Comoro kushirikiana na Tanzania katika sekta za kimkakati asema Rais Azali Anena
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazumgumzo na Rai...
Latest Post
January 24, 2024
BALOZI FATMA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA JUMUIYA MBALIMBALI NCHINI OMANu
Written By CCMdijitali on Wednesday, January 24, 2024 | January 24, 2024
Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Mohammed amekutana kwa nyakati tofauti na Viongozi wa Jumuiya ya Maimamu wa Kitanzania waliopo Oman pamoja na Uongozi wa Jumuiya ya Al-Wadood Charitable Group ya Oman waliomtembelea ofisini kwake jijini Muscat hivi karibuni.
Pamoja na mambo mengine, Jumuiya hizo zilimtembelea Balozi Fatma kwa lengo la kujitambulisha kwake rasmi baada ya kuteuliwa kuiwakilisha Tanzania nchini humo pamoja na kuwasilisha maoni ya Jumuiya hiyo kuhusu ajira zao nchini Oman na changamoto wanazokabiliana nazo
Katika taarifa yao, maimamu wa kitanzania wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sheikh Zubeir Nkwavi waliwasilisha maoni kuhusu ajira zao nchini humo na changamoto wanazokabiliana nazo. Walieleza kuwa, Jumuiya hiyo ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2020 imefanikiwa kusajili wanachama 88 wakiwemo maimamu na walimu katika misikiti mbalimbali nchini Oman.
Pia Jumuiya hiyo imefanikiwa kuendesha shughuli mbalimbali ikiwemo kusaidiana wakati wa misiba, kutoa michango wakati wa maafa, kuendesha mafunzo ya dini na kuanzisha mfuko wa akiba nchini humo.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo, Umoja huo unakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa Bima za Afya kwa wanachama wake, kukosa mlezi wa Jumuiya na kukosa udhamini wa masomo na kumuomba Mhe. Balozi Fatma kuwasaidia kutafuta suluhu ya changamoto hizo kwa kushirikiana na Serikali ya Oman.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Fatma aliwashukuru Viongozi hao na kuwapongeza kwa kufanikiwa kupata ajira nchini Oman na hivyo kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira nchini Tanzania.
Kuhusu mikataba ya ajira alisema ipo haja ya kuwepo makubaliano baina ya Taasisi za Kidini za nchi mbili hizi ili kuwa kuweka mustakbali mzuri wa ajira zao.
Kadhalika Balozi Fatma aliwaahidi viongozi hao kuwa, atazungumza na Mamlaka husika za nchini Oman katika kutafuta suluhisho kwa changamoto zinazowakabili pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuwa na mikataba rasmi ya ajira ili kupata haki zinazostahili ikiwemo bima ya Afya, likizo na stahiki nyingine.
Kwa upande wao, Jumuiya ya Al-Wadood Charitable Group ambayo inajihusisha na utoaji wa misaada kwa watu wenye mahitaji, wajane, wasiojiweza na yatima hapa nchini ikiongozwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sheikh Abdulqadir Al-Jahdhamy waliwasilisha taarifa na mipango yao ya mwaka kuhusu utoaji wa misaada hiyo.
Naye Mhe. Balozi Fatma ameishukuru Jumuiya hiyo kwa misaada yao nchini na kuwaomba kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kusaidia miradi mbalimbali ya kupunguza umasikini na ukali wa maisha kwa Watanzania. Pia amewaomba kusaidia kujenga mabweni katika mikoa yenye uhitaji hususan kwa wanafunzi wa kike.
Jumuiya ya Al-Wadood Charitable Group pia imekuwa ikishiriki katika ujenzi wa misikiti, kutoa vifaa tiba, kuchimba visima na kugharamia masomo kwa Watanzania katika mikoa mbalimbali nchini
January 22, 2024
Written By CCMdijitali on Monday, January 22, 2024 | January 22, 2024
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo ameongoza mapokezi ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku Tatu.
Akiwa nchini, Mhe. Guozhong anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Pia, atatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na eneo la makaburi ya Wataalam wa kichina waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA pamoja na Makumbusho ya Taifa.
January 21, 2024
DIPLOMASIA YA TANZANIA YAZIDI KUNG’ARA KIMATAIFA
Written By CCMdijitali on Sunday, January 21, 2024 | January 21, 2024
Diplomasia ya Tanzania imezidi kung’ara kimataifa kufuatia viongozi wakuu kutoka mataifa mbalimbali kufanya ziara nchini kwa lengo la kuimarisha na kudumisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na mataifa hayo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), alipozungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Akielezea ziara za viongozi hao nchini Waziri Makamba amesema tarehe 22 Januari 2024 atawasili Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China na Mjumbe wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China, Mhe. Liu Guozhong ambaye atakuwa nchini tarehe 22 - 24 Januari , 2024.
“Mara baada ya kuwasili nchini, kiongozi huyo anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa (Mb.), pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Dotto Biteko (Mb.),” alisema Waziri Makamba.
Amesema Kiongozi mwingine mkuu anayetarajiwa kuwasili nchini ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mheshimiwa Salvador Valdes Mesa, ambaye atafanya ziara ya kikazi ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 23 – 25 Januari, 2024. Pamoja na mambo mengine, ziara hiyo imelenga kuendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Cuba.
Waziri Makamba, amesema Mheshimiwa Mesa anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Husein Ali Mwinyi na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Akson.
Pamoja na mambo mengine, Mheshimiwa Mesa atamtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere na kushiriki mkutano wa wanachama wa urafiki kati ya Tanzania na Cuba, Watanzania waliosoma Cuba na Taasisi ya Pan African Movement na kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa za viuadudu ya Biolarvicide cha Kibaha, Pwani.
Kiongozi mwingine anayetarajiwa kuwasili nchini ni Rais wa Jamhuri ya Poland, Mheshimiwa Andrzej Duda atakayewasili nchini kwa ziara ya kikazi tarahe 8 – 9 Februari 2024.
Akiwa nchini, Mheshimiwa Duda atakutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo lengo la ziara hiyo ni kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Poland.
Amesema Tanzania na Poland zinashirikiana katika miradi ya maendeleo ya miundombinu, uhifadhi wa wanyama pori, elimu, maji, usimamizi wa mazingira, utalii, biashara, uwekezaji na ushirikiano wa mabunge.
Aidha, ziara hiyo inatarajia kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano katika maeneo ya ulinzi na usalama, nishati na gesi, madini, usafiri, ulinzi wa mitandao, utamaduni na uchumi wa buluu.
Mbali na viongozi wakuu wa mataifa tajwa kufanya ziara nchini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya Kitaifa nchini Indonesia kuanzia tarehe 24 – 26 Januari 2024, kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Mheshimiwa Joko Widodo. Ziara hiyo ya Kitaifa inafuatia ziara ya Kitaifa ya Rais Joko Widodo aliyoifanya nchini Tanzania mwezi Agosti 2023.
“Ziara hii inalenga kukukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Indonesia kupitia sekta mbalimbali za biashara na uwekezaji, kilimo, nishati, madini, mifugo, uvuvi, uchumi wa buluu, elimu, utalii na ulinzi,” aliongeza Waziri Makamba.
Kadhalika, Waziri Makamba amewaeleza waandishi kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia pia kufanya Ziara ya Kitaifa Vatican tarehe 11 – 12 Februari, 2024 kufuatia mwaliko wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Papa Francis.
Waziri Makamba ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Vatican, atakuwa na mazungumzo na Baba Mtakatifu Papa Francis pamoja na Katibu wa Vatican, Mhe. Pietro Parolin. Uhusiano kati ya Tanzania na Vatican ulianza miaka ya 1960 wakati ambapo Vatican ilianzisha Ubalozi wake hapa nchini.
Tangu wakati huo Vatican kupitia Kanisa Katoliki imekuwa mstari wa mbele katika kujishughulisha na masuala ya kiroho, amani, elimu na program za afya. Kwenye ziara hiyo Mhe. Rais Samia ataongozana na wawakilishi watano wa waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania kutoka kwenye jumuiya mbalimbali za kanisa hilo.
Amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya Kitaifa nchini Norway, tarehe 13-14 Februari 2024 kufuatia mwaliko kutoka kwa Mfalme Herald wa Norway na Malkia Sonja. Ameongeza kuwa ziara hiyo inafanyika ikiwa ni miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway.
“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa na mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Norway akiwemo Mfalme Herald. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Rais pia atashiriki Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Norway pamoja na Kongamano la Nishati la Oslo,” alisema Waziri Makamba
Tanzania na Norway zinashirikiana kupitia sekta mbalimbali zikiwemo biashara, uwekezaji, nishati kama mafuta na gesi, elimu na masuala ya kodi na utawala bora.
Kuanzia mwaka 2010, Serikali ya Norway imekua ikishirikiana na Tanzania kwenye programu mbalimbali za maendeleo zilizo gharimu takribani TZS. 300 bilioni. Programu hizo zimesaidia na kuimarisha sekta muhimu za kiuchumi ikiwa ni pamoja na Sekta ya Nishati; Sekta ya Elimu; Sekta ya Mafuta na Gesi; Mpango wa Usimamizi wa Fedha za Umma; programu za Mabadiliko ya Tabianchi; na programu za Usimamizi wa Misitu.
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anaandika historia kupitia ziara hii nchini humo kwani mara ya mwisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea nchi hiyo kwa Ziara ya Kitaifa ilikua mwaka 1976.
January 19, 2024
RC KINDAMBA AWAASA TANGA KUSHIRIKI UWEKEZAJI WA NDANI
Written By CCMdijitali on Friday, January 19, 2024 | January 19, 2024
Na Zuberi Mgaya , MUM-TANGA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Waziri Kindamba amewataka wakazi wa mkoa huo kutumia fursa za ki-uchumi kushiriki katika uwekezaji wa ndani ili kukuza uchumi wao na taifa.
Mhe Kindamba ameyasema hayo leo, Januari 19, 2024 ofisini kwake alipozungumza na ujumbe kutoka Kituo cha Uwekezaji (TIC) unaohamasisha mabadiliko ya fikra kuhusu uwekezaji na wazawa kushiriki uwekezaji wa ndani.
Mhe Kindamba amesema hali ya uchumi wa mkoa na wakazi wa Tanga inazidi kuboreka, akitolea mfano ukuaji wa pato la taifa (GDP) mkoani humo kutoka Shilingi Shilingi Trilioni 5.7 kwa mwaka 2018 kufikia Trilioni 7.9 kwa mwaka 2022 na kipato cha mtu mmoja mmoja kutoka Shilingi milioni 2.4 (2018) kufikia Shilingi milioni 3 kwa mwaka 2022.
Mhe Kindamba amesema, Serikali imejidhatiti kuimarisha, kuongeza na kuendeleza viwanda na biashara, na kutoa kipaumbele kwa biashara ya mazao ya mkonge, korosho na mihogo.
Amesema jitihada hizo zimefanikisha kupatikana wawekezaji kwenye viwanda vya kuchakata muhogo wilayani Handeni kitakachogharimu Dola za Marekani milioni 50 na kile cha samaki ambacho mchakato wa uwekezaji wake unaendelea.
Miongoni mwa sekta alizozitaja kuwa sehemu ya fursa za uwekezaji ni utalii hususani kwenye fukwe za bahari, ukanda wa milima ya Lushoto na misitu ya asili iliyopo wilayani Muheza.
Mhe Kindamba amezielekeza mamlaka za udhibiti mkoani humo, zijiepushe na hulka ya kufunga biashara za wawekezaji wenye kasoro, badala yake wafanye mazungumzo na kutoa elimu ya namna bora ya kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza sekta hiyo.
Awali Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema, amesema mkoa huo umeweka mikakati ya kuwawezesha wananchi wake kuzing’amua na kuzitumia fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani humo.
Naye Meneja wa Uhamasishaji na Uwekezaji wa Ndani wa TIC, Ndugu Felix John, amewataka wanachi kubadili fikra na mitazamo yao kutoka katika kuamini kwamba ni uwekezaji unawahusu raia wa kigeni peke yao.
Mwandishi wa Habari hii ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Mawasiliano kwa Umma katika Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM).
Mwisho.
Labels:
MIKOANI
January 19, 2024
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA MABORESHO YA KANUNI ZA MADALALI
Na Munir Shemweta, WANMM
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo imeipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi, Malipo na Nidhamu kwa Madalali wa Baraza na Wasambaza Nyaraka za mwaka 2023 katika Sheria ya Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Sura ya 216.
Akizungumza wakati wa wasilisho la Taarifa ya marekebisho hayo tarehe 19 Januari 2024 jijini Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ramadhani Suleiman Ramadhani amesema, wizara hiyo imezingatia mapendekezo ya Kamati katika kufanya maboresho na kamati yake haina budi kuipongeza Wizara ya Ardhi kwa kazi nzuri.
‘’Wizara imezingatia mapendekezo ya Kamati hivyo niwapongeze kwa kazi nzuri ya kufanya marekebisho yaliyozingatia maoni ya Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo ‘’ alisema Mhe. Ramadhani.
Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu mkoani Mtwara Yahya Mhata amesema, maboresho yaliyofanyika yanonesha jinsi gani Wizara ya Ardhi ilivyo jipanga na kutoa pongeza kwa wizara hasa Katibu Mkuu wa wizara hiyo aliyemueleza kuwa ndiye Mtendaji Mkuu.
‘’Wizara iko ‘smart’ napenda niishukuru na kuipa pongezi kwa maboresho ya Kanuni za Madalali na zaidi nimpongeze Mtendaji Mkuu wa wizara’’ alisema Yahya.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Method Msokele aliwaeleza wajumbe wa kamati kuwa, Kanuni zilizofanyiwa marekebisho zitajulikana kama Kanuni za Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi, Malipo na Nidhamu kwa Madalali wa Baraza na Wasambaza Nyaraka za mwaka 2023.
‘’Kanuni hizi zitasomwa pamoja na Kanuni za Uteuzi, Malipo na Nidhamu kwa Madalali wa Baraza na Wasambaza Nyaraka za mwaka 2023 ambapo hapa zitarejewa kama Kanuni Kuu’’. Alisema Msokele.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda aliishukuru Kamati kwa ushauri wake wakati wa kufanya marekebisho ya kanuni za Madalali na kuahidi wizara kusimama katika mhimili wakati wa kutekeleza majukumu yake.
‘’Niwashukuru sana wajumbe wa Kamati hii, mmetupa ushirikiano wakati wote wa maboresho ya Kanuni za Madalali na niwaahidi Wizara yangu itasimama katika mhimili wakati wote wa kutekeleza majukumu yake’’ alisema Mhe. Pinda
January 19, 2024
SERIKALI YAENDELEA KUSHUSHA GHARAMA ZA ULETAJI MAFUTA KULETA AHUENI KWA WANANCHI
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, juhudi zinazofanywa na Wizara ya Nishati, Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) zimepelekea gharama za uletaji wa mafuta nchini (premium) kuendelea kushuka na hivyo kuchangia katika unafuu wa gharama za mafuta ikiwemo ya dizeli na petroli.
Amesema hayo tarehe 19 Januari 2024 jijini Dodoma wakati Wizara ya Nishati ilipowasilisha taarifa kuhusu mwenendo wa biashara ya mafuta nchini kwa kipindi cha mwezi Septemba hadi Disemba 2023, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. Kikao ambacho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, Katibu Mkuu, Mhandisi, Felchesmi Mramba, baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Watendaji wa Wizara ya Nishati.
“ Wizara ya Nishati, EWURA na PBPA, kwa kweli wamefanya kazi kubwa mno ya kushusha gharama za uagizaji mafuta kutoka nje ya nchi, hapo awali gharama hizi zilikuwa zikiongezeka kila mwezi lakini wamesimamia vizuri suala hili na gharama hizi zimeanza kushuka na hivi karibuni mlisikia Waziri wa Kenya akisema bei za mafuta nchini humo zipo juu na za Tanzania zipo chini sababu ya premium, na wengine pia walio nje wanatoa ushuhuda kwamba walau sisi gharama zetu zina unafuu.” Amesema Dkt. Biteko
Dkt. Biteko ameeleza kuwa PBPA ambayo inasimamia uagizaji wa mafuta kwa pamoja, ina umuhimu mkubwa nchini kwani ndiyo inayopelekea nchi kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta yanayotosheleza mahitaji ya nchi na yenye viwango vya ubora unaohitajika, Serikali kufahamu kiwango cha mafuta kinachoingia nchini, kupanga ukusanyaji wa mapato kwa kutumia takwimu sahihi na kupanga bei elekezi ya mafuta.
Amesema kuwa, Serikali itaendelea kuisimamia kwa ukamilifu Taasisi hiyo ili iendelee kufanya kazi kwa ufanisi kwani tayari imekuwa ni mfano wa kuigwa kwa nchi zinazotuzunguka na kuwataka watendaji wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa maadili na bila kumuonea mtu yeyote.
January 19, 2024
SERIKALI KUIMARISHA HALI YA LISHE KWA VIJANA BALEHE NCHINI
Na. WAF - Dar es Salaam
Serikali kupitia Wizara ya Afya imedhamiria kuimarisha na kuwekeza kwenye Afya za vijana balehe hasa katika hali za Lishe, Afya ya Akili pamoja na elimu ili kujikinga na magongwa yakuambukiza ikiwemo VVU/UKIMWI ikiwa ni kipaumbele cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo wakati akifungua Kongamano la Tano la Kisayansi kuhusu masuala ya vijana balehe (15-19) lenye lengo la kujadili namna ya kubadili Tafiti za Afya kwa Vijana wa rika balehe na Lishe kuwa za vitendo.
“Vijana hawa balehe wana changamoto nyingi ikiwemo ya masuala ya lishe, Afya ya Uzazi, Afya ya Akili, lakini pia vijana wengi wanakabiliwa na upungufu wa damu kwa asilimia 38-40, uzito mkubwa, uzito mdogo pamoja na ukosefu wa vitamini.” Amesema Waziri Ummy
Waziri Ummy Mwalimu amesema, Kangamano hilo limekutanisha wanasayansi mbalimbali kutoka Afrika, Marekani na Ulaya ili kujadili kwa pamoja ni vipi Tanzania itaweza kutumia Tafiti za Kisayansi katika kufanya maamuzi ya kisera pamoja na masuala ya Afya ya Uzazi.
“Katika Kongamano hili pia tumeona kuzinduliwa kwa utafiti ambao umeonesha kwamba, endapo wakina mama wajawazito watapewa madini ya ‘calcium’ tunaweza tukapunguza kifafa cha mimba kinachochangia vifo vya kina mama wajawazito.” Amesema Waziri Ummy
Aidha Waziri Ummy amesema, utafiti huo umeonesha badala ya kuwapa dozi ya Mg 1,500 kwa siku hata wakipewa dozi ya Mg 500 kwa siku inaweza kusaidia matokeo mazuri kwa kinamama wajawazito kutopata kifafa cha mimba ambapo pia itapumguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga.
Mwisho, Waziri Ummy ametoa wito kwa Watanzania ikiwemo vijana kuzingatia mtindo bora wa maisha ikiwemo ulaji kwa kupunguza mafuta, chumvi na Sukari pamoja na kufanya mazoezi ili kuepuka Magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwa vijana nao wanakabiliwa na magonjwa hayo.
Labels:
KITAIFA
January 18, 2024
WAZIRI BASHUNGWA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOA DODOMA
Written By CCMdijitali on Thursday, January 18, 2024 | January 18, 2024
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amewasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa, Rosemary Senyamule, kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo, leo tarehe 19 Januari 2024
Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara katika wilaya za Mkoa wa Dodoma na miradi mingine inayotekelezwa katika Sekta ya Ujenzi mkoani humo.
Miradi atakayokagua na kutembelea ni pamoja ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato na Majengo, ujenzi wa Barabara ya Mzunguko (Outer Ring Road), ujenzi wa Barabara ya Ntyuka-Mvumi- Kikombo, barabara ya Hogoro – Machenje - Kongwa, ujenzi wa barabara ya Kongwa - Mpwapwa sehemu ya Mpwapwa - Mwanakianga na Mpwapwa - Ving’awe pamoja na Ukaguzi wa eneo la Mtanana, Kongwa.
Labels:
MIKOANI
January 18, 2024
MRADI LTIP KUONGEZA USALAMA WA MILKI ZA ARDHI NCHINI
Na Eleuteri Mangi, WANMM
Tanzania itekeleza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) ambao chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa lengo la kupanga, kupima, kumilikisha na kutoa hati miliki za ardhi kuongeza usalama wa milki za ardhi nchini.
Akihitimisha Kikao Kazi cha Asasi za Kiraia ambacho kimefanyika kwa siku mbili hivi karibuni jijini Dodoma, Mratibu Msaidizi wa Mradi huo Dkt. Upendo Matotola amesema mradi huo unatumika kama mfano kwa ulimwengu na kuwasisitiza washiriki hao kuijenga nchi kwa pamoja ili kujenga taswira njema ya Tanzania kimataifa.
“Tunajua kabisa tunapopanga, tunapopima, na kumilikisha vipande vya ardhi, Uchumi wetu unaongezeka kwa sababu ardhi iliyopangwa na kupimwa inaongezeka thamani na inapoongezeka thamani, shughuli za kiuchumi nazo zinaongezeka” amesema Dkt. Upendo.
Katika kutekeleza mradi huo, Dkt. Upendo amesema kuwa Serikali inatoa kipaumbele kwa sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kijamii katika kutekeleza masuala ya ardhi na kusisitiza kuwa Serikali itabaki na jukumu la kujenga uwezo, mazingira wezeshi, utawala na usimamizi wa ardhi nchini.
Akizungumza na washiriki hao Dkt. Upendo amesema, “Sisi wote ni wazalendo, tunapenda mradi huu uendelee kutekelezwa vizuri kama ulivyokusudiwa kuleta matokeo chanya yenye tija kwa taifa letu ili kutoa fursa kwa miradi mingine kutekelezwa hapa nchini, tunaposema vibaya kuhusiana na mradi, tunajichafua wenyewe.”
Aidha, amewasistiza washiriki hao kuwa ufanisi wa mradi huo unategemea ushiriki wao mzuri kwa kutoa utaalamu wao kwa kufanyakazi kwa uaminifu na uadilifu kwa uzalendo kwa kutanguliza maslahi ya taifa lao.
Kwa upande wao mshiriki wa kikao kazi hicho Bw. Innocent Jaji kutoka Maswa na Bi. Mariam Mohamed kutoka Mvomero wamesema kuwa Asasi za Kiraia zinajukumu la kushirikiana na serikali katika kutelekeza mradi huo kwa kutoa elimu ya masuala ya ardhi makundi maalumu wakiwemo wanawake, wazee, watoto na watu wenye ulemavu wapate haki zao katika umiliki wa ardhi.
Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) ambao unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia umeanza kutekelezwa mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika 2027 ambapo jukumu lake ni kurasimisha ardhi kwa wananchi katika maeneo ya mijini na vijijini.
Labels:
KITAIFA
January 18, 2024
SERIKALI IMEAMUA KWA DHATI KUWEKEZA KWENYE MIRADI YA NISHATI
📌 Mkandarasi Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) alipwa kwa asilimia 88.7
📌 Mradi wafikia asilimia 95.8
Dodoma
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, ameeleza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeamua kwa dhati kuwekeza katika miradi ya nishati nchini huku lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa upatikanaji umeme nchini unakuwa mkubwa kuliko mahitaji ya nchi.
Amesema hayo tarehe 18 Januari 2024 jijini Dodoma wakati Wizara ya Nishati ilipowasilisha taarifa kuhusu hali ya uzalishaji na usambazaji umeme nchini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Kikao ambacho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, Katibu Mkuu, Mhandisi, Felchesmi Mramba, baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Watendaji wa Wizara ya Nishati.
“Moja ya vipaumbele vikubwa vya Serikali ni Sekta hii ya Nishati na ndio maana fedha zimekuwa zikitolewa za kutekeleza miradi mbalimbali ya Nishati ikiwemo mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ambao gharama yake ni shilingi Trilioni 6.5 na mpaka sasa Serikali imeshamlipa mkandarasi shilingi Trilioni 5.7 ambayo ni sawa na asilimia 88.7.” Amesema Dkt.Biteko
Kuhusu usimamizi wa mradi wa JNHPP amesema kuwa, Serikali iko makini katika usimamizi wake na kwamba kuna mamlaka mbalimbali zinazosimamia mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kwa ufanisi akitolea mfano Timu Maalum ya Wataalam iliyoundwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kusimamia mradi huo ambayo inaongozwa na Profesa Idris Kikula.
Kuhusu hali ya miundombinu ya umeme nchini, Dkt. Biteko amesema kuwa, itaendelea kufanyiwa matengenezo ili iweze kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme kwa ukamilifu wake, huku juhudi za kujenga miundombinu mingine mipya ikiendelea.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga alieleza Kamati kuwa, mradi wa umeme wa JNHPP kwa sasa umefikia asilimia 95.8 na kwamba mtambo namba Tisa utakaozalisha megawati 235 umeshakamilika na mtambo Namba 8 na namba 7 iko mbioni kukamilika.
@tanesco_official_page @wizara_ya_nishati_tanzania
Labels:
KITAIFA
January 18, 2024
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Januari 18, 2023 amewasilisha Maazimio ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile.
WAZIRI UMMY AWASILISHA MAAZIMIO YA KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII, WIZARA YA AFYA
Miongoni mwa hoja alizowasilisha ni pamoja na Uwekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba kufanywa na Bohari ya Dawa, Uingizwaji nchini wa bidhaa bandia za chakula, dawa na Vipodozi pamoja na Dawa za Asili.
Waziri Ummy Mwalimu ameambatana na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu, Naibu Katibu Mkuu Dkt. GraceWaziri Ummy Awasilisha Maazimio Ya Kamati Ya Bunge Ya Huduma Na Maendeleo Ya Jamii, Wizara Ya Afya
Labels:
KITAIFA
January 18, 2024
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 18, 2024 amewasili nchini Uganda ambapo atamuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) ulioanza tarehe 15 - 20 Januari, 2024 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+China utakaofanyika tarehe 21-22 Januari, 2024, Kampala - Uganda.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI NCHINI UGANDA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 18, 2024 amewasili nchini Uganda ambapo atamuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) ulioanza tarehe 15 - 20 Januari, 2024 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+China utakaofanyika tarehe 21-22 Januari, 2024, Kampala - Uganda.
Labels:
KIMATAIFA
January 18, 2024
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza wakati wa Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Mifumo ya Usalama wa Chakula uliyoshirikisha Muungano wa wadau wa usalama wa chakula duniani.
Mkutano huo umefanyika Kando ya Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika Davos nchini Uswisi.
MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO AZUNGUMZA- DAVOS USWISI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza wakati wa Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Mifumo ya Usalama wa Chakula uliyoshirikisha Muungano wa wadau wa usalama wa chakula duniani.
Mkutano huo umefanyika Kando ya Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika Davos nchini Uswisi.
Labels:
KIMATAIFA