CPA MAKALLA: CCM ITAWALETEA WAGOMBEA WASIO NA MAKANDOKANDO

  Na Richard Mwaikenda, Mwanza   Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akiwaahidi wananchi kwa...

Latest Post

Rais Magufuli atunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya wa JWTZ Ikulu DSM

Written By CCMdijitali on Sunday, November 27, 2016 | November 27, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, 
leo tarehe 26 Novemba, 2016 ametunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 194 wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kundi la 59/15 katika viwanja vya 
Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hii ni mara ya kwanza kwa Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni nje ya 
Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kilichopo mkoani Arusha, na ni mara ya kwanza kwa 
Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni ndani ya Ikulu.

Maafisa hao ambao 168 ni wanaume na 26 ni wanawake, wametunukiwa Kamisheni
 katika cheo cha Luteni Usu na sasa wamekuwa Maafisa Wapya wa JWTZ.

Kabla ya kutunuku Kamisheni, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli 
amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Maafisa wanafunzi wa JWTZ na baadaye akashuhudia
uhodari wa askari kutoka kikosi cha maadhimisho cha JWTZ waliofanya onesho la
gwaride la kimyakimya.

Akizungumza baada ya chakula cha mchana katika ukumbi wa Ikulu, Rais na Amiri Jeshi Mkuu 
Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,
Makamanda na Askari wote wa JWTZ kwa jukumu kubwa wanalolitekeleza la
kuhakikisha nchi ipo salama na amesema Serikali itahakikisha inaboresha zaidi
maslai na mazingira ya kazi kwa Jeshi hilo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Aidha, Rais Magufuli amesema ameamua tukio hili la kutunuku Kamisheni lifanyike Ikulu 

Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa heshima kwa Maafisa wa JWTZ kama ambavyo
 Viongozi wengine Serikalini wamekuwa wakipata heshima ya kuapishiwa Ikulu.

"Kwamba Mawaziri tunapotaka kuwaapisha tunawaapishia hapa, Wakuu wa Mikoa tunawaapishia hapahapa, Makatibu Wakuu tunawaapishia hapahapa, kwa nini hawa Maafisa wa Jeshi tusiwaapishie hapahapa kwenye nyumba yao? Nyinyi ndio mnalinda nchi, nyinyi ndio mnasimamia usalama wa nchi hii, lakini nikiuliza hapa inawezekana wengine mpaka wamekuwa Mabrigedia Jenerali hawajawahi kukanyaga Ikulu, wakati hapa ni kwenu"
amesema Rais Magufuli.

Sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi hao zimehudhuriwa na Waziri Mkuu 

Mhe.Kassim Majaliwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi
na Wakuu wa Jeshi la Ulinzi wastaafu na Majenerali wastaafu wa JWTZ.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
26 Novemba,2016

 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati ya kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016

 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride la heshima linaloundwa na Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016

 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati ya kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26,2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26,2016. PICHA NA IKULU

Rais Magufuli atunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya wa JWTZ Ikulu DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, 
leo tarehe 26 Novemba, 2016 ametunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 194 wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kundi la 59/15 katika viwanja vya 
Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hii ni mara ya kwanza kwa Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni nje ya 
Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kilichopo mkoani Arusha, na ni mara ya kwanza kwa 
Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni ndani ya Ikulu.

Maafisa hao ambao 168 ni wanaume na 26 ni wanawake, wametunukiwa Kamisheni
 katika cheo cha Luteni Usu na sasa wamekuwa Maafisa Wapya wa JWTZ.

Kabla ya kutunuku Kamisheni, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli 
amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Maafisa wanafunzi wa JWTZ na baadaye akashuhudia
uhodari wa askari kutoka kikosi cha maadhimisho cha JWTZ waliofanya onesho la
gwaride la kimyakimya.

Akizungumza baada ya chakula cha mchana katika ukumbi wa Ikulu, Rais na Amiri Jeshi Mkuu 
Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,
Makamanda na Askari wote wa JWTZ kwa jukumu kubwa wanalolitekeleza la
kuhakikisha nchi ipo salama na amesema Serikali itahakikisha inaboresha zaidi
maslai na mazingira ya kazi kwa Jeshi hilo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Aidha, Rais Magufuli amesema ameamua tukio hili la kutunuku Kamisheni lifanyike Ikulu Jijini 
Dar es Salaam kwa lengo la kutoa heshima kwa Maafisa wa JWTZ kama ambavyo Viongozi
wengine Serikalini wamekuwa wakipata heshima ya kuapishiwa Ikulu.

"Kwamba Mawaziri tunapotaka kuwaapisha tunawaapishia hapa, Wakuu wa Mikoa tunawaapishia hapahapa, Makatibu Wakuu tunawaapishia hapahapa, kwa nini hawa Maafisa wa Jeshi tusiwaapishie hapahapa kwenye nyumba yao? Nyinyi ndio mnalinda nchi, nyinyi ndio mnasimamia usalama wa nchi hii, lakini nikiuliza hapa inawezekana wengine mpaka wamekuwa Mabrigedia Jenerali hawajawahi kukanyaga Ikulu, wakati hapa ni kwenu"
amesema Rais Magufuli.

Sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi hao zimehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi
na Wakuu wa Jeshi la Ulinzi wastaafu na Majenerali wastaafu wa JWTZ.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
26 Novemba,2016

 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati ya kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016

 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride la heshima linaloundwa na Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016

 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati ya kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26,2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26,2016. PICHA NA IKULU

Mhe. Luhaga Mpina aongoza zoezi la usafi na upandaji miti mjini Singida.

Written By CCMdijitali on Saturday, November 26, 2016 | November 26, 2016

Na Evelyn Mkokoi – Singida.

Katika kutekeleza agizo la Serikali la usafi wa mazingira kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi, wananchi wa Mkoa wa Singida wamejitokeza kwa kwingi katika zoezi hilo lililofanyika kitaifa mwezi huu mkoani humo.

Akishiriki zoezi hilo Mkoani Singida kitaifa, Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida na wana  singida kwa ujumla kwa jitihada walizoonyesha kwani kila eneo la Singida Jumamosi ya leo Limeonekana kuwa nadhifu kabla hata ya muda wa kuanza kufanya usafi tofauti na mikoa mingine ambayo amewahi kushiriki zoezi hilo.

Akiongea na Hadhara iliyojitokeza katika siku ya usafi Mjini Singida Leo, Mpina alisema kuwa usafi wa mazingira  unapunguza magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa kipindu pindu na hivyo taifa likiwa safi litaweza kuokoa ngumukazi yake, na kupunguza gharama ambazo zingetumika kutibu maradhi hayo.

“Ukiona Msichana mzuri barabarani ujue kagharamiwa ukiona kijana mtanashati vilevile ujue kagharamiwa Mkiona taifa zuri na safi ujue limegharamiwa na wananchi wake wamejipanga vizuri, hivyo wana singida Muendelee kujitahidi katika suala zima la usafiwa mazingira.” Alisisitiza Mpina.

Zoezi la usafi wa Mazingira Mkoani Singida lilienda sambamba na zoezi la upandaji miti ambapo, Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki  na wananchi katika zoezi la kupanda miti
mkoani Singida ambapo alipanda mti aina ya mpararachichi katika eneo la stand mpya ya Misuna.

Picha ⬇⬇


 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na wananchi wa Mji wa Singida wakikusanya uchafu katika siku ya Usafi Kitaifa Mjini Singida.

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipeleka uchafu katika kizimba cha uchafu cha soko  kuu la Singida lililoko katika Mtaa wa Ipembe.

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiandaa mche wa mti kitalam kabla ya kuupanda katika zoezi la usafi na upandaji miti mjini Singida.

Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina Akipanda Mti aina ya Mparachichi katika eneo la Misuna Stand Mpya Mjini Singida leo katika Zezi la usafi wa mazingira Kitaifa. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA JENGO LA UMOJA WA MATAIFA LIKALOTUNZA KUMBUKUMBU ZA MAHAKAMA YA UMOJA WA MATAIFA ZA MAUAJI YA RWANDA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,amezindua majengo ya ofisi za Umoja wa Mataifa zitakazotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua majengo hayo kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kudumisha mahusiano.

Majengo hayo yamejengwa katika eneo la Laki laki mkoani Arusha baada ya
Serikali ya Tanzania kuipatia Umoja wa Mataifa eneo lenye ukubwa wa ekari 16.17 bure kwa ajili ya kujenga hayo ya kihistoria hapa nchini.

Tanzania inaomba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kusaidia kupatikana kwa
wote waliohusika na mauaji hayo ya kimbari ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wahanga wa mauaji hayo.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa litakalotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa litakalotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Mahakama hiyo wakati ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa litakalotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha,kutoka kushoto ni John Hocking (Msajili MICT ), Theodor Meron (Rais wa MICT ) , Miguel de Serpa Suares (Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Taifa katika masuala ya kisheria ) ,kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt.Augustine Mahiga, Mkuu wa mkoa wa Arusha mhe. Mrisho Gambo,Serge Brammertz (Mwendesha Mashitaka wa MICT ) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Mohamed Chande Othman (kulia)

.......................................................................


MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA KIWANDA CHA A TO Z MKOANI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuviimarisha vyuo vya ufundi stadi nchini –VETA- ili viweze kutoa wahitimu bora ambao watakidhi katika soko la ajira hasa kwenye viwanda vilivyopo na vitajengwa nchini.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na uongozi wa kiwanda cha A to Z kilichopo mkoani Arusha katika ziara yake ambayo
imeingia siku ya Pili ya kutembelea viwanda mbalimbali mkoani humo ili kujua changamoto zinazokabili viwanda hivyo na serikali kuzitafutia ufumbuzi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imetenga fedha za kutosha zitakazotumika kuviimarisha vyuo vya Veta ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayosidia vijana kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu pindi watakapoajiriwa au kujiajiri wenyewe.

Kuhusu maslahi kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha A to Z,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kulinda na kutetea haki za wafanyakazi kwa kutoa maslahi mazuri ambayo yatawezesha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii.

Makamu wa Rais pia amesisitiza usawa katika ulipaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa ndani na wa nje ya nchi walioajiriwa kwenye kiwanda hicho ili kuondoa tofauti za mishahara hali ambayo ijenga motisha kwa wafanyakazi.Kiwanda cha A to Z kilichopo eneo la Kisongo mkoani Arusha ambacho kinatengeneza vyandarua, nguo na mifuko mbalimbali ikiwemo ya saruji kimeajiri zaidi ya wafanyakazi 7500 ambapo asilimia 80 ya wafanyakazi wote ni wanawake.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wawekezaji kote nchi walipe kodi za serikali mapema kodi ambazo zitatumika kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania itaendelea kujenga na kuimarisha mazingira bora kwa wawekezaji ili kuhakikisha wawekezaji wanafanyakazi zao vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa na ya wawekezaji.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiangalia nguo zinazotengenezwa na Kiwanda cha A to Z. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Kalpesh Shah, na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo. Makamu wa Rais amefanya  ziara kwenye kiwanda hicho ikiwa sehemu ya kutambua mchango wa wawekezaji wa ndani na changamoto wanazokutana nazo ili kupata majibu ya kurahisisha kufanikisha Tanzania mpya ya Viwanda. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akitembezwa  Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Kalpesh Shahkatika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Kalpesh Shah akipata maelezo ya namna kiwanda cha A to Z kinavyofanya utafiti wa kupambana na wadudu wanaoharibu mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha utafiti cha Africa Technical Research Centre Dkt.Johson Ouma Odera. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia afungua awamu ya 3 ya Uhawilishaji wa Kaya Masikini - Arusha

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia amefungua awamu ya tatu ya uhawilishaji wa Kaya Maskini kupitia Mpango wa Tasaf – III unaoendelea katika Mitaa ya Jiji la Arusha.

Akiongea na wananchi wa Mtaa wa Lolovono, Olmokeya, Madukani na Muriet, Mkurugenzi Kihamia amesisitiza matumizi bora ya Fedha za Tasaf kwa kuanzisha miradi midogo midogo itayowawezesha kuongeza kipato chao na hatimaye kujikwamua kwenye umasikini.

Mpango huu unahusisha Mitaa 70 na Kaya 5377 za Jiji la Arusha.
Kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 kiasi cha Fedha ni kilichotolewa ni Tsh Mil 612.












Hukumu ukatili kwa wanawake, watoto kuharakishwa

Habari Leo 

SERIKALI imeanzisha utaratibu wa kuharakisha kesi zinazohusu unyanyasaji na ukatili wa wanawake na wasichama wadogo ili hukumu zitolewe mapema na wahusika watakaokutwa na hatia wafungwe haraka.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati akizungumza baada ya matembezi yaliyoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo (WiLDAF), na mashirika ya kutetea haki za binadamu, ikiwa ni kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza jana hadi Desemba 10.

Waziri Ummy alisema serikali haiwezi kuendelea kuvumilia kuona wanaume wakijihusisha na mapenzi na wasichana wadogo wakati wakiwaacha wanawake wakubwa.

Alisema ingawa sheria imerekebishwa na kuwa kali lakini bado kesi za matukio hayo zimekuwa zikichukua muda mrefu hivyo kuwanyima haki watu waliotendewa matukio ya udhalilishaji wa kingono ama ukatili.

Ummy alisema serikali imeamua kuanzisha utaratibu wa kuharakisha kesi hizo zinapofikishwa kwenye madawati ya jinsia polisi na mahakamani ili hukumu zitoke mapema.

Mratibu wa WiLDAF, Dk Judith Odunga, alisema takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa watoto wa kike wanaacha shule kabla ya kupevuka huku watoto wa kike wakikatisha masomo yao wakiwa shule za sekondari kuliko wa kiume.

Alisema mazingira yasiyo salama kwa shule yana madhara makubwa na kwamba watoto wanapokuwa shule na kufanyiwa ukatili wakingono wako katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya Ukimwi.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Maria Karadenizi alisema matukio ya ukatili dhidi ya wanawake yako kwenye mataifa mbalimbali duniani na jitihada zinahitajika kwa ajili ya kuyamaliza.




Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiongea katika uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni  Mkurugenzi wa  WiLDAF Dkt.Judith Odunga ,Balozi wa Ireland nchini Bw.Paul Sherlock(wa tatu kushoto), na Kamanda wa Polisi kanda maalum ACP Lucas Mkondya.
  Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt.Judith Odunga akitoa neno la ufunguzi katika  uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu na ni  Mratibu Mkazi kutoka Umoja wa Mataifa nchini Bi.Maria Karadenizli 



Balozi wa Ireland nchini Bw.Paul Sherlock akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.kulia kwake ni  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na  Watoto Mhe.Ummy Mwalimu, Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt.Judith Odunga, Kamanda wa Polisi kanda maalum ACP Lucas Mkondya na Mkuu wa Dawati la Jinsia,ACP Mary Nzoki.
Waandamaji kutoka Taasisi na Asasi mbalibali  wakionyesha ujumbe mbalimbali unaopinga ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisaini katika ubao wenye kauli mbiu katika uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Video ⏩⏩


Mhe.Seleman Said Jafo aongea na Walimu wa Shule ya Sekondari Segera,Wilayani Handeni

Serikali imewataka maafisa elimu kupanga muda wa kusikiliza kero za walimu na kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza morali ya walimu kufundisha. Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Seleman Said Jafo alipokuwa 
akiongea na walimu wa shule ya sekondari Segera iliyopo 
wilayani Handeni, wakati wa ziara ya kiserikali
Wilayani Handeni na Mkoa wa Tanga.

Mhe.Jafo alisema kuwa wapo baadhi ya Maafisa elimu ambao
wanajifanya kuwa ni Miungu watu linapokuja suala la kusikiliza na
kutatua kero za walimu. Waziri Jafo alisema “Wapo walimu wanaotembea
umbali mrefu kufuata huduma makao makuu ya Halmashauri kwa wakubwa wao mara nyingi wameshindwa kutatuliwa kero zao hali inayopelekea usumbufu, Kuanzia leo 24/11/2016 napiga marufuku tabia hiyo”.

Aliongeza msisitizo kuwa Maafisa elimu wapo kwa lengo la kuwasikiliza walimu na kuwasaidia kutatua kero zao ili waweze kujikita katika ufundishaji wa wanafunzi. Alisema kuwa walimu ni watu muhimu sana nchini ila wamekuwa wakikatishwa tamaa na utendaji wa baadhi ya
maafisa elimu. Aliongeza kuwa kero kubwa ya walimu ni
kutokupanda madaraja kwa wakati na kutopata stahiki zao ikiwa ni
pamoja na posho za likizo,uhamisho na madai Mengine.

Wakati huohuo, Naibu Waziri aliiagiza Halmashauri ya
Wilaya ya Handeni kukamilisha miradi yote ya SEDP-II ambayo
haijakamilika kuhakikisha inakamilika kabla au ifikapo tarehe
20/12/2016. Alisema kuwa katika kusimamia miradi hiyo na miradi ya
maendeleo kwa ujumla kila mtu lazima atimize wajibu wake na kuhakikisha
fedha iliyotengwa na kutolewa inatumika vizuri na thamani yake kuonekana
kwa muda mrefu (value for money).

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Said Jafo akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari Segera, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Wiliam Makufwe na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe.

 Picha ya pamoja ya Mhe. Selemani Said Jafo na waalimu wa shule ya sekondari ya Segera. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni akitoa utambulisho mfupi kwenye ukumbi wa Halmashauri.

 Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

Viongozi wakisikiliza kwa makini maagizo ya Naibu Waziri ikiwa ni pamoja na kuwa na usimamizi bora wa rasilimali fedha

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU APOKEA VIFAA VYA MACHO VYENYE THAMANI YA MILIONI 320

Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii.

WIZARA ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto imepokea vifaa vya huduma za macho vyenye thamani ya milioni 321, 234,002 kutoka kwa Shirika la Christian Blind Blind Mission kupitia benki ya Standard Chartered kupitia mradi wa "Seeing is Believing, Child Eye Health" jijini Dar es salaam.

Akipokea misaada hiyo, Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu ameshukuru kwa msaada huo kwani kupata vifaa hivyo vitasaidia katika uboreshaji wa afya ya macho hususani kwa watoto ambapo vitazuia ulemavu wa kutokuona.

Ummy amesema kuwa, vifaa hivyo vitaboresha huduma za macho na jamii nzima itanufaika kwa uwepo wa vifaa hivi kwani matumizi yake hayataishia kwa watoto tu bali hata watu wazima wanaokabiliwa na matatizo ya macho.

"vifaa hivi vitasambazwa katika sehemu tofauti nchini na vitawalenga watu wote sio watoto tu, hii ni kutokana na kutaka kupunguza athari za magonjwa ya macho kwani hupelekea kuleta ulemavu kwani kulingana na mahitaji kuwa mengi husuani kwa watoto huduma hizi hazijafikia kiwango kinachoshauriwa na Shirika la Afya duniani,"amesema Ummy.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Sanjay Rughani amesema kuwa wametoa vifaa hivyo kwa ajili ya kuwasaidia watu wote wenye matatizo ya macho wakiwemo watoto kwani wanaamini kuwa macho ni kiungo muhimu sana kwa binadamu.

Vifaa hivyo ambavyo vitagawanywa sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali na Mikoani kama Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Rufaa ya kanda Bungando,Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya,Hospitali za Rufaa za mikoa ya ilala,Kinondoni,temeke,Mbeya,Rukwa,manyara,Tabora,Mwanza na Halmashauri za miji ya mbeya na babati pamoja na Halmashauri za Wilaya za Babati, Mbulu, Simanjiro,Kiteto,Igunga,Sikoine na Nzega.

 Waziri wa Afya, MaendeleoyaJamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu wa pili kulia akipokea Dubini ya kufanyia operesheni ya macho kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Standard Chartered Bw. Sanjay Rughani watatu kushoto wakati wa kukabidhi vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 320 leojijini Dar es salaam, wa kwa kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wizara Dkt. Mohammed Mohammed.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Kifaa cha uchunguziwa macho Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa Dkt. Daisy Majamba kulia wakati wa kukabidhiana vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 320 leo jijini Dar es salaam.

Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu kulia akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kukabidhiana vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 320 leo jijini Dar es salaam.

 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link