CPA MAKALLA: CCM ITAWALETEA WAGOMBEA WASIO NA MAKANDOKANDO

  Na Richard Mwaikenda, Mwanza   Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akiwaahidi wananchi kwa...

Latest Post

Mwenyekiti wa Chipukizi Kata ya Sekei awa kivutio kwenye Semina Kata ya Sekei,Jijini Arusha.

Written By CCMdijitali on Friday, April 29, 2016 | April 29, 2016

  • Awataka viongozi kufuatilia kwa karibu Utekelezaji wa Ilani ya CCM,kwa kupata za taarifa ya kila baada ya miezi mitatu.

  • Awataka Viongozi kufanya ziara za kutembelea miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.

  • Awasihi viongozi kuwa karibu na Wananchi kwa kuwatembelea,kusikiliza kero zao na kuzitafutia majawabu.

  • Awataka Viongozi wote kutimiza Haki na Wajibu wa Mwanachama,Malengo na Madhumuni ya CCM na Masharti ya Uanachama

Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Sekei Ndg Said Abdul Said,Mwenyekiti wa Chipukizi Kata ya Sekei Bi Nasra ,Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua na baadhi ya viongozi wa UVCCM Kata ya Sekei,mara baada ya semina iliyofanyika 28/04/2016, kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Kata ya Sekei.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akitoa ufafanuzi wa Katiba ya CCM juu ya Haki na Wajibu wa Mwanachama wa CCM.

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akisisitiza jambo kwenye  ziara ya Kujenga Chama Kata ya Sekei 28/04/2016




Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akiwataka Viongozi wa ngazi wa ngazi zote kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kupata taarifa za kila baada ya miezi mitatu,kama inavyoelekezwa kwenye Ilani aliyoishika mkononi kwenye ziara ya Kujenga Chama Kata ya Sekei 28/04/2016
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha ndani ya Jiji la Arusha 28/04/2016, kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Kata ya Sekei.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha ndani ya Jiji la Arusha 28/04/2016, kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Kata ya Sekei.

Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Kata,wakifuatilia kwa makini.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha ndani ya Jiji la Arusha 28/04/2016, kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Kata ya Sekei.
Ndg Badi Mushi,Balozi akitoa neno la kushukuru na kupongeza Uongozi wa CCM Wilaya ya Arusha,kwa semina nzuri ya kujenga Uhai wa Chama.
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Kata,wakifuatilia kwa makini.
Ndg Chifu Maswanya, akitoa neno la kushukuru na kupongeza Uongozi wa CCM Wilaya ya Arusha,kwa semina nzuri ya kujenga Uhai wa Chama.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Sekei Ndg Khalid Issa,akifungua kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha ndani ya Jiji la Arusha 28/04/2016, kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Kata ya Sekei.

Mwenyekiti wa Chipukizi Kata ya Sekei Bi Nasra na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua ,mara baada ya semina iliyofanyika 28/04/2016, kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Kata ya Sekei.
Mwenyekiti wa Chipukizi Kata ya Sekei Bi Nasra ,Kiongozi wa UVCCM Kata ya Sekei Ndg Godliving Kissilana Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua ,mara baada ya semina iliyofanyika 28/04/2016, kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Kata ya Sekei.

Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha / Ndg jasper Kishumbua

MAMA MARIA ALIPOTEMBELEA DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI

Written By CCMdijitali on Thursday, April 28, 2016 | April 28, 2016

 Mama Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa na mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam. Mama Maria, ambae hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye furaha kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka mingi iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina la Mwalimu na siyo yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na nvijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa..
PICHA NA IKULU


Mke wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini Jijini Dar es salaam na kuipongeza serikali na wananchi wote wa Tanzania kwa kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo kubwa na la kisasa kwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.

Mama Maria Nyerere aliyeongozana na Mwanae Mheshimiwa Makongoro Nyerere amesema kukamilika kwa daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 254.12 kumekamilisha mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja katika eneo hilo la mkondo wa bahari lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti haikuwezekana.

Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuamua Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere kwa heshimu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na amebainisha kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi vijavyo kutambua juhudi zilizofanywa na mmewe katika ujenzi wa nchi.

“Mimi ninamshukuru sana Rais kwa maana ilikuwa lipewe jina lake, lakini yeye Mungu akamjaalia akasema kwamba hapana tukumbuke tulikotoka, kwa hiyo najisikia vizuri sana, na familia nayo inajisikia vizuri sana, lakini zaidi na watanzania wanajisikia vizuri sana, kwa maana watakuwa wanaulizana Nyerere alikuwa ni nani?” Amesisitiza Mama Maria Nyerere.

Daraja la Nyerere lenye urefu wa meta 680, upana wa meta 32, njia sita za magari na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5, lilifunguliwa na Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 19 Aprili, 2016 na linakuwa kiunganishi muhimu kati ya Kigamboni na katikati ya Jiji la Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016

Singapore kuboresha Bandari ya Dar

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia ) na ujumbe wake kabla ya mazungumzo yao , Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Habari leo

WAZIRI wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dk Koh Poh Koon amesema wamepanga kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuwa kiunganishi cha biashara kati ya nchi hiyo na mataifa mengine ya Afrika Mashariki (EAC).

Dk Koon aliyasema hayo jana wakati alipomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma, na kwamba Singapore ipo tayari kutoa fursa kwa wataalamu wa Tanzania kwenda kufanya kazi katika Bandari ya Singapore ili kupata uzoefu utakaosaidia uendeshaji wa bandari za Tanzania.

Dk Koon ambaye ameambatana na wafanyabiashara wakubwa wapatao 40, alimweleza Waziri Mkuu kwamba Kampuni ya Hyflux ya Singapore, imeanza kuwekeza nchini kwa kujenga eneo maalumu la uchumi mkoani Morogoro, ambako ndani ya kipindi cha miaka mitano wanatarajia kujenga miundombinu wezeshi ya kuweka viwanda vya kati, maeneo ya biashara na nyumba za makazi zipatazo 37,000.

“Jiwe la msingi la mradi huo litawekwa tarehe 29 Aprili 2016 na Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage,” alisema waziri huyo wa Singapore.

Mbali na ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji, Dk Koon alimweleza Waziri Mkuu kwamba nchi yake itaisaidia Tanzania kujenga uwezo wa kiufundi katika maeneo mbalimbali ya menejimenti na uendeshaji wa bandari na ufundi katika sekta ya gesi na mafuta.

“Hadi sasa makampuni ya Singapore yaliyowekeza nchini ni pamoja na Pavillion Energy ambayo imewekeza kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 katika sekta ya gesi na inatarajia kuwekeza zaidi dola za kimarekani bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa kinu cha kuchakata gesi (LNG plant) kitakachojengwa mikoa ya Kusini kwa ubia na makampuni ya gesi kutoka Ulaya na Marekani,” alifafanua.

Alisema Kampuni ya PIL ya Singapore inatarajia kuwekeza Dola za Marekani milioni 400 kwa ajili ya kuanzisha kituo cha kutoa huduma kwa kampuni ya gesi. Alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo pamoja na kuweka mikakati ya kuinua uchumi na kupanua wigo wa biashara.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Majaliwa aliishukuru Serikali ya Singapore kwa uwekezaji unaofanywa na kampuni zake nchini na kwa misaada ya kiufundi ambayo wameitoa kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Ili kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kukuza uchumi, Waziri Mkuu amezikaribisha kampuni nyingine za Singapore kuja nchini kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda, mahoteli, kilimo na nishati.

Alimuahidi Dk Koon kwamba Tanzania ipo tayari kukamilisha mazungumzo ya kusaini Mkataba wa Kuvutia na kulinda uwekezaji baina ya nchi mbili na Mkataba wa Kuepuka kutoza ushuru mara mbili ili kuvutia uwekezaji zaidi kutoka Singapore.

Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka Watanzania kutumia fursa ya ushirikiano kati ya Singapore na Tanzania, kuanzisha biashara mpya zitakazowanufaisha wote.

Alisema Singapore ina uwezo mkubwa kibiashara pamoja na uzoefu wa siku nyingi kwenye uendeshaji wa bandari hivyo Tanzania itapata nafasi ya kujifunza namna ya uendeshaji katika sekta hizo.

Alisema Tanzania imefungua milango ya uwekezaji kwa wafanyabiashara wa Singapore, kuja kuwekeza katika sekta za viwanda, usafiri wa anga na kwenye Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZ).

Balozi Seif ashiriki kikao cha Kuteua Kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Kinduni Wilaya ya Kaskazini “B”.

 Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Masheha, Madiwani, Wazee wanaoheshimika wa Jimbo la Mahonda katika Kikao cha Kuteua Kamati ya Maendeleo ya Jimbo hilo kilichofanyika Ofisi ya CCM Jimbo hilo iliyopo Kinduni Wilaya ya Kaskazini “B”.
 Baadhi ya Viongozi wa Jimbo la Mahonda waliokutana kuunda Kamati ya Maendeleo ya Jimbo hilo utakaoratibu Mfuko wa Jimbo unaolenga kuunga mkono nguvu za Wananchi kwenye miradi waliyoianzisha.
Balozi Seif akisisitiza jambo wakati akifafanua kifungu cha Sheria cha Baraza la Wawakilishi kilichoanzishwa cha kuanzishwa kwa mfuko wa jimbo ya mwaka 2012.
Picha na –OMPR – ZNZ.

 Press Release:-

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ai Iddi alisema kwamba nia ya Serikali Kuu ya kuanzisha kwa mfuko wa Jimbo ni kusaidia nguvu za Wananchi katika kuunga mkono Miradi ya Kijamii na uchumi waliyoianzisha katika majimbo yao.

Alisema masharti makuu ya mfuko huo ni uwepo wa Kamati ya Maendeleo itayoundwa rasmi kwa mujibu wa sheria ya Baraza la Wawakilishi Kifungu cha 9 cha kuwanzishwa kwa Mfuko wa Jimbo chini ya Uwenyekiti wa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo linalohusika.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema hayo katika Kikao Maalum alichokiitisha kuchaguwa wajumbe Tisa wa kuunda Kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Mahonda Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Jimbo hilo iliyopo Kiduni Wilaya ya Kaskazini “B”.

Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini nguvu na kazi kubwa inayofanywa na Wananchi wake wanaofikia hatua ya kuanzisha miradi ya kiuchumi, maendeleo na ile ya Kijamii ili kujikomboa na ukali wa maisha sambamba na kupunguza umaskini.

Alisema juhudi hizo za Wananchi ndizo zilizopelekea Serikali Kuu kupitia chombo chake cha kutunga Sheria yaani Baraza la Wawakilishi kuunda sheria ya kuanzishwa kwa mfuko wa Jimbo unaopatiwa fedha zinazolengwa kuunga mkono jitihada za Wananchi hao.

Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda alifafanua kwamba Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jimbo watakuwa na wajibu wa kutembelea miradi iliyoanzishwa na Wananchi katika Wadi na Shehia zao na baadae kuiwasilisha katika Kamati yao ya Maendeleo.

Alisema mfumo huo umewekwa ili kuipa nafasi Kamati kutafakari na kuichambua miradi iliyowasilishwa ili kupata fursa ya kutoa baraka zake kwa kuidhinisha mradi wa Wananchi utakaostahiki kuungwa mkono kupitia fedha za mfuko wa Jimbo.

Akizungumzia suala la Kipindupindu lililoikumba Taifa hivi sasa Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema ili kuepukana na maradhi hayo ya kuambukiza, jamii lazima ikubali kubadilika katika kukabiliana na janga hilo kwa kuweka mazingira bora kwenye maeneo wanayoishi.

Aliwaagiza Viongozi wa Majimbo, Wadi na Shehia kuwatahadharisha Wananchi wa maeneo yao wakati wanapohisi mabadiliko ya afya zao kwa kuharisha au kutapika waharakishe kukimbilia kwenye vituo vya afya ili wapatiwe huduma za haraka kwa lengo la kujikinga na mripuko wa maradhi ya kuambukiza hasa Kipindupindu.

Balozi Seif alitanabahisha kwamba maradhi ya Kipindupindu yaliyochukuwa muda mrefu katika Historia ya maradhi hayo hapa Zanzibar kwa kudumu takriban Miezi Saba sasa tayari yameshagusa Wilaya zote na kuathiri kila familia hapa Nchini.

“ Kipindipundu hivi sasa tayari kimeshagusa takriban Wilaya zote Nchini. Na kwa mujibu wa takwimu za siku mbili zilizopita kwenye Kituo cha Afya cha Chumbuni pekee kimepokea na kulaza wagonjwa 88 hali ambayo jamii ndio yenye jukumu la kuyaondosha maradhi hayo ”. Alisema Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda.


Aliwapongeza Viongozi wa Jimbo la Mahonda pamoja na wale wa Wilaya nzima ya Kaskazini “B” kwa umakini wao wa kusimamia uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni katika njia ya amani na utulivu.

Alisema hatua hiyo imetoa sura nzuri kiasi kwamba Viongozi wa Kitaifa wamepata faraja na mwanzo mzuri wa kuanza kuwatumikia Wananchi wao kwa kuwaletea maendeleo kama walivyoahidi wakati wakitangaza Sera na Ilani zao.

Katika Mkutano huo Viongozi hao ambao ni Madiwani Masheha, Wazee mashuhuri pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” walipata fursa ya kuwachagua wajumbe Tisa watakaounda Kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Mahonda.

Kwa mujibu wa sheria na Taratibu zilivyoagiza za Baraza la Wawakilishi waliochaguliwa ni pamoja na Masheha Wawili, Madiwani Wawili, Wazee Wawili wanaoheshimika katika Jimbo, Mtu Mmoja wa Mahitaji Maalum pamoja na Mmoja anayewakilisha asasi za Kiraia zilizomo ndani ya Jimbo Husika.

Hata hivyo Katibu atakayekuwa mtendaji muandamizi wa Kamati hiyo anatarajiwa kuchaguliwa katika mkutano wa kwanza utakaoitishwa wa Kamati hiyo kwa kushirikisha uongozi wa Halmashauri ya Wilaya.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
27/4/2016.

Mwenezi wa Jiji la Arusha ,atua Kata ya Sombetini,katika ziara ya Kujenga Chama.

Written By CCMdijitali on Wednesday, April 27, 2016 | April 27, 2016

  • Awataka Viongozi wa ngazi zote kutimiza Wajibu mkubwa wa kufuatilia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa ngazi zao.
  • Awataka  wajiwekee ratiba za kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa katika maeneo yao na endapo watakuta utekelezaji una hitilafu,watoe taarifa kwa Viongozi wa Serekali ngazi ya juu yao.
  • Aidha aliwataka Viongozi hao kuongeza jitihada za kuwa karibu na Wananchi na kuwasemea na kuwatetea.
  • Pia aliwataka wafanye ziara na Mikutano baina ya Viongozi wa Chama na Wananchi ya kufafanua na kueleza fursa mbali zinazopatikana Serekalini
 Katibu Mwenezi CCM Wilaya ya Arusha,Ndg Kishumbua Jasper akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM Kata ya Sombetini 26/04/2016
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Sombetini Ndg Thomas Kivuyo ,akifungua  kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama inayofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata zote 25 ndani ya Jiji la Arusha.  waendelea na ziara ya Kujenga Chama Kata ya Sombetini 26/04/2016
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama inayofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata zote 25 ndani ya Jiji la Arusha. waendelea na ziara ya Kujenga Chama Kata ya Sombetini 26/04/2016
Ndg Okoth ,Mwenyekiti wa Jumuiya ya WAZAZI Tawi la Sombetini akitoa neno la kushukuru na kupongeza Uongozi wa CCM Wilaya ya Arusha,kwa semina nzuri ya kujenga Uhai wa Chama.

Muasisi wa Chama Cha Mapinduzi katika picha ya pamoja na Kada wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Rahim - kwa jina maarufu Mgosi
Muasisi wa Chama Cha Mapinduzi katika picha ya pamoja , Katibu Mwenezi CCM Wilaya ya Arusha,Ndg Kishumbua Jasper (aliyechuchumaa) na Kaimu Katibu Kata Ndg William Kivuyo (Katibu wa Uchumi na Fedha Kata )
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama inayofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata zote 25 ndani ya Jiji la Arusha. waendelea na ziara ya Kujenga Chama Kata ya Sombetini 26/04/2016
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Arusha-Ndg Jasper Kishumbua

Viongozi wa Kata ya Unga Ltd katika Semina ya Kujenga Chama - Arusha

Written By CCMdijitali on Tuesday, April 26, 2016 | April 26, 2016


Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua , akiwafunda  Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama.

Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Unga ltd,Bi Sophia - Katibu wa Uchumi na Fedha Kata na Katibu wa Siasa na Uenezi Kata Bi Muhone, wakiwa katika kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama inayofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika  Kata zote 25 ndani ya Jiji la Arusha.
 Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha,katika ziara ya Kujenga Chama ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha,anayoifanya Kata zote 25 ndani ya Jiji la Arusha,akiangalia jiwe la Msingi lililowekwa mwaka 02/02/1982 na aliyekuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa Marehemu Daudi Mwakawago, katika Ofisi ya CCM Kata ya Unga Ltd.
  Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha,katika ziara ya Kujenga Chama anayoifanya Kata zote 25 ndani ya Jiji la Arusha,akiangalia jiwe la Msingi lililowekwa mwaka 02/02/1982 na aliyekuwa Katibu  Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa Marehemu Daudi Mwakawago, katika Ofisi ya CCM Kata ya Unga Ltd.
 Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Arusha,Ndg Musa Mkanga,katika ziara ya Kujenga Chama inayofanywa na  Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, katika Ofisi ya CCM Kata ya Unga Ltd.

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Martin Munisi ,akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Tawi la Unga Ltd ,katika ziara ya Kujenga Chama inayofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, katika Ofisi ya CCM Kata ya Unga Ltd.akishuhudiwa na Katibu wa CCM Tawi hilo.
Picha zote na katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua

Balozi Seif ahutubia kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani

Written By CCMdijitali on Monday, April 25, 2016 | April 25, 2016

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiyaongoza Matembezi ya maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani yaliyoanzia mbele ya Ubalozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China Mazizini na Kuishia viwanja vya Maisara Suleiman.

Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo na Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Juma Malik Akil.

 Baadhi ya vikundi vya mazoezi Nchini zikishiriki kwenye matembezi ya maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani zilizofikia kilele chake uwanja wa Maisra Suleiman Mjini Zanzibar.
 Wanavikundi vya mazoezi ya viungo wakinyoosha miili yao mara baada ya kumaliza matembezi yao kuadhimisha siku ya Malaria Dunani yanayofanyika kila ifikapo Tarehe 25 ya Mwezi April.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akihutubia kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani zilizofikia kilele chake katika uwanja wa Maisara.

Kulia ya Balozi Seif Ali Iddi ni Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo na Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Juma Malik Akil.

Picha na – OMPR – ZNZ.

 Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameonya kwamba ukaidi unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu Mitaani kuendelea kukiuka maagizo ya Wizara ya Afya na kufanya biashara za vyakula ovyo unaweza kuiangamiza jamii mara moja dhidi ya maradhi ya Kipindu pindu yanayoonyesha kuongezeka kwa kasi kila kukicha.


Alisema kutokana na janga hilo jamii kwa sasa inalazimika kuwa makini katika kujigomba yenyewe kuelekea kwenye utekelezaji wa maagizo na ushauri wa wataalamu wa afya bila ya kuisubiri Serikali kuu kuchukuwa hatua za kupambana na wale wanaokiuka yaliyopigwa marufuku kuyafanya kwa wakati huu.


Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani mara baada ya kuyaongoza matembezi ya maalum ya maadhimisho hayo yaliyoanzia mbele ya Ubalozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China Mazizini na kuishia katika viwanja vya michezo Maisara Suleiman Mjini Zanzibar.


Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina nia mbaya ya kumkomoa mtu au mfanyabiashara kutokana harakati zake za kujitafutia riziki bali lengo lake ni kunusuru maisha ya Watu kutokana na mripuko wa maradhi ya Kipindu pindu unaoendelea kuangamiza maisha ya Wananchi kila wakati.


“ Jamii bado kaidi katika kutekeleza ushauri unaotolewa na Wataalamu mbali mbali kwani wamekuwa na tabia wanapoelekezwa kwenda kulia wao hupinga na kuelekea kushoto jambo ambalo linanisikitisha sana ”. Alisema Balozi Seif.


Aliwataka wananchi wote katika maeneo yao kuchukuwa juhudi ya tahadhari dhidi ya mapambano ya maradhi hayo ya kuambukiza kwa kuondosha vyianzio vya maradhi hayo ikiwa ni pamoja na vidimbwi vya maji machafu ya kinyesi pamoja na kuchemsha maji ya kunywa.


Alisema licha ya kwamba Wananchi kipindi hichi wanaadhimisha siku ya Malaria Duniani lakini pia ni vyema wakawa na tahadhari ya kukumbuka kujilinda na matatizo ya Kipindu Pindu kinacholeta fadhaa kwa sasa kwenye mitaa tofauti hapa Nchini.


Akizungumzia siku ya Malaria Duniani Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema alisimia 55% ya wagonjwa wa Malaria wanaoripotiwa katika Vituo vya Afya katika kipindi hichi ni wale wanaosafiri kutoka Zanzibar na maeneo mengine ya nje ya Visiwa hivi.


Balozi Seif alisema kwa vile maambukizo ya malaria kwa mfumo huu hayataweza kuondoka kabisa, Hivyo aliwaomba ni vyema kwa wasafiri wote kutumia vyandarua mahali popote wanapokwenda nje ya Zanzibar.
Alisema hatua hii muhimu inaweza kusaidia na kwenda sambamba na Mpango Mkakati wa Serikali kupitia kitengo chake cha mapambano dhidi ya malaria Zanzibar wa ondoa malaria kabisa ifikapo mwaka 2018.


Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Juma Malik Akil alisema mpango wa kujikinga na homa ya Malaria unaendelea kufanikiwa kufuatia taaluma inayotolewa na wataalamu wa Afya kuwafikia Wananchi kupitia vyombo vya Habari.


Dr. Malik alisema huduma za uchunguzi wa malaria zimeimarika zaidi na kufikia asilimia 100% inayokwenda sambamba na upigaji dawa pamoja na utoaji wa vyandarua kwa Wananchi wakilengwa zaidi akina Mama Waja wazito na Watoto.


Hata hivyo Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya Zanzibar alisema wapo baadhi ya wananchi wanaoamua kutumia vyandarua vyao wakati wa msimu wa mvua za masika pekee jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.


“ Hadi sasa nyumba zipatazo 90,000 Unguja na Pemba tayari zimeshapigwa dawa na Watu wapatao Laki 459,000 wamepata kuchunguzwa homa ya Malaria hadi mwaka 2015 ”. Alisema Dr. Juma Malik Akil.


Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya Zanzibar alifahamisha kwamba katika hatua nyengine ya kupambana na homa ya Malaria ndani ya kipindi cha mwaka huu wa 2016 mpango umeandaliwa kuendelea kugawa vyandarua unaotarajiwa kuanza rasmi hapo kesho Jumatatu.


Dr. Malik alisema Mpango huo unakusudiwa kutolewa vyandarua Laki 780.000 ikilinganishwa na vyandarua Laki 216,000 vilivyotolewa mwaka 2014 na kuwafaidisha wananchi wapatao Laki 434,000.


Aliwaomba Wananchi watakaohitaji kupata huduma ya vyandarua hivyo watumie utaratibu wa kujiorodhesha majina yao kupitia kwa masheha wa shehia zao ili kukimbia usumbufu unaoweza kuja kujitokeza hapo baadae.


Akimkaribisha mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ya siku ya Malaria Duniani Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo alisema maradhi ya malaria licha ya juhudi zilizochukuliwa katika kupambana nayo lakini bado yanaendelea kuathiri wananchi na hata Taifa kwa kutumia rasilmali kubwa katika kupambana nayo.


Waziri Mahmoud alisema juhudi za mapambano dhidi ya maradhi ya Malaria ni vizuri zikaendelea kushirikisha wadau wa sekta zote lengo likiwa kufikia kuupiga vita ugonjwa huo kwa asilimia 0.05%.


Ujumbe wa Mwaka huu wa Siku ya Malaria Duniani unaoadhimishwa kila ifikapo Tarehe 25 ya mwezi Aprili kwa hapa Zanzibar unasema:- “ Ili kuondoa matatizo ya malaria kwa wanaosafiri ni vyema wakatumia vyandarua mahali popote wanapokwenda ”.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
24/4/2016.

Mwenezi CCM Wilaya Arusha achanja mbuga Kata ya Sekei na Themi ziara ya "Kazi ya Kujenga Chama"

  • Awapongeza Viongozi wa Kata ya Sekei kwa ushindi walioupata katika Uchaguzi mdogo wa Wajumbe wa Serekali ya Mitaa ya Laurei na Sanawari

  • Ampongeza Bi Elinipa john kwa kushinda Mtaa wa Laurei


Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua,akimpongeza Bi Elinipa john kwa kushinda Mtaa wa Laurei kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Serekali ya Mtaa,katika kikao cha Semina ya Kukijenga Chama Cha mapinduzi kilichofanyika katika Ofisi ya CCM Kata ya Sekei 24/04/2016
 Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua,katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kata na Matawi ya Themi mara baada ya  kikao cha Semina ya Kukijenga Chama Cha Mapinduzi kilichofanyika katika Viwanja vya Taso Jijini Arusha 23/04/2016 Jumamosi
 Mwenyekiti wa  UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Martin Munisi,katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kata na Matawi ya Themi mara baada ya kikao cha Semina ya Kukijenga Chama Cha Mapinduzi kilichofanyika katika Viwanja vya Taso Jijini Arusha 23/04/2016 Jumamosi


Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua,katika pichaakiagana  na baadhi ya Viongozi wa Kata na Matawi ya Themi mara baada ya kikao cha Semina ya Kukijenga Chama Cha Mapinduzi kilichofanyika katika Viwanja vya Taso Jijini Arusha 23/04/2016 Jumamosi
Picha zote na Idara ya Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha.
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link