CPA MAKALLA: CCM ITAWALETEA WAGOMBEA WASIO NA MAKANDOKANDO
Na Richard Mwaikenda, Mwanza Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akiwaahidi wananchi kwa...
DKT. TAX AKUTANA NA KAIMU NAIBU WAZIRI WA MAREKANI
Written By CCMdijitali on Wednesday, July 24, 2024 | July 24, 2024
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), akizungumza na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb), amekutana kwa mazungumzo na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho Dkt. Tax amemuhakikishia Mhe. Bass kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Marekani katika masuala yenye manufaa kwa nchi hizi mbili na wananchi wake.
Amesema ziara ya Mhe. Bass nchini ni ushahidi wa uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili huku ikonesha umuhimu mkubwa katika kuendelea kudumisha na kuimarisha maelewano, ushirikiano na urafiki kati ya Tanzania na Marekani na kuongeza kuwa kwa miaka mingi kumekuwa na majadiliano ya wazi kwa ajili ya kujenga na kuweka misingi ya ushirikiano madhubuti kati ya Tanzania na Marekani.
“Nina Imani kuwa kupitia ushirikiano na uhusiano wetu sio kwamba tutakabiliana na changamoto zinazotukabili kwa pamoja bali pia tutanufaika na fursa zilizopo mbele yetu ili kuchochea ukuaji na ustawi wa pamoja, alisema Dkt. Tax.
Naye Mhe. Bass akizungumza katika kikao hicho amesema ziara yake nchini ina lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Tanzania na kuahidi kuwa Marekani inaiona Tanzania kama mdau wa kimkakati katika ushirikiano wa maendeleo.
Ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ya Marekani na kuongeza kuwa ni matarajio yake kuwa kupitia majadiliano mbalimbali ambayo yemekuwa yakifanyika yatasaidia nchi yake kuibua kwa undani maeneo muhimu ambayo Serikali ya Tanzania inahitaji kuendelea ushirikiana na Marekani.
Tanzania na Marekani zimekuwa zikishirikina katika nyanja za afya kupitia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Shirika la Misaada la USAID, elimu, kilimo, biashara na uwekezaji, ulinzi na usalama.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass katika picha ya pmoja baada ya kumaliza mazungumzo yao katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiwa na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass pamoja na Katibu Mkuu Balozi Samwel Shelukindo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Batle (kulia) alipofika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiwa na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass alipofika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Batle (kulia) akiwa na ujumbe wake katika kikao kati ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass alipofika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam |
Katibu Mkuu Balozi Samwel Shelukindo (kushoto) akiwa na watumishi wa wizara katika kikao kati ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass alipofika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Batle alipomsindikiza Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaamm, kulia ni Katibu Mkuu Balozi Shelukindo akisalimiana na Balozi wa Marekani Mhe. Michael Batle |
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), akisalimiana na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass alipokutana naye kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam |
Naibu Waziri Ofisi ya Makamo Muungano na asema elimu kubwa inahitajika kwa Wananchi kuacha matumizi ya Mkaa na Kuni
Naibu Waziri Ofisi ya Makamo Muungano na Mazingira Khamis Hamza Chilo (wa tatu kushoto)Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Haji Shaaban Waziri (wa kwanza kulia ) Mdau wa maendeleo ya Jimbo la Uzini Lucia Mwaipopo (wa pili kulia) na Katibu wa App skills Foundation Tinnah Didas Masaburi wakisikiliza maelezo mafupi yanahusu Mazingira, utumiaji wa nishati sahihi ya kupikia na ufahamu wa dhana ya uchumi wa buluu kwa Sister Agnes Paulo (wa pili kushoto)wa parokia ya Kanisa la Katoliki na Chuo cha Utalii cha Machui. |
BALOZI SHELUKINDO AFUNGUA JPC YA KWANZA KATI YA TANZANIA NA COMORO
Written By CCMdijitali on Monday, July 22, 2024 | July 22, 2024
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amefungua Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Muungano wa Visiwa vya Comoro katika Ngazi ya Wataalam unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22-24 Julai 2024.
Akizungumza katika mkutano huo wa kihistoria, Balozi Shelukindo ameelezea kuridhishwa kwake na ukuaji wa mzunguko wa biashara kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro ambao umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
“Mzunguko wa biashara kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka mitatu iliyopita kutoka Dola za Marekani milioni 6.75 mwaka 2021 hadi Dola milioni 54.67 mwaka 2023”,alisema Balozi Shelukindo.
Balozi Shelukindo amesema ukuaji huo wa biashara ni mafanikio makubwa na kusisitiza kuwa bado kuna haja kwa nchi hizo mbili kuongeza uwigo wa ushirikiano wa kiuchumi kwa kutumia fursa zilizopo kwa tija ya pande zote mbili.
Amesema mikutano hiyo ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano inatoa fursa kwa nchi hizo mbili kupanua na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kupitia nyanja mbalimbali.
Amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina nia ya dhati ya kupanua ushirikiano na Visiwa vya Comoro kupitia sekta mbalimbali, zikiwemo diplomasia, ulinzi na usalama, masuala ya kisheria, fedha, biashara, uwekezaji, utalii, kilimo, uchumi wa buluu, mafuta na gesi, miundombinu, TEHAMA, afya, elimu, michezo, sanaa na utamaduni.
Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa Visiwa vya Comoro Mhe. Balozi Fatima Alfeine akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano huo ameeleza kuwa mkutano huo hautalenga kujadili namna ya kutatua changamo pekee bali kwa pamoja kuibua maneo mapya ya ushirikiano yatakayo chochea zaidi maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa pande zote mbili.
“Kutokana na uhimu wa mkutano huu wa kihistoria, ujumbe wetu umejumuisha wataalam kutoka sekta zote muhimu, kwa sababu tuna dhamira ya dhati sio tu ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na undugu wa kihistoria uliopo kati yetu bali kuhakikisha kuwa kwa pamoja tunaweka mazingira wezeshi na rafiki zaidi kwa wananchi wa pande zote mbili kunufaika zaidi kiuchumi kupitia fursa lukuki zilizopo”. Ameeleza Balozi Fatima Alfeine
Mkutano huo wa siku tatu unashirikisha wadau kutoka Sekta za Diplomasia, Sheria, Ulinzi, Biashara, Kilimo, Biashara, Uwekezaji, Uchumi wa Buluu, ICT na Nishati.
Mkutano wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro ukiendelea jijini Dar es Salaam. |
Mkutano wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro ukiendelea jijini Dar es Salaam. |
Mkutano wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro ukiendelea jijini Dar es Salaam. |
NAIBU KATIBU MKUU MAMBO YA NJE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO UINGEREZA
Written By CCMdijitali on Friday, July 19, 2024 | July 19, 2024
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miradi ya Wizara amekagua miradi ya maendeleo iliyoko jijini London, Uingereza kuanzia tarehe 14 hadi 18 Julai, 2024.
Katika ziara hiyo Kamati imekagua jengo la ofisi, makazi na kiwanja cha serikali. Vilevile, imefanya kikao cha mashauriano na ubalozi na wataalam wa ujenzi na uwekezaji nchini humo juu ya namna bora ya kuendeleza milki hizo za Serikali.
Katika ziara hiyo Kamati pia imekabidhi nyumba moja kwa mtumishi wa Ubalozi ambayo ukarabati wake umekamilika kwa asilimia 100 na hivyo kupunguza gharama za kulipia kodi ya pango kwa Serikali ambayo imekuwa ikilipwa kabla ya kukamilika kwake.
Ziara hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa mpango mahsusi wa Wizara wa kuendeleza viwanja na milki zake zilizopo nje ya nchi, ambao ulielezwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) wakati alipowasilisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 bungeni jijini Dodoma mwezi Mei, 2024.
Ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ikiendelea. |
Picha ya pamoja. |
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFANYA KIKAO KAZI
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kuendeleza ushirikiano katika kazi utakaoleta manufaa makubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Akifungua kikao kazi kati ya Mahakama ya Tanzania, Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar na Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Zanzibar Beach Resort, Mhe. Hemed amesema Taasisi hizo zinapaswa kuwa na maazimio ya pamoja katika kuzifanya maboresho mbali mbali sheria zote zinazohusiana na malipo ya fidia kwa wafanyakazi na taratibu zote zinazotumika katika kutoa huduma hio.
Mhe. Hemed amesema waajiri wote Tanzania Bara na Zanzibar wanapaswa kubeba dhamana kwa wafanyakazi wao pindi wanapopata majanga yatokanayo na kazi kwa kuchukua hatua za haraka ikiwemo kutoa taarikwa kwa WCF na ZSSF ndani ya muda uliowekwa kisheria ili wafanyakazi au wategemezi wao waweze kupata mafao stahiki kwa wakati.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema uwepo wa Majaji wa Mahkama Kuu kwa pande zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao kazi hicho kinatoa fursa kwao kujifunza namna ya kufanya kazi na WCF pamoja na ZSSF hasa katika kuboresha huduma za kimahakama kwa kutambua hatua mbali mbali katika uchakataji wa madai ya wafanyakazi waliopata madhila yatokanayo na kazi wanzozifanya.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewahakikishia washiriki wa kikao kazi hicho kuwa Serikali zote mbili zitaendelea kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kuboresha mahusiano yenye lengo la kuleta ustawi wa wafanyakazi pindi wanapokuwa kazini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana na watu wenye ulemavu MERY MAGANGA amesema vikao kazi kama hivi vinaumuhimu mkubwa sana katika kudumisha Muungano wa Tanzania pamoja na kuimarisha utendaji kazi kwa wafaanyakazi jambo ambalo huleta tija kubwa kwa Taifa.
MAGANGA amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kati ya pande zote mbili za Muungano kwa kuhakikisha sheria ya fao la Fidia linatekelezwa kwa haki na usawa kwa wafanyakazi wote sambamba na kuwataka washiriki wote wa kikao hicho kwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo yale ambayo watakubaliana katika mkutano huo.
Nae Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. MUSTAPHER SIYANI amesema lengo kuu la kikao kazi hicho kufanyika Zanzibar ni kudumisha Muungno na kuweka mazingira bora na rafiki yenye kuvutia wawekezaji hasa pakiwa na mfumo Imara wa utowaji na upatikaniji wa haki nchini.
SIYANI amesema kikao hiki kitawakumbusha Majaji, watendaji wa mahakama na wadau wa haki juu ya utekelezaji wa nguzo ya pili ya upatikanaji wa haki na kuwasaidia katika kutafuta utatuzi wa migogoro ya kazi katika Taasisi mbali mbali zilizopo nchini.
Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. JOHN MDUMA amesema Utiaji wa saini wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja kati ya WCF na ZSSF unathibitisha mahusiano imara waliyonayo kwa muda mrefu yanayodhihirisha utayari wa kuwasaidi wafanyakazi hasa pale wanapopata majanga wakiwa kazini.
Dkt. MDUMA amesema WCF wameona ipo haja na umuhimu wa kuwajengea uwezo Wazanzibari katika kuzifahamu vyema huduma za mafao ya fidia kazini ili kuweza kutoa haki kwa mfanyakazi ama wategemezi wao pindi mfanyakazi atakapopata ajali akiwa kazini.
Katika kikao hicho Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ameshuhudia utiaji wa saini kati ya WCF na ZSSF ya makubaliano ya kufanya kazi kwa ushirikiano jambo ambalo litaleta tija na mafanikio makubwa kwa wafanya kazi wa pande zote mbili za jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR)
Leo tarehe 19. 07. 2024 MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- KIKAO KAZI
..............................................................
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- ZIARA YA KUKAGUA UJENZI WA MIRADI YA ZSSF
Written By CCMdijitali on Tuesday, July 9, 2024 | July 09, 2024
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameuagiza Uongozi wa Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kuwasimamia vyema wakandarasi na washauri elekezi wanaojenga miradi yao ili kuhakikisha wanamaliza kwa wakati uliopangwa na kwa kiwango cha hali ya juu.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbali mbali inayojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).
Mhe. Hemed amesema miradi yote ya kimaendeleo inayojengwa na Serikali inadhamira ya kuwaondolea wanachi changamoto ya makaazi, kuwainua kichumi sambamba na kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo endelevu kwa maslahi ya vizazi vya sasa na baadae.
Mhe. Hemed amesema wakati umefika kwa wakandarasi wanaopewa dhamana ya kujenga miradi ya Serikali kuhakikisha wanaikamilisha kwa wakati uliopangwa na kushindwa kukamilisha kwa wakati ni kuifelisha dhamira njema ya Rais Dkt Hussen Mwinyi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.
Mhe.Hemed amesema kukamilika kwa miradi ya maegesho ya magari iliyopo Kijangwani na Malindi Mjini Unguja na Nyumba za bei nafuu zilizopo viwanja vya Magereza kutawaondolea wananchi changamoto ya makaazi pamoja na msongamano wa kuegesha magari sehemu zisizo salama jambo linalopelekea kupotea kwa haiba ya mji Mji wa Zanzibar.
Sambamaba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesisitiza kuwa Serikali haitakuwa na muda wa nyongeza kwa Mkandarasi yoyote ambae atashindwa kukamilisha miradi aliyopewa kwa wakati na kuwaagiza washauri elekezi kutoa adhabu ya penalt kwa kampuni itakayokwenda kinyume na makubalino ya kimkataba.
Aidha Mhe.Hemed ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kuendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Mwinyi za kuondoa changamoto mbali mbali zinazowakabili sambamaba na kuwaletea maendeleo wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Nae Naibu Waziri wa fedha na mipango Zanzibar Mhe. JUMA MAKUNGU JUMA amesema miradi inayojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) inaendana na dhamira ya viongozi ya kuweka mzingira bora kwa kila mwananchi hivyo Serikali kupitia Wizara ya fedha itahakikisha inasimamia vizuri ujenzi wa miradi hio kwa maslahi ya Taifa.
Mhe. Juma amesema majengo hayo yatawasaidia wafanya biashara kufanya biashara zao bila ya usumbufu wowotea na amewatoa hofu wanachama wa ZSSF kuwa fedha zao wanazochangia katika mfuko huo zipo salama na kila mwanachama atapatiwa haki yake kwa mujibu wa michango aliyochangia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hfadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Bwana Nassor Ameir Shaaban amesema ZSSF imekusudia kujenga vituo vitano(5) vya kisasa vya maegesho ya magari vitakavyotoa huduma ndani ya mji wa Zanzibar.
Amesema ZSSF imedhamiria kuwaondoshea wananchi wa Zanzibar changamoto ya huduma ya usafiri wa daladala ambapo imejipanga kutafuta kampuni ambayo italeta mabasi makubwa na ya kisasa yatakayotoa huduma ya usafiri ndani ya Zanzibar.
Miradi iliyokaguliwa na Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ni pamoja na MRADDI WA ENEO LA BIASHARA NA MICHEZO MBWENI, UJENZI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU ZA MJI WA DKT HUSSEIN MWINYI ZILIZOPO VIWANJA VYA MAGEREZA, UJENZI WA VITUO VYA MAEGESHO YA MAGARI KIJANGWANI NA MALINDI UNGUJA.
WAZIRI BYABATO AIPONGEZA BURUNDI KWA KUDUMISHA AMANI NA USALAMA
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato amepoingeza Jamhuri ya Burundi kwa kuendelea kulinda na kudumisha amani na usalama nchini humo.
Naibu Waziri Byabato amasema hayo alipokuwa akihutubia Jumuiya ya Wadiplomasia na wageni wengine waalikwa kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Vilevile alibainisha kuwa katika kipindi hicho cha miaka 62 dunia imeshuhudi Taifa hilo likipiga hatua muhimu ya maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo siasa na uchumi.
“Hakika mtakubaliana nami kuwa katika kipindi cha miaka 62, Burundi imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika nyanja za kisiasa na kiuchumi. Mathalani, kisiasa tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Amani hapa jijini Dar es Salaam mwaka 2006, Burundi imeweza kudumisha amani na usalama nchini kote pamoja na kukuza demokrasia na utawala bora” Alieleza Naibu Waziri Byabato
Mbali na hayo Waziri Byabato aliongeza kuwa Tanzania na Burundi zimeendelea kuwa na ushirikiano wa karibu wakati wote, ukichagizwa na mkaba uliosaniwa mwaka 1975 wa uanzishaji wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ambao ulifungua ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati ikiwemo elimu, afya, kilimo, biashara na uwekezaji, utalii,nishati, usafirishaji, ulinzi na usalama na masuala ya uhamiaji.
Kwa upande wake Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe. Leontine Nzeyimana alieleza kuwa katika kipindi cha miaka 62 ya uhuru, Taifa hilo linajivunia kuendelea kudumisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Mataifa mbalimbali duniani na nchi jirani katika Kanda ya Afrika Mashariki.
Balozi Nzeyimana aliendelea kubainisha kuwa katika nyanja ya uchumi Burundi inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Tanzania, ambapo mradi wa SGR unatarajiwa kuliunganisha Taifa hilo na Bandari ya Dar es Salaam hivyo kutoa mchango mkubwa katika kurahishisha na kuongeza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Burundi.
Takwimu zinaonyesha kuwa biashara kati ya Tanzania na Burundi inaendelea kukua ambapo ilifikia dola milioni 212.8 mwaka 2022/2023 kutoka dola 61.3 milioni mwaka 2017/2018. Huku takriban asilimia 95 ya mizigo ya Burundi ikipitia Bandari ya Dar es Salaam.
Tanzania na Burundi zinashirikiana kwa karibu katika ngazi za kikanda na kimataifa ikiwemo EAC, ICGRL, AU, UN, Jumuiya ya Nchi zisizofungamana na Siasa za Upande wowote (NAM).
Aidha Naibu Waziri Byabato alisisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Burundi ili kuimarisha zaidi uhusiano kwa manufaa ya pande zote mbili na watu wake. Vile vile, kuendelea kuwa mshirika wa wakati wote na wa kuaminika wa Burundi kwenye masuala ya kikanda na kimataifa.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi iliyofanyika jijini Dar es Salaam
WAZIRI MAKAMBA AMUAGA BALOZI WA DENMARK
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amemuaga Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing – Spandet baada ya kumaliza muda wake wa kuhudumu hapa nchini katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri Makamba amempongeza Balozi Mette kwa kazi nzuri aliyoifanya nchini katika kipindi cha uwakili wake, sio tu kwa kukuza na kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Denmark vilevile kwa mchango wake hadhimu kwenye utekelezaji wa programu na miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ambayo imechangia katika ukuaji wa maendeleo nchini.
Aidha Waziri Makamba amempongeza Balozi Mette kwa mchango wake alioutoa katika kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya TabiaNchi na masuala ya amani na usalama.
Kwa upande wake Balozi Mette ameeleza kuwa licha kuendelea kukua kwa uhusiano wa kidiplomasia bado juhudi zaidi zinahitajika katika kukuza kiwango cha biashara na uwekezaji katika ya Tanzania na Denmark.
Aidha, Balozi Mette ameishukuru Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi mahiri wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa ushirikiano mzuri alioupata wakati wote akitimza majukumu yake hapa nchini.
Natambua kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, licha kumaliza kipindi changu cha kuhudumu kama Balozi, nitaendelea kutoa mchango wangu kwa namna mbalimbali ili kuhakikisha kiwango cha biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Denmark kinaongezeka.Alieleza Balozi Mette
Tanzania na Denmark zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, afya, elimu na biashara na uwekezaji.
VIJIJI 45 VYAWEKEWA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI UVINZA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akisisitiza jambo wakati wa mwanzo wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philio Isdori mkoani Kigoma tarehe 8 Julai 2024. |
Na Munir Shemweta, WANMM UVINZA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesema jumla ya vijiji 45 kati ya vijiji 61 katika wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma vimewekewa mipango ya matumizi ya ardhi.
Mhe. Pinda amesema hayo leo tarehe 8 Julai 2024 katika wilaya ya Uvinza wakati wa mwanzo wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdori Mpanga mkoani Kigoma.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi, mji wa Uvinza kwa sasa unakuwa kwa kasi na wizara yake kupitia Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo iliamua kuviwekea vijiji vya wilaya ya Uvinza Mipango ya Matumizi ya Ardhi ili kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile kilimo na ufugaji.
"Uamuzi wa kuviwekea mipango ya matumizi ya ardhi vijiji 45 katika wilaya ya Uvinza ni njia sahihi ya kupunguza mgongano wa matumizi ya ardhi na zoezi litaendelea katika vijiji vilivyobakia 16 ambavyo viko kwenye mpango kazi " amesema Mhe. Pinda.
Mhe. Pinda alielezea pia mgogoro baina ya wananchi wa kijiji cha Mpeta na Ranchi ya NARCO, mgogoro uliosababishwa na wananchi wa kijiji hicho kutoridhika na hekta 2,500 walizopatiwa kutoka kipande cha ranchi ambapo kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi tayari serikali imesikia kilio cha wananchi hao na kuwapatia hekta nyingine 5,240 ili ziweze kutosheleza mahitaji.
Hata hivyo, amemtaka Mkuu wa wilaya ya Uvinza pamoja na mkurugenzi wa halmashauri kukaa na viongozi wengine wa wilaya hiyo kuhakikisha hekta zilizotolewa zinagawiwa kwa wananchi kwa lengo la kukidhi mahitaji.
Akikeukia mgogoro baina ya wilaya ya Kasulu na Uvinza kuhusiana na kitalu cha uwindaji alichopatiwa mwekezaji, Mhe. Pinda amemueleza Makamu wa Rais kuwa, kitalu alichopewa muwekezaji ramani yake ina mapungufu hivyo ameielekeza ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Kigoma kukutana na halmashauri za wilaya husika husika ili kupata tafsiri sahihi ya ramani kwa lengo kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango ameanza ziara yake mkoani Kigoma leo tarehe 8 Julai 2024 ambapo mbali na mambo mengine amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile umeme na barabara.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akisisitiza jambo wakati wa mwanzo wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philio Isdori mkoani Kigoma tarehe 8 Julai 2024. |
Sehemu ya wananchi waliojitokeza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango tarehe 8 Julai 2024 |
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya mawaziri na viongozi wengine wa mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango (hayupo pichani) wakati wa mwanzo wa ziara yake mkoani Kigoma tarehe 8 Julai 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI) |
DKT. MPANGO AAGIZA KUKAMILIKA UJENZI WA BARABARA YA MALAGARASI -UVINZA IFIKAPO MACHI 2025.
Written By CCMdijitali on Monday, July 8, 2024 | July 08, 2024
“Hii barabara imesuasua sana hasa kipindi cha mvua, na huku Kigoma bado tunapata mvua nyingi kwa hiyo Waziri tutumie kipindi hiki cha kiangazi kukimbiza hii barabara iishe kama ulivyoahidi na sisi tupite hapa tukiwa tumevaa suti, Simamieni hili Waziri pamoja timu yako”, ameeleza Dkt. Mpango.
WAZIRI MAKAMBA AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI 15 WA EAC
Written By CCMdijitali on Saturday, July 6, 2024 | July 06, 2024
Mkutano kazi huo umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 07 Mei, 2024.
Mawaziri kutoka nchi Nane Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki za Burundi, DRC, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Uganda, na Mwenyeji Tanzania wanahudhuria mkutano huo. Mkutano huo pia unahudhuriwa na Makatibu Wakuu kutoka wizara hizo pamoja na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.