MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Mkutano wa 14 wa Mapitio na Mpango wa pamoja wa Utekelezaji katika Sekta ya Afya - ZANZIBAR
Written By CCMdijitali on Thursday, February 20, 2025 | February 20, 2025
Na Rahma Khamis Maelezo 20/2/2025
Makamu wa Pili wa Rais Mhe Hemed Suleiman Abduulla amewataka watoa huduma za afya kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ili kupunguza malalamiko yanayotolewa na wananchi dhidi yao.
Wito huo ameutoa katika Ukumbi wa Madinat - Albahr Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akifungua mkutano wa 14 wa Mapitio na Mpango wa pamoja wa Utekelezaji katika Sekta ya Afya.
Amesema kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ni kufuata msingi wa maadili ya kazi ya utoaji wa huduma za afya kutasaidia kupunguza malalamiko yanayotolewa na baadhi ya hudumu wakati wa kuwahudumia wagonjwa.
Mhe. Hemed amewaomba Washirika wa Maendeleo kuelekeza nguvu zao katika kuisaidia Wizara ya Afya kwa kuweka miundombinu ya kidijitali ya ukusanyaji wa taarifa za afya ili juhudi zinazochukuliwa na Serikali na Wadau ziweze kutatua changammoto ikiwemo ya upatikanaji wa taarifa sahihi za takwimu za afya.
Naye Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui amesema kuwa bila ya kuimarisha afya ya msingi hawatafikia malengo hivyo wataendelea kuimarisha miundombinu na vifaa tiba vya kisasa ili kutoa huduma bora kwa jamii.
Waziri Mazrui ameeleza kuwa vifo vya watoto vimepungua kutoka 1940 kwa mwaka 2023 hadi kufikia 1847 kwani lengo la Serikali ni kupunguza vifo vya mama na mtoto
Aidha amewasisitiza madaktari na wataalamu wa Afya kubuni miundombinu bora itakayoweza kuwasaidia mama wajawazito ili kupunguza kifafa cha mimba sambamba na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt Amuor Suleiman amesema kuwa kwa mwaka 2022 hadi 2024 Wizara imefanikiwa kutoa huduma za afya katika vituo vya ngazi ya chini (vituo vidogo) pamoja na kuanzisha mfuko wa huduma za afya kwa ajili ya kutoa huduma bora nchini ambapo Serikali imetenga bilioni 344 kwa Sekta ya Afya ili kuimarisha afya za wananchi.
Aidha amefahamisha kuwa Wizara imefanikiwa kuzalisha hewa tiba pamoja na kununua Magari makubwa ambayo yanatoa huduma za afya, ambulance kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii, kununua vifaa vya kugundukia maradhi yanayowakabili wananchi ikiwemo kansa Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeimarika.
Akizungumzia maradhi yanayoongoza hadi kufikia sasa ni pamoja na maradhi ya mfumo wa hewa, maradhi ya kuharisha pamoja maradhi ya UTI, ipo haja ya kutilia mkazo kwa mwaka ujao ili kupunguza matatizo hayo.
Dk Amour ameeleza kuwa kwa upande wa watoto chini ya miaka mitano matatizo ya mfumo wa kupumua pamoja na maradhi ya ngozi ambapo maradhi yanayoongoza kusababisha vifo ni maradhi yasiyoambukiza hivyo mikakati madhubuti inahitajika ili kupunguza idadi ya vifo hivyo ikifuatiwa na vifo vya watoto wachhanga.
Mkutano huo umewashirikisha wadau mbalimbali wa Afya wakiwemo washirika wa kimataifa ambapo Kaulimbiu ya mkutano huo ni "Uwepo wa Mfumo Bora wa Huduma za Afya ya msingi uliyoungwanishwa,ubunifu unaojengwa kwa ushahidi ili kufikia Upatikanaji wa Afya Jumuishi kwa wote”.
RAIS MWINYI AISHUKURU WB KWA MSAADA WA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR
Written By CCMdijitali on Tuesday, February 18, 2025 | February 18, 2025
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Benki ya Dunia kwa Msaada wa kiasi cha Dola Milioni 100 kwa ajili kuimarisha Miundombinu ya Sekta ya Afya hapa nchini.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Mwa Afrika Milena Stefanova na ujumbe wake, Ikulu Zanzibar tarehe 18 Februari 2025.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameuelezea Ujumbe huo kuwa Serikali ina Malengo Mahsusi ya kuifanya Zanzibar kuwa kituo Bora cha Matibabu kwa Nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa Ujumla na kuipongeza Benki ya Dunia kwa kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.
Naye Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini Mwa Afrika Milena Stefanova ameeleza kuwa Benki hiyo inaridhika na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Zanzibar za kuimarisha huduma za Afya na kuahidi kuendelea na misaada kwa ustawi wa watu wake.
Kwa upande mwingine Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazroui ameeleza kuwa Wizara hiyo inajipanga vema kuhakikisha fedha hizo zinaenda kutumika kufanikisha lengo la kuifanya Zanzibar kuwa kituo cha pekee cha Utalii waTiba na Matibabu na Mafunzo ya Afya ( HEALING ISLAND)kama zilivyo nchi za India na THailand
WASIRA AZUNGUMZA NA BALOZI WA JAMHURI YA KOREA NCHINI.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Ndg. Stephen M. Wasira amefanya mazungumzo na Mhe. Eunju Ahn, Balozi wa Jamhuri wa Korea Nchini, tarehe 18/2/2025 katika Ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamebadilishana mawazo katika namna mbalimbali yanayohusu ushirikiano wa nchi ya Tanzania na Korea.
WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA UMOJA WA ULAYA NCHINI.
- Pia ateta na Balozi wa Jamhuri ya Korea
- Awaahidi kuendeleza ushirikiano
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Februari 18, 2025 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Christine Grau, Ofisini ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tanzania itaendelea kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji na nchi za Umoja wa Ulaya.
“Inatia faraja sana kuona kuna ukuaji wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na nchi za Umoja wa Ulaya, Umoja wa Ulaya umewekeza takriban euro bilioni tatu nchini, hii kwa kiasi kikubwa imechangia kutengeneza ajira na makusanyo ya kodi. ”
Amesema kuwa Tanzania itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuzivutia sekta binafsi kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tanzania inathamini msaada mkubwa ambao unatolewa na Umoja wa Ulaya katika kuchangia shughuli za maendeleo nchini.
“Katika kipindi cha 2021-2027, Umoja wa Ulaya umetenga euro milioni 703 ili kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, tunakushukuru hasa kwa kujitolea kwenu kuimarisha ushirikiano huu. ”
Awali, Mheshimiwa Majaliwa alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Ahn-Eun-Ju ambaye alimweleza kuwa Tanzania inajivunia ushirikiano na nchi hiyo kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.
“Tanzania na Jamhuri ya Korea zinaushirikiano mkubwa wa kibiashara kwa miaka mingi, mnamo mwaka 2023, kiwango cha ufanyajibiashara kilifikia dola milioni 672.7, ikilinganishwa na dola milioni 280.4 mwaka 2022.”
“Tunatambua kuwa makampuni ya Jamhuri ya Korea yamewekeza katika sekta mbalimbali nchini Tanzania, kama vile viwanda, usafirishaji na ujenzi, hivyo kuchangia maendeleo ya nchi zetu. Tunathamini uwekezaji huu. ”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alimweleza balozi huyo kuwa aone namna ya kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata nafasi za kazi nchini Korea hasa kwenye sekta ya uzalishaji. “Kwa upande wetu sisi tutahakikisha Watanzania wanakuwa na vigezo stahiki vinavyohitajika ili waweze kufanya kazi. ”
Kwa upande wake Balozi Ju alimweleza Mheshimiwa Majaliwa kuwa katika kipindi chote atakachohudumu kama balozi nchini atahakikisha anasimamia na kuendeleza masuala ya uwekezaji kwa faida ya nchi zote mbili.
MKUTANO WA ZEC
Na Maelezo Zanzibar 17/02/2025
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jaji George J. Kazi amewataka wananchi waliofikia umri wa kupiga kura kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kupata haki yao ya msingi.
Jaji Kazi ameyasema hayo katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar katika mkutano na wadau kuhusu Uandikishaji wapiga kura wapya wa awamu ya pili.
Amesema kila mwananchi aliyefikia umri wa mika 18 ana haki ya kuandikisha katika daftari la wapiga kura na kufuata vigezo vya kuwa mpiga kura
Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa jumla ya wapiga kura wapya 78922 nchini wanaokadiriwa kuandikishwa katika daftari la wapiga kura kwa mujibu wa takwimu za sensa ilifanyika 2022.
Amesema zoezi la uandikishaji wapiga kura wapya awamu ya Pili limeshakamilika kisiwani Pemba ambapo zoezi limefanyika kwa Amani na utulivu kwa wananchi wenye sifa walipata haki yao hiyo ya msingi.
Ameeleza kuwa upande wa Unguja zoezi hilo linatarajiwa kuanza tarehe 22 mwezi huu huko wilaya Kaskazini ‘A’ na kumalizika tarehe 17 mwezi wa Machi katika Wilaya ya Mjini.
Aidha Jaji Kazi amewasisitiza wanasiasa kuacha kutumia kauli za uchochezi na viashiria vya uvunjifu wa amani ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa Amani na utulivu na kuwakilisha wakala wao katekeleza majukumu yao.
Akitoa Mada kuhusu Taarifa na Utaratibu wa uandikishaji wa wapiga kura awamu ya pili na uendeshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2025 Mkurugenzi Tume ya Uchaguzi Thabit Idarous Faina amesema uandikishaji wapiga kura wapya utafanyika katika vituo vilivyotangazwa na Tume mbele ya mawakala wa uandikishaji na kila mwananchi atakaefika kituoni kuomba kuandikishwa atawasilisha kitambulisho cha Mzanzibar mkaazi kwa karani muandikishaji.
Nae mwasilishaji kutoka Kurugenzi ya Huduma za sharia Ndugu Maulid Ame Mohamed amesema uandikishaji na uendelezaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Zanzibar umeainishwa na kufafanuliwa katika kifungu cha 7(1) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 kimetoa haki kwa kila Mzanzibari aliyetimiza umri wa miaka 18 kupiga kura kwa uchaguzi unaofanyika Zanzibar.
Amefafanua kuwa kifungu hicho kinaeleza kuwa Kila mzanzibar aliyemitiza umri wa miaka 18 anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Zanzibar na wananchi na haki hiyo itatumiwa kwa kufuata masharti ya kifungu cha (2) cha kifungu hicho pamoja na masharti mengine Katika hayo nayo ni sheria inayotumika Zanzibar kuhusu mambo ya uchaguzi.
Nao washiriki wa mkutano huo wameomba watu wenye kupatiwa mazingira rafiki na kuzingatia uwiano katika zoezi hilo pamoja na wamesisitiza kudumisha katika kipindi chote cha uandikishaji hadi kufikia uchaguzi mkuu.
Akifunga mkutano Makamu mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Aziza Iddi Suweid amewataka wadau hao kuhamasisha jamii kuhusiana na zoezi zima la uandikishaji pamoja na kuvisisitiza vyombo vya habari kusikiliza na kufuata utaratibu uliowekwa na Tume ya Utangazaji katika kutoa taarifa kipindi chote cha uchaguzi ili kwenda sambamba sharia zilizowekwa na Tume hiyo.
Mkutano huo umewashirikihsa wadau mbalimbali wa Uchguzi vikiwemo vyombo vya Usalama, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, vyama vya siasa, asasi za kiraia, watu wenye ulemavu pmoja na taasisi za habari wenye kauli mbiu "Kura haki yako, Amani wajibu wako’’
EAC YAIPONGEZA TANZANIA KWA MAANDALIZI YA KONGAMANO NA MAONESHO YA PETROLI
Written By CCMdijitali on Friday, February 14, 2025 | February 14, 2025
• Tanzania, Rwanda na Uganda zakubaliana kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa Kufua Umeme Nsongezi wa 39MW
Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la Jumuiya ya Afrika Mashariki umeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukamilisha maandalizi ya Kongamano na Maonesho ya 11 ya Petroli ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika tarehe 5 hadi 7 Machi 2025 jijini Dar es Salaam.
Pongezi hizo zimetolewa kwenye mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.
Uenyeji wa Tanzania katika Kongamano hilo unatokana na Maamuzi ya Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati uliofanyika Februari 14, 2024 ambao uliamua Tanzania kuwa Mwenyeji wa Kongamano na maonesho hayo.
Kongamano na Maonesho hayo ni mkakati unaolenga kutangaza fursa zilizopo katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu rasilimali za mafuta na gesi asilia na kuielezea jiolojia ya ukanda wa Afrika Mashariki ili kuvutia uwekezaji, kuendelezaji wa miundombinu, udhibiti wa uharibifu wa mazingira, usimamizi wa taarifa za mafuta na gesi asilia.
Pia linalenga kutangaza maeneo mapya ya utafutaji na kutangaza maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya nishati katika ukanda.
Malengo mengine ni kubadilishana uzoefu kuhusu sera, sheria, kanuni na utaalamu unaotumika kwenye sekta ya nishati, kuhamasisha uwekezaji, utafutaji, uzalishaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia. Vilevile Kongamano hilo linatoa fursa ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Kongamano na maonesho hayo yanatoa fursa adhimu kwa Tanzania kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya Nishati hususan katika sekta ndogo ya mafuta na gesi na hivyo kuongeza wigo wa kupata wawekezaji kwenye sekta hiyo.
Mbali na hayo, Mkutano 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC limepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali katika sekta ya nishati, petroli na madini ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Nsongezi wenye Megawati 39 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera utakaotelezwa kwa pamoja baina ya Tanzania, Rwanda na Uganda.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini uliongozwa na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb.), Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (Mb.), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi- Zanzibar Bw. Zahor Alharousy na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
| Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC uliofanyika jijini Arusha |
| Meza Kuu wakiongoza mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea katika Makao Mkuu ya Jumuiya jijini Arusha. |
![]() |
| Ujumbe wa Tanzania, Uganda na Rwanda wakionesha hati ya makubaliano (MOU) ya ujenzi wa Kufua Umeme wa Nsongezi 39MW. |
MAJALIWA AITAKA TARURA KUWASIMAMIA WAKANDARASI BINAFSI
Written By CCMdijitali on Thursday, February 13, 2025 | February 13, 2025
▪️Asisitiza Serikali itaendelea kuwawezesha wawekezaji wazawa
▪️Aeleza mpango wa Serikali wa kukabiliana na ugonjwa wa Malaria nchini
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ihakilishe inatoa kandarasi za ujenzi na ukarabati wa barabara kwa wakandarasi wenye uwezo wa kujenga kwa viwango vinavyoendana na thamani ya fedha.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Februari 13, 2025) wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Abbasi Tarimba aliyehoji kwanini Serikali isianze kutumia vikosi kazi vya Manispaa au TARURA badala ya wakandarasi binafsi katika ukarabati wa barabara zilizoharibika, katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, bungeni jijini Dodoma.
"Tunaitaka TARURA iwasimamie wakandarasi binafsi wanapopewa kazi, wawe na uwezo wa kujenga barabara za kudumu kwa mujibu wa viwango vilivyopo ili barabara ziweze kutumika kwa muda mrefu."
Amesema kuwa awali mfumo wa ujenzi wa barabara za vijijini uliokuwa unaruhusu Halmashauri kukarabati barabara zake ulibaini kuwa na mapungufu hasa kutokana na uwezo tofauti wa kifedha wa baadhi ya Halmashauri.
“Serikali iliwasikiliza waheshimiwa Wabunge ambao wakati wote mlipokuwa mnaomba baadhi ya barabara zenu kwenye Halmashauri zihamishiwe TANROADS, kutokana na maombi ya mara kwa mara tuliamua kuunda TARURA inayoshughulikia barabara za vijijini na mijini na inafanya vizuri.”
Kadhalika Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa fedha kwa TARURA kwa ajili ya matengenezo ya muda mfupi. “TARURA tumieni fedha hii vizuri ili kufanya ukarabati kwenye barabara zenye uhitaji wa kukarabatiwa ili ziendelee kutumika.”
Wakati huohuo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya udhibiti wa ugonjwa wa Malaria ikiwemo uendeshaji wa kampeni ya usafi ambayo inagusa pia maeneo yenye mazalia ya mbu. “Pia tunaendelea na utoaji wa neti kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kujikinga na Malaria”.
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa hamasa kwa wawekezaji kujenga viwanda vya kutengeneza dawa za kutibu ugonjwa malaria na za kupuliza jwenye mazalia ya vijidudu vya Malaria.
“Wengi mnafahamu kuwa pale Kibaha mkoani Pwani tunacho kiwanda cha kutengeneza dawa za kunyunyiza kwenye mazalia ya mbu, Halmashauri sasa zinapaswa kutenga fedha ili kwenda kununua dawa na kunyunyiza kwenye maeneo yote yenye mazalia ya mbu. ”
Akijibu Swali la Mwanaisha Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuwalinda na kujenga ushindani wa wawekezaji wazawa, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imetengengeza mazingira nafuu ya uwekezaji kwa wazawa kwa kupunguza kiwango cha uwekezaji kutoka Dola laki moja hadi dola elfu hamsini.
“Tumeendelea pia kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara kwa wazawa ikiwemo kupunguza kiwango cha kodi kwa bidhaa zinazozalishwa ndani na hata mchakato wa upataji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji. ”
BALOZI NCHIMBI: CCM KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA NDANI NA NJE
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza dhamira yake ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa ndani na kimataifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
CCM ambacho ni chama tawala nchini kimeeleza kuwa kitasimamia Serikali ili kuendeleza uhusiano mzuri na mataifa na taasisi mbalimbali, ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, alipokutana kwa nyakati tofauti na mabalozi wa Korea Kusini, Norway na Uingereza katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi, tarehe 13 Februari 2025.
Katika mazungumzo yake na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Ahn Eunju, Balozi Nchimbi alisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Korea Kusini, hasa katika nyanja za maendeleo ya kiuchumi na teknolojia.
Katika mazungumzo yake na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tones Tinnes, Balozi Nchimbi alibainisha kuwa Norway ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania, huku uhusiano wao ukiwa umejengwa katika misingi imara kwa miongo mingi.
Vilevile, katika mazungumzo yake na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Marianne Louise Young, Balozi Nchimbi alisema kuwa uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Uingereza, pamoja na ushirikiano wa karibu na Serikali ya Chama cha Labour, unalenga kuhakikisha wananchi wa pande zote mbili wananufaika na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Kwa nyakati tofauti, katika mazungumzo yao na Katibu Mkuu wa CCM, mabalozi hao walipongeza maamuzi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliomchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Nchimbi kuwa mgombea mwenza, na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM.
WAZIRI KOMBO AZUNGUMZA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Elias Magosi pembezoni mwa Kikao cha 46 cha Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika kilichofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 13 na 14 Februari, 2025.
Mazungumzo ya viongozi hao yaliangazia juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano ili kujenga mtangamano imara wenye amani na usalama ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kukuza uchumi katika kanda ya SADC na Afrika kwa ujumla.
Aidha, Waziri Kombo amempongeza Mhe. Magosi kwa ushindi uliopatana kwa kanda ya kusini kufuatia uchaguzi uliofanyika katika kikao hicho cha Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika ambapo ukanda huo umefanikiwa kuibuka na ushindi wa nafasi tano (5) katika taasisi za Umoja huo.
Pamoja na masuala mengine viongozi hao pia wamejadili juu ya mandalizi ya mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika pembezoni mwa Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia.










.jpg)









.jpeg)




.jpeg)

.jpeg)






.jpg)
.jpg)
.jpg)




,%20Balozi%20Dkt.%20Emmanuel%20John%20Nchimbi,%20akizungumza%20na%20Balozi%20wa%20Jamhuri%20ya%20Korea,%20Mhe.%20Ahn%20Eunju,%20walipokutana%20kwa%20ajili%20ya%20mazungumzo,%20Ofisi%20Ndogo%20ya%20Makao%20Makuu%20ya%20CCM,%20Lum%20(1).heic)
,%20Balozi%20Dkt.%20Emmanuel%20John%20Nchimbi,%20akizungumza%20na%20Balozi%20wa%20Jamhuri%20ya%20Korea,%20Mhe.%20Ahn%20Eunju,%20walipokutana%20kwa%20ajili%20ya%20mazungumzo,%20Ofisi%20Ndogo%20ya%20Makao%20Makuu%20ya%20CCM,%20Lumumba.heic)







