MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...

Latest Post

VIONGOZI WANALOJUKUMU LA KUZINGATIA MATUMIZI YA TAKWIMU ZA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022.

Written By CCMdijitali on Monday, December 11, 2023 | December 11, 2023

 

MBUNGE WA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI MHE DKT D.JOHN PALLANGYO



Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Dkt. John Danielson Palangyo, amesema kuwa viongozi wa wananchi wanalojukumu la kuzingatia matumizi ya Takwimu sahihi za Matokeo ya Sensa ya Watu na makazi ili kupanga shughuli na kufikia malengo ya Serikali.

Akizungumza wakati wa mkutano wa Mafunzo ya usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022 kwa viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii, mkoa wa Arusha, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa AIM MALL Jijini Arusha leo 11.12.2023, Dkt. pallangyo amewataka viongozi walioshiriki mafunzo hayo kuyazingatia ili kwenda kuelimisha jamii namna na faida ya matumizi ya Takwimu hizo.

Ameweka wazi kuwa, Takwimu za Matokeo ya Sensa licha ya kuwa ni Dira ya maendeleo ya Taifa, lakini viongozi na watanzania wanalojukumu ya kuzitumia ili ziweze kufikia malengo ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Serikali.

"Kwa niaba ya wananchi wa Arumeru Mashariki, tunaipongeza Serikali ya awamu ya sita, kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kisekta katika jimbo langu, ipo miradi yenye kutumia fedha nyingi a,bayo imetekelezwa na kukamilika huku ikitoa fura kwa wananchi kuitumia na kupata huduma ndani ya maeneo yao, ile hali ya wananchi kuuza vitu na mali zao ili kujenga madarasa kwa sasa kwetu imekuwa ni histori, Serikali imejenga madarasa mengi, tunamshukuru Mhe. Rais Samia, na niwatake wanaArumeru wote kumuunga mkono" Amebainisha Mhe. Dkt. Pallangyo


Mkutano huo umefunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi Utumishi na Rasilimali Watu, mkoa wa Arusha, David Lyamongi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, ukiwa na lengo la kuyajengea uwezo makundi mbalimbali ya kijamii juu ya matumizi sahihi ya matokeo ya Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022.

Makundi hayo ni pamoja na viongozi wawakilishi wa wananchi, viongozi wa Siasa, dini na mila, Watendaji wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, watendaji wa kata, kamati ya Sensa Mkoa pamoja na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo watu wenye mahuitaji maalum.





 

 

WAZANZIBARI NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAMETAKIWA KUWALEA WATOTO WAO KWA KUZINGATIA MILA, SILKA NA DESTURI ZA KIZANZIBARI

Written By CCMdijitali on Friday, December 8, 2023 | December 08, 2023

 


 

Wazanzibari na Waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuwalea watoto wao kwa kuzingatia Mila, Silka na Desturi za kizanzibari ili kupata kizazi chema chenye Kufuata maadili.

 

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid Maungani mara baada ya kumaliza  Ibada ya Sala ya Ijumaa.

 

Amesema wazazi na walezi wanapaswa kuwalea watoto wao kwa kufuata silka na mila za kizanzibari jambo ambalo kitasaidia kuondosha kabisa vitendo vya udhalilishaji  hasa kwa wanawake na watoto jambo ambalo linaiharibu sifa Zanzibar.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni wajibu wa kila Mzanzibari kupiga vita suala la udhalilishaji na kuwataka wakaazi wa Maungani na maeneo jirani kuhakikisha wanapita nyumba hadi nyumba kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na kuhakikisha wanawafichua wale wote ambao wanatabia ya kufanya vitendo hivyo,.

 

Alhajj Hemed amewataka waumini na  Wazanzibari kushirikiana na kuacha muhali na kwenda kutoa ushahidi Mahakamani pale ambapo wanatakiwa kufanya hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

 

 

Akizunguzia suala la madawa ya kulevya  Alhajj Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar kuachana na tabia ya kuwakodisha nyumba watu ambao hawawafahamu na hawana taarifa zao za  kutosha ili kuondosha wimbi la watumiaji na wauzajiwa wa madawa ya kulevya nchini.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi itahakikisha inaondosha kabisa suala la madawa ya kulevya kwa kuweka sheria ngumu amabzo zitawabana waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa madawa ya kulevya.

 

 

 

 Akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Maalim SULEIMAN MWINCHUMU   amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kuchunga nafsi zao na kujielekeza katika  kufanya amali njema ambazo zitawaepusha na kupata hasara hapa duniani na kesho akhera.

Amesema kuwa wazazi watakapo weza kuchunga nafsi zao pamoja na kuwachunga watoto dhidi ya wao katika kujiunga na vikundi viovyo watakuwa wameisaidia jamii na taifa kwa ujumla kwaani Taifa lenye maendeleo linahitaji nguvu kazi isiyo na mmong’onyoko wa maadili.

 




Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Leo tarehe..08.12.2023

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR- AHAHIRISHA BARAZA LA WAWAKILISHI.

 

 

 

 

 


 

 

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuimarisha huduma za kijamii zikiwemo Afya, Elimu na Maji safi na salama.

 

Ameyasama hayo alipokuwa akiuakhirisha Mkutano wa Kumi na Tatu(13) wa Baraza la Kumi (10) la Wawakilishi katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Jijini  Zanzibar.

 

Mhe. Hemed amesema Serikali itaendelea kusimamia Miradi ya Ujenzi wa Skuli, Hospitali na Miradi ya Maji safi na salama kwa lengo la kuhakikisha Wananchi wanapata huduma hizo katika maeneo ya karibu ikiwa ni utekelezajiwa  Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka ‪2020-2025‬ pamoja na ahadi zilizotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussen Ali Mwinyi wakati wa Kampeni za Uchaguzi 2020.

 

Amesema kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  ipo katika hatua za kuboresha Daftari la wapiga kura ambapo amewahimiza Wananchi kuitumia nafasi yao ya kidemokrasia kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kufata maelekezo yanayotolewa na Tume ya Uchaguzi.

 

Aidha Mhe. Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema  Serikali itahakikisha inapambana kwa nguvu zake zote kuondosha kabisa vitendo vya utumiaji wa dawa za kulevya na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia wa wanawake na watoto ambavyo vinaendelea kuiathiri Jamii ya Wazanzibari.

 

Sambamba na hayo amesema katika kuhakikisha mapato ya Serikali yanazibitiwa, Serikali imeimarisha Mfumo wa usimamizi wa fedha wa IFMIS na kuanzisha Mfumo wa Zan-malipo, mfumo wa manunuzi wa E- Proz, mfumo wa ukusanyaji wa kodi wa kutumia mashine ya( EFD) mfumo wa payroll na mfumo wa bajeti na matumizi (BAMAS).   

 

Amefahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuchukua jitihada mbali mbali katika kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi ya wafanyakazi, hivyo  amewataka watumishi kuendelea kuimarisha nidhamu na uwajibakaji kwa maslahi mapana ya nchi.

 

Mhe. Hemed amesema kuwa michezo ni jambo muhimu linalowaunganisha wananchi walio wengi Duniani hivyo Serikali inakamilisha ukarabati wa  Ujenzi wa Kiwanja cha Amani Unguja na Gombani Pemba ambapo kukamilika kwake mandhari na haiba ya viwanja hivyo yatakuwa na muonekano wenye hadhi ya Kimataifa.

 

Sambmba na hayo Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Timu ya Vijana chini ya Umri wa miaka 15 Karume Boys kwa kutwaa Ubingwa wa mashindano ya CECAFA 2025 yaliyofanyika Uganda na kupata Mkono wa Dhahabu wa Kipa bora jambo ambalo limeiletea heshima nchi yetu.

 

Mhe. Hemed ametoa pole kwa wananchi walioatirika na Mafuriko ndani ya Zanzibar na Tanzania Bara hasa kwa wakazi wa Manyara kufuatia Mafuriko ya Maporomoko ya Udongo yaliyotokea katika Kijiji cha Katesh na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 68 na majeruhi zaidi ya 100.

 

 

Katika Mkutano wa Kumi na Tatu(13) wa Baraza la Kumi(10) la Wawakilishi, Baraza limepokea, limejadili na kupitisha Miswaada Sita(6) ya Sheria pamoja na kuwasilishwa Barazani Ripoti ya Saba ya Utekelezaji wa Tume ya Maadili kwa mwaka 2022/2023.

 





Imetolewa na kitengo cha Habari (OMPR)

Leo tarehe 08.12.2023

Rais Dk.Mwinyi amuwakilishs Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ufunguzi wa Mkutano wa Benki ya Dunia(IDA20)

Written By CCMdijitali on Wednesday, December 6, 2023 | December 06, 2023




Zanzibar,

06 Disemba, 2023

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema imeweka kipaumbele kwenye kukuza uchumi wake na kuongeza uwekezaji wa huduma za jamii ikiwemo afya, elimu, afya na huduma nyingine za jamii ikiwemo kuimarisha umeme na maji safi vijijini.

Aidha, imeeleza inavyojikita kwenye kilimo kinachozingatia zaidi hali ya hewa ili kuendana sambamba na nyakati za mavuno kwa lengo la kuwaletea tija Watanzania.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutanao wa Kimataifa wa tathmini ya muda, kati ya mzunguko wa 20 wa Mapitio ya benki ya Dunia (IDA) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema, Tanzania inavyoshirikiana na Benki ya Dunia kwa kufanyakazi madhubuti ya kuwaondoa mamilioni ya watu kutoka kwenye umaskini na kuwaletea mabadiliko kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na benki hiyo.

Alisema, Tanzania imezindua mpango wa “Kujenga Kesho Bora” ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaidia wanawake na vijana wengi kupatiwa mafunzo, rasilimali ardhi kwa ajili ya kilimo cha kisasa, kuwawezesha kiuchumi, pembejeo na uongezaji thamani wa mazao ya kilimo na ufugaji katika kujitegemea wenyewe kiuchumi na kujikimu. 

“Tunashukuru Benki ya Dunia na washirika wengine kwa msaada wao kwa mpango huu”. Alishukuru Dk. Samia.

Rais Dk. Mwinyi alieleza, kwa msaada wa IDA wa dola za Marekani milioni 200 kwa Mpango wa Umeme Vijijini umeisaidia Tanzania kuwafikia zaidi ya watu milioni 2.5,  hali iliyoisaidia nchi kufikia viwango vya upanuzi wa haraka barani Afrika kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Alisema, zaidi ya watu milioni 4.5, wamefikiwa na huduma bora za jamii ikiwemo umeme vijijini, hospitali na ujenzi wa shule za vijijini.

Alisema mpango huo uliongeza fursa za ajira, biashara na matokeo bora kwa wanafunzi walioishi maeneo mbali na shule. Pia alisema, mpango ulikuwa na matokeo mazuri kiasi ya kuvutia ufadhili wa ziada wa dola za Marekani milioni 335 kusaidia kufikia matokeo bora zaidi kwa jamii za vijijini.

Akizungumzia sekta ya maji, chini ya miaka mitano ya mfuko wa msaada wa dola za Marekani milioni 300 kwa ajili ya Mpango Endelevu wa Ugavi wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira uliwezesha upatikanaji wa maji safi kwa zaidi ya watu milioni 4.7, nusu yao wakiwa wanawake. 

Alieleza, mpango huo pia uliboresha upatikanaji wa huduma za vyoo kwa zaidi ya watu milioni 6.6, vituo vya afya 1,904 na skuli za msingi 1,095. 

Pia, Rais Dk. Mwinyi alizungumzia mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya Tabianchi (COP28) uliofanyika Dubai ambako Rais Dk. Samia alitetea ajenda ya kusaidia kupunguza nishati mimea zinazoathiri mazingira mara baada ya kuongoza uzinduzi wa mradiri wa nishati safi ya kupikia itakayowanufaisha wanawake wengi, Afrika (AWCCSP).

Akizungumzia Zanzibar inavyonufaika na fursa kutoka Benki ya Dunia, Rais Dk. Mwinyi alieleza uchumi wa Zanzibar unategemea Utalii kwa kiasi kikubwa hasa utalii wa utamaduni. Alisema, hifadhi ya Mji Mkongwe ambao ni urithi wa Dunia wa UNESCO, ulinufaika na Benki ya Dunia kupitia mradi wa “huduma za Mijini, Zanzibar” (ZUSP) ambao ulipata msaada kutoka IDA wenye thamani ya dola za Marekani milioni 93 ili kuboresha upatikanaji wa huduma za mijini na kuhifadhi urithi huo wa kitamaduni.

Alieleza pia mradi huo ulikarabati kipande cha mita 340 cha ukuta wa bahari ya Mizingani uliokuwa hatarini kuporomoka na kuzorotesha usafiri wa kivuko kwa wafanyabiashara na watalii. Sambamba na kuboresha barabara kuu ya Mji Mkongwe.

Alieleza Benki ya Dunia pia imesaidia Tanzania kupitia Mitandao ya Hifadhi ya Jamii ambayo ilitolewa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na Mradi wa Ushirikiano wa Usafiri kwa ajili ya kuboresha barabara.

Alisema, ushirikiano mwema uliopo baina ya Tanzania na Benki ya Dunia umesaidia maisha ya mamilioni ya watu nchini nakuongeza kuwa ushirikiano huo utaendelea kudumu.

Rais, Dk. Mwinyi aliiomba Benki ya Dunia na washirika wake, kuendelea kuimarisha usaidizi wao kwa nchi wanufaika wa IDA ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Pia Dk. Mwinyi aligusia eneo la biashara huria kwa mataifa wanufaika wa Benki ya Dunia na washirika wake, ili kuimarisha ushindani na uundaji wa nafasi za kazi kupitia ushirikiano wa kikanda na biashara, kwa bara la Afika na maeneo mengine ya dunia,
“Tunaamini IDA na IFC zinahitaji kuongeza usaidizi ili kukuza sekta binafsi inayostawi, jambo la msingi ni kuunganisha biashara za Kiafrika katika minyororo ya thamani ya kimataifa na kuvutia FDIs.” Alieleza Rais Dk. Mwinyi.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Rais wa Benki ya Dunia na washirika wake, Ajei Banga alimpa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mtihani wa majanga ya kimaumbile yaliyowakumba Watanzania wa Manyara, nakueleza kuwa Benki ya Dunia ilipokea taarifa kwa masikitiko makubwa.

Mapema akizungumza kwenye mkutano huo waziri wa Fedha wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Lameck Nchemba aliiomba Benki ya Dunia kuwaongeza watanzania wa Mkoa wa Manyara walioathiriwa na mafuriko hivi karibuni kupitia fao la benki hiyo la majanga ya kimaumbile.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salum, alieleza mafanikio makubwa ya mkutano huo wa Kimataifa wa tathmini ya muda, kati ya mzunguko wa 20 wa Mapitio ya benki ya Dunia (IDA) yamefikiwa kutokana na jukudi kubwa za uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na msaada mkubwa waliopata kutoka kwa Mwakilishi Mkaazi wa benki hiyo, Bw. Nathan Balete.

Zaidi ya wageni 300 kutoka mataifa mbalimbali dunia wamehudhuria mkutano huo wenye lengo la kufanya mapitio ya miradi inayoungwa mkono na benki hiyo, pamoja na mambo mengine pia utaangalia namna bora ya utekelezwaji wa miradi ya maendeleo na namna ya kuongezwa fedha na ruzuku kwa miradi itakayofanya vizuri zaidi kwa mataifa wanufaika.

IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR.














NAIBU WAZIRI PINDA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI KIEGEYA MOROGORO

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akifurahi na Mwenyekiti wa Wakulima Haleluya Minga mara baada ya kumaliza na kuufunga        rasmi mgogoro wa ardhi katika eneo la Kiegeya mkoa wa Morogoro tarehe 5 Desemba 2023.

    
    Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO

    Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda amemaliza na kuufunga wa wananchi 767 wa Kiegeya mkoani Morogoro.

    Wananchi hao ni wale waliovamia na kulima katika shamba la Tungi Sisal Estate la Mwekezaji Star Infrastructure.

    Mhe Pinda amemaliza na kuufunga mgogoro huo tarehe 5 Desemba 2023 alipokutana na wawakilishi wa wakulima wakioongozwa na Mwenyekiti wao Haleluya Minga katika ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro.

    Naibu Waziri wa Ardhi alifika mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwasikiliza ili kupata ukweli ambapo baada ya kuwasikiliza kwa takriban saa nne alibaini udanganyifu katika maelezo ya wakulima na kuwapa taarifa kuwa mwekezaji ni mmiliki halali na alitoa ekari 4000 alizoombwa na serikali na wao wamevamia sehemu mpya.

    ‘’Niwatake muwe waungwana na mfuate taratibu za kisheria za kupata ardhi na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wakataokaidi maelekezo ya serikali na mgogogoro huu kuhusu wananchi 767 nimeufunga rasmi’’ alisema Pinda


     ‘’Kesi yenu ilipitiwa katika ngazi mbalimbali na utafiti wake umefanyika mpaka uwandani na kuonesha kuwa ninyi hamna haki, kwanza mko tofauti na idadi yenu inaongezeka kila siku kutoka 319 hadi 767 na bado inaendelea hivyo katika mazingira ya kawaida inawawia vigumu kuwasaidia’’ alisema Mhe. Pinda.


    Mwenyekiti wa wakulima hao Haleluya Minga mbali na kumshukuru Naibu Waziri kwa kuamuzi wake wa kwenda kuwasikiliza wakulima hao alimueleza kuwa, kuongezeka kwa idadi ya wakulima kulitokana na wao kutokuwa na utaratibu wa vikao na baada ya kugundua hilo ndipo walipokutana na kuchagua uongozi.

    ‘’Kupanda kwa idadi ya wakulima kutoka 319 hadi 767, kwanza hatukuwa na utaratibu wa viakao na tulikuwa hatufahamiani na ilifika mahali kulikuwa na ongezeko tukaamua kuwa na uongozi wa pamoja’’ alisema Haleluya.


    Hata hivyo, Naibu Waziri Pinda amewataka wakulima hao kuwa watulivu na matumizi ya nguvu hayatasaidai kwa kuwa kamati ya mkoa, ofisi ya mkurugenzi wa manispoaa ya Morogoro na ile ya Taifa zinethibitisha kuwa wao siyo wamiliki halali wa maeneo hayo.

    Awali Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro Frank Minzikunte alieleza historia ya shamba hilo kuwa inaanzia mwaka 1951 kwa kumilikishwa kwa Mwekezaji na mwaka 1983 serikali ilimuomba mwekezaji ekari 4000 kwa muda ili wananchi wafanye kilimo cha kufa na kupona.

    Aliongeza kuwa, mwaka 2021 serikali ilimuomba mwekezaji kuziachia moja kwa moja ekari hizo ambapo baada ya majadiliano ya muda mrefu mwekezaji aliridhia na wananchi waliokuwa wamepewa mwaka 1983 wakatambuliwa na takriban wananchi 3777 walitambuliwa na kuingia mkataba na halmashauri ya upimaji shirikishi kama ilivyoelekezwa na serikali.

    Hata hivyo, Kamishna huyo wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro alisema, wakati kutambua wananchi hao lilijotokeza kundi la wananchi 319 waliodaia kulima nje ya ekari zilizotolewa na mwekezaji kwa wakulima na ndipo serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliunda tume kwa ajili ya kusikiliza malalamiko pamoja na kero nyingine zinazowakabili wananchi katika ekari 4000.

 

 

 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akizungumza na wawakilishi wa Wakulima wakati wa kutafuta suluhu  mgogoro wa ardhi katika eneo la Kiegeya mkoa wa Morogoro tarehe 5 Desemba 2023.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wakulima mara baada ya kumaliza na kuufunga rasmi mgogoro wa ardhi katika eneo la Kiegeya mkoa wa Morogoro tarehe 5 Desemba 2023.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akipata maelezo kutoka kwa mwananchi wa mkoa wa Morogoro wakati wa kusikiliza kero za ardhi mkoani humo tarehe 5 Desemba 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA MKUTANO WA BODI YA GPE

Written By CCMdijitali on Tuesday, December 5, 2023 | December 05, 2023

  

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA MKUTANO WA BODI YA GPE MJINI UNGUJA LEO

 
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah leo amefungua rasmi mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Maendeleo ya Elimu Duniani (GPE) unaoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hio, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja, leo.
 
Mkutano huo wa siku mbili, unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na nje ya Marekani na Ulaya, tangu Shirika hilo lianzishwe na mataifa tajiri duniani ya G7 miaka 20 iliyopita.
 
Kwa mujibu wa Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza GPE, shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu Tanzania bara na Zanzibar.
 
Bodi ya Wakurugenzi ya GPE inaundwa na majimbo 20 yanayowakilisha washirika wote wa ushirikiano, ambapo katika mkutano wa bodi wanahudhuria Mjumbe wa Bodi na mjumbe mbadala wa Bodi wanawakilisha kila jimbo.
 
Bodi ya Wakurugenzi ya GPE huweka sera na mikakati ya ushirikiano, huku ikiakisi hali pana na tofauti ya ubia na inajumuisha wanachama kutoka serikali za nchi zenye mapato ya chini na washirika wote wa maendeleo: wakiwemo wafadhili, mashirika ya kiraia, sekta binafsi na wakfu, na mashirika ya kimataifa na benki za kikanda.
 
Nchi washirika wa GPE ni Afghanistan, Albania, Algeria, Angola, Bangladesh, Belize, Benin, Bhutan, Bolivia,  Burkina Faso, Burundi, Cabo Verde, Cambodia, Cameroon, Central African Republic, Chad, Comoros, Congo, Democratic Republic ofCongo, Republic of,  Côte d'Ivoire, Djibouti, Dominica, na  Egypt.
 
Nchi zingine ni El Salvador, Eritrea, Eswatini, Ethiopia, Fiji, The Gambia, Georgia, Ghana, Grenada, Guatemala, Guinea, Guinea-Bissau, Guyana, Haiti, Honduras, India, Indonesia, Kenya, Kiribati, Kyrgyz Republic, Lao PDR, Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Maldives, Mali, Marshall Islands, Mauritania, FS Micronesia, Moldova, Mongolia na Morocco.
 
Zingine ni Mozambique, Myanmar, Nepal, Nicaragua, Niger, Nigeria, Pacific region, Pakistan, Papua New Guinea, Philippines, Rwanda, Saint Lucia, Saint Vincent and the Grenadines, Samoa, São Tomé and Príncipe, Senegal, Sierra Leone, Solomon Islands, Somalia, South Sudan, Sri Lanka, Sudan, Tajikistan.
 
Tanzania, Timor-Leste, Togo, Tonga, Tunisia, Tuvalu, Uganda, Ukraine, Uzbekistan, Vanuatu, Viet Nam, West Bank and Gaza, Yemen, Zambia na Zimbabwe pia ni nchi washirika.  Syria si nchi mwanachama lakini imepokea ufadhili kwa idhini ya Bodi ya GPE.
 
 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Elimu Duniani (GPE) Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kitabu Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah kabla hajafungua rasmi mkutano wa Bodi hio katika hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja, leo.


 
 
 
 

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Elimu Duniani (GPE) Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Wake Bi Suzan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu Laura Fringeti kabla hajafungua rasmi mkutano wa Bodi hio katika hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja, leo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Elimu Duniani (GPE) Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akioingoza mkutano wa Bodi hio katika hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja, leo.

 

 Na Ofisi ya Rais Mstaafu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Elimu Duniani (GPE) Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah baada ya kufungua  rasmi mkutano wa Bodi hio katika hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja, leo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Elimu Duniani (GPE) Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah baada ya kufungua  rasmi mkutano wa Bodi hio katika hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja, leo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Elimu Duniani (GPE) Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Wake Bi Suzan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu Laura Fringeti  akifungua rasmi mkutano wa Bodi hio katika hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja,

leo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Elimu Duniani (GPE) Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Wake Bi Suzan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu Laura Fringeti  akifungua rasmi mkutano wa Bodi hio katika hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja,

leo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Elimu Duniani (GPE) Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Wake Bi Suzan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu Laura Fringeti  akifungua rasmi mkutano wa Bodi hio katika hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja,

leo.

WANANCHI NGORONGORO WANAHAMISHWA KWA KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU

Written By CCMdijitali on Monday, December 4, 2023 | December 04, 2023

Mhe. Geofrey Pinda, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la masuala ya Ardhi tarehe 4 Desemba 2023 mkoani Morogoro. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)


Na Munir Shemwera, WANMM MOROGORO

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amesema Wananchi wa Ngorongoro wanaohamishwa kutoka eneo la hifadhi kwenda kijiji cha Msomera Handeni mkoa wa Tanga wamehamishwa kwa kuzingatia haki za binadamu.

Mhe. Pinda amesema hayo tarehe 4 Desemba 2023 mkoani Morogoro wakati akifungua kongamano la siku mbili linaloratibiwa na Jukwaa la Ardhi Tanzania (TALA) kujadili masuala ya ardhi.

Amesema, pamoja na uwepo wa taasisi zenye mapenzi mema na serikali lakini zipo baadhi yake za binafsi zinazofanya biashara kwa kuuza nafsi za watanzania wanaoishi Ngorongoro kwa kuwarubini na kuelezea maneno yasiyokuwa na uhalisia kuhusu kuhamishwa kwa wananchi wanaoishi kwenye hifadhi hiyo.

Amelitaka Jukwaa la Ardhi Tanzania (TALA) na wadau wa mkutano huo kwenda kijiji cha Msomera mkoani Tanga na watakapotoka huko serikali iko tayari kupokea maoni kwa kuwa wao ni watanzania na wanawasemea watanzania wenzao.

Akigeukia suala la haki za binadamu, Naibu Waziri Pinda amesema ni haki gani anazozikosa mwananchi anayeishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro na kwanini asitafutiwe haki hiyo?  Ameweka wazi kuwa, Seikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inafanya jitihada kuhakikisha inawajengea uwezo wale waliohamishiwa kijiji cha Msomera.

‘’Leo wananchi hao wanaweza kwenda benki wakakopoa, wana ardhi ya kudumu na hati, hakuna mtu atakayewabughudhi, kuwanyang’anya na wametengewa maeneo makubwa ya kuchungia mifugo yao na tunaendelea kuboresha na tunachimba mabwawa kuhakikisha wananchi hawatupwi na wanalindwa na mali zao’’ alisema Pinda.

Amesema, Ngorongoro kwa mujibu wa Sheria ilikuwa siyo rahisi kupeleka huduma nyinginezo kwa sababu sheria inayolinda eneo hilo ilikuwa ni sheria iliyotaka kutoharibiwa Ecolojia ya Ngorongoro.

Naibu Waziri Pinda amewaambia washiriki wa kongamano hilo kuwa si vizuri kupotoshana katika suala la Ngorongoro na kueleza kuwa, pale inapopatikana nafasi ya kujadili basi yajadiliwe matokeo halisi ya kitaifa na kusisitiza kuwa ni lazima kujengeana ubora kwa maisha ya watanzania.

Kongamano hilo la siku mbili lililobeba kauli mbiu ya Usalama wa Milki za Ardhi kwa Uhakika wa Chakula limejadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya ardhi ikiwemo Haki za Wanawake katika Muktadha wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi na Usalama wa Chakula, Mipango ya Matumizi ya Ardhi na Uratibu wa Takwimu pamoja na Hali ya Haki za Ardhi kwa Vijana na Utekelezaji ya Mikakati na Uhamasishaji Vijana Kushiriki katika Kilimo.

Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Ardhi Tanzania lililohitimishwa tarehe 5 Desemba 2023 mkoani Morgoro.

Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Ardhi Tanzania lililohitimishwa tarehe 5 Desemba 2023 mkoani Morgoro.

Mhe. Geofrey Pinda, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda akizungumza katika Kongamano la masuala ya Ardhi linaloratibiwa na Jukwaa la Ardhi Tanzania (TALA) tarehe 4 Desemba 2023 mkoani Morogoro





GPE and CAMFED Host Roundtable on Education with Tanzanian CSOs

Written By CCMdijitali on Wednesday, November 29, 2023 | November 29, 2023

 Retired President Dr. Kikwete shares space in a Roundtable discussion on Education with Tanzanian CSOs in Dar es salaam

The Chair of the Board of Directors of the Global Partnership for Education (GPE), H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Retired President of the United Republic of Tanzania, along with GPE’s Chief Executive Officer, Ms. Laura Frigenti, in a group photo with members of CSOs after their roundtable today at the Campaign for Female Education (CAMFED) Tanzania offices in Dar es Salaam.

The Chair of the Board of Directors of the Global Partnership for Education (GPE), H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Retired President of the United Republic of Tanzania, along with GPE’s Chief Executive Officer, Ms. Laura Frigenti, participate in a roundtable discussion with CSOs today at the Campaign for Female Education (CAMFED) Tanzania offices in Dar es Salaam.


 

 
Dar es Salaam, 29th November 2023 - The Chair of the Board of Directors of the Global Partnership for Education (GPE), H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Retired President of the United Republic of Tanzania, along with GPE’s Chief Executive Officer, Ms. Laura Frigenti, are set to participate in a significant roundtable discussion today at the Campaign for Female Education (CAMFED) Tanzania offices in Dar es Salaam.
 
According to Ms. Anna Sawaki, CAMFED Tanzania’s Director of Programs and Partnership, the primary objective of the roundtable is to collectively emphasise the importance of prioritising education on the political agenda.  
 
Additionally, she said, the event aims to recognise the pivotal role of Civil Society Organisations (CSOs) in advocating for education and actively contributing to policy dialogue within local education groups.  
 
“The roundtable will also provide an opportunity for CSO representatives to share their successful practices and experiences in supporting the transformation of education systems”, Ms Sawaki explained.
 
Among the CSOs expected to attend the roundtable are HakiElimu, PESTALOZZI, Shule Direct, UWEZO, Ubongo Kids, Lyra in Africa, World Vision, Binti Salha Foundation, TEN/MET, TEM/MET, CAMFED, CAMFED Tanzania, Transforming Life Tanzania, and Gender Networking (TGNP).
 
The Global Partnership for Education (GPE) is  the largest global fund exclusively dedicated to reshaping education in lower-income countries. Operating as a unique, multi-stakeholder partnership, GPE works towards delivering quality education to ensure that every child, regardless of gender, has access to hope, opportunity, and agency.
 
For the past two decades, GPE has been actively disbursing funds and providing support to develop robust and resilient education systems in countries marked by extreme poverty or conflict. The focus is on enabling more children, particularly girls, to receive the education necessary for personal growth and contribution to building a more prosperous and sustainable world.
 
GPE's distinctive model has played a pivotal role in helping partner countries make significant strides in enhancing access, learning outcomes, and equity, resulting in improved educational opportunities for millions of boys and girls.
 
On the other hand, CAMFED, a pan-African movement, is leading a revolutionary approach to delivering girls' education. Through a gold-standard system of accountability to the young people and communities they serve, CAMFED has established a model that significantly improves the prospects of girls becoming independent and influential women.
 
CAMFED's work is driven at the grassroots level by local committees and teams comprising graduates, teachers, parents, government officials, and other volunteers who dedicate their time and expertise to ensure more girls successfully complete their education. The organisation’s governance structures include the boards of each national entity.
 
The roundtable represents a significant collaboration between GPE and CAMFED, bringing together key stakeholders and CSOs to reinforce the collective commitment to advancing education, particularly in regions facing the most pressing needs. This collaborative effort aligns with GPE's mission of transforming education systems and CAMFED's dedication to revolutionising girls' education across Africa.
 
Ends
 

PSSSF YATENGA MUDA MAALUM WA MAJUMA MANNE KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANACHAMA A

Written By CCMdijitali on Friday, November 24, 2023 | November 24, 2023

PSSSF YATENGA MUDA MAALUM WA MAJUMA MANNE KUSIKILIZA NA KUZIPATIA UFUMBUZI CHANGAMOTO ZA WANACHAMA NCHI NZIMA TANZANIA NA ZANZIBAR.

NA K-VIS BLOG/KHALFANS AID, ARUSHA

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetenga muda maalum wa majuma manne kuanzia Novemba 27 hadi Disemba 22, 2023, kwa lengo la kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali za wanachama, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, CPA. Hosea Kashimba, amesema.

CPA. Kashimba amesema hayo kwenye banda la PSSSF katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Novemba 24, 2023.

“Iwapo kuna mwanachama yeyote mwenye changamoto yoyote inayohusu uanachama, michango na mafao, afike katika ofisi za PSSSF zilizo jirani naye Tanzania bara na Zanzibar, tutamsikiliza na kutatua changamoto yake.” Alisisitiza.

Alisema zoezi hilo litakuwa likifanyika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, Jumatatu hadi Ijumaa.

“Lakini hata baada ya kipindi hicho maalum kufikia ukomo, bado tutaendelea kuwapatia huduma wanachama wetu, lengo hasa ni kuhakikisha wanachama wetu wanafurahia huduma zetu wakati wote.” Alisema CPA. Kashimba.

Pia amerejelea angalizo kwa wanachama na wastaafu, kuwa wasikubali kupokea maelekezo yoyote kutoka kwa watu wasiowajua endapo wanahisi wanachangamoto yoyote kuhusiana na uanachama wao au mafao yao.

“Tunawaasa wanachama wetu hususan wale wanaokaribia kustaafu, watambue kuwa huduma zetu zinatolewa bure bila malipo yoyote, na kama wanachangamoto yoyote wapige simu namba ya bure ‪0800 110 040‬ au kupitia mitandao yetu ya kijamii kupitia anuani ya PSSSFTZ.” Alifafanua CPA. Kashimba.

CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu PSSSF,


 

CHONGOLO: WALIPENI MADENI, WAHISHENI MALIPO YA WAKANDARASI

Written By CCMdijitali on Thursday, November 23, 2023 | November 23, 2023

 

 


 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Daniel Godfrey Chongolo amesema kupitia utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi ya 2020 – 2025, CCM itahakikisha Serikali inaendelea kuweka mazingira bora na kuwajengea uwezo makandarasi na washauri waelekezi wazawa, ili waweze kutekeleza miradi mingi na mikubwa ndani ya nchi na hata kushindana nje ya Tanzania, ikiwemo kulipwa madeni yao na kuwahishiwa malipo ya kazi katika miradi wanayotekeleza.

Ndugu Chongolo amesema hatua ya kuwatumia wakandarasi na washauri waelekezi wazalendo wa Kitanzania katika miradi hiyo mbalimbali ya ujenzi itaokoa fedha nyingi, ambazo kwa sasa zinalipwa kwa makandarasi wa nje, hivyo zitabakia katika mzunguko wa fedha na uchumi ndani ya nchi, zitaongeza kipato kwa wahusika, huku pia wakipata nafasi ya kuongeza ujuzi na kutengeneza fursa za ajira kwa Watanzania.

Mbali ya kuwataka watendaji wa Serikali, hususan katika Wizara ya Ujenzi kuacha mitazamo hasi dhidi ya wakandarasi na wahandisi wazawa kuwa hawawezi kazi, pia amewataka baadhi ya makandarasi wa ndani nao kuacha kuichafua tasnia ya ujenzi, kwa kuwa na kampuni za mfukoni (briefcase company), ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi, hali ambayo inajenga na kuhalalisha dhana kuwa kuna wazawa wanafanya utapeli kwa kutumia taaluma hiyo.

Katibu Mkuu Ndugu Chongolo amesema hayo jana Jumanne, Novemba 21, 2023, wakati akitoa salaam za Chama Cha Mapinduzi kwenye Mkutano wa Makandarasi na Washauri Waelekezi Wazawa, uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention, jijini Dodoma, ambapo amewaambia kuwa CCM inatambua changamoto zote zinazowasibu, likiwemo suala la madeni wanayodai na kucheleweshewa malipo yao katika miradi anuai wanayotekeleza maeneo mbalimbali nchini.

“Mkutano huu ni muhimu sana. Jana nimekaa na mawaziri wote wawili hawa, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Fedha hadi usiku wa manane, ilibidi tukae kwa muda mrefu sana. Nilitaka kwanza kujua masuala kadhaa kabla sijaja hapa leo. Na hasa nililowaita na kuzungumza nao ni kuhusu malipo yenu. Nina uhakika hapa tukisema tupitishe karatasi kila mtu aandike changamoto yake, jambo la kwanza kila mmoja litakuwa ni malipo, malipo, malipo.


“Wamenieleza kwa kina jinsi wanavyochukua hatua kadhaa, hasa kutekeleza maelekezo na maagizo ya Mhe. Rais Dokta Samia Suluhu Hassan amewaagiza kuhakikisha wanafanya msawazo wa malipo ya madeni ya wakandarasi na pia kila mkandarasi alipwe anapo-raise certificate. Pia labda niseme hapa, ni muhimu mkaenda pia kujifunza kwa wenzenu wa REA (Wakala wa Umeme Vijijini) ili utaratibu ule wanaotumia kulipa wakandarasi wa umeme, uweze kutumika pia huku Ujenzi. Kule hakuna malalamiko sana,” amesema Katibu Mkuu Chongolo.


Pamoja na kuipongeza Serikali kwa kufanya mabadiliko ya Sheria ya Manunuzi, iliyopandisha kiwango cha thamani ya miradi inayoweza kutekelezwa na wakandarasi wa ndani, kutoka mradi wa thamani ya Tsh. 10 bilioni, hadi kufikia mradi wa Tsh. 50 bilioni, Katibu Mkuu Ndugu Chongolo ameitaka Serikali, kupitia Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Fedha, kuweka utaratibu wa kisheria ambao utakaolazimu ushirikishwaji wa makandarasi wazawa katika miradi yote mikubwa nchini.

“Hili la ushirikishwaji kwenye miradi mikubwa ya kimkakati kama SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere, hili tunaweza kulimaliza kwa kuweka sheria ya kulazimisha wakandarasi wakubwa wanapoomba miradi hapa kwetu basi waje na wakandarasi wa ndani kama ilivyo kwa Washauri Majenzi yaani consultants.  Hii pia ni nzuri kwa maslahi mapana ya nchi yetu.


“Mfano tunafanya mradi mkubwa wa SGR lakini mkandarasi akimaliza akiondoka siku tukitaka kufanya ‘ka extension kadogo hata ka kilometa moja, hatutaweza kwa sababu hatukuweka wakandarasi wetu wapate ujuzi.  Ni kupitia watu wetu kushiriki, ndiyo tungeweza kufanya kama ambavyo baadhi ya nchi zingine duniani zinafanya kujenga uwezo kwa watu wao kwa kitu kinachoitwa ‘Technological Transfer" amesema Katibu Mkuu Chongolo.


Ndugu Chongolo amewahakikishia Makandarasi na Washauri Waelekezi hao wa ndani kuwa CCM itasimamia maslahi yao, kwa kadri ambavyo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025 ilivyoahidi kuwa Chama kitaielekeza Serikali kuhakikisha inaweka mazingira rafiki na bora, ikiwa ni pamoja na kujengewa uwezo wa kupata kazi nyingi zaidi za fedha za Mfuko wa Barabara na kuwawazesha kupata mikopo ili washiriki kikamilifu kwenye miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, madaraja, majengo, maji na mingine mingi.

Katibu Mkuu Chongolo pia aliwataka wazawa hao kutanguliza mbele weledi, uaminifu, kujali rasilimali watu na thamani ya fedha wanapofanikiwa kupata miradi hiyo ya Serikali inayotumia fedha za umma, huku akitoa wito kuwataka waache ubinafsi wa kila mtu kupambana mmoja mmoja katika kutafuta miradi, badala yake watambue umuhimu wa kuungana (Joint Ventures), na wafanye hivyo mapema, si wakati wa kutafuta miradi pekee, ili kujenga kuaminiana katika ubia wa kibiashara wanaokuwa wameingia.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Daniel Godfrey Chongolo

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Daniel Godfrey Chongolo


MFUMO UNGANISHI KUONDOA CHANGAMOTO SEKTA YA ARDHI- PINDA

Written By CCMdijitali on Wednesday, November 22, 2023 | November 22, 2023

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda akizungumza na Menejiment ya Wizara pamoja na Timu ya wataalamu wanaoboresha Mfumo Unganishi wa Kutunza Taarifa za Ardhi jijini Arusha tarehe 22 Novemba 2023.  Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera.



Na Munir Shemweta, WANMM ARUSHA

Serikali imesema Mfumo Unganishi wa Kutunza Taarifa za Ardhi unaoboreshwa na timu ya wataalamu jijini Arusha utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto mbalimbali za sekta ya ardhi nchini.

Mfumo huo unaotarajiwa kuanza katika mikoa mitano ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Tanga utarahisisha na kuharakisha upatikanaji wa huduma za sekta ya ardhi kwa kuwa wananchi watakuwa wakipata huduma kwa njia ya mtandao.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda mkoani Arusha tarehe 22 Novemba 2023 alipokutana na kuzungumza na Menejiment ya Wizara pamoja na Timu ya wataalamu inayooboresha Mfumo huo. 

Amesema, sekta ya ardhi imekuwa na changamoto nyingi lakini hatua ya wizara ya Ardhi kufanya maboresho ya kimfumo kutasaidia kuondoa kero na kelele za wananchi kwenye masuala ya ardhi.

‘’Kikubwa ambacho nimeanza kufarijika ni kwamba ‘mmeadvance’ mpaka hapa mlipofika katika kuboresha mfumo, hongereni sana baada ya muda tutakwenda kumaliza kelele za wananchi wa nchi hii’’ alisema Mhe. Pinda.

Kupitia maboresho ya mfumo huo unganishi wa kutunza taarifa za ardhi changamoto zote za sekta ya ardhi ikiwemo upatikanaji namba ya malipo, malipo ya ada mbalimbali, upatikanaji hati, uthamini pamoja na migogoro ya ardhi zinaenda kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya kimtandao.

Kwa mujibu wa Pinda, itachukua muda kufikia malengo yaliyokusudia katika kuboresha mfumo huo kwa sababu kinachofanyika sasa ni kuwahamisha wananchi kutoka kwenye mfumo waliouzoea na kwenda katika teknolojia mpya.

Hata hivyo, amewatahadharisha wataalamu wanaoboresha mfumo huo pamoja na maofisa wa wizara ya ardhi kuwa makini kutokana na upinzani wanaoweza kuupata kutoka kwa baadhi ya watu aliowaeleza kuwa ni wanufaika wa mifumo ya sasa ambayo wizara ya ardhi inaenda kuachana nayo.

‘’lazima mkawe standby wakurugenzi na maofisa, wale waliokuwa wanakula kupitia mfumo wa kawaida mjue ndiyo ‘threat’ namba moja wao ndiyo watakaoanza kusema mfumo wa ardhi bure kabisa lazima tutengeneze timu ya kuwaattack’’ alisema Pinda.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemera alimueleza Mhe. Pinda kuwa, Menejiment ya wizara imepitia kila hatua ya jinsi mfumo unavyofanya kazi lengo likiwa kufanya maboresho yatakayowezesha idara za wizara hiyo kutekeleza majukumu kwa ufanisi.

‘’Kupitia mawasilisho ya wataalamu tungetamani mfumo ukamilike mapema lakini kwa kuwa kazi hiyo inahitaji utaalamu, tunaamini kazi hiyo itakamilika ndani ya muda mfupi’’ alisema Lucy

Mkurugenzi wa Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi Bw. Flateny Michael Hassan alisema, kufutia wizara ya ardhi kuwa na changamoto kadhaa kwenye mifumo yake imeonekana upo uhitaji wa kuunganisha mifumo yote ili kuwa na mfumo mmoja utakaohusika na sekta ya ardhi.

Amebainisha kuwa, kazi inayofanyika ya kuboresha mfumo kwa sasa imefikia asilimia 75 na ni matarajio yake mapema Januari 2023 mfumo utaanza kutumika katika mkoa wa Arusha kabla ya kuendelea na mikoa mingine.

Ameyataja maboresho yanayoendelea kufanyika kuwa ni pamoja na mfumo unaoruhusu watumishi wa sekta ya ardhi kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi zao, mfumo unaoruhusu wananchi kuomba huduma kwa njia ya mtandao na huduma ya Mobile App ambapo mwananchi anaweza kupata huduma kupitia simu ya kiganjani.

‘’Katika maboresho yanayoendelea, kuna mifumo mitatu wa kwanza ni Back Office unaoruhusu watumishi kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi, wa pili ni Public Portal unaoruhusu wananchi kuomba huduma online na wa tatu ni Mobile App ambapo wananchi wanaomba huduma kupitia simu janja’’ alisema Flateny.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa katika jitihada   mbalimbali za kuhakikisha huduma za sekta ya ardhi zinapatikana kwa urahisi na haraka na uboreshaji mfumo huo pamoja na uwepo wa Klinik za Ardhi ni sehemu jitihada hizo ambazo zinaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wananchi.

--------------------------------MWISHO-------------------------------------


Sehemu ya Menejiment ya Wizara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda (Hayupo pichani).

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemera akizungumza wakati Naibu Waziri Mhe. Geofrey Pinda alipokutana na Menejiment na Timu ya wataalamu wanaoboresha Mfumo Unganishi wa Kutunza Taarifa za Ardhi jijini Arusha tarehe 22 Novemba 2023.

Menejiment na timu ya wataalamu wanaoboresha Mfumo Unganishi wa Kutunza Taarifa za Ardhi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Geofrey Pinda (haupo pichani) alipokutana nao jijini Arusha tarehe 22 Novemba 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)







 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link