CPA MAKALLA: CCM ITAWALETEA WAGOMBEA WASIO NA MAKANDOKANDO
Na Richard Mwaikenda, Mwanza Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akiwaahidi wananchi kwa...
AWAMU YA TATU KAMPENI YA CHANJO YA POLIO KUANZA TAREHE 1-4 SEPTEMBA 2022
Written By CCMdijitali on Tuesday, August 30, 2022 | August 30, 2022
MAFUNZO KWA VIJANA SEPTEMBA 2 NA 3 MAKUMBUSHO YA TAIFA (POSTA) DAR ES SALAAM YATAKAYOENDESHWA NA TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE NA UNA-TANZANIA
Written By CCMdijitali on Monday, August 29, 2022 | August 29, 2022
Serikali ya awamu ya nane inayakaribisha mashirika ya bima kuja Zanzibar kuwekeza - Dr Mwinyi.
28/08/022 JAPAN YATOA DOLA BILIONI 30 KUSAIDIA NCHI ZA AFRIKA
Written By CCMdijitali on Sunday, August 28, 2022 | August 28, 2022
Serikali ya Japan imetangaza kutoa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 30 katika kipindi cha miaka mitatu (2022 – 2025) kwa Nchi za Bara la Afrika ili kuziwezesha kutekeleza programu na miradi ya maendeleo itakayoleta mageuzi ya kiuchumi barani humo.
Kiasi hicho cha fedha kimetangazwa kutolewa na Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Fumio Kishida wakati wa mkutano wa 8 wa Wakuu wa Nchi na Serikali kati ya Japan na Nchi za Afrika kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (Tokyo International Conference on African Development – TICAD 8 Summit) uliofanyika mjini Tunis nchini Tunisia terehe 27 - 28 Agosti 2022.
Kupitia Mkutano huo Mhe. Fumio amezihakijishia nchi za Afrika kuwa Serikali ya Japan itaendelea kushirikiana nao kwa karibu kwa kuchangia maendeleo kupitia programu na miradi mbalimbali.
Mhe. Fumio pia amezihakikishia nchi hizo kuwa Serikali ya Japan itaendelea kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na changamoto zinazokwamisha juhudi za Afrika za kujikwamua kiuchumi. Amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kama vile milipuko ya magonjwa, mabadiliko ya Tabia Nchi na upungufu wa chakula.
Akizungumzia kuhusu kiasi cha fedha kilichotelewa, Mhe. Fumio amesema kupitia mpango wa TICAD sekta binafsi za pande zote mbili (Japan na Afrika) zimeendelea kustawi, hivyo Serikari yake itaendelea kuhamasisha Kampuni za Japan kuendelea kuwekeza Afrika katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda, kilimo, Afya, nishati ya umeme na teknolojia.
Kuhusu mgawanyo wa fedha hizo Mhe. Fumio amesema kuwa pamoja na TICAD kufanikiwa katika maeneo mengi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya na elimu, Japan katika kipindi cha miaka miatatu ijayo (2022/23-24/25) itaangazia pia maeneo muhimu yanayogusa maisha ya watu ya kila siku.
Ameyataja maeneo hayo kuwa ni mapinduzi ya kijani, Mabadiliko ya tabia nchi, kukuza uwekezaji, kuendeleza hali ya maisha ya Waafrika, ambapo kiasi cha Dola za Marekani bilioni 5 zitatolewa kufanikisha mpango huo.
Maeneo mengine ni Afya na maendeleo ya rasilimali watu. Katika sekta ya afya Japan itachangia kiasi Dola za Marekani bilioni 1.08 kuiwezesha Afrika kukabiliana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria. Mhe. Fumio aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Serikali yake inatarajia kuwajengea uwezo zaidi ya watu 300,000 kutoka bara la Afrika katika sekta ya viwanda, afya, elimu, sheria na utawala.
Akizungumza katika mkutano huo Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameeleza umuhimu wa Bara la Afrika kuendelea kushikirikiana na Jumuiya ya Kimataifa katika kutatua changamoto zinazolikabili bara hilo katika ukuzaji wa uchumi.
Mhe. Mjaliwa akiongelea madhara yaliyo sababishwa na athari za UVIKO 19 na Vita vya Urisi na Ukraine ikiwemo mfumuko wa bei wa bidhaa, ametoa rai kwa Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika katika jitihada zake za kujigemea kiuchumi, ili kuhakikisha zinaendelea kutoa huduma bora na muhimu kwa wananchi wake na kuwawezesha wananchi katika shughuli zao zinazowagusa moja kwa moja kama vile kuendeleza kilimo na utalii.
Naye Rais wa Tunisia Mhe. Kais Saied ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa TICAD 8, akifungua mkutano huo amesema Japan ni mbia wa kweli wa maendeleo ya Afrika kwa kuwa wakati wote imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Afrika katika kutafuta suluhu ya changamoto zinazolikabili bara hilo, na kuchangia katika kundeleza sekta mhimu kama vile elimu, kilimo, teknolojia, ujenzi wa miundombinu ya uchukuzi na usafirishaji, mabadiliko ya tabia nchi sambamba na kutoa mikopo yenye riba ndogo na masharti nafuu.
Mkutano wa 8 wa TICAD umehudhuriwa na zaidi ya washiriki 3000 kutoka nchi 55 za Bara la Afrika na Mashirika mbalimbali ya Kimataifa, umebeba kauli mbiu isemayo “Kukuza Maendeleo Endelevu ya Afrika kwa ajili ya Waafrika” (“Promoting Africa-led, African-owned sustainable development”)
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) akifuatilia Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8) unaoendelea mjini Tunis, nchini Tunisia. Waliopo kando yake niNaibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Mbarouk (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba (kushoto)
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Rais wa Tunisia Mhe. Kais Saied alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Palais de Congres mjini Tunis nchini Tunisia.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Rais wa Tunisia Mhe. Kais Saied wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa TICAD8.
Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika, Ujumbe wa Serikali ya Japan, watendaji na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya kimataifa walioshiriki mkutano wa TICAD8 wakiwa katika picha ya pamoja.
MKUTANO WA NANE WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA TICAD (TICAD 8) WAANZA KUFANYIKA MJINI TUNIS, TUNISIA
Written By CCMdijitali on Saturday, August 27, 2022 | August 27, 2022
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) akifuatilia Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8) unaoendelea mjini Tunis, nchini Tunisia.