Comoro kushirikiana na Tanzania katika sekta za kimkakati asema Rais Azali Anena
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazumgumzo na Rai...
RAIS DK.MWINYI ASEMA ZANZIBAR KUWA KIVUTIO CHA KIJANI NA UTALII ENDELEVU
Written By CCMdijitali on Wednesday, September 27, 2023 | September 27, 2023
Zanzibar,
27 Septemba, 2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametoa rai kwa wadau wa kilimo kuendelea kuliimarisha tamasha la Kilimo Hai liwe kubwa zaidi na endelevu ili kuwavutia watalii.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipofungua tamasha la kwanza la Kilimo Hai kwenye viwanja vya maonesho ya kilimo, Kizimbani Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema, mwezi Febuari mwaka huu kwenye maadhimisho ya siku ya utalii duniani, Serikali ilizindua azimio la utalii endelevu lililoazimia kuitangaza Zanzibar kuwa kivutio cha kijani na kuzitaka hotel zote za utalii nchini zitumie mazao ya Kilimo Hai na kuweka vyakula vya asili ya Zanzibar.
Pia alieleza azma ya Serikali kwa hoteli hizo za kitalii kuona uchakataji wa taka unatengenezewa kuwa malighafi endelevu na kutunza mazingira na kuongeza kuwa Serikali haina budi kuendelea kuchukua hatua ya kutimiza asili ya Zanzibar na kuhakikisha watalii wanaokuja Zanzibar wanaendelea kufahamu utamaduni wa Zanzibar.
Dk. Mwinyi pia alipongeza shughuli za uzalishaji na utengenezaji wa vitu vya asili ikiwemo ufinyanzi wa vyungu, kudarizi vikoi, ushonaji kofia za asili, matumizi ya mapakacha na masusu, mikoba ya ukili na mikeka kwa sehemu kubwa vinaendana na sera ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kusaidia kukuza uchumi.
Aliongeza, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wa sekta hiyo, tayari wamemaliza rasimu ya mikakati ya Kilimo Hai kwa Zanzibar na kueleza maeleza matumai yake ya utekelezaji wa mikakati hiyo, itakuwa suluhisho la changamoto za sekta ya Kilimo Hai inayokabiliana nazo ikiwemo pembejeo za kibaolojia, elimu kwa wakulima na wafugaji pamoja na upatikanaji wa masoko ndani na nje ya nchi.
Dk. Mwinyi, alibainisha kuwa Serikali inafamu fursa zilizomo ndani ya Kilimo Hai na kueleza dhamira yake endapo mkakati ulioandaliwa ukatengenezewa programu madhubuti na utekelezaji utakaowapa fursa vijana kuanzisha biashara za kutengeneza viatilifu na mbolea hai kwa kusaidia upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi na kuitangaza Zanzibar kama kivutio cha kijani.
Akizungumzia matumizi ya mbolea za kemikali kwenye utoaji wa elimu kwa watumiaji na walaji, Rais Dk. Mwinyi alieleza haja ya kuifahamisha jamii kuhusu faida kwenye kuimarisha lishe ili kusaidia kupunguza maradhi yasiyoambukiza kama presha, kisukari na moyo.
Hata hivyo, alieleza uhalisia wa tamasha hilo unaonekana pia kwenye shughuli nyengine za ujasiriamali.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Kilimo Shamatta Shaame Khamis alieleza azma ya Wizara hiyo inavyoendeleza jitihada za Serikali kushirikiana na taasisi zote zilizomo Zanzibar zinazojishughulisisha na sekta ya kilimo kwa ujumla wake na kueleza mafaniko waliyofikia.
Alisema, Serikali pia inatoa huduma kwa wakulima wanaozalisha mazao kwa kutumia mbolea za kemikali na kuwapa elimu ya namna bora ya kutumia pamoja na kuishajihisha jamii namna bora ya kutumia viatifu kwaajili ya kuendeleza uzalishaji maalumu.
Naye, Mwakilishi wa Jimbo la Bububu, Mudrik Ramadhan Soraga alieleza fursa za wanchi wa jimbo hilo hasa kwa Shehia za Dole na Kizimbani wanavyonufaika na fursa za Kilimo Hai na kueleza wanavyojikita kwenye kilimo cha spices na mbogamboga kwa kutumia mbinu bora za kilimo chenye tija kwa afya.
Mwenyekiti wa taasisi ya Zanzibar Organic Initiativie (ZOI) Dk. Mwatima Abdala Juma alisisitiza haja kwa wakulima na jamii kwa ujumla kuendelea kukiimarisha Kilimo Hai ili kuimarisha afya za watu na afya ya udongo kwa kuepuka matumizi ya mbolea zenye kemikali.
IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR
WAZIRI BYABATO AHIMIZA KASI NA UFANISI WA PROGRAMU NA MIRADI INAYOTEKELEZWA JIJINI MWANZA KUPITIA LVBC
Written By CCMdijitali on Tuesday, September 26, 2023 | September 26, 2023
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki amewataka watendaji na wasimamizi wanaosimamia utekelezaji wa programu na miradi mbalimbali katika jiji la Mwanza kupitia Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (Lake Victoria Basin Commission –LVBC) kuhakikisha inatelezwa kwa kasi na ufanisi ili iwanufaishe wananchi wenye uhitaji.
Naibu Waziri Byabato amebainisha hayo wakati akiendelea na ziara ya kikazi ya ukaguzi wa ufanisi wa programu na miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa kupitia LVBC.
“Nitoe rai kwenu watendaji na wasimamizi wote wa miradi hii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa katika Kanda ya Ziwa kupitia LVBC kuhakikisha sote kwa umoja wetu tunafanya kazi usiku na mchana kutimiza adhma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kuona Wananchi wa Tanzania wananufaika moja kwa moja na fursa zinazotokana na Jumuiya kijamii na kiuchumi”.alisema Mhe. Byabato
Akiwa jijini Mwanza tarehe 26 Septemba 2023 Naibu Waziri Byabato ametembelea mradi wa ujenzi wa miundombinu ya majitaka na usafi wa mazingira chini ya programu ya pamoja ya usimamizi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji (Lake Victoria Basin Integrated Water Resources Management Programme LVB – IWRMP) katika eneo la Pasiansi. Progamu hii inalenga kuchangia katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji ya Ziwa Victoria ili kuongeza ubora na upatikanaji wake kwa matumizi mbalimbali, ikihusisha usambazaji wa majisafi kwa kaya zilizopo maeneo ya milimani na ujenzi wa miundombinu ya majitaka na vyoo vya kisasa. Maeneo mengine yanayotarajia kunufaika na programu hiyo katika Jiji la Mwanza ni pamoja na Kitangiri, Mabatini, Kirumba na Nyamanoro.
Sanjari na hayo kupitia utekelezaji wa mradi huu wa kupanua miundombinu ya majitaka katika Jiji la Mwanza wenye thamani ya shilingi bilioni 12.7 kutaweizesha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kukarabati na kupanua mtandao wake wa majitaka kwa takriban 14.4km na kuunganisha kaya 1,600 kwenye mtandao huo.
Programu na Miradi mingine aliyozitembelea Mhe. Byabato jijini Mwanza ni pamoja na; ujenzi wa Makao Makuu ya Kituo cha Uratibu wa Utafutaji wa Uokozi katika Ziwa Victoria (Maritime Rescue Coordination Centre – MRCC), Ukarabati wa Meli ya Utafiti ya Jumuiya (RV Jumuiya) iliyopo Ziwa Victoria katika Bandari ya Mwanza Kusini unaofanywa na Kampuni ya kitanzania ya Mundao Engineering na eneo la Machinjio lililopo eneo la Nyakato ikiwa ni sehemu ya Programu ya Usimamizi wa Mazingira katika Ziwa Victoria
Katika hatua nyingine Wananchi wa Pasiansi kwa nyakati tofauti wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa kuvutia utekelezaji wa mradi wa kupanua miundombinu ya majitaka katika Jiji la Mwanza ambao wameutaja kuleta mageuzi makubwa katika utunzaji wa mazingira na upatikanaji wa maji safi.
“Hapo mwanzoni kabla ya kufikiwa na mradi huu sisi tunaoishi maeneo ya huku chini ya mlima tulikuwa tunaathiriwa sana na uchafu kutoka kwa wenzetu wanaoishi huko mlimani, tunaishukuru sana Serikali kwa kutekeleza mradi huu ambao umemaliza kabisa tatizo hilo, kwa sababu kila kaya imepata choo bora sambasamba na mifumo ya majitaka iliyo imara”. Alieleza Mzee William Mchomvu mkazi wa Pasiansi.
Hii ni ziara ya kwanza kwa Naibu Waziri Byabato toka ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa wa Naibu Waziri anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Katika ziara hiyo Naibu Waziri Byabato ameambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Mhandisi Abdillah Mataka katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria yenye Makao Makuu yake mjini Kisumu, Kenya ilianzishwa na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Itifaki iliyosainiwa tarehe 29 Novemba, 2003. Jukumu la Kamisheni hiyo ni kuratibu usimamizi endelevu wa Bonde la Ziwa Victoria ikiwemo utekelezaji wa Miradi ya Mazingira, Miundombinu ya Kiuchumi na Kijamii katika Bonde la Ziwa Victoria kwa manufaa ya Nchi Wanachama hususan zinazopakana katika Bonde hilo ambazo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kenya, Jamhuri ya Rwanda na Jamhuri ya Uganda.
Kamisheni hii inaongozwa na Katibu Mtendaji ambapo kwa sasa nafasi hiyo inashikiliwa na Dkt. Masinde Bwire kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MAKAMU WA PILI AZINDUA MRADI WA - ZANZIBAR
Kuwepo kwa mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya lazima Zanzibar (ZIQUE) pamoja na miradi mengine kumeleta mafanikio makubwa ikiwemo kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia yaliyopelekea kuimarika kwa ufaulu kwa wanafunzi katika mitihani yao ya Taifa hasa katika masomo ya Sayansi.
Akizundua Mradi wa ZIQUE huko katika Viwanja vya Skuli ya Msingi ya Salim Turkey Mpendae, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Miradi hii imesaidia sana kufikisha na kuboresha huduma ya elimu katika maeneo mbali mbali nchini yakiwemo katika visiwa vidogo vidogo Unguja na Pemba ambapo kasi ya ufaulu kwa mitihani ya kidato cha nne imeongezeka na kufikia asilimia 72.2 kwa mwaka 2022.
Ameeleza kuwa uwepo wa vituo vya ubunifu wa kisayansi na kutolewa mafunzo kwa walimu hasa wa masomo ya Sayansi, Hisabati na Kingereza kumechangia sana kuimarika kwa ubora wa elimu inayotolewa nchini.
Aidha Mhe Hemed amefahamisha kuwa kutokana na kasi ya uimarishaji wa miundombinu ya Elimu matarajio ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa tatizo la uhaba wa nafasi kwa Wanafunzi kuingia Skuli Awamu mbili linakwenda kumalizika na kutoa nafasi kwa wanafuzi wa Zanzibar kusoma kwa Awamu mmoja tu.
Mhe. Hemed ameeleza kuwa Mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya lazima Zanzibar umelenga pia kuwajengea uwezo zaidi walimu ili kuimarisha ufanisi wa kazi zao katika kusomesha kwa kufuata mitaala ya umahiri (CBC) na kuwasihi walimu kushiriki ili kwenda sambamba na mitaala inayozingatia umahiri na kupelekea wanafunzi kufanya vizuri zaidi kwa maendeleo yao, jamii na Taifa kwa ujumla.
Sambamba na hayo ameutaka uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kusimamia vyema utekelezaji wa Mradi huo na miradi Mengine sambamba na kuwataka wananchi kuendelea kuitunza miundombinu inayojengwa na Serikali ili iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.
Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa amemuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa mradi wa ZIQUE utatekelezwa kwa makubaliano waliyokubaliana na Benki ya Dunia na utakamilika ndani ya miaka mitatu badala ya miaka sita ya makubaliano ya awali.
Waziri Lela amefahamisha kuwa Wizara ya Elimu imejipanga kumyanyua mtoto wa kike hasa katika masomo ya Sayansi na kuongeza ubora na kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa Zanzibar.
Akitoa maelezo ya mradi huo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Ndg. Khamis Abdulla Said amesema mradi wa ZIQUE utaboresha elimu ya lazima na mfumo wa elimu kwa kuzalisha wanafunzi wenye ujuzi, maarifa, mafunzo ya walimu kazini, matumizi ya Teknolojia na kupitia mitaala ya Vyuo vya Ualimu ili mitaala hiyo iendane na ufundishaji wa kidijitali.
Amesema kuwa Wizara ya Elimu imejipanga kuvifanyia ukarabati Vyuo viwili vya Ualimu kwa Unguja na Pemba sambamba na kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa Takwimu na matumizi yake pamoja na uwajibikaji kwa Watendaji wa Wizara ya elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa amesema mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya lazima Zanzibar utaondoa changmoto ya katika sekta ya elimu na kuhakikisha Wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia Tanzania Bw. Nathan Balete kwa kuzingatia umuhimu wa Elimu ndiko kulikoifanya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzindua mradi wa ZIQUE ili kusaidia uboreshaji wa miundombinu elimu ya lazima, kukuza mazingira ya kujifunzia na kufundishia na kuimarisha matumizi ya Teknolojia Maskulini.
Amesema Benki ya Dunia ipo tayari kufanya kazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuhakikisha mradi wa ZIQUE na miradi mengine inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kutoa matunda chanya yaliyokusudiwa.
……………………
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
26 Septemba,2023
Gunmen kill 14, kidnap 60 in attacks in northern Nigeria
Written By CCMdijitali on Monday, September 25, 2023 | September 25, 2023
By Ahmed Kingimi
September 24, 20239:52 PM GMT+3
MAIDUGURI, Nigeria, Sept 24 (Reuters) - Gunmen in Nigeria killed eight people on Sunday and abducted at least 60 others in two communities of northwest Zamfara state, residents and a local traditional leader said, two days after armed men kidnapped dozens from a university in the state.
Elsewhere, in the northeast of the country suspected Islamist insurgents ambushed a convoy of vehicles under military escort, killing two soldiers and four civilians, said a police source and a motorist who witnessed the attack.
The attackers set fire to five vehicles and drove off with one truck, the witness said.
President Bola Tinubu is yet to spell out how he will tackle widespread insecurity. His economic reforms, including the removal of a costly fuel subsidy and freeing the naira currency, have increased the cost of leaving, angering citizens.
Residents said gunmen early on Sunday tried to attack a forward army base in a rural Magami community of Zamfara, but were repelled. Zamfara is one of the states worst affected by kidnappings for ransom by armed gangs known locally as bandits.
The attackers set fire to five vehicles and drove off with one truck, the witness said.
President Bola Tinubu is yet to spell out how he will tackle widespread insecurity. His economic reforms, including the removal of a costly fuel subsidy and freeing the naira currency, have increased the cost of leaving, angering citizens.
Residents said gunmen early on Sunday tried to attack a forward army base in a rural Magami community of Zamfara, but were repelled. Zamfara is one of the states worst affected by kidnappings for ransom by armed gangs known locally as bandits.The gunmen in three groups attacked the army base and the communities of Magami and Kabasa, said a traditional leader who declined to be named for security reasons.
He said 60 people, mostly women and children, were kidnapped.
"The bandits rode many motorcycles with guns and other weapons (and) were shooting sporadically," Shuaibu Haruna, a resident of Magami, told Reuters by telephone.
Four people were killed during the attack, said Haruna, who attended their burial.
Isa Mohd from Kabasa community said four people were also killed and dozens of others kidnapped.
Police and army did not respond to requests for comment.
Attacks in the northwest are part of widespread insecurity in Nigeria. Islamist fighters still carry out deadly attacks in the northeast, gangs and separatists attack security forces and government buildings in the southeast, and clashes involving farmers and herders continue to claim lives.
Reporting by Ahmed Kingimi in Maiduguri; Writing by MacDonald Dzirutwe; Editing by David Holmes
ZIARA YA MAKAMU WA PILI KOJANI ZANZIBAR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema kukamilika kwa ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Ghorofa Kojani kutasaidia kuboresha sekta ya elimu kisiwani humo kutaondoa changamoto ya uahaba wa madarasa, walimu na vifaa vya kusomea na kusomeshea.
Akikagua jengo hilo linaloendelea kujengwa katika kisiwa cha Kojani Mhe. Hemed amesema katika kuhakikisha Sekta ya Elimu inaimarika katika Kisiwa cha Kojani Serikali itaajiri Walimu wazawa ambao watafundisha kwa ari na upendo ili kutatua changamoto ya uhaba wa Walimu Kisiwani humo.
Amesema kukamilika kwa Skuli hiyo wanafunzi watapata fursa ya kusoma katika mazingira mazuri pamoja na kuwa na vifaa kwa kisasa vitakavyowasadia kupata ujuzi wa masomo wanayopatiwa.
Amewanasihi Wazazi na Walezi katika Kisiwa cha Kojani kuachana na tabia ya kuwakatisha Masomo Wanafunzi wa Kike na kuwazesha badala yake wawahimize katika kusoma ili kupata Wataalamu wa fani mbali mbali ambao watasaidia katika kukiletea maendeleo kisiwa hicho na Zanzibar kwa ujumla.
Aidha Mhe. Hemed amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetenga shilingi Bilioni ishirini kwa ajili ya kuboresha Miundombinu ya Afya na kuwaahidi wananchi wa Kojani kuwa kituo cha Afya kipya kitajengwa na huduma zote stahiki zitapatikana katika Kituo hicho.
Amemalizia kwa kuwataka Wananchi wa Kojani kutoa ushirikiano katika ujenzi huo wa Skuli ya ghorofa na miradi mengine ya maendeleo itakayojengwa katika Kisiwa hicho ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Nane ya kuwaletea maendeleo Wananchi wake.
Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa ameeleza kuwa Jengo la Skuli ya Msingi Kojani litakuwa na huduma mbali mbali na limezingatia miundombinu ya Wanafunzi wenye mahitaji maalum ili nao wapate elimu ya lazima.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali imeona umuhimu wa kujenga Skuli hiyo ya ghorofa na tayari kuna mpango wa kujenga Skuli nyengine eneo la Makaani na kutoa elimu ya ufundi hasa uvuvi wa kisasa ili wanafunzi watakapohitimu masomo yao waweze kujiajiri kupitia sekta ya uvuvi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndg. Khamis Abdallah Said ameeleza kuwa Wizara inatenga fedha za kutosha ili watoto wasome bure na kutoa Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu ili waje kuisaidia Serikali.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kisiwa cha kojani Sheikh Suleiman Salim Hamad amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwafikishia huduma mbali mbali ikiwemo ujenzi wa Skuli za ghorofa hali ambayo itasaidia wanafunzi kuvuka na kufuata elimu maeneo jirani.
…………………
Imetolewa na Kitengo cha habari (OMPR)
25/09/2023
WAZIRI SILAA ATAKA WANANCHI KULINDA MAENEO YA WAZI
Na Munir Shemweta, WANMM
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amewataka wananchi kuyalinda na kuyaendeleza maeneo ya wazi kulingana na matumizi yaliyopangwa.
Silaa ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo ya wazi Mbweni jijini Dar es Salaam.
"Niwatake watanzania wengine wote wanaokaa katika maeneo ya wazi wayaprotect, yako maeneo Mwananyamala yamegeuzwa gerage, yapo mengine yamegeuzwa sehemu ya kutupa takataka hatuwezi kuwa na miji ya namna hiyo" alisema
Kwa mujibu wa Waziri Silaa, ni lazima mamlaka za kusimamia mipango miji na ardhi pamoja wananchi kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao katika kuyalinda na kuyaendeleza maeneo ya wazi.
Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi amesema, anayo orodha ndefu ya maeneo ya wazi yaliyofunguliwa biashara na asingependa maeneo hayo yakitumika kibiashara.
Ametaka watanzania wote kwa ujumla kuwa walinzi namba moja wa maeneo ya wazi ambapo alifafanua kuwa, zipo 'open space' nyingi leo hazipo na watu huanza kidogo kidogo kujenga ama biashara kwenye maeneo hayo.
Amezitaka halmashauri zote nchini kuendelea kuhamamisha wananchi kuyalinda na kuyaendeleza maeneo ya wazi kulingana na mipango iliyopo.
Ziara ya Waziri Silaa kukagua maeneo ya wazi Mbweni Dar es Salaam ni moja ya jitihada zake za kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa wakati akianza kuhudumu Wizara ya Ardhi ya kutaka maeneo yote ya wazi kubaki wazi ndani ya siku mia moja.
------------MWISHO---------
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa akisisitiza jambo mbele ya wakazi wa Mbweni alipokwenda kukagua maeneo ya wazi Mbweni Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. |
RAIS SAMIA AZIDI KUONESHA HURUMA YAKE KWA WANANCHI
Written By CCMdijitali on Friday, September 22, 2023 | September 22, 2023
RAIS SAMIA AZIDI KUONYESHA HURUMA YAKE KWA WANANCHI
· Aelekeza wananchi waliovamia Bwawa la Mindu kupatiwa viwanja
· Waziri Slaa ahitimisha migogoro ya ardhi Morogoro usiku
Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza wananchi 357 wa kata ya Mindu mkoani Morogoro waliovamia eneo la hifadhi ya bwawa la Mindu mita 500 kupatiwa viwanja.
Uamuzi huo unafuatia mgogoro wa muda mrefu baina ya wananchi na serikali kufuatia Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kutaka wananchi hao kuondolewa ili kulinda chanzo hicho cha maji.
Akizungumza na wananchi hao tarehe 22 Septemba 2023 wakati wa akifuatilia utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri, Silaa amesema, madai ya wananchi kuwa umbali wa mita 500 ulioanishwa kulinda eneo la bwawa la Mindu hayana ukweli kwa kuwa lengo la serikali si kujipatia eneo bali kulinda chanzo hicho cha maji.
‘’Ingelikuwa tunapima halafu tunawaondosha wananchi na kugawana viwanja, kimoja RC, kingine DC na kamishna tungesema tunawabana ili tupate maeneo, tunapima kulinda bwawa ambalo mimi si mkazi wa eneo hili tunalinda bwawa hili kwa faida wa wana morogoro mkiwemo ninyi’’ alisema.
Akielezea zoezi la uthamini lililofanyika, Waziri Silaa amesema hilo lilikuwa zoezi maalum ambalo lilibaini wananchi walioko ndani ya mita 500 wako kwenye eneo la hifadhi la bwawa la Mindu na kubainisha kuwa hapo ndipo linapokuja suala la haki halali na ile haramu.
‘’Fidia ya hapa si fidia ya compasation iliyotokana na mtu aliyechukuliwa ardhi yake yenye mali ndani yake bali ni fidia iliyotokana na busara, hekima na huruma ya Rais. Tungelifuata Maamuzi ya Baraza la Mawaziri la tarehe 23 Sept 2019 maana yake mkuu wa wilaya angeagizwa kufikia tarehe fulani kila mtu aondoke’’ alisema Silaa.
Kwa mujibu wa Waziri Silaa, fidia kwa wananchi waliovamia eneo la hifadhi ya bwawa la Mindu haipo lakini kwa mujibu wa wataalamu wa ardhi wananchi 357 ndiyo wanaopaswa kulipwa kifuta jacho ikiwa ni huruma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kama mkono wa heri kuwasaidia kuhamisha mali zao.
Hata hivyo, alisema baada ya kufanya mawasiliano na Rais Samia Suluhu Hassan alimuelekeza amuambie Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro awapatie viwanja wananchi wanaopisha uhifadhi wa eneo la bwawa ili waweze kujenga nyumba za kuishi.
Awali Diwani wa Kata ya Mindu mkoani Morogoro Zuberi Mkalaboko alimueleza Waziri wa Ardhi kuwa, wananchi wa eneo hilo hawana tatizo la kupisha uhifadhi wa bwawa isipokuwa kero zao kubwa ni tatu alizozitaja kuwa, ni ushirikishwaji, vipimo vilivyofanywa na wataalamu wa ardhi pamoja na fidia wanayotaka kulipwa wananchi hao.
‘’Mhe Waziri, kero za wananchi wa Mindu ni maeneo matatu, kwanza ushirikishwaji, pili fidia inayolipwa na tatu vipimo vilivyofanywa na wataalamu hawa’’ alisema Diwani Mkalaboko.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mbali na kutembelea eneo la Mindu na CCT-Forest alihitimisha ziara yake ya siku moja mkoani Morogoro kwa kutembelea kata ya Chamwino eneo lenye mgogoro la Pombe Shop ambapo ilimlazimu kuutatua mgogoro wa eneo hilo usiku ambapo aliuhitimisha kwa kumuelekeza Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro kuwatafutia viwanja wananchi 57 kuondoka kwa hiari kupisha ujenzi wa shule.
‘’Tumekaa hapa mpaka usiku kuhangaikia watoto wenu, eneo hili lilikuwa la umma na litaendelea kuwa la umma’’ alisema Silaa
----------------------------------MWISHO----------------------------------------------------
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akizungumza na wananchi wa eneo la Pombe Shop Chamwino Morogoro usiku alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi tarehe 22 Sept 2023. |
Sehemu ya wananchi wa eneo la Pombe Shop Chamwino Morogoro wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Mhe Jerry Silaa usiku alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo hilo tarehe 22 Sept 2023. |
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akimsikiliza mwananchi katika eneo la Pombe Shop alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi tarehe 22 Sept 2023. |
WAZIRI MWIGULU NCHINI HISPANIA
🇹🇿🇪🇸
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), |
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), yuko Madrid, Hispania ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara, na Utalii wan chi hiyo, Bi. Xiana Mendez, ambapo Hispania imeonesha nia ya kushiriki katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa kutoa mkopo, dhamana ya mikopo na Bima kwa kampuni za nchi hiyo zitakazojenga reli hiyo kuanzia Makutopora hadi Mwanza na Kipande cha kuanzia Tabora - Kigoma hadi Malagarasi, kutokana na umuhimu wa mradi huo kwa maendeleo ya nchi.
"asali na mazao mengine ya baharini na kwenye misitu, ni miongoni mwa rasilimali zinazopewa kipaumbele kupitia mikakati ya uwekezaji na kukuza uchumi Mkoani Tanga.”- RC KINDAMBA
TFS kutumia mikoko ya Tanga kuzalisha asali
Na Mashaka Mgeta, TANGA
Wakala wa Misitu (TFS) kupitia Shamba la Nyuki Mwambao wilayani Handeni, umeazimia kutumia maeneo ya ukanda wa mikoko, kufuga nyuki ili kuzalishaji asali itakayokidhi lengo la kufikia tani 50 kwa mwaka 2023/2024.
Afisa Nyuki Msaidizi katika Shamba la Nyuki Mwambao, Nkwimba Maige, ameyasema hayo kwenye kikao cha wataalamu wa uvuvi na nyuki mkoani Tanga, kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Waziri Kindamba.
Maige amesema Shamba la Nyuki Mwambao lenye maeneo ya uhifadhi katika kata za Kabuku na Kang’ata wilayani Handeni, limeyapitia maeneo ya ukanda wa mikoko kwenye wilaya za Pangani, Tanga na Mkinga na kubaini kuwa yanafaa kwa uzalishaji mkubwa wa asali.
‘’Sasa tunakwenda kuweka mizinga 140 ya awali wakati tukisubiri mingine 800…lengo letu ni kwamba, asali itakayopatikana kwenye maeneo hayo ichangie kufikia lengo la uzalishaji wa tani 50 kwa mwaka huu wa fedha,’’ amesisitiza zaidi Maige
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Kindamba amesema asali na mazao mengine ya baharini na kwenye misitu, ni miongoni mwa rasilimali zinazopewa kipaumbele kupitia mikakati ya uwekezaji na kukuza uchumi wa mkoa huo.
Mhe. Kindamba amesema, azma ya kuwekeza mizinga ya nyuki kwenye maeneo ya mikoko, itasaidia kuibua fursa kubwa za kiuchumi zitakazoacha alama ya mafanikio mkoani humo.
Amesema ili kutoa hamasa kubwa kwa wakazi wa mkoa huo kujihusisha na uzalishaji wa asali, anatafuta maeneo yakiwamo ya ukanda wa mikoko na mashamba ya mkonge yenye muda mrefu, ili awekeze katika ufugaji wa nyuki.
Naye Mhifadhi Msaidizi wa TFS wilayani Tanga, Issa Mziray amesema eneo la hifadhi ya mikoko lina ukubwa wa hekta 9,501 ambapo Tanga ina hekta 2,966, Mkinga (4813) na Pangani (1,722).
@wazirikindamba
@tanzania_forest #tanzaniaforestservices
@matukio_tanga @tanga_jiji @ccm_dijitali @wizarayamaliasilinautalii @wizara_ya_kilimo @michuzijr @millardayo @
TANZANIA NA IRELAND KUSHIRIKIANA KATIKA UTAMADUNI NA MICHEZO
Na Shamimu Nyaki
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Septemba 22, 2023 ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam, Waziri Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewasilisha ombi kwa nchi hiyo isaidie kutoa mafunzo kwa Watalaamu wa michezo hapa nchini katika eneo la usimamizi wa miundombinu ya michezo pamoja na wataalamu wa kufundisha michezo.
"Nawakaribisha katika nchi yetu muweze kufanya maandalizi ya misimu ya ligi zenu kwa kuwa nchi yetu ina maeneo mazuri hapa Dar es Salaam - Kigamboni, Tanga, Arusha na Zanzibar.
Kwa upande wake Balozi huyo Mhe. Mary O' Neill amekubali maombi hayo na kuahidi kuwa mwezi Novemba mwaka huu atakuja Msanii Nguli wa fani ya Uchoraji Mick O'Dea ambaye atatoa uzoefu kwa wasanii wa hapa nchini akibainisha kuwa Wizara imemkaribisha ashirikiane na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo katika fani hiyo kwakua ni Taasisi Bora inayotoa mafunzo kwenye eneo hilo.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu ameikaribisha nchi hiyo kupitia Ubalozi huo kushirikiana na Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kutoa mafunzo kwenye fani zinazotolewa chuoni hapo.