MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...

Latest Post

Balozi Seif apokea msaada wa vifaa kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Written By CCMdijitali on Wednesday, April 20, 2016 | April 20, 2016

 Balozi Seif akipokea msaada wa vifaa kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzaia Dkt. Rufaro Chatora Ofgisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 Hali halisi ya Bara bara iliyotoka Amani chini kuelekea kwa wazee welezo ambayo imebomoka vibaya kutokana na kasi ya maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka maeneo ya welezo juu.
 Baadhi ya Nyumba mbali mbali zilizojaa maji kufuatia mafuriko ya kuamkia Jumapili iliyopita katika Mtaa wa Kara kana Chumbuni Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif akiwa na Uongozi wa Wilaya ya Magharibi zote mbili “A” na “ B” akikagua Bara bara itokayo Kwerekwe kuelekea Fuoni Makaburini ambayo imefunikwa na maji kufuatia mvua za juzi usiku.
 Bara bara ya Kwerekwe kuelekea Fuoni ikionekana kama shamba lililotelekezwa kutokana na kufukiwa na majani ya mayungi yungi yaliyokokotwa na maji na kupiga kambi kati kati ya bara bara hiyo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwapungia Mkono Wananchi wa maeneo mbali mbali waliohifadhiwa katika Skuli ya Sekondari ya mwanakwerekwe baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko juzi usiku.


Hali halisi ya eneo la Ziwa Maboga liliopo Kijiji cha Kisauni ambalo maji yake yamefurika hadi katika makaazi ya wananchi wa eneo hilo waliojenga pembezoni mwa ziwa hilo.
Picha na – OMPR – ZNZ.

 Press Release:-
 

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzaia Dkt. Rufaro Chatora alisema uwezo wa jamii kwa kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na maradhi ya kipindu pindu unawezekana na ni rahisi iwapo kila Mwananchi atachukua juhudi katika kudumisha mazingira yaliyomzunguuka katika eneo lake.


Alisema tahadhari ya athari yoyote inapaswa kuchukuliwa mapema katika kukinga badala ya kuendeleza tabia iliyozoeleka ya kusubiri kutibu inayochukuwa wakati mrefu na gharama kubwa.


Mwakilishi huyo wa Shirika la Afya Duniani { WHO } Dr. Rufaro Chatora alieleza hayo wakati akikabidhi msaada wa dawa na vifaa mbali mbali vilivyotolewa na Shirika hilo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Vuga Mjini Zanzibar.


Msaada huo wa Dawa na Vifaa uliogharimu jumla ya shilingi Milioni 39,463,313/- umelenga kuhudumia wagonjwa walioathirika na maradhi ya kipindu pindu katika kambi mbali mbali hapa Zanzibar yaliyoanza tokea mwezi septemba kwamba 2015.


Dr. Rufaro alisema juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa baina ya Viongozi wa Serikali kwa kushirikiana na Wananchi katika kuweka mikakati itakayosaidia mapambano ya kukabiliana na maradhi ya Kipindupindu yanayoonekana kuwa tishio kwa maisha ya jamii.


Aliahidi kwamba Shirika la Afya Duniani kwa kushirkiana na lile la kuhudumia Watoto { Unicef } litaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali pamoja na Wananchi wa Zanzibar kwenye mapambano yao ya kukabiliana na maradhi mbali mbali yanayowasumbua Wananchi.


Akipokea msaada na vifaa hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya itaendelea kutoa elimu kwa umma jinsi ya namna ya wananchi wanavyoweza kujiepusha na maradhi tofauti ikiwemo Kipindu pindu.


Balozi Seif alisema maradhi ya kuambukiza kama Kipindu pindu ni hatari na chanzo chake yanayotokana na mazingira mabovu ya makaazi pamoja na udhibiti wa vyakula usiozingatia kanuni za afya.


Alisema uwezo wa kudhibiti maradhi ya kipindu pindu upo hapa Nchini kama Zanzibar ilivyofanikiwa katika kudhibiti maradhi ya malaria yaliyopungua kabisa na kufikia hadi asilimia 0.35%.


Balozi Seif aliyapongeza Mashirika ya Kimataifa ya Afya { WHO } na lile la kuhudumia Watoto { UNICEF } kwa juhudi za mashirika hayo katika kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika Sekta ya Afya.


Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliendelea na ziara yake ya kukagua sehemu mbali mbali zilizoathirika miundombinu yake kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita.


Ziara hiyo ilianzia eneo la Karakana ambapo alipata kujionea hali halisi ya athari hiyo ambapo Mkurugenzi wa Kamisheni ya Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad alisema eneo hilo linaweza kupata salama ya athari ya mafuriko baada ya kumalizika kwa mtaro mkubwa unaoendelea kujengwa katika eneo hilo.


Baadaye Balozi Seif aliangalia Bara bara inayotoka Mwanakwerekwe kuelekea Fuoni ambayo kwa saba bado haijaweza kutoa huduma kutokana na kufurika kwa maji katika ziwa liliopo pembezoni mwa Soko la Mwanakwerekwe. 


Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Nd. Ayoub Mohammed Mahmoud alisema Uongozi wa Wilaya hiyo kwa kushirikiana na Taasisi zinazohusika zinajiandaa kuanza usafi baada ya kupunguwa kwa kina cha maji kwenye bara bara hiyo ili kuona athari zitazojitokeza na baadae iendelea kutoa huduma ya usafiri kama kawaida.


Nd. Ayoub hata hiyo alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Wilaya zote mbili za Magharibi “A” na “B” bado hazijawa na miundombinu ya mitaro ya kupitishia maji ya mvua inayoweza kudaidia wakati wa msimu wa masika.


Akikagua mafuriko katika ziwa Maboga liliopo Kisauni baada ya kuwazuru na kuwapa pole waathirika wa mvua hizo waliohifadhiwa katika Skuli ya Mwanakwerekwe “C” Balozi Seif aliuagiza Uongozi wa Shehia ya Kisauni kwa kushirikiana na Wilaya ya Magharibi “B” kumbomolea mtu ye yote atakayejenga katika eneo hilo.


Balozi Seif alitoa agizo hilo kufuatia nyumba nyingi zilizojengwa ndani ya eneo la ziwa Maboga kufunikwa kabisa na maji ya mvua licha ya kwamba eneo hilo linakuwa kavu wakati wa kiangazi.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kamwe haitamvumilia Mtu ye yote atakayekiuka agizo hilo la kujenga eneo hilo la ziwa hata kwa wale wenye tabia ya kujenga usiku na kumaliza pia watabomolewa.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
19/4/2016.

Mwenyekiti wa CCM Mkoani Arusha akutana Wenezi wa Wilaya zote Mkoani.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ,Mkoa wa Arusha Ndg Lekule Laizer (MNEC) akiongea na Makatibu Wenezi na Siasa Wilaya za Arusha Mjini-Ndg Jasper Kishumbua, Longido, Ndg Emmanuel Sirikwa, Arumeru Ndg Johnas Kitolo na Katibu Mwenezi wa Mkoa Arusha Ndg Shaaban Mdoe (kushoto)19/04/2016 katika Ofisi ya Mwenyekiti CCM Mkoa wa Arusha.
 Katibu Mwenezi na Siasa wa Mkoa Arusha Ndg Shaaban Mdoe akiongea na Makatibu Wenezi na Siasa Wilaya za, Longido- Ndg Emmanuel Sirikwa,Ngorongoro- Ndg James P.Moringe,Meru -Ndg Elienea P.Kitomari na  Arumeru Ndg Johnas Kitolo na  (kushoto)19/04/2016 katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.
 Katibu Mwenezi na Siasa wa Mkoa Arusha Ndg Shaaban Mdoe akiongea na Makatibu Wenezi na Siasa Wilaya za, Longido- Ndg Emmanuel Sirikwa,Ngorongoro- Ndg James P.Moringe, Arumeru -Ndg Johnas Kitolo na Arusha Mjini -Ndg Jasper Kishumbua19/04/2016 katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.
 Katibu Mwenezi na Siasa wa Mkoa Arusha Ndg Shaaban Mdoe akiongea na Makatibu Wenezi na Siasa Wilaya za, Longido- Ndg Emmanuel Sirikwa,Ngorongoro- Ndg James P.Moringe, Arumeru -Ndg Johnas Kitolo na Arusha Mjini -Ndg Jasper Kishumbua19/04/2016 katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha
Makatibu Wenezi na Siasa Wilaya za Ngorongoro- Ndg James P.Moringe,Meru -Ndg Elienea P.Kitomari na Monduli - Ndg Grosper Mollel na (kulia)19/04/2016 katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.
 Makatibu Wenezi na Siasa Wilaya za Longido- Ndg Emmanuel Sirikwa na  Ngorongoro- Ndg James P.Moringe, 19/04/2016 katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.
 Katibu Mwenezi na Siasa wa Mkoa Arusha Ndg Shaaban Mdoe katika kikao na Makatibu Wenezi wa Wilaya zote za Mkoa wa Arusha , kilichofanyika 19/04/2016 katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.
 Katibu Mwenezi na Siasa Wilaya ya Longido- Ndg Emmanuel Sirikwa  katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha 19/04/2016.
 Katibu Mwenezi na Siasa Wilaya ya Ngorongoro- Ndg James P.Moringe katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha 19/04/2016.
 Katibu Mwenezi na Siasa Wilaya ya Meru -Ndg Elienea P.Kitomari katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha 19/04/2016.
 Katibu Mwenezi na Siasa Wilaya ya Monduli -Ndg Grosper Mollel katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha 19/04/2016.
 Katibu Mwenezi na Siasa Wilaya ya Arumeru -Ndg Johnas Kitolo, katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha 19/04/2016.
 Katibu Mwenezi na Siasa wa Mkoa Arusha Ndg Shaaban Mdoe akiongea na Makatibu Wenezi na Siasa Wilaya za, Longido- Ndg Emmanuel Sirikwa,Ngorongoro- Ndg James P.Moringe,Meru -Ndg Elienea P.Kitomari na Arumeru Ndg Johnas Kitolo na (kushoto)19/04/2016 katika Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ,Mkoa wa Arusha Ndg Lekule Laizer (MNEC) akiongea na Katibu Mwenezi na Siasa Wilaya za Arusha Mjini-Ndg Jasper Kishumbua na Katibu Mwenezi wa Mkoa Arusha Ndg Shaaban Mdoe (kushoto)19/04/2016 katika Ofisi ya 
Mwenyekiti CCM Mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ,Mkoa wa Arusha Ndg Lekule Laizer (MNEC) akiongea na Makatibu Wenezi na Siasa Wilaya za  Longido, Ndg Emmanuel Sirikwa, Arumeru Ndg Johnas Kitolo,Ngorongoro- Ndg James P.Moringe,Meru -Ndg Elienea P.Kitomari na Katibu Mwenezi wa Mkoa Arusha Ndg Shaaban Mdoe (kushoto)19/04/2016 
katika Ofisi ya Mwenyekiti CCM Mkoa wa Arusha.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua


CCM Wilaya ya Arusha ,yapata ushindi wa kishindo ktk Uchaguzi Serekali Mitaa.

Written By CCMdijitali on Monday, April 18, 2016 | April 18, 2016

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Wakaazi wa Mtaa wa Makao Mapya Kata ya Sinoni, wakishangilia ushindi mara baada ya matokeo kutangazwa.

 Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata ya Sinoni , Bi Hilda Malisa akitangaza matokeo ya Uchaguzi jana katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi ya Sinoni .
Mgombea wa Chadema Ndg Nurusindiko Kivuyo (kulia) akisikiliza matokeo katika chumba cha Uchaguzi jana 17/04/2016 wa  Mtaa wa Makao Mapya Kata ya Sinoni.

 Dolee tuuuuuu.....
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Wilfred Soileli,akiwapongeza Wakazi na  Wanachama wa CCM katika Ofisi ya Kata ya Sinoni,mara baada ya mgombea wa CCM kutangazwa mshindi,jana 17/04/2016
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Martin Munisi,akiongea na baadhi ya Wanachama wa CCM katika Ofisi ya Kata ya Sinoni ,mara baada ya mgombea wa CCM kutangazwa mshindi,jana 17/04/2016.

CHAMA Cha Mapinduzi wilaya ya Arusha Mjini kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa wenyeviti wa serikali ya mtaa kwa kupata viti vitano na CHADEMA vitatu.

Uchaguzi huo ulifanyika (Jana) juzi kutokana na wenyeiti wa mitaa tisa kuhamia katika vyama mbalimbali vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Akizungumza na UHURU ofisini kwake katibu wa CCM wilaya ya Arusha mjini Feruzi Bano alisema ushindi huo unatokana na kasi ya Rais Dk John Magufuli ya utumbuaji majipu ambayo imewakuna wananchi wengi na kuanza kuipenda CCM

Bano alitaja mitaa ambayo CCM imeshinda ni pamoja na mtaa wa Olamuriaki katika kata ya Sombetini na mtaa wa Shangarau kaya ya Moivaro ambapo katika mitaa yote hiyo CCM imepita bila kupingwa baada ya CHADEMA kushindwa kusimamisha wagombea.

Alitaja mitaa mingine ambayo CCM imeshinda ni pamoja na mtaa wa Makao mapya kata ya Sinoni,mtaa wa Bondeni kata ya Kati,mtaa wa Kilimaji kata ya Moshono.

Kwa upande wa wajumbe wa serikali za mitaa alisema CCM ilipata ushindi wa kishindo kwa kupata wajumbe watatu huku CHADEMA ikiambulia mjumbe mmoja.

Kwa mujibu wa Bano CCM ilishindwa kushinda katika mitaa hiyo mitatu kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inayesha jijini hapa juzi hali iliyosababisha wana CCM wenye umri mkubwa kushindwa kwenda kupiga kura .

Aliongeza sababu nyingine kuwa ni karatasi za kupigia kura kutokuwa na muhuri wa Halmashauri ya Jiji pamoja na kutukuwa na vitambulisho vya kuonyesha kama kweli waliopiga kura katika mitaa hiyo walikuwa wakazi husika.

Katika uchaguzi huo kwenye kata ya Daraja mbili mtaa Sanare CCM na CHADEMA wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa serikali ya mtaa walifungana hivyo uchaguzi huo utarudiwa tena baada ya msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi wa Jiji Juma Iddy kutangaza tarehe nyingine ya uchguzi

Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka atua Mkoani Arusha leo.

Written By CCMdijitali on Saturday, April 16, 2016 | April 16, 2016


 Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM Mkoani Arusha, akishuhudiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa ,MNEC Ndg Michael lekule Laizer Mkoani Arusha leo.


 Kushoto - kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha ,MNEC Ndg Michael Lekule Laizer akiwa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoani Arusha ,Ndg Shaaban Mdoe na Mwenyekiti wa CCM Wilayani Arusha Ndg Wilfred Soileli, wakimsubiri Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka ,katika Ofisi za CCM Mkoani Arusha leo.
 Mwenyekiti wa CCM Wilayani Arusha Ndg Wilfred Soileli, akimpokea  Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendekamara baada ya kuwasili katika eneo la  Ofisi za CCM Mkoani Arusha leo,na aliyeshika mwamvuli ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Longido Ndg Papaa Nakuta.
 Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akiteta jambo na baadhi ya viongozi waliofika kumlaki kiongozi huyo leo  katika Ofisi ya CCM Mkoani Arusha.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha ,MNEC Ndg Michael Lekule Laizer kiteta jambo na baadhi ya viongozi waliofika kumlaki, Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka leo katika Ofisi ya CCM Mkoani Arusha.
 Mwenyekiti wa CCM Wilayani Arusha Ndg Wilfred Soileli na katibu wa UWT Mkoani Arusha Bi Fatuma Tsea, wakimsikiliza kwa makini Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka leo katika Ofisi ya CCM Mkoani Arusha.
 Dr Kilumbe S. Ng'lenda (MNEC) Afisa kutoka Makao Makuu ya CCM Taifa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilayani Arusha Ndg Wilfred Soileli na kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Longido Ndg Papaa Nakuta,katika Ofisi za CCM Mkoani Arusha leo.


Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka ,akiondoka katika   Ofisi ya CCM Mkoani Arusha,akishuhudiwa na Mwenyekiti wa CCM Wilayani Arusha Ndg Wilfred Soileli na Makamu wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido  
Bi Esupat Ngulupa.Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg jasper Kishumbua

Uhamiaji wasafishwa Dar na Kilimanjaro

Written By CCMdijitali on Wednesday, February 24, 2016 | February 24, 2016

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga

Na Habari Leo

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ameagiza watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioko katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na Kilimanjaro (KIA), wahamishwe na kupelekwa maeneo mengine nchini, wakiwemo wale wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Katika maagizo ya waziri huyo, amesisitiza kuwa anataka kuwepo na mabadiliko makubwa katika vitengo mbalimbali vya idara ya uhamiaji ili kuboresha huduma na kuimarisha uadilifu katika vitengo hivyo.

Aidha, utafiti uliofanywa hivi karibuni, umeonesha kuwa matatizo ya rushwa katika idara ya uhamiaji, yanashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na asilimia 30, asilimia 20 ni uongozi mbovu na asilimia 20 ni matumizi mabaya ya madaraka.

Kitwanga alitoa maagizo hayo Dar es Salaam jana, alipozungumza katika kikao cha ndani na viongozi wa idara ya uhamiaji na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara.

Pamoja na watumishi hao wa Idara ya Uhamiaji wa viwanja hivyo vya ndege kutakiwa kuhamishwa, wengine walioagizwa na waziri huyo kuhamishwa ni kutoka Kitengo cha Pasipoti, Uhasibu, Hati za Ukaazi na Kitengo cha Upelelezi, vyote vya Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Aidha, ameagiza pia kuwa Wakuu wote wa Vitengo vya Upelelezi vya wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam, Tunduma, Mtukula, Holili na Kasumulo, wahamishiwe maeneo mengine, wakiwemo watumishi wote waliokaa kwa zaidi ya miaka mitatu katika vituo hivyo.

“Hatua hii inayochukuliwa ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa yatakayofanywa katika Idara ya Uhamiaji ili kuboresha huduma zinazotolewa na Idara hii ambayo ni moja ya Idara muhimu za Serikali,” alisisitiza Kitwanga.

Alisema katika kuisafisha idara hiyo, uangalifu mkubwa utachukuliwa ili kuhakikisha kuwa hakuna mtumishi anayeonewa wala kupendelewa, lengo likiwa ni kuvunja mtandao wa wapokea rushwa na wasiowajibika.

Alisema kutokana na utafiti uliofanywa hivi karibuni, umeonesha kuwa matatizo ya rushwa katika Idara ya Uhamiaji yanashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na asilimia 30, asilimia 20 ni uongozi mbovu na asilimia 20 ni matumizi mabaya ya madaraka.

Aidha, alisema asilimia 15 inahusisha vitendea kazi, mifumo hafifu ya kufanya kazi, asilimia 10 huduma mbovu na asilimia tano ukabila na upendeleo.

Aliwataka viongozi na watumishi wote katika idara hiyo kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya kazi na kuepuka vitendo vya kupokea rushwa na kusaidia wahamiaji haramu na wauza dawa za kulevya.

Nape: Maslahi tasnia ya habari kulindwa

Written By CCMdijitali on Monday, February 22, 2016 | February 22, 2016

 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye


Imeandikwa na Halima Mlacha -Habari Leo

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha maslahi ya wanahabari na tasnia ya habari nchini vinalindwa na kupewa uhuru wa kutosha lakini kwa kutanguliza maslahi ya taifa.

Pia amebainisha kuwa Muswada wa Sheria ya Kusimamia Vyombo vya Habari uko katika hatua za mwisho baada ya kushirikisha na kujumuisha mapendekezo ya wadau wa habari na kusisitiza kuwa endapo sheria hiyo itapitishwa itakuwa ni sheria bora itakayoijenga tasnia hiyo na itadumu kwa muda mrefu.

Amevitaka vyombo vya habari nchini kutumia fursa iliyopo kuibua matatizo yaliyopo kwenye jamii na hivyo Serikali kuvitumia kama sehemu ya kupatia taarifa na kuzifanyia kazi kwa maslahi ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.

Nape aliyasema hayo juzi usiku katika kipindi cha Siku 100 za Rais John Magufuli madarakani katika sekta ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kilichorushwa na televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Alisema tangu Rais John Magufuli aingie madarakani amekuwa akiishi yale anayoyazungumza na hivyo ndivyo Serikali yake itakavyokuwa kwani hata yeye tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Habari aliahidi kuijenga na kuilinda tasnia hiyo jambo ambalo ameapa kulifanikisha.

“Nawahakikishia wanahabari kwamba wako salama chini ya Serikali ya Awamu ya Tano na uongozi wake,” alisisitiza.

Alisema alipoanza kazi ya uwaziri, alikutana na makundi mbalimbali ya wadau wa habari wakiwemo wanahabari na wahariri wa habari lengo likiwa ni kukusanya na kuangalia mambo ambayo hayako sawa katika tasnia hiyo na kupokea maoni yao yaingizwe kwenye Muswada wa Sheria ya Habari.

Alisema kupitia maoni aliyoyakusanya kutoka katika makundi hayo ya wadau wa habari, mapendekezo yao yamefanyiwa kazi kwa kutumika kwenye muswada wa sheria hiyo ya habari ambayo iko katika hatua za mwisho na inatarajiwa kuwasilishwa bungeni.

Alisema sheria hiyo ya habari kwa kuzingatia mapendekezo hayo, itakuwa ni sheria nzuri, bora na itakayoijenga tasnia ya habari, na ni sheria itakayochukua muda mrefu kufanyiwa marekebisho kutokana na ubora wake.

Akizungumzia uhuru wa vyombo vya habari, alisema uhuru huo ulianza kupanuliwa tangu Serikali zilizopita ikiwemo ya Awamu ya Nne na umekuwa ukitekelezwa kwa kuzingatia sheria zilizopo za habari na maslahi ya taifa.

Alisema ndani ya Serikali ya Awamu ya Nne, uhuru wa vyombo vya habari nchini ulipanuliwa kwa wigo mkubwa ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika.

“Najua kumekuwa na malalamiko mengi hasa ndani ya siku hizi 100 za Mheshimiwa Rais, pale nilipolifungia gazeti la Mawio. Nilichukua hatua ile baada ya kupitia kwa umakini mwenendo mzima wa gazeti lile na kwa kweli lilikuwa na makosa na ndio maana hata baada ya hatua kuchukuliwa, Mawio wenyewe hawapigi kelele wanaopiga kelele ni wengine,” alisisitiza.

Alisema gazeti lile mwenendo wake wa uandishi ulikuwa hauendani na maadili ya uandishi wa habari na kukiuka sheria ya vyombo vya habari kupitia taarifa zake mojawapo ikiwemo ya kumtangaza kinyume cha Sheria ya Uchaguzi mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kuwa ndiye Rais mteule wa Zanzibar.

Aidha, alisema pia alifuatilia mwenendo wa namna gazeti hilo linavyojibu barua za kulionya na kuonekana kama linajibizana na Msajili wa Magazeti na hata lilipoandika habari ya kumtangaza Maalim Seif kuwa Rais wa Zanzibar, majibu yake ya kujieleza yalikuwa ni ya kejeli na kiburi.

“Walipoandikiwa barua ya kujieleza kuhusu habari hiyo yenye uchochezi, walijibu eti wanaishangaa Serikali kwa nini inahoji wao kumtangaza mshindi Zanzibar, na kusisitiza kuwa walipaswa kupongezwa. Huu ni uhaini kutangaza Rais bila kuwa na mamlaka. Huu ni uchochezi na ndio maana tulichukua hatua,” alisema Nape.

Alisema pamoja na kwamba sheria iliyotumika kulifungua gazeti hilo inalalamikiwa akiwemo yeye mwenyewe kutoridhika nayo, ni vyema vyombo vya habari vitakatambua kuwa sheria hiyo bado ipo hadi pale utakapopitishwa Muswada wa Sheria ya Habari.

Alivitaka vyombo vya habari kuitekeleza kwa vitendo changamoto aliyoitoa Rais Magufuli wakati akizungumza na wazee hivi karibuni, kwa kuandika habari za utafiti zinazoibua masuala nyeti yanayohitaji kufanyiwa kazi na Serikali kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

“Hata mheshimiwa Rais Magufuli alisema tutumie vyombo vya habari kupata taarifa muhimu za kufanyia kazi. Ili Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dk Magufuli ifanikiwe, ni lazima itoe uhuru wa kutosha kwa vyombo vya habari kufanya kazi zake,” alisema Nape.

Katika hatua nyingine, Nape amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linakuwa chombo cha kuaminika na linafanya kazi zake kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali hiyo.

Aidha, amesema imepanga kuanza kulipa madeni yote ambayo shirika hilo na Shirika la Magazeti ya Serikali, Tanzania Standard Newspapers (TSN) wachapishaji wa magazeti ya Daily News, SpotiLeo na HabariLeo, inaidai Serikali ili mashirika hayo yajiendeshe kwa ufanisi.

Nape alisema katika kufanikisha azma hiyo tayari akiwa Waziri mwenye dhamana ameunda Bodi mpya ya TBC na Rais Magufuli ameshamteua Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Herbert Mrango baada ya Bodi iliyopita kumaliza muda wake kwa mujibu wa sheria.

“Tunataka TBC kuwa chombo cha umma kinachoaminika nchini kuanzia kwenye vipindi na taarifa za habari na matukio. Kila Mtanzania anaona kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Ni kasi kubwa hata taasisi zilizo chini ya wizara zetu ikiwemo TBC, tunataka ziende na kasi hiyo,” alisisitiza Nape.

Pamoja na hayo, Waziri Nape alisema Serikali inatambua kuwa shirika hilo linakabiliwa na tatizo la uchakavu wa mitambo na kukabiliwa na madeni makubwa ambayo taasisi za Serikali zinadaiwa na kuahidi kulifanyia kazi.

“Tayari Rais Magufuli ameagiza madeni yote ambayo TBC inadai taasisi za Serikali yaanze kulipwa pamoja na madeni ambayo Shirika la Magazeti la Serikali (TSN) linazidai taasisi hizo. Mashirika haya yanaidai Serikali fedha nyingi inabidi yalipwe ili yafanye kazi zake kwa ufanisi,” alisisitiza.

Jecha: Tunamtambua Maalim Seif mgombea


Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha


Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Zanzibar na Habari Leo

LICHA ya Chama cha Wananchi (CUF) na vyama vingine sita vya siasa kuandika barua ya kueleza kutoshiriki Uchaguzi Mkuu wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha amesema ofisi yake bado inawatambua wagombea wa vyama hivyo.

“Mgombea Urais wa CUF na wagombea wake wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani, na vyama vingine sita waliandika barua kwa ZEC wakisema hawatashiriki uchaguzi huo. Kwa bahati mbaya, wagombea wote na vyama vyao vya siasa vinavyodai kususia, wameshindwa kufuata taratibu.

“Inaelezwa wazi katika Kifungu cha 31 na 37A na Sura ya 46 na 50 ya Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar, kuhusu taratibu za uteuzi wa wagombea na jinsi gani wagombea wanaweza kujitoa katika uchaguzi. Hakuna hata mgombea mmoja aliyefuata sheria hiyo,” alisema Jecha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.

Jecha alisema kulingana na kanuni, ni jukumu la chama cha siasa kuandika kwa ZEC kuhusu kuondoa udhamini wake kwa mgombea. Alisema hata CUF ambayo mgombea wake ni Maalim Seif Shariff Hamad, imeshindwa kufuata kanuni hizo.

“Ni muhimu sana kuelewa na kufuata sheria za uchaguzi. Tumekuwa tukiwasiliana na vyama vyote 14 vya siasa, sambamba na kusambaza vifaa vya uchaguzi kwa wilaya zote kumi na moja kabla ya kuvitawanya baadaye kwenye vituo 1,580 vya kupigia kura,” alisema Jecha.

Alisema wagombea wote 14 wa urais, watu wanaowania Uwakilishi kutoka katika majimbo 54 na wagombea 111 katika ngazi ya Udiwani, bado wanaendelea kutambulika kama wagombea halali kwa uchaguzi wa mwezi ujao.

Jecha amekiri kupokea barua kutoka CUF na vyama vingine sita wakisema hawatashiriki uchaguzi huo, wakati vyama vingine vinane kikiwamo CCM, ACT, ADC CCK AFP, SAU, TLP na ADA-TADEA vimethibitisha kushiriki.

“Tunakamilisha taratibu ili kuwapatia wagombea wote wa urais ulinzi kwa saa 24 hadi wakati matokeo ya uchaguzi yatakapokuwa yametangazwa,” alisema Jecha na kuongeza kuwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litawekwa katika sehemu mbalimbali ili wapiga kura waone vituo vyao vya kupigia kura.

Alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya marudio ya uchaguzi huo yanaendelea vizuri na tayari uteuzi na kuajiri maofisa wa uchaguzi na wafanyakazi wengine umefanyika na kufuatiwa na mafunzo kuhusu jinsi gani ya kusimamia vizuri uchaguzi.

Alisema mafunzo kwa ajili ya wasimamizi wa uchaguzi (ngazi ya majimbo) yanatarajiwa kuanza leo hadi Februari 28, wakati mafunzo kwa maofisa wa vituo vya kupigia kura yataanza Machi 11 hadi 13, mwaka huu.

Mafunzo kwa ajili ya mawakala wa vyama vya siasa na maofisa wa kusimamia usalama yatafanyika Machi 14 na 15, mwaka huu, kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa ZEC.

Mwenyekiti huyo wa ZEC alisema maandalizi ya awali ya kuchapisha karatasi za kura yamekamilika, na mchapaji ambaye hakutaka kumtaja anaendelea na kazi ya kuchapa karatasi hizo ambazo zinatarajiwa kuletwa Zanzibar mapema mwezi ujao.

“Tunawaomba wananchi wajiandae kwa uchaguzi wa marudio na wagombea wote kutoka vyama tofauti vya siasa kufuata kanuni na sheria za uchaguzi,” alisema Jecha.

Uchaguzi huo wa marudio wa Machi 20, mwaka huu utafanyika baada ya ule wa Oktoba 25, mwaka jana, kufutwa kutokana na kasoro mbalimbali zilizoufanya usiwe huru na wa haki. Juhudi za kuwapata wasemaji wa CUF jana hadi tunaenda mitamboni hazikufanikiwa.

Wabunge na Maseneta wa Bunge la Marekani wamuombea Rais Magufuli

Written By CCMdijitali on Saturday, February 20, 2016 | February 20, 2016


Wabunge na Maseneta wa Bunge la Marekani wakimuombea Rais Magufuli, ili aweze kufanya kazi zake vizuri walipotembelea ofisi za Spika wa Bunge kwa mazungumzo mafupi jana. Rais Magufuli siku zote amekuwa akisisitiza na kuomba wananchi wamuombee.

Rwanda wampongeza Magufuli

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk Agustine Mahiga


Imeandikwa na Katuma Masamba - Habari Leo

 WAFANYABIASHARA wa Rwanda wamepongeza hatua zinazochukuliwa na Rais John Magufuli katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa kuimarisha ufanisi wa bandari, kukuza biashara baina ya Tanzania na nchi jirani.

Aidha wamesema tangu Rais Magufuli aanze kuchukua hatua hizo, mizigo yao imekuwa salama zaidi na wamefanikiwa kuipata kwa urahisi tofauti na zamani ambapo mingi ilikuwa ikipotea.

Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza baada ya kutua nchini akitokea Kigali, Rwanda, Balozi Mahiga alisema pia Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame amemhakikishia kuwa ataendelea kushawishi wafanyabiashara wake kutumia Bandari ya Dar es Salaam, ili kukuza uhusiano wa kibiashara uliopo.

“Nilipata bahati ya kuzungumza na wafanyabiashara wa kule... wamepongeza sana hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli pale bandarini kwa sababu wanasema sasa hivi itawasaidia sana kuhakikisha usalama wa mizigo yao,” alisema Blozi Mahiga.

Alisema wafanyabiashara hao pia wameomba mkutano wa pamoja na wenzao wa Tanzania, ili kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo fursa za uwekezaji ndani ya Rwanda na Tanzania.

Alisema Rais Kagame anaunga mkono ujenzi wa reli itakayotumika kusafarisha mizigo kwa kuwa ni njia mojawapo ya kukuza uchumi wa nchi hizo mbili rafiki.

Akizungumzia safari yake hiyo, Balozi Mahiga alisema, alienda nchini humo kujadiliana masuala mbalimbali aliyoagizwa na Rais Magufuli kwa Rais wa nchi hiyo, ambapo walijadili masuala matatu, ikiwemo machafuko yanayoendelea Burundi.

Alisema kuhusu machafuko ya Burundi, Rais Kagame alikanusha tuhuma zinazotolewa na nchi hiyo pamoja na jumuiya za kimataifa kuwa anahusika katika kuchochea machafuko hayo.

Kwa mujibu wa Balozi Mahiga, maandamano ya nchi nzima yaliyofanyika wiki iliyopita nchini Burundi ya kuishutumu Rwanda kuhusika na machafuko nchini mwao, yalishitua nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kutokana na baadhi ya maneno ya chuki yaliyokuwa yakitolewa na wananchi hao dhidi ya nchi hiyo.

Alisema hali hiyo, ilihofiwa kwamba ingeweza kuvunja mazungumzo ya kutafuta suluhu yanayoendelea.

“Nilimuuliza Rais Kagame kuhusu hili suala, akasema hatachukua hatua yoyote licha ya kwamba wananchi wake wamemlazimisha kufanya kitu. Lakini alisema atashiriki katika majadiliano ya kutafuta suluhu ya Burundi. “Sisi tulikuwa tunahofia kuwa huenda akachukua hatua ambazo zingeweza kuleta matatizo na hata mazungumzo yanayoendelea kuvunjika, lakini ameniambia hatachukua hatua yoyote inayoweza kusababisha kuvunjika kwa uhusiano,” alisema Balozi Mahiga.

Hata hivyo, alisema Rais Kagame alilalamikia nchi yake kushutumiwa kwa kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wakimbizi wa Burundi, ili kuipindua Serikali ya nchi hiyo na kutaka Jumuiya za Kimataifa, kuwaondoa wakimbizi zaidi ya 70,000 na kuwahamishia nchi nyingine za jirani.

“Aliniambia kuwa kuendelea kuwa na hawa wakimbizi katika nchi yake, kunaweza kumletea matatizo makubwa, kwa sababu amekuwa akilaumiwa sana. Hivyo kuliko lawama, ni bora hizi Jumuiya za Kimataifa zikawaondoa wakimbizi,” alisema.

Alisema kwa mujibu wa Rais Kagame, Rwanda itaendelea kushiriki katika mijadala mbalimbali ya kutafuta suluhu ya Burundi na itahakikisha Burundi inakuwa salama.

Jambo lingine walilozungumza na Rais Kagame ni mkutano wa marais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotarajiwa kufanyika mwisho wa mwezi nchini Tanzania, ambapo pia alikuwa katika hatua ya mwisho katika kukamilisha ajenda na watakaoshiriki mkutano huo.

Waziri Mkuu Majaliwa aibukia bandari ya Tanga

 Matishari matatu ambayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa maandishi kuwa ni nani aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila kuzingatia viwango na ubora uliokusudiwa na serikali.. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Habari Leo

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kushitukiza ya kukagua Bandari ya Tanga na kumtaka Mkuu wa Bandari hiyo (Port Master), Henry Arika ampelekee maelezo kuhusu ukiukwaji wa ununuzi wa tishari ifikapo leo saa 6 mchana.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Tanga jana mchana kushiriki maziko ya Mzee Ally Mwalimu Makwaya, ambaye ni baba mzazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, aliamua kuzuru bandari hiyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege akiwa njiani kurejea Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo fupi, Waziri Mkuu alikataa kuingia ofisini (bandarini) na akataka apelekwe mahali tishari tatu za bandari hiyo zilipo.

Katika maswali aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Arika alikiri kuwa matishari hayo hayafanyi kazi kama inavyotakiwa kwa sababu yanasubiri kusukumwa na tugboat (meli ndogo).

“Nataka kesho saa 6 mchana uniletee barua yenye maelezo ni kwa nini mlinunua tishari tatu ndogo badala ya mbili kubwa, wakati mnajua Serikali ilitenga Dola za Marekani milioni 10.113, kwa ajili ya kununua tishari mbili zenye uwezo wa kujiendesha zenyewe. “Nataka maelezo ni kwa nini mlizinunua tangu mwaka 2011 lakini zimekaa bila kufanya kazi hadi Novemba mwaka jana? 

Na kwa nini mnaendelea kutumia fedha za Serikali kwa kukodisha tishari kutoka Mombasa, badala ya kutengeneza za kwenu au kufundisha vijana wa Kitanzania? Kwani tunao wahitimu wangapi wa fani hii?” Alihoji Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema anazo taarifa kwamba moja ya tishari lilidondoka baharini, wakaenda kutafuta huko na kulivuta hadi pwani ndiyo maana yameshindwa kufanya kazi inavyotakiwa.

Katika majibu yake, Arika alisema wao waliagiza tishari hizo kupitia ofisi ya Bandari Makao Makuu ambayo iko Dar es Salaam.

“Pia wakati zinaagizwa sikuwepo hapa Tanga. Nimekuja mwishoni mwa mwaka jana,” alisema Mkuu huyo wa Bandari ambaye inaelezwa alitokea Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza awaite watu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Bandari na Jeshi la Polisi wakae na kutafuta mbinu za kudhibiti njia za panya zinazotumika kupitisha sukari ya magendo.

“Mkuu wa Mkoa simamia hawa watu, msaidiane kudhibiti uingizaji wa sukari kwa njia za panya. Kuna majahazi yanaleta sukari kutoka Brazil. “Mheshimiwa Rais amepiga marufuku uingizaji wa sukari kutoka nje ili viwanda vyetu vya ndani viongeze uzalishaji. Dhibitini bandari zote ndogondogo hadi Pangani,” aliagiza Waziri Mkuu.

Alisema changamoto inayoikabili Serikali ni kwamba hata Shirika la Viwango Tanzania (TBS) au Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) hawawezi kukagua sukari hizo na hazijulikani ubora wake licha ya kuwa zinafika kwa walaji.

 Waziri Mkuu Kassim Majliwa akizungumza na Mkuu wa bandari ya Tanga, Henry Arika (kulia kwake ) na Mhandisi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Felix Mahangwa ( kulia wakati alipotembelea bandari ya Tanga Februari 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kssim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry Arika (kulia kwake) kukagua bandari hiyo Februari 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link