CPA MAKALLA: CCM ITAWALETEA WAGOMBEA WASIO NA MAKANDOKANDO
Na Richard Mwaikenda, Mwanza Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akiwaahidi wananchi kwa...
GPE and CAMFED Host Roundtable on Education with Tanzanian CSOs
Written By CCMdijitali on Wednesday, November 29, 2023 | November 29, 2023
Retired President Dr. Kikwete shares space in a Roundtable discussion on Education with Tanzanian CSOs in Dar es salaam
Dar es Salaam, 29th November 2023 - The Chair of the Board of Directors of the Global Partnership for Education (GPE), H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Retired President of the United Republic of Tanzania, along with GPE’s Chief Executive Officer, Ms. Laura Frigenti, are set to participate in a significant roundtable discussion today at the Campaign for Female Education (CAMFED) Tanzania offices in Dar es Salaam.
According to Ms. Anna Sawaki, CAMFED Tanzania’s Director of Programs and Partnership, the primary objective of the roundtable is to collectively emphasise the importance of prioritising education on the political agenda.
Additionally, she said, the event aims to recognise the pivotal role of Civil Society Organisations (CSOs) in advocating for education and actively contributing to policy dialogue within local education groups.
“The roundtable will also provide an opportunity for CSO representatives to share their successful practices and experiences in supporting the transformation of education systems”, Ms Sawaki explained.
Among the CSOs expected to attend the roundtable are HakiElimu, PESTALOZZI, Shule Direct, UWEZO, Ubongo Kids, Lyra in Africa, World Vision, Binti Salha Foundation, TEN/MET, TEM/MET, CAMFED, CAMFED Tanzania, Transforming Life Tanzania, and Gender Networking (TGNP).
The Global Partnership for Education (GPE) is the largest global fund exclusively dedicated to reshaping education in lower-income countries. Operating as a unique, multi-stakeholder partnership, GPE works towards delivering quality education to ensure that every child, regardless of gender, has access to hope, opportunity, and agency.
For the past two decades, GPE has been actively disbursing funds and providing support to develop robust and resilient education systems in countries marked by extreme poverty or conflict. The focus is on enabling more children, particularly girls, to receive the education necessary for personal growth and contribution to building a more prosperous and sustainable world.
GPE's distinctive model has played a pivotal role in helping partner countries make significant strides in enhancing access, learning outcomes, and equity, resulting in improved educational opportunities for millions of boys and girls.
On the other hand, CAMFED, a pan-African movement, is leading a revolutionary approach to delivering girls' education. Through a gold-standard system of accountability to the young people and communities they serve, CAMFED has established a model that significantly improves the prospects of girls becoming independent and influential women.
CAMFED's work is driven at the grassroots level by local committees and teams comprising graduates, teachers, parents, government officials, and other volunteers who dedicate their time and expertise to ensure more girls successfully complete their education. The organisation’s governance structures include the boards of each national entity.
The roundtable represents a significant collaboration between GPE and CAMFED, bringing together key stakeholders and CSOs to reinforce the collective commitment to advancing education, particularly in regions facing the most pressing needs. This collaborative effort aligns with GPE's mission of transforming education systems and CAMFED's dedication to revolutionising girls' education across Africa.
Ends
PSSSF YATENGA MUDA MAALUM WA MAJUMA MANNE KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANACHAMA A
Written By CCMdijitali on Friday, November 24, 2023 | November 24, 2023
PSSSF YATENGA MUDA MAALUM WA MAJUMA MANNE KUSIKILIZA NA KUZIPATIA UFUMBUZI CHANGAMOTO ZA WANACHAMA NCHI NZIMA TANZANIA NA ZANZIBAR.
NA
K-VIS BLOG/KHALFANS AID, ARUSHA
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetenga muda maalum wa
majuma manne kuanzia Novemba 27 hadi Disemba 22, 2023, kwa lengo la kusikiliza
na kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali za wanachama, Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko huo, CPA. Hosea Kashimba, amesema.
CPA.
Kashimba amesema hayo kwenye banda la PSSSF katika Maadhimisho ya Wiki ya
Huduma za Fedha Kitaifa, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
Novemba 24, 2023.
“Iwapo
kuna mwanachama yeyote mwenye changamoto yoyote inayohusu uanachama, michango
na mafao, afike katika ofisi za PSSSF zilizo jirani naye Tanzania bara na
Zanzibar, tutamsikiliza na kutatua changamoto yake.” Alisisitiza.
Alisema
zoezi hilo litakuwa likifanyika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja
jioni, Jumatatu hadi Ijumaa.
“Lakini
hata baada ya kipindi hicho maalum kufikia ukomo, bado tutaendelea kuwapatia
huduma wanachama wetu, lengo hasa ni kuhakikisha wanachama wetu wanafurahia
huduma zetu wakati wote.” Alisema CPA. Kashimba.
Pia
amerejelea angalizo kwa wanachama na wastaafu, kuwa wasikubali kupokea
maelekezo yoyote kutoka kwa watu wasiowajua endapo wanahisi wanachangamoto
yoyote kuhusiana na uanachama wao au mafao yao.
“Tunawaasa
wanachama wetu hususan wale wanaokaribia kustaafu, watambue kuwa huduma zetu
zinatolewa bure bila malipo yoyote, na kama wanachangamoto yoyote wapige simu
namba ya bure 0800 110 040 au kupitia mitandao yetu ya kijamii kupitia anuani
ya PSSSFTZ.” Alifafanua CPA. Kashimba.
CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu PSSSF, |
CHONGOLO: WALIPENI MADENI, WAHISHENI MALIPO YA WAKANDARASI
Written By CCMdijitali on Thursday, November 23, 2023 | November 23, 2023
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Daniel Godfrey Chongolo amesema kupitia utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi ya 2020 – 2025, CCM itahakikisha Serikali inaendelea kuweka mazingira bora na kuwajengea uwezo makandarasi na washauri waelekezi wazawa, ili waweze kutekeleza miradi mingi na mikubwa ndani ya nchi na hata kushindana nje ya Tanzania, ikiwemo kulipwa madeni yao na kuwahishiwa malipo ya kazi katika miradi wanayotekeleza.
Ndugu Chongolo amesema hatua ya kuwatumia wakandarasi na washauri waelekezi wazalendo wa Kitanzania katika miradi hiyo mbalimbali ya ujenzi itaokoa fedha nyingi, ambazo kwa sasa zinalipwa kwa makandarasi wa nje, hivyo zitabakia katika mzunguko wa fedha na uchumi ndani ya nchi, zitaongeza kipato kwa wahusika, huku pia wakipata nafasi ya kuongeza ujuzi na kutengeneza fursa za ajira kwa Watanzania.
Mbali ya kuwataka watendaji wa Serikali, hususan katika Wizara ya Ujenzi kuacha mitazamo hasi dhidi ya wakandarasi na wahandisi wazawa kuwa hawawezi kazi, pia amewataka baadhi ya makandarasi wa ndani nao kuacha kuichafua tasnia ya ujenzi, kwa kuwa na kampuni za mfukoni (briefcase company), ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi, hali ambayo inajenga na kuhalalisha dhana kuwa kuna wazawa wanafanya utapeli kwa kutumia taaluma hiyo.
Katibu Mkuu Ndugu Chongolo amesema hayo jana Jumanne, Novemba 21, 2023, wakati akitoa salaam za Chama Cha Mapinduzi kwenye Mkutano wa Makandarasi na Washauri Waelekezi Wazawa, uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention, jijini Dodoma, ambapo amewaambia kuwa CCM inatambua changamoto zote zinazowasibu, likiwemo suala la madeni wanayodai na kucheleweshewa malipo yao katika miradi anuai wanayotekeleza maeneo mbalimbali nchini.
“Mkutano huu ni muhimu sana. Jana nimekaa na mawaziri wote wawili hawa, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Fedha hadi usiku wa manane, ilibidi tukae kwa muda mrefu sana. Nilitaka kwanza kujua masuala kadhaa kabla sijaja hapa leo. Na hasa nililowaita na kuzungumza nao ni kuhusu malipo yenu. Nina uhakika hapa tukisema tupitishe karatasi kila mtu aandike changamoto yake, jambo la kwanza kila mmoja litakuwa ni malipo, malipo, malipo.
“Wamenieleza kwa kina jinsi wanavyochukua hatua kadhaa, hasa kutekeleza maelekezo na maagizo ya Mhe. Rais Dokta Samia Suluhu Hassan amewaagiza kuhakikisha wanafanya msawazo wa malipo ya madeni ya wakandarasi na pia kila mkandarasi alipwe anapo-raise certificate. Pia labda niseme hapa, ni muhimu mkaenda pia kujifunza kwa wenzenu wa REA (Wakala wa Umeme Vijijini) ili utaratibu ule wanaotumia kulipa wakandarasi wa umeme, uweze kutumika pia huku Ujenzi. Kule hakuna malalamiko sana,” amesema Katibu Mkuu Chongolo.
Pamoja na kuipongeza Serikali kwa kufanya mabadiliko ya Sheria ya Manunuzi, iliyopandisha kiwango cha thamani ya miradi inayoweza kutekelezwa na wakandarasi wa ndani, kutoka mradi wa thamani ya Tsh. 10 bilioni, hadi kufikia mradi wa Tsh. 50 bilioni, Katibu Mkuu Ndugu Chongolo ameitaka Serikali, kupitia Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Fedha, kuweka utaratibu wa kisheria ambao utakaolazimu ushirikishwaji wa makandarasi wazawa katika miradi yote mikubwa nchini.
“Hili la ushirikishwaji kwenye miradi mikubwa ya kimkakati kama SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere, hili tunaweza kulimaliza kwa kuweka sheria ya kulazimisha wakandarasi wakubwa wanapoomba miradi hapa kwetu basi waje na wakandarasi wa ndani kama ilivyo kwa Washauri Majenzi yaani consultants. Hii pia ni nzuri kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
“Mfano tunafanya mradi mkubwa wa SGR lakini mkandarasi akimaliza akiondoka siku tukitaka kufanya ‘ka extension kadogo hata ka kilometa moja, hatutaweza kwa sababu hatukuweka wakandarasi wetu wapate ujuzi. Ni kupitia watu wetu kushiriki, ndiyo tungeweza kufanya kama ambavyo baadhi ya nchi zingine duniani zinafanya kujenga uwezo kwa watu wao kwa kitu kinachoitwa ‘Technological Transfer" amesema Katibu Mkuu Chongolo.
Ndugu Chongolo amewahakikishia Makandarasi na Washauri Waelekezi hao wa ndani kuwa CCM itasimamia maslahi yao, kwa kadri ambavyo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025 ilivyoahidi kuwa Chama kitaielekeza Serikali kuhakikisha inaweka mazingira rafiki na bora, ikiwa ni pamoja na kujengewa uwezo wa kupata kazi nyingi zaidi za fedha za Mfuko wa Barabara na kuwawazesha kupata mikopo ili washiriki kikamilifu kwenye miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, madaraja, majengo, maji na mingine mingi.
Katibu Mkuu Chongolo pia aliwataka wazawa hao kutanguliza mbele weledi, uaminifu, kujali rasilimali watu na thamani ya fedha wanapofanikiwa kupata miradi hiyo ya Serikali inayotumia fedha za umma, huku akitoa wito kuwataka waache ubinafsi wa kila mtu kupambana mmoja mmoja katika kutafuta miradi, badala yake watambue umuhimu wa kuungana (Joint Ventures), na wafanye hivyo mapema, si wakati wa kutafuta miradi pekee, ili kujenga kuaminiana katika ubia wa kibiashara wanaokuwa wameingia.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Daniel Godfrey Chongolo |
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Daniel Godfrey Chongolo |
MFUMO UNGANISHI KUONDOA CHANGAMOTO SEKTA YA ARDHI- PINDA
Written By CCMdijitali on Wednesday, November 22, 2023 | November 22, 2023
‘’Kikubwa ambacho nimeanza kufarijika ni kwamba ‘mmeadvance’ mpaka hapa mlipofika katika kuboresha mfumo, hongereni sana baada ya muda tutakwenda kumaliza kelele za wananchi wa nchi hii’’ alisema Mhe. Pinda.
‘’lazima mkawe standby wakurugenzi na maofisa, wale waliokuwa wanakula kupitia mfumo wa kawaida mjue ndiyo ‘threat’ namba moja wao ndiyo watakaoanza kusema mfumo wa ardhi bure kabisa lazima tutengeneze timu ya kuwaattack’’ alisema Pinda.
‘’Kupitia mawasilisho ya wataalamu tungetamani mfumo ukamilike mapema lakini kwa kuwa kazi hiyo inahitaji utaalamu, tunaamini kazi hiyo itakamilika ndani ya muda mfupi’’ alisema Lucy
‘’Katika maboresho yanayoendelea, kuna mifumo mitatu wa kwanza ni Back Office unaoruhusu watumishi kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi, wa pili ni Public Portal unaoruhusu wananchi kuomba huduma online na wa tatu ni Mobile App ambapo wananchi wanaomba huduma kupitia simu janja’’ alisema Flateny.
Sehemu ya Menejiment ya Wizara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda (Hayupo pichani). |
TANZANIA MWENYEJI WA TAMASHA LA DUNIA LA WATU WENYE USIKIVU HAFIFU
Hadi sasa washiriki zaidi ya 200 wa tamasha hilo wameshawasili tayari nchini wanatoka mataifa ya Afrika Kusini, Australia, Belarus, Brazil, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Guyana, Haiti, Hispania, India, Iran, Italia, Kenya, Kongo DRC, Malasia, Macedonia, Marekani, Mexico, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Pakistan, Poland, Romania, Rwanda, Senegal, Siera Leone, Sudan Kusini, Thailand, Tunisia, Jamhuri ya Czechoslovakia, Ufaransa, Uganda, Ujerumani, Ukraine, Urusi, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.
WAZIRI MAKAMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI EAC JIJINI ARUSHA
Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri wa EAC pamoja na mambo mengine umejadili masuala kuhusu Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya mkutano cha Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2022 hadi 24 Novemba, 2023; utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya kuhusu Majadiliano ya Ombi la Shirikisho la Jamhuri ya Somalia kujiunga na EAC; juhudi za utafutaji wa Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo; Hali ya Kifedha ya Mfuko wa Akiba wa Jumuiya; majadiliano kuhusu Katiba ya Fungamano la kisiasa la Jumuiya; Tathmini ya miswada iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki; na Utoaji wa Tuzo kwa washindi wa mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Jumuiya unapigwa kwenye Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha |
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha |
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha |
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukiwa umesimama wakati wimbo wa Jumuiya unapigwa kwenye Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha |
DKT. BITEKO AKAGUA MAJENGO YA WIZARA YA NISHATI; SERA, URATIBU NA BUNGE
DKT. BITEKO AKAGUA MAJENGO YA WIZARA YA NISHATI; SERA, URATIBU NA BUNGE MJI WA SERIKALI- MTUMBA
NAIBU WAZIRI KIKWETE AZINDUA USAMBAZAJI WA MIFUMO KUBORESHA UWAJIBIKAJI KAZINI
Written By CCMdijitali on Tuesday, November 21, 2023 | November 21, 2023
DKT. BITEKO AIAGIZA TPDC KUANDAA MPANGO WA MUDA MREFU WA UPATIKANAJI GESI NCHINI
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuja na mpango wa muda mrefu utakaoonesha jinsi nchi itakavyoweza kuongeza kiasi cha gesi asilia
Amesema kuwa kufanya hivyo kutawezesha kuwepo kwa hazina ya kutosha ya nishati hiyo inayotumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme, viwandani, majumbani na katika magari.
Dkt. Biteko ameyasema hayo tarehe 21 Novemba, 2023 wakati wa kikao chake na Bodi na Menejimenti ya TPDC ambacho kililenga kufahamiana, kubadilishana mawazo juu ya utendaji kazi na Mhe. Dkt. Doto Biteko kuelekeza matarajio ambayo nchi inayahitaji kutoka TPDC.
“TPDC tujiulize, Je uwezo wetu wa kuzalisha Gesi Asilia unaweza kujibu mahitaji yetu ya Gesi ? tujiulize hili na tuchukue hatua. Tutambue kuwa mahitaji ya Gesi Asilia ni makubwa kwa sasa kwani dunia inahama kutoka matumizi ya mafuta na kwenda kwenye Gesi Asilia hivyo lazima tujipange, na pia tukumbuke tumesaini makubaliano ya kusafirisha nishati hii kwenda Uganda, Zambia na Kenya hivyo lazima tuwe na Gesi ya kutosha.” Amesisitiza Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko pia amewataka TPDC kutokuwa na urasimu katika uchukuaji wa maamuzi mbalimbali ikiwemo kwenye shughuli za utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia ili kutorudisha nyuma sekta hiyo nchini.
Kuhusu maelekezo aliyoyatoa wakati wa ziara yake, katika Kisiwa cha Songosongo mkoani Lindi na Kijiji cha Madimba na Msimbati mkoani Mtwara, Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, maisha ya wananchi katika maeneo hayo ambayo kuna visima na mitambo ya Gesi Asilia lazima yabadilike na wapewe huduma bora ikiwemo maji, umeme, afya na usafiri.
“Nashukuru mmeanza kufanyia kazi maagizo niliyoyatoa kwa haraka, ikiwemo ya kuweka taa za barabarani Kijiji cha Msimbati, kupeleka umeme wa uhakika Madimba na Msimbati unaotoka kwenye mitambo ya Gesi Asilia, kupeleka kivuko kisiwa cha Songosongo na malipo ya mafao kwa wastaafu wa Knight Support ambao walikuwa wakilinda mitambo na visima vya Gesi Asilia Songosongo ambao hawakulipwa muda mrefu, watu hawa wanahitaji huduma bora.”
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko |
SHIBUDA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUMTEUA MAKONDA KUWA MWENEZI WA CCM
Written By CCMdijitali on Monday, November 20, 2023 | November 20, 2023
MAGALLE SHIBUDA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUMTEUA MAKONDA KUWA MWENEZI WA CCM KWANI AMEONESHA JUHUDI NA SHABAHA ZA KUUNDA DARAJA RAFIKI KWA KAZI ZA RAIS SAMIA NA WATANZANIA
- Asema Makonda amejenga uhusiano rafiki wa Kanda ya ziwa kwa kutoa Ahsante kwa uwajibikaji wa Serikali ya awamu ya 6 ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan
- Amejenga na kuleta wokovu wa mlango wa kutokea huzuni za ndani zilizounda ugumu wa mioyo katika kufumbua maono ya Ahsante_
MHE. BITEKO ATOA MAAGIZO KWA MSAJILI WA HAZINA
Written By CCMdijitali on Friday, November 17, 2023 | November 17, 2023
MHE. BITEKO ATOA MAAGIZO KWA MSAJILI WA HAZINA KUELEZA SABABU YA MASHIRIKA YA UMMA KUTOSHIRIKI SHIMMUTA 2023
RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NCHINI MHE KYLE NUNAS JIJIJINI DAR ES SALAAM LEO
Written By CCMdijitali on Thursday, November 16, 2023 | November 16, 2023
MCHAKATO HADHI MAALUM KWA DIAPSORA KUKAMILIKA MWAKA 2024
Written By CCMdijitali on Tuesday, November 14, 2023 | November 14, 2023
“Miongoni mwa masuala yatakayopewa kipaumbele kwenye Hadhi Maalum ni haki ya kurithi au kurithishwa mali kwa diaspora wa Kitanzania aishiye nje ya nchi. Ili kutekeleza hili kuna maeneo ya sheria yetu lazima yabadilishwe ili watoto wenu wanaoishi huku nje waweze kurithi au kumiliki ardhi” alisema Waziri Makamba.
“Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi imara wa Mama Samia Suluhu Hassan, imeelekeza kuokoa Mtanzania au Watanzania popote pale walipo pindi majanga yanapowakuta. Imefanya hivyo kuwaokoa Watanzania waliokua masomoni Ukraine, imewarejesha nyumbani Watanzania waliokuwa Sudan na hivi karibuni Israeli” Mhe. Makamba aliongeza.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Carilone Chipeta akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Mheshimiwa Waziri na Diaspora uliofanyika Jijini The Hague, Uholanzi. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi katika kikao kilichofanyika Jijini The Hague, Uholanzi ambapo amewasisitiza Watanzania hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Taifa lao.
SERIKALI KUENDELEA KUWABEBA WATUMISHI
Written By CCMdijitali on Monday, November 13, 2023 | November 13, 2023
SERIKALI KUENDELEA KUWABEBA WATUMISHI WANAOFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU-KIKWETE.
Akijibu swali la Ziada, alimuhakikishia Mbunge na Bunge kuwa Serikali inatambua changamoto za Watumishi katika Halmashauri yao na nyengine Nchini kwa kuwa iko timu iliyokwisha zunguka nchi nzima kukagua mazingira ya Watumishi hivyo upatikanaji wa fedha na mipango ya huduma kwa Watumishi itawahakikishia mazingira mazuri ya Watumishi wanaofanya kazi katika mazingira Magumu.
MAJALIWA ASISITIZA NIDHAMU, MAADILI, UBUNIFU KWA WATUMISHI WA UMMA
Written By CCMdijitali on Saturday, November 11, 2023 | November 11, 2023
“Nitoe wito kwa kila mtumishi kuzingatia nidhamu ya kazi na maadili ya utumishi wa umma, Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatekeleza falsafa ya Kazi Iendelee. Kwa msingi huo watumishi wote wa umma mnao wajibu wa kufuata na kutekeleza falsafa hii. ”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza watumishi hao kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao vizuri na kwa weledi. “Kujituma kwenu, ushirikiano na bidii vimewezesha Serikali na hususan Ofisi ya Waziri Mkuu kupata mafanikio makubwa. ”
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amelipa madai malimbikizo ya mishahara ya watumishi 121,858 yenye jumla ya shilingi bilioni 207.97, pia amepandisha madaraja watumishi 91,841 na shilingi bilioni 73.4 zimetumika kuwalipa watumishi hao”