MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
JAMII MPYA TANGA YAANDAA KONGAMANO LA KUMPONGEZA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN
Written By CCMdijitali on Monday, August 28, 2023 | August 28, 2023
Dc Kilindi alishukuru shirika lisilo la kiserikali World Vision ADP Mgera
ZIARA YA MAKAMU WA PILI JIMBO LA KIWANI NA CHAMABNI
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla akimkabidhi Kadi ya CCM Ndg. Said Zubeir Muhammed (wape Salam) alierejesha Kadi ya ACT Wazalendo na kuamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Wanachama wa CCM wakila kiapo cha utii mara baada ya zoezi la kukabidhiwa kadi wanachama wapya waliojiunga CCM wakati wa ziara ya kuimarisha Chama Jimbo la Chambani.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amewataka Viongozi na wanachama wa CCM kuongeza nguvu katika kukiimarisha Chama kwa kuweka mipango na mikakati sahihi itakayowavutia wananchi na wapenda Amani itakayowavutia wapinzani kujiunga na CCM.
Akiendelea na ziara ya kuimarisha Chama katika Jimbo ya Chambani na Jimbo la Kiwani Mhe. Hemed amewataka Wananchi kujiunga na CCM ambayo inatekeleza ahadi zake kwa kasi kubwa na kuwaletea maendeleo ya haraka.
Sambamba na hayo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewataka viongozi wa CCM kuendelea kuinadi na kuitekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kutekeleza miradi mbali mbali ya kimkakati na maendeleo ambayo itawanufaisha wazanzibari wote inayotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Amewasisitiza Viongozi wa Kamati za Siasa za Jimbo, Wilaya na Mkoa kuendelea kudumisha umoja na mshikamano uliopo ndani ya Chama kwa kufuata miongozo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Amesema CCM itaendelea kutekeleza ahadi zake kwa kuziondoa changamoto zilizopo na zitakazojitokeza ikiwa ni pamoja na kuajiri Walimu na Madaktari walio na sifa katika fani hzio
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefafanua kuwa Serikali itazijenga barabara zote kwa kiwango cha Lami sambamba na kupeleka miundombinu ya maji katika vijiji ambavyo huduma hiyo haijafika kikiwemo kijiji cha Miamboni ambacho kimekosa huduma hiyo kwa muda mrefu.
Mhe.Hemed ameeleza kuwa Jimbo la Kiwani ni miongoni mwa Majimbo yaliyobahatika kupata miradi mingi ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya Kendwa, ujenzi wa skuli Nne za Ghorofa pamoja na ujenzi waTangi la Maji safi na Salama lenye ujazo wa Lita Milioni moja.
Amesema kutokana na maendeleo makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt. Hussen Ali Mwinyi kuna kila sababu Wananchi kuwapa kura nyingi ifikapo 2025 ili waweze kuendelea kuwafanyia mambo mazuri kwa wakati sahihi .
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg Abdallah Muhamed Madishi amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa maamuzi yake ya kuwajengea Soko kubwa la Kisasa la Mtambile ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara na wajasiriamali kufanya shughuli zao kwa ufanisi na Wananchi kupata huduma stahiki katika sehemu sahihi.
Ameeleza kuwa juhudi hiyo inadhihirisha azma ya Rais Dkt. Mwinyi ya kuwawekea mazingira mazuri wajasiriamali na wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika sehemu salama na kuacha na kufanya biashara sehemu zisizo rasmi
Nae Muwakilishi...... Mhe. Maryam Azzan na Mhe. Shadya Muhamed wameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kufikisha huduma mbali mbali kwa wananchi ikiwemo Afya, elimu, maji safi na Salama, umeme na barabara ili wananchi waweze kupata huduma bora kwa masafa ya karibu na maeneo yao.
Wameeleza kuwa ni wajibu wa Viongozi wa CCM kuanzia Shina hadi Taifa kufuata nyayo za Viongozi wakuu wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuhubiri Amani na utulivu pamoja na kueleza mema yanayofanywa na Serikali zao.
Katika ziara hiyo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amepokea zaidi ya Wanachama 500 wakiwemo wanachama wapya na waliotoka vyama vya upinzani.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao Ndg. Said Zubeir Muhamed (wape Salam) kutoka Chama Cha ACT Wazalendo ameeleza kuwa ameamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kutokana na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na dhamira thabiti ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwaletea maendeleo wazanzibari wote bila ya kujali tofauti zao za kisiasa.
Ziara hiyo ni muendelezo wa Ziara ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Hemed Suleiman Abdulla kutembelea majimbo yote ya hamsini ya uchaguzi ambapo tayari ameshatembelea Majimbo arobaini na Tano kwa lengo la kuimarisha Chama.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
28 Agosti, 2023
KATIBU MKUU YAKUBU AWAPA NONDO ZA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU MAAFISA UTAMADUNI NA MICHEZO
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Saidi Yakubu amefungua kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo leo Agosti 27, 2023 mkoani Njombe ambapo ametoa maagizo manne makubwa kwa maafisa hao ikiwemo kuongeza ushiriki wa jamii katika michezo na kuibua vipaji vya Utamaduni, Sanaa na michezo katika maeneo yao.
Amewaagiza maafisa hao, kuandaa mikakati itakayosaidia vijana kutumia majukwaa mbalimbali kuonesha vipaji vyao pamoja na kuandaa mkakati wa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili ambao umeanza kujitokeza katika jamii.
"Serikali inaendelea kuongeza wataalamu wa michezo kupitia Chuo Cha Michezo Malya ambacho sasa kinafanyiwa maboresho makubwa ikiwemo ujenzi wa hosteli mpya ambayo itasaidia ongezeko la udahili wa wanafunzi chuoni hapo", amesema Katibu Mkuu Yakubu.
Bw. Yakubu ametoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha Kitengo cha Utamaduni na Michezo kinatengewa bajeti ya kutosha ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Katibu Mkuu Yakubu ametumia nafasi hiyo kugawa vifaa vya michezo ikiwemo mipira 54 ya mchezo wa Mpira wa Miguu, Kikapu na Wavu ambayo itagawiwa kwa mikoa yote nchini kwa ajili ya mashindano ya Samia Cup yanayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.
"Wizara ya Fedha watakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzingatia sheria, kanuni, taratibu pamoja na miongozo"
"Kesi yeyote ya ardhi itakayoonekana watendaji katika serikali au wenyeviti wa vijiji wanahusika wahusika hao watafikishwa mahakamani kwa majina yao na sio taasisi"- DC Kilindi, Tanga
DKT. TAX AWAPA WAKUU WA MIKOA MBINU ZA KUTEKELEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI
Written By CCMdijitali on Sunday, August 27, 2023 | August 27, 2023
Rais Mwinyi amesema kuna haja kwa Zanzibar kuongeza vivutio vingi vya utalii kwa kubuni matukio maalumu ya kuwavutia wageni wengi na kuviimarisha vivutio vya asili vilivyomo Tanzania.
Written By CCMdijitali on Saturday, August 26, 2023 | August 26, 2023
WAZIRI MABULA AWASILISHA VIPAUMBELE VYA SEKTA YA ARDHI KATIKA SEMINA YA MA-RC NA MA-RAS
KIBAHA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maedeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amewasilisha vipaumbele vya wizara yake kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika semina ya uongozi katika Chuo cha Mwalimu Nyerere kilichopo kibaha mkoani Pwani.
Katika wasilisho lake leo tarehe 26 Agosti 202, Waziri Mabula alizungumzia masuala ya ukusanyaji mapato yatokanayo na sekta ya ardhi, mipango miji pamoja na maeneo ya uwekezaji ambayo yote wakuu hao wa mikoa wanalo jukumu la kusimamia kwenye mikoa yao.
Dkt Mabula aliwataka wakuu wa mikoa kusaidia katika kuongeza hamasa katika suala la ukusanyaji mapato ya serikali yatokanayo na sekta ya ardhi.
"Niwaombe mkasimamie mikakati ya ukusanyaji maduhuli hayo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wananchi waliopo katika maeneo kulipa kodi ya pango la ardhi.
Kwa mujibu wa Dkt Mabula Rais Samia alitoa msamaha wa riba ya kodi kwa miezi 10 mafanikio yalionekana japo si kwa kiwango kilicho tarajiwa.
Pia aliwataka wakuu wa mikoa kuzisimamia halmashauri katika kutenga fedha katika bajeti za maendeleo ya sekta ya ardhi ili kuhakikisha ardhi inapangwa, kupimwa na kumilikisjwa.
"Halmashauri zitambue kuwa jukumu hilo bado ni la kwao na wanahitaji kuendelea kushiriki kikamilifu katika kutenga fedha ili kutekeleza majukumu yao na kuwezesha watumishi waliopo katika halmashauri kufanya kazi" alisema Dkt Mabula.
--------MWISHO------
Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao cha wakuu wa mikoa na makatibu tawala kinachoendelea katika chuo cha uongozi cha Mwalimu J K Nyerere kibaha mkoani Pwani tarehe 26 Agosti 2023.
Sehemu ya washiriki semina ya uongozi inayofanyika katika chuo cha uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kibaha mkoa wa Pwani.
Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao cha wakuu wa mikoa na makatibu tawala kinachoendelea katika chuo cha uongozi cha Mwalimu J K Nyerere kibaha mkoani Pwani tarehe 26 Agosti 2023.
Baadhi ya wakuu wa mikoa wakifuatilia wasilisho la Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakati wa semina ya uongozi inayofanyika katika chuo cha uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kibaha mkoa wa Pwani. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)



