CPA MAKALLA: CCM ITAWALETEA WAGOMBEA WASIO NA MAKANDOKANDO
Na Richard Mwaikenda, Mwanza Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akiwaahidi wananchi kwa...
FINLAND NCHI YA KWANZA YA NORDIC KUJADILIANA KIDIPOLOMASIA NA TANZANIA
Written By CCMdijitali on Thursday, December 14, 2023 | December 14, 2023
“Huu ni mkutano wetu wa kwanza wa majadiliano ya kidiplomasia kati ya Finland na Tanzania ambapo umelenga kuimarisha ushirikiano, kubadilishana ujuzi na uzoefu wa masuala mbalimbali yanayohusu diplomasia na maendeleo katika sekta mbalimbali baina ya nchi zetu”.
Mkutano ukiendela |
Mkutano ukiendela |
MANENO YA NAIBU WAZIRI PINDA YATAKA KUMLIZA DIWANI WA KISAKI SINGIDA
Written By CCMdijitali on Tuesday, December 12, 2023 | December 12, 2023
Na Munir Shemweta, WANMM SINGIDA
Maneno ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Geophrey Pinda wakati wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kisaki na Mwekezaji wa Sekta ya Nyuki katika eneo la Kisaki B Manispaa ya Singida mkoani Singida nusra yamlize Diwani wa Kata ya Kisaki Moses Shaban kutokana na kujaa hekima na busara.
Naibu Waziri Pinda alifika kijiji cha Kisaki kilichopo mpakani mwa manispaa ya Singida na na wilaya ya Ikungi mkoani Singida tarehe 11 Desemba 2023 kwa lengo la kusikiliza na kutatua mgogoro wa ardhi baina ya Wananchi na Mwekezaji wa Nyuki.
"Nikupongeze sana Mhe Naibu Waziri naweza kusema hata kama hutujafika mwisho wa jambo hili, umenipa hadidu za rejea kumkumbuka Mizengo Pinda alipokuwa waziri mkuu hekima yake na maelekezo yake juu ya utendaji kazi". Alisema Shaban
"Nilikuwa nimesimama na kukusikiliza natamani kulia kwa sababu umekuja katika mgogoro huu hakika umeiwakilisha vyema serikali ". Alisema
Diwani huyo wa Kata ya Kisaki amesema, maneno yaliyozungumzwa na Naibu Waziri Mhe Geophrey Pinda kuhusu utatuzi wa mgogoro baina ya wananchi na Mwekezaji ni tunu yenye afya na mbolea katika kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.
"Umeongoza kikao kilaini na kitamu hata aliyekuwa na hasira zimepotea na hata yule aliyekuwa na silaha ameshusha nakupongeza sana". Aliongeza Diwani Shaban
Kwa upande wake, Naibu waziri wa ardhi Geophrey Pinda aliwataka wananchi wa kisaki katika manispaa ya Singida mkoa wa Singida kuhakikisha wanadumisha amani katika muda wote wa kushughulikia migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.
"Niwatangazie kipande cha amani wote bila kujali ukoo wa nani na muwe na lugha moja iliyo bora. Siri ya mgongano inapata adui anayeingia bila matatizo"alisema mhe. Pinda.
Amewataka wananchi wa kijiji cha Kisaki kwenda kuanza vikao vya suluhu ya mgogoro wao na suala la kukutana na serikali basi ofisi ya mkuu wa wilaya ya Singida italisimamia kwa kuwa suala hilo lishatoka katika ngazi ya kijiji.
Awali mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili alieleza kuwa Mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa kijiji cha Kisaki na Mwekezaji wa Sekta ya Nyuki katika eneo la Kisaki B ulifika ofisini kwake mwaka 2022 ambapo wananchi walidai maeneo kutwaliwa Mwekezaji.
Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya ya Singida alisema, kufuatia kadhia hiyo aliunda Tume ili kubaini kama madai ni ya kweli au la ambapo Tume ilimalia kazi mei 2023 na kupeleka mrejesho katika ofisi yake oktoba 2023.
VIONGOZI WANALOJUKUMU LA KUZINGATIA MATUMIZI YA TAKWIMU ZA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022.
Written By CCMdijitali on Monday, December 11, 2023 | December 11, 2023
MBUNGE WA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI MHE DKT D.JOHN PALLANGYO |
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Dkt. John Danielson Palangyo, amesema kuwa viongozi wa wananchi wanalojukumu la kuzingatia matumizi ya Takwimu sahihi za Matokeo ya Sensa ya Watu na makazi ili kupanga shughuli na kufikia malengo ya Serikali.
Akizungumza wakati wa mkutano wa Mafunzo ya usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022 kwa viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii, mkoa wa Arusha, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa AIM MALL Jijini Arusha leo 11.12.2023, Dkt. pallangyo amewataka viongozi walioshiriki mafunzo hayo kuyazingatia ili kwenda kuelimisha jamii namna na faida ya matumizi ya Takwimu hizo.
Ameweka wazi kuwa, Takwimu za Matokeo ya Sensa licha ya kuwa ni Dira ya maendeleo ya Taifa, lakini viongozi na watanzania wanalojukumu ya kuzitumia ili ziweze kufikia malengo ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Serikali.
"Kwa niaba ya wananchi wa Arumeru Mashariki, tunaipongeza Serikali ya awamu ya sita, kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kisekta katika jimbo langu, ipo miradi yenye kutumia fedha nyingi a,bayo imetekelezwa na kukamilika huku ikitoa fura kwa wananchi kuitumia na kupata huduma ndani ya maeneo yao, ile hali ya wananchi kuuza vitu na mali zao ili kujenga madarasa kwa sasa kwetu imekuwa ni histori, Serikali imejenga madarasa mengi, tunamshukuru Mhe. Rais Samia, na niwatake wanaArumeru wote kumuunga mkono" Amebainisha Mhe. Dkt. Pallangyo
Mkutano huo umefunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi Utumishi na Rasilimali Watu, mkoa wa Arusha, David Lyamongi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, ukiwa na lengo la kuyajengea uwezo makundi mbalimbali ya kijamii juu ya matumizi sahihi ya matokeo ya Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022.
Makundi hayo ni pamoja na viongozi wawakilishi wa wananchi, viongozi wa Siasa, dini na mila, Watendaji wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, watendaji wa kata, kamati ya Sensa Mkoa pamoja na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo watu wenye mahuitaji maalum.
WAZANZIBARI NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAMETAKIWA KUWALEA WATOTO WAO KWA KUZINGATIA MILA, SILKA NA DESTURI ZA KIZANZIBARI
Written By CCMdijitali on Friday, December 8, 2023 | December 08, 2023
Wazanzibari na Waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuwalea watoto wao kwa kuzingatia Mila, Silka na Desturi za kizanzibari ili kupata kizazi chema chenye Kufuata maadili.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid Maungani mara baada ya kumaliza Ibada ya Sala ya Ijumaa.
Amesema wazazi na walezi wanapaswa kuwalea watoto wao kwa kufuata silka na mila za kizanzibari jambo ambalo kitasaidia kuondosha kabisa vitendo vya udhalilishaji hasa kwa wanawake na watoto jambo ambalo linaiharibu sifa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni wajibu wa kila Mzanzibari kupiga vita suala la udhalilishaji na kuwataka wakaazi wa Maungani na maeneo jirani kuhakikisha wanapita nyumba hadi nyumba kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na kuhakikisha wanawafichua wale wote ambao wanatabia ya kufanya vitendo hivyo,.
Alhajj Hemed amewataka waumini na Wazanzibari kushirikiana na kuacha muhali na kwenda kutoa ushahidi Mahakamani pale ambapo wanatakiwa kufanya hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizunguzia suala la madawa ya kulevya Alhajj Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar kuachana na tabia ya kuwakodisha nyumba watu ambao hawawafahamu na hawana taarifa zao za kutosha ili kuondosha wimbi la watumiaji na wauzajiwa wa madawa ya kulevya nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi itahakikisha inaondosha kabisa suala la madawa ya kulevya kwa kuweka sheria ngumu amabzo zitawabana waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa madawa ya kulevya.
Akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Maalim SULEIMAN MWINCHUMU amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kuchunga nafsi zao na kujielekeza katika kufanya amali njema ambazo zitawaepusha na kupata hasara hapa duniani na kesho akhera.
Amesema kuwa wazazi watakapo weza kuchunga nafsi zao pamoja na kuwachunga watoto dhidi ya wao katika kujiunga na vikundi viovyo watakuwa wameisaidia jamii na taifa kwa ujumla kwaani Taifa lenye maendeleo linahitaji nguvu kazi isiyo na mmong’onyoko wa maadili.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Leo tarehe..08.12.2023
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR- AHAHIRISHA BARAZA LA WAWAKILISHI.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuimarisha huduma za kijamii zikiwemo Afya, Elimu na Maji safi na salama.
Ameyasama hayo alipokuwa akiuakhirisha Mkutano wa Kumi na Tatu(13) wa Baraza la Kumi (10) la Wawakilishi katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Jijini Zanzibar.
Mhe. Hemed amesema Serikali itaendelea kusimamia Miradi ya Ujenzi wa Skuli, Hospitali na Miradi ya Maji safi na salama kwa lengo la kuhakikisha Wananchi wanapata huduma hizo katika maeneo ya karibu ikiwa ni utekelezajiwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 pamoja na ahadi zilizotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussen Ali Mwinyi wakati wa Kampeni za Uchaguzi 2020.
Amesema kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ipo katika hatua za kuboresha Daftari la wapiga kura ambapo amewahimiza Wananchi kuitumia nafasi yao ya kidemokrasia kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kufata maelekezo yanayotolewa na Tume ya Uchaguzi.
Aidha Mhe. Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali itahakikisha inapambana kwa nguvu zake zote kuondosha kabisa vitendo vya utumiaji wa dawa za kulevya na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia wa wanawake na watoto ambavyo vinaendelea kuiathiri Jamii ya Wazanzibari.
Sambamba na hayo amesema katika kuhakikisha mapato ya Serikali yanazibitiwa, Serikali imeimarisha Mfumo wa usimamizi wa fedha wa IFMIS na kuanzisha Mfumo wa Zan-malipo, mfumo wa manunuzi wa E- Proz, mfumo wa ukusanyaji wa kodi wa kutumia mashine ya( EFD) mfumo wa payroll na mfumo wa bajeti na matumizi (BAMAS).
Amefahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuchukua jitihada mbali mbali katika kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi ya wafanyakazi, hivyo amewataka watumishi kuendelea kuimarisha nidhamu na uwajibakaji kwa maslahi mapana ya nchi.
Mhe. Hemed amesema kuwa michezo ni jambo muhimu linalowaunganisha wananchi walio wengi Duniani hivyo Serikali inakamilisha ukarabati wa Ujenzi wa Kiwanja cha Amani Unguja na Gombani Pemba ambapo kukamilika kwake mandhari na haiba ya viwanja hivyo yatakuwa na muonekano wenye hadhi ya Kimataifa.
Sambmba na hayo Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Timu ya Vijana chini ya Umri wa miaka 15 Karume Boys kwa kutwaa Ubingwa wa mashindano ya CECAFA 2025 yaliyofanyika Uganda na kupata Mkono wa Dhahabu wa Kipa bora jambo ambalo limeiletea heshima nchi yetu.
Mhe. Hemed ametoa pole kwa wananchi walioatirika na Mafuriko ndani ya Zanzibar na Tanzania Bara hasa kwa wakazi wa Manyara kufuatia Mafuriko ya Maporomoko ya Udongo yaliyotokea katika Kijiji cha Katesh na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 68 na majeruhi zaidi ya 100.
Katika Mkutano wa Kumi na Tatu(13) wa Baraza la Kumi(10) la Wawakilishi, Baraza limepokea, limejadili na kupitisha Miswaada Sita(6) ya Sheria pamoja na kuwasilishwa Barazani Ripoti ya Saba ya Utekelezaji wa Tume ya Maadili kwa mwaka 2022/2023.
Imetolewa na kitengo cha Habari (OMPR)
Leo tarehe 08.12.2023
Rais Dk.Mwinyi amuwakilishs Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ufunguzi wa Mkutano wa Benki ya Dunia(IDA20)
Written By CCMdijitali on Wednesday, December 6, 2023 | December 06, 2023
“Tunashukuru Benki ya Dunia na washirika wengine kwa msaada wao kwa mpango huu”. Alishukuru Dk. Samia.
Akizungumzia Zanzibar inavyonufaika na fursa kutoka Benki ya Dunia, Rais Dk. Mwinyi alieleza uchumi wa Zanzibar unategemea Utalii kwa kiasi kikubwa hasa utalii wa utamaduni. Alisema, hifadhi ya Mji Mkongwe ambao ni urithi wa Dunia wa UNESCO, ulinufaika na Benki ya Dunia kupitia mradi wa “huduma za Mijini, Zanzibar” (ZUSP) ambao ulipata msaada kutoka IDA wenye thamani ya dola za Marekani milioni 93 ili kuboresha upatikanaji wa huduma za mijini na kuhifadhi urithi huo wa kitamaduni.
Pia Dk. Mwinyi aligusia eneo la biashara huria kwa mataifa wanufaika wa Benki ya Dunia na washirika wake, ili kuimarisha ushindani na uundaji wa nafasi za kazi kupitia ushirikiano wa kikanda na biashara, kwa bara la Afika na maeneo mengine ya dunia,
“Tunaamini IDA na IFC zinahitaji kuongeza usaidizi ili kukuza sekta binafsi inayostawi, jambo la msingi ni kuunganisha biashara za Kiafrika katika minyororo ya thamani ya kimataifa na kuvutia FDIs.” Alieleza Rais Dk. Mwinyi.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salum, alieleza mafanikio makubwa ya mkutano huo wa Kimataifa wa tathmini ya muda, kati ya mzunguko wa 20 wa Mapitio ya benki ya Dunia (IDA) yamefikiwa kutokana na jukudi kubwa za uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na msaada mkubwa waliopata kutoka kwa Mwakilishi Mkaazi wa benki hiyo, Bw. Nathan Balete.
NAIBU WAZIRI PINDA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI KIEGEYA MOROGORO
Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda amemaliza na kuufunga wa wananchi 767 wa Kiegeya mkoani Morogoro.
Wananchi hao ni wale waliovamia na kulima katika shamba la Tungi Sisal Estate la Mwekezaji Star Infrastructure.
Mhe Pinda amemaliza na kuufunga mgogoro huo tarehe 5 Desemba 2023 alipokutana na wawakilishi wa wakulima wakioongozwa na Mwenyekiti wao Haleluya Minga katika ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro.
Naibu Waziri wa Ardhi alifika mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwasikiliza ili kupata ukweli ambapo baada ya kuwasikiliza kwa takriban saa nne alibaini udanganyifu katika maelezo ya wakulima na kuwapa taarifa kuwa mwekezaji ni mmiliki halali na alitoa ekari 4000 alizoombwa na serikali na wao wamevamia sehemu mpya.
‘’Niwatake muwe waungwana na mfuate taratibu za kisheria za kupata ardhi na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wakataokaidi maelekezo ya serikali na mgogogoro huu kuhusu wananchi 767 nimeufunga rasmi’’ alisema Pinda
‘’Kesi yenu ilipitiwa katika ngazi mbalimbali na utafiti wake umefanyika mpaka uwandani na kuonesha kuwa ninyi hamna haki, kwanza mko tofauti na idadi yenu inaongezeka kila siku kutoka 319 hadi 767 na bado inaendelea hivyo katika mazingira ya kawaida inawawia vigumu kuwasaidia’’ alisema Mhe. Pinda.
Mwenyekiti wa wakulima hao Haleluya Minga mbali na kumshukuru Naibu Waziri kwa kuamuzi wake wa kwenda kuwasikiliza wakulima hao alimueleza kuwa, kuongezeka kwa idadi ya wakulima kulitokana na wao kutokuwa na utaratibu wa vikao na baada ya kugundua hilo ndipo walipokutana na kuchagua uongozi.
‘’Kupanda kwa idadi ya wakulima kutoka 319 hadi 767, kwanza hatukuwa na utaratibu wa viakao na tulikuwa hatufahamiani na ilifika mahali kulikuwa na ongezeko tukaamua kuwa na uongozi wa pamoja’’ alisema Haleluya.
Hata hivyo, Naibu Waziri Pinda amewataka wakulima hao kuwa watulivu na matumizi ya nguvu hayatasaidai kwa kuwa kamati ya mkoa, ofisi ya mkurugenzi wa manispoaa ya Morogoro na ile ya Taifa zinethibitisha kuwa wao siyo wamiliki halali wa maeneo hayo.
Awali Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro Frank Minzikunte alieleza historia ya shamba hilo kuwa inaanzia mwaka 1951 kwa kumilikishwa kwa Mwekezaji na mwaka 1983 serikali ilimuomba mwekezaji ekari 4000 kwa muda ili wananchi wafanye kilimo cha kufa na kupona.
Aliongeza kuwa, mwaka 2021 serikali ilimuomba mwekezaji kuziachia moja kwa moja ekari hizo ambapo baada ya majadiliano ya muda mrefu mwekezaji aliridhia na wananchi waliokuwa wamepewa mwaka 1983 wakatambuliwa na takriban wananchi 3777 walitambuliwa na kuingia mkataba na halmashauri ya upimaji shirikishi kama ilivyoelekezwa na serikali.
Hata hivyo, Kamishna huyo wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro alisema, wakati kutambua wananchi hao lilijotokeza kundi la wananchi 319 waliodaia kulima nje ya ekari zilizotolewa na mwekezaji kwa wakulima na ndipo serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliunda tume kwa ajili ya kusikiliza malalamiko pamoja na kero nyingine zinazowakabili wananchi katika ekari 4000.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA MKUTANO WA BODI YA GPE
Written By CCMdijitali on Tuesday, December 5, 2023 | December 05, 2023
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA MKUTANO WA BODI YA GPE MJINI UNGUJA LEO
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah leo amefungua rasmi mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Maendeleo ya Elimu Duniani (GPE) unaoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hio, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja, leo.
Mkutano huo wa siku mbili, unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na nje ya Marekani na Ulaya, tangu Shirika hilo lianzishwe na mataifa tajiri duniani ya G7 miaka 20 iliyopita.
Kwa mujibu wa Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza GPE, shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu Tanzania bara na Zanzibar.
Bodi ya Wakurugenzi ya GPE inaundwa na majimbo 20 yanayowakilisha washirika wote wa ushirikiano, ambapo katika mkutano wa bodi wanahudhuria Mjumbe wa Bodi na mjumbe mbadala wa Bodi wanawakilisha kila jimbo.
Bodi ya Wakurugenzi ya GPE huweka sera na mikakati ya ushirikiano, huku ikiakisi hali pana na tofauti ya ubia na inajumuisha wanachama kutoka serikali za nchi zenye mapato ya chini na washirika wote wa maendeleo: wakiwemo wafadhili, mashirika ya kiraia, sekta binafsi na wakfu, na mashirika ya kimataifa na benki za kikanda.
Nchi washirika wa GPE ni Afghanistan, Albania, Algeria, Angola, Bangladesh, Belize, Benin, Bhutan, Bolivia, Burkina Faso, Burundi, Cabo Verde, Cambodia, Cameroon, Central African Republic, Chad, Comoros, Congo, Democratic Republic ofCongo, Republic of, Côte d'Ivoire, Djibouti, Dominica, na Egypt.
Nchi zingine ni El Salvador, Eritrea, Eswatini, Ethiopia, Fiji, The Gambia, Georgia, Ghana, Grenada, Guatemala, Guinea, Guinea-Bissau, Guyana, Haiti, Honduras, India, Indonesia, Kenya, Kiribati, Kyrgyz Republic, Lao PDR, Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Maldives, Mali, Marshall Islands, Mauritania, FS Micronesia, Moldova, Mongolia na Morocco.
Zingine ni Mozambique, Myanmar, Nepal, Nicaragua, Niger, Nigeria, Pacific region, Pakistan, Papua New Guinea, Philippines, Rwanda, Saint Lucia, Saint Vincent and the Grenadines, Samoa, São Tomé and Príncipe, Senegal, Sierra Leone, Solomon Islands, Somalia, South Sudan, Sri Lanka, Sudan, Tajikistan.
Tanzania, Timor-Leste, Togo, Tonga, Tunisia, Tuvalu, Uganda, Ukraine, Uzbekistan, Vanuatu, Viet Nam, West Bank and Gaza, Yemen, Zambia na Zimbabwe pia ni nchi washirika. Syria si nchi mwanachama lakini imepokea ufadhili kwa idhini ya Bodi ya GPE.
WANANCHI NGORONGORO WANAHAMISHWA KWA KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU
Written By CCMdijitali on Monday, December 4, 2023 | December 04, 2023
‘’Leo wananchi hao wanaweza kwenda benki wakakopoa, wana ardhi ya kudumu na hati, hakuna mtu atakayewabughudhi, kuwanyang’anya na wametengewa maeneo makubwa ya kuchungia mifugo yao na tunaendelea kuboresha na tunachimba mabwawa kuhakikisha wananchi hawatupwi na wanalindwa na mali zao’’ alisema Pinda.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Ardhi Tanzania lililohitimishwa tarehe 5 Desemba 2023 mkoani Morgoro. |
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Ardhi Tanzania lililohitimishwa tarehe 5 Desemba 2023 mkoani Morgoro. |