TANZANIA YAPONGEZWA KUWA KINARA WA MASUALA YA AMANI NA USALAMA UKANDA WA MAZIWA MAKUU
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa kwa kuwa kinara katika masuala mbalimbali yanayolenga kuleta amani na usalama katika Ukanda wa...
Dkt. Abbasi: Tutaionesha Dunia Utamaduni Wetu Kutokea Moshi
Written By CCMdijitali on Thursday, January 20, 2022 | January 20, 2022
“Maandalizi yanakamilika na tayari vikundi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huu vinaendelea na mazoezi na wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania wameendelea kuwasili hapa Moshi.
“Tamasha hili linafungua njia ya matamasha mengine ya Utamaduni wetu kuendelea hapa nchini.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aongoza Kikao cha Maalum cha Kamati Kuu ya CCM
AWANI ZA MAKAZI KUIBADILISHA TANZANIA KUWA YA KIDIJITALI
Anwani za Makazi kuwa Msingi wa Utambuzi wa Kila Mwananchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi (kushoto) akiongea na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Mariam Mtunguja, baada ya kuwasili ofisini kwake mkoani humo kwa ajili ya kufungua semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa Mkoa huo kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mbaraka Mwinshee leo Januari 19, 2022.
Na Prisca Ulomi, WHMTH, Morogoro
Serikali imejikita kutekeleza mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi nchi nzima kwa
lengo la kuibadilisha Tanzania kuwa ya kidijitali kwa kuwa anwani za makazi na postikodi
ni msingi wa utambuzi wa kila mwananchi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape
Nnauye ambaye amewakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi wakati
akifungua mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi, watendaji na wataalam wa Mkoa
wa Morogoro kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi.
Dkt. Yonazi amesema kuwa anwani za makazi na postikodi ni msingi wa utambuzi ili kila
mwananchi aweze kutambuliwa pale alipo ambapo nia ya Serikali ni kuihakikisha kuwa
kila mtaa, barabara, inakuwa na jina la mtaa na kila nyumba inakuwa na namba ya
nyumba
Vile vile, ameitaka Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro kusimamia utekelezaji wa mfumo
huu ili ifikapo Mwezi Mei mwaka huu jambo hili liwe limekamilika kwa kuwa utekelezaji
wa mfumo huu utaiwezesha Serikali kuwa na sensa bora ya watu na makazi
inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inayoratibu jambo hili, imeelekeza taasisi zote za
Serikali nchi nzima zinatekeleza mfumo huu wamiliki wote wa majengo na nyumba nao
waweke namba za nyumba kwenye nyumba na majengo yao na wataalam wote
waliojengewa uwezo watumike vizuri kutekeleza mfumo wa anwani za makazi na
postikodi na jambo hili liwe ajenda kwenye vikao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Mariam Mtunguja akizungumza kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa huo, Martine Shigela amesema kuwa kimsingi tumechelewa kutekeleza
mfumo huu wa anwani za makazi, ila kwa kuwa viongozi mtajengewa uelewa, ni
matumaini yangu kuwa kwa pamoja tutashirikiana na wataalam wetu kutekeleza jambo
hili kwenye maeneo yetu ndani ya muda uliopangwa na niahidi kuwa Mkoa wa
Morogoro hatutawaangusha Wizara.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi, amesema kuwa mfumo wa anwani za makazi na postikodi
ni moja ya aina ya mawasiliano kama zilivyo aina nyingine za mawasiliano na mfumo huu
unahusisha eneo husika ambapo utamuwezesha mwananchi kutoka sehemu moja
kwenda sehemu nyingine; utarahisisha shughuli za kiuchumi, kijamii na utawala
Wakitoa salamu za shukrani kwa niaba ya viongozi wengine, Mwenyekiti wa CCM Wilaya
ya Morogoro Mjini Fikiri Juma, amesema kuwa viongozi watoe majina ya mitaa ndani ya
siku moja ili kufanikisha utekelezaji na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal
Kihanga amesema watahamasisha wananchi kununua vibao vya nyumba ili kufaniisha
uwekaji wa mfumo wa anwani za makazi kwenye Mkoa huo
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Mhe. Rais samia aongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo Ikulu Chamwino Dodoma
Written By CCMdijitali on Wednesday, January 19, 2022 | January 19, 2022
HANDENI YAFANYA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI.
Mwenyekiti
wa baraza la wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen akiongea kwenye Baraza la wafanya kazi. |
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imefanya kikao cha baraza la wafanyakazi Ili kupitia mpango wa rasimu ya bajeti ya Halmashauri ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen (Aliyevaa tai nyekundu) amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwatetea wananchi hivyo watanzania na wafanyakazi wote kwaujumla wazidi kumuombea Rais Afya njema Ili wazidi kuuona upendo wake kwa wafanyakazi.
MKUU WA MKOA WA TABORA AJUMUIKA NA WANAFUNZI WA SHULE SHIKIZI KUPANDA MITI WILAYANI SIKONGE
TABORA YA KIJANI INAWEZEKANA
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani akijumuika na mwanafunzi kuchimba shimo kwa ajili ya kuotesha kwenye shule shikizi ya Gezaulole Wilayani Sikonge. |
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani akijumuika na mwanafunzi wa shule shikizi ya Gezaulolekwa kuotesha mti Wilayani Sikonge. |
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani akijumuika na mwanafunzi wa shule shikizi ya Gezaulolekwa kuotesha mti Wilayani Sikonge. |
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Batilda Burian jana
tarehe 18 Januari, 2022 na Viongozi wa Wilaya ya Sikonge walijumuika na
wanafunzi wa shule shikizi ya Gezaulole kupanda miti katika eneo la
Shule hiyo iliyopo Wilayani Sikonge. Mkoa wa Tabora umejiwekea malengo
ya kupanda miti milioni 12 kwa mwaka.
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKIJARIBU PIKIPIKI
WATAALAMU WA SEKTA YA ARDHI NCHINI WATAKIWA KUWA WABUNIFU - KIKWETE NAIBU WAZIRI
Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Ridhiwani Kikwete (MB) amewaagiza Makamishina wa Ardhi kote wasaidizi wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanaweka vipimo vya utendaji kazi watumishi wa sekta ya ardhi kila baada ya mwezi mmoja ili kupima utendaji wao kwa lengo la kuleta tija katika sekta ya Ardhi
Aidha aliwataka wataalamu wa sekta ya Ardhi nchini kuwa wabunifu sambamba na kutoa huduma bora na kwa wakati ili kusaidia serikali na wananchi kwa ujumla. #RK #kaziimeanza #ardhiyetuhakiyetu #matokeochanya
DC LUSHOTO AKAGUA ZOEZI LA UPOKEAJI NA UANDIKISHWAJI WA WANAFUNZI DARASA LA KWANZA NA AWALI
MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO ATEMBELEA NA KUKAGUA ZOEZI LA UPOKEAJI NA UANDIKISHWAJI WA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA NA AWALI KATIKA SHULE ZA MSINGI HALMASHAURI YA WILAYA YA LUSHOTO
Alieleza "Mwalimu wapokeeni Wanafunzi na Kuwaandikisha bila Masharti, Serikali imeweka Utaratibu Mzuri msiuvuruge, Kama Mwanafunzi hana Sare za Shule apokelewe na Mzazi wake apewe muda wa Kulitekeleza hilo bila Mwanafunzi kuzuiwa kuingia Darasani na Michango inayoruhusiwa ni ile tuu ambayo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imeipitisha na kutoa Kibali cha Mchango"
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro akiwa Shule ya Msingi Mbula katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto |
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro akiwa Shule ya Msingi Mbula katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto |