YA SHULE YA MSINGI YA MURRIET.

BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIUPUNGIA UMATI WA WANANCHI WALIOJITOKEZA KATIKA SHEREHE FUPI ZA KUKABIDHI MADARASA MAWILI YA SHULE YA MSINGI YA MURRIET.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA AKIWA NA KATIBU WA SIASA NA UENEZI CCM WILAYA YA ARUSHA NDG JASPER KISHUMBUA MARA BAADA YA KUPATA MLO WA MCHANA JIJINI ARUSHA .
,NAIBU MEYA WA JIJI LA ARUSHA KWA NIABA YA MSTAHIKI MEYA WA JIJI MHESHIMIWA PROSPER MSOFE,AKITOA NENO LA KUSHUKURU KATIKA HAFLA FUPI YA KUKABIDHI MADARASA MAWILI YA SHULE YA MSINGI YA MURRIET.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA, WAKISHANGILIA MARA BAADA YA KUGAWA ZAWADI ZA MIFUKO NA MIPIRA YA MGUU KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA MURRIET.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA, WAKIGAWA ZAWADI ZA MIFUKO NA MIPIRA YA MGUU KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA MURRIET.

BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA WAKIWA NA DIWANI WA KATA YA SOKON I MHESHIMIWA MICHAEL KIVUYO WAKIGAWA ZAWADI ZA MIFUKO NA MIPIRA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA MURRIET.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA,NAIBU MEYA WA JIJI LA ARUSHA KWA NIABA YA MSTAHIKI MEYA WA JIJI MHESHIMIWA PROSPER MSOFE,WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAALIMU WA SHULE YA MSINGI YA MURRIET.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA,NAIBU MEYA WA JIJI LA ARUSHA KWA NIABA YA MSTAHIKI MEYA WA JIJI MHESHIMIWA PROSPER MSOFE, MUWAKILISHI WA MAMBO YA UCHUMI NA BIASHARA NCHINI KUTOKA JAMHURI YA WATU WA CHINA NDG Lin Zhi yOUNG NA MENEJA MKUU WA KAMPUNI YA JINGXI GEO -ENGINEERING (GROUP) CORPORATION YA NCHINA CHINA, ILIYOJENGA MADARASA HAYO.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA,KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAZEE WA MILA NA VIONGOZI WA KATA YA SOKON I , AKIWEMO KATIBU WA SIASA NA UENEZI WA CCM WILAYA YA ARUSHA NDG JASPER KISHUMBUA , KATIKA SHEREHE FUPI YA KUKABIDHI MADARASA YA SHULE YA MSINGI YA MURRIET.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA,WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BAADHI YA WAZAZI WALIOHUDHURIA KATIKA SHEREHE FUPI YA KUKABIDHI MADARASA.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA, WAKIKAGUA MOJAWAPO YA MADARASA YA SHULE YA MSINGI YA MURRIET YALIKABIDHIWA , MARA BAADA YA SHEREHE FUPI YA KUKABIDHI MADARASA HAYO MAWILI.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKISHIRIKI KUCHEZA NGOMA YA ASILI YA KABILA LA KIMASAI.
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIONDOKA KUELEKEA UWANJA WA KIMATAIFA WA KILIMANJAROBALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, MHESHIMIWA Lv YouQing AKIWA NA MWENYEJI WAKE MKUU WA WILAYA YA ARUSHA NDUGU CHRISTOPHER KANGOYE ALIYEMPOKEA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA, WAKIZINDUA RASMI MADARASA HAYO.

Labels:
ARUSHA
March 12, 2015
MWAKILISHI WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI ZANZIBAR AISHAURI SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Written By CCMdijitali on Thursday, March 12, 2015 | March 12, 2015
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani hapa Zanzibar Dr. Andermichael Ghirmay akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibnar Balozi Seif hapo Baraza la Wawakilishi Mbqweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Saleh Mohammed Jidawi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani { WHO } hapa Zanzibar Dr. Andemicheal Ghirmay ofisini kwake jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani hapa Zanzibar Dr. Andermichael Ghirmay akimuelezea Balozi Seif Mikakati ya WHO iliyoweka katika kuisaidia Zanzibar.
Picha na –OPMR –ZNZ.
Press Release:-
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani Hapa Zanzibar Dr. Andemichael Ghirmay ameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujiweka tayari kukabiliana na miripuko ya maradhi yoyote yanayoweza kutokea visiwani ili kulinda ustawi wa Wananchi na wageni wanaoingia Nchini.
Alisema Zanzibar imekuwa kituo kikubwa kinachopokea watu wengi kutoka nchi mbali mbali Duniani kufuatia kuimarika kwa Sekta ya Utalii kiasi kwamba tahadhari ya huduma za afya kwa wananchi pamoja na wageni wanaoingia nchini ni vyema ikazingatiwa kwa umakini.
Dr. Andemichael Ghirmay alitoa ushauri huo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi huko Ofisini kwa Balozi iliyopo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema juhudi za pamoja kati ya Serikali, watendaji wa Sekta ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi na mashirika ya maendeleo ya Kitaifa na Kimataifa lazima zichukuliwe katika kudhibiti maradhi hasa yale ya miripuko ambayo mengi kati yao huchipuka kutokana na maingiliano ya wasafari za Kimataifa.
Mwakilishi huyo wa Shirika la Afya Duniani hapa Zanzibar Dr Andemichael ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya kwa utayari wake ilipojiandaa kukabiliana na maradhi ya Ebola endapo yangetokea nchini ambayo yaliwahi kuenea Magharibi mwa Nchi za Bara la Afrika katika miezi ya hivi karibuni.
Dr. Andemichael Ghirmay alisema katika kuimarisha huduma za Afya kwa Nchi wanachama Shirika hilo la Afya Duniani litaendelea kutoa msukumo zaidi wa kitaalamu kwa Zanzibar katika mapambano dhidi ya maradhi mbali mbali yanayowasumbua wananchi.
Alieleza kwamba Shirika hilo katika mipango yake sita iliyojipangia ya kutoa elimu, Ushauri na kusaidia Utafiti kwa Nchi wanachama Zanzibar imo katika mchakato wa kuendelea kuungwa mkono na shirika hilo katika kupambana na maradhi mbali mbali sambamba na kusaidia Utafiti katika maradhi hayo.
Mwakilishi huyo wa shirika la Afya Duniani Dr. Andemichael Ghirmay amepongeza ushirikiano anaoendelea kuushuhudia uliopo kati ya Wananchi, Wafanyabiashara pamoja na Viongozi wao wa Majimbo katika ujenzi wa Vituo vya Afya katika Majimbo yao.
“ Mimi kama Mtaalamu wa Sekta ya Afya nimefarajika sana kuona mshikamano uliopo kati ya Wabunge na Wawakilishi kwa kushirikiana na wafanyabiashara pamoja na wananchi wao katika ujenzi wa vituo vya huduma za Afya katika Majimbo yao“. Alisema Dr. Andemichael Ghirmay.
Akitoa shukrani zake kwa mchango mkubwa unaotolewa na Shirika la Afya Duniani { WHO } hapa Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika sekta ya Afya kufuatia kuungwa mkono na Shirika hilo.
Balozi Seif alisema zipo huduma nyingi za afya zinazoendelea kutolewa katika Hospitali mbali mbali kubwa sambamba na vituo vya Afya vya Wilaya na Vijiji ambazo msingi wake mkubwa unatokana na shirika hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliliomba Shirika la Afya Duniani kupitia Mwakilishi wake huyo hapa Zanzibar liendelee kuisaidia Zanzibar kiuwezeshaji, vifaa pamoja na Taaluma ili ifikie lengo lake la kutoa huduma za afya kwa wananchi waliowengi Mjini na Vijijini.
Alisema Sera ya Serikali kupitia Wizara ya Afya ni kuona wananchi wote ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba wanaendelea kupata huduma za afya si zaidi ya umbali wa kilomita tano kwenye makazi wanayoishi.
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Saleh Mohamed Jidawi alisema kwamba Uongozi wa Shirika la Afya Duniani umekuwa karibu mno na Wizara ya Afya Zanzibar.
Dr. Jidawi alisema Shirika hilo ni kiungo kikubwa kinachoendelea kuisaidia Zanzibar katika mapambano yake dhidi ya udhibiti wa maambukizi ya vizuri wa Ukimwi, chanjo kwa akina Mama Wajawazito na Watoto pamoja na kukabiliana na maradhi ya kichocho.
“ Wizara ya Afya tumefanikiwa vyema katika kupambana na udhibiti wa maradhi ya Kichocho na maambukizi ya kuenea kwa virusi vya ukimwi hapa nchini kutokana na kuungwa mkono na wenzetu wa WHO “. Alisema Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya Zanzibar.
Alisema mchango wa Utafiti na utaalamu wa Shirika shirika hilo katika mapambano dhidi ya maradhi ya Malaria umeiwezesha Zanzibar kudhitibi maradhi ya Malaria chini ya Asilimia 0.6%.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
12/3/2015.
Labels:
KITAIFA
March 10, 2015
Watoto 18 waliofungiwa Moshi wadai kubebeshwa matofali mgongoni
Written By CCMdijitali on Tuesday, March 10, 2015 | March 10, 2015
Baadhi ya watoto 18 waliokuwa wakihifadhiwa kwenye nyumba iliyopo Kata ya Pasua, mkoani Kilimanjaro. Picha na Dionis Nyato
Na Rehema Matowo na Fina Lyimo,Mwananchi
Kwa ufupi
Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela imeeleza kuwa hayo yalibainika katika mahojiano baina ya watoto na askari wa dawati la jinsia.
Moshi. Jeshi la Polisi wilayani hapa, limedai kuwa watoto waliokutwa ndani ya nyumba katika eneo la Pasua, Manispaa ya Moshi siyo wakazi wa Kilimanjaro na walikuwa wakiishi kwenye mateso makubwa.
Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela imeeleza kuwa hayo yalibainika katika mahojiano baina ya watoto na askari wa dawati la jinsia.
Alisema watoto hao wanatoka mikoa mbalimbali ikiwamo Tanga, Mara, Kagera, Mbeya na Dodoma.
Kamanda Kamwela alisema pia wamegundua kuwa watoto walikuwa wakiishi kwenye mazingira magumu ikiwamo kulala chini katika chumba kidogo.
Alisema polisi linawashikilia watu wawili (mume na mke) ambao wanatuhumiwa kuwahifadhi watoto hao.
Kamanda huyo alisema watoto hao wana umri wa kwenda shule, lakini walikuwa hawasomi.
Alisema polisi wanachunguza aina ya masomo ya dini waliyokuwa wakifundishwa.
“Lazima tuchunguze uhalali wa masomo ya dini waliyokuwa wakisoma ili tujue kama kweli watoto hawa walipelekwa na wazazi wao au la, kwa kuwa watoto hao walipaswa kuwa shuleni” alisema Kamanda Kamwela.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga alisema watoto hao walikuwa wakiishi kwenye mazingira magumu, huku wakipewa adhabu kali ikiwamo kubeba matofali mgongoni pindi wanapokosea.
“Maelezo ya watoto yanaonyesha walikuwa wakiteswa, adhabu hizi kwa watoto ni kubwa, bado tunawachunguza ili tujue kila kitu na walichukuliwaje huko majumbani kwao,” alisema Makunga.
Alisema kwa wazazi watakaowatambua watoto wao, wanapaswa kwenda na uthibitisho ikiwamo cheti cha kuzaliwa au uthibitisho mwingine utakaoonyesha ni mzazi halisi.
Makunga alisema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa, watuhumiwa hao wana kituo kingine kinachohifadhi watoto.
Alisema kwa sasa hawezi kueleza zaidi hadi polisi watakapomaliza upelelezi wao.
Majirani wanena
Aisha Mohamed na Marsela Minja ambao ni majirani wa watuhumiwa walidai kuwa awali nyumba hiyo ilikuwa na mmiliki mwingine, lakini alijinyonga miaka michache baada ya kuuza eneo hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walidai kuwa mmiliki wa kwanza wa nyumba hiyo alikuwa na ujirani mwema na wakazi wa eneo hilo.
Marsela alisema mmiliki wa sasa tabia yake ni tofauti kwa kuwa anawazuia watu kuchota maji na pia kajenga ukuta mrefu kuzingira nyumba hiyo.
Alisema tangu mmiliki huyo ahamie katika nyumba hiyo miaka mitatu iliyopita, hawakuwa na mazoea na jirani yeyote.
Wananchi hao walidai wiki mbili zilizopita mmiliki huyo alifunga ndoa na wao walishuhudia magari mawili ya kifahari yakiingia kwenye geti na baada ya muda yaliondoka.
“Sisi hatuwafahamu sana kwa sababu hutoka na magari wakiwa wamejifunika hadi usoni, hivyo siyo rahisi kuwafahamu...hatujawahi kuwaona watoto wakienda shule wala dukani,” alisema Marsela.
“Ukipita kwa huku nyuma ndiyo utawasikia wakifundishwa masuala ya dini, lakini wakikosea wanapewa adhabu ya kupanda ukuta , lakini hata ukiwasemesha hawajibu zaidi ya kulia,” alisema Aisha.
Mtaalamu azungumza
Mtaalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Chris Mauki alisema kitendo cha watoto hao kukosa uhuru na mazingira ya kuchangamana na watu wa aina mbalimbali kitawaathiri kisaikolojia.
“Wasiposaidiwa kuendana na mazingira hata wakitoka watakuwa na matatizo, kwa sababu walishakosa baadhi ya hatua muhimu katika makuzi yao, kwa sababu mtoto anapopelekwa shule siyo kwa ajili ya kusoma tu bali kuchangamana,” alisema Dk Mauki.
Chanzo
Sakata la watoto hao liligundulika Machi 7 mwaka huu, saa 12.00 jioni baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa mzazi mmoja mkazi wa Kata Pasua aliyedai watoto wake watatu kutoroshwa.
Mzazi huyo aliwaambia polisi kuwa alipata taarifa kuwa watoto wake wamehifadhiwa katika nyumba hiyo, ndipo askari walipofuatilia na kuwakuta watoto 18.
Juzi saa tatu asubuhi, mamia ya wakazi wa Moshi walifika katika nyumba hiyo, huku wakiimba kutaka kuwaona watoto wao baada ya kuwakuta askari kanzu wakilinda eneo hilo.
Askari hao walizidiwa nguvu na kukiita Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwenda kuwatawanya wananchi ili watoto hao watolewe na kupelekwa kituoni kwa mahojiano.
Baadaye Mkuu wa Kituo cha Polisi Moshi, Deusdedit Kasindo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Norvatus Makunga walifika katika nyumba hiyo na kuzungumza na mmiliki.
Mmiliki huyo alidai watoto hao walipelekwa na wazazi wao kwa lengo la kufundishwa dini. Polisi waliwachukua watoto hao na kuwapeleka kituoni kwa mahojiano.
Labels:
KITAIFA
March 10, 2015
ZIARA YA KINANA YATUA JIMBO LA KIBAJAJ JIMBO LA MTERA.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji uliojengwa kwa msaada wa shirika la Oxyfarm katika kijiji cha Mvumi mission,jimbo la Mtera wilayani Chamwino.Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji akishihudia tukio hilo adhimu. Kinana amelishukuru shirika hilo kwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa kisima hicho kwa muda mfupi
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji uliojengwa kwa msaada wa shirika la Oxyfarm katika kijiji cha Mvumi mission,jimbo la Mtera wilayani Chamwino.Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde ( Kibajaji )
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wakazi wa kijiji cha Mvumi mission,jimbo la Mtera mapema leo mara baada ya kuzindua mradi wa maji uliojengwa kwa msaada wa shirika la Oxyfarm
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Mtera,katika kijiji cha Mvumi Mission ,wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi wengine wa wilaya na mkoa wa Dodoma wakikagua mradi wa ujenzi wa madarasa shule ya Msingi Suli yaliyogharamiwa na shirika la Neigbourhood kutoka Korea ya Kusini,kwa kiasi cha shilingi bilioni tatu,ujenzi huo pia unahusisha vyumba vya walimu pamoja zahanati ya kijiji cha Suli.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji akimwagilia maji mti alioupanda katika shule ya sekondari Fufu,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Kinana alikagua bweni la wasichana na kupanda miti katika suala zima la kulinda mazingira.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutanno huo wa hadhara.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde (Kibajaji ) akiwahutubia wananchi wa Fufu,jimbo la Mtera wilayani Chamwino .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa Fufu,jimbo la Mtera wilayani Chamwino .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia baadhi ya wakazi wa kijiji cha Manzase kata ya Fufu,,jimbo la Mtera wiyani Chamwino mkoani Dodoma,leo jioni katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Manzase.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Manzase Kata ya Fufu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia mapema leo jioni katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Manzase.