TANZANIA YAPONGEZWA KUWA KINARA WA MASUALA YA AMANI NA USALAMA UKANDA WA MAZIWA MAKUU
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa kwa kuwa kinara katika masuala mbalimbali yanayolenga kuleta amani na usalama katika Ukanda wa...
Latest Post
October 31, 2023
RAIS WA UJERUMANI KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA MAJIMAJI, SONGEA
Written By CCMdijitali on Tuesday, October 31, 2023 | October 31, 2023
Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujeruman Mhe. Dkt Frank Walter Steinmeier anatarajiwa kutembelea Makumbusho ya Kumbukumbu ya Vita vya MajiMaji Songea tarehe 1 Novemba 2023. Makumbusho hiyo ina historia kubwa ya Vita vya MajiMaji wakati wa harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wajerumani.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali Laban Thomas amesema maandalizi ya kuupokea ugeni huo yamekamilika ambapo baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songea ataenda moja kwa moja katika Makumbusho hiyo ya Vita vya MajiMaji.
Amesema akiwa katika Makumbusho hiyo atapata historia ya makumbusho hiyo na kutoa heshima kwa mashujaa waliokufa katika vita hivyo vilivyopiganwa mwaka 1905- 1907.
Kanali Thomas ameongeza kuwa pamoja na kutoa heshima kwa mashujaa wa Vita vya Majimaji, Rais huyo wa Ujerumani atakutana na baadhi ya wahanga wa vita hivyo na kutembelea Shule ya Msingi MajiMaji.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamshna Benard Wakulyamba amesema Wizara ya Maliasili na Makumbusho ya Taifa wanaosimamia Makumbusho ya MajiMaji wamekamilisha maandalizi kwa ajili ya kumpokea Rais huyo wa Ujerumani.
Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier yupo nchini kwa Ziara ya Kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi tarehe 01 Novemba 2023.
Ziara hii mbali na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Ujerumani, pia imelenga kukuza na kuimarisha misingi ya biashara na uwekezaji.
October 31, 2023
TANZANIA – UJERUMANI KUJIKITA ZAIDI KATIKA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani zimeeleza dhamira yao ya kujikita zaidi katika kuendeleza na kukuza ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya pande zote mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (Julia) na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier (kushoto) |
Hayo yamebainishwa na Viongozi Wakuu wa mataifa hayo mawili rafiki, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia ameeleza kuwa licha ya Tanzania na Ujerumani kuwa ushirikiano mzuri na wa muda mrefu katika shughuli mbalimbali za maendeleo hususani katika sekta ya Afya, elimu, usambazaji wa maji safi na salama, hifadhi ya mazingira, ulinzi na usalama, haki za binadamu na utawala bora na hifadhi ya maliasili bado kuna fursa kubwa ya kukuza zaidi ushirikiano wa kibiashara na uchumi kwa manufaa ya watu wa pande zote mbili.
“Katika mazungumzo yetu tumeelekeza timu za pande zote mbili kukaa na kufanya majadiliano ya mara kwa mara ili kubaini maeneo mapya ya ushirikiano ambayo yatatusaidia kupiga hatua kwa haraka zaidi katika kukuza biashara na uwekezaji kwa manufaa ya watu wetu” Alisema Rais Samia.
Katika hatua nyingine Rais Samia ameeleza kuwa katika mazungumzo na mgeni wake Rais Frank-Walter Steinmeier wamekubaliana kufungua majadiliano katika masuala kadhaa ya kihistoria ikiwemo kuhusu suala la mabaki ya kale ya Tanzania yaliyohifadhiwa nchini Ujerumani.
Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier ameeleza kuwa Ujerumani itaendelea kufungua milango ya ushirikiano zaidi kwa Tanzania katika kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya sasa na vizazi vijavyo.
“Ujerumani tutatendelea kujikita katika kuangazia maeneo mapya ya ushirikiano ikiwemo kuongeza nguvu ya kusaidia maendeleo ya nishati jadilifu nchini Tanzania na uchumi wa kidijiti ambao utatengeneza ajira nyingi zaidi kwa vijana. Tunafanya haya yote tukiamini kuwa hatusherekei urafiki wetu pekee bali maendeleo ya kiuchumi” Alieleza Rais Frank-Walter Steinmeier
Mbali masuala ya biashara na uchumi Rais Frank-Walter Steinmeier ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita ikiongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa hatua kubwa iliyopiga katika kuboresha mazingira ya Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Rais Frank-Walter Steinmeier ametumia fursa hiyo kuzishukuru familia za wahanga wa Vita vya Majimaji za jijini Songea kwa kumwalika kuzitembelea huku akieleza kuwa ni faraja kubwa kwake ikiwa ni mwendelezo wa ishara ya utayari wa kusonga mbele pamoja licha ya yaliyojiri katika historia.
Labels:
KITAIFA
October 29, 2023
DUA MAALUMU YA KUMUOMBEA DKT: SAMIA NA TAIFA LAFANYIKA MKOANI MBEYA
Written By CCMdijitali on Sunday, October 29, 2023 | October 29, 2023
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera Leo Oktoba 29 2023 ameshiriki Kongamano la Jukwaa la Wanawake wa Kiislamu Tanzania Mkoa wa Mbeya (JUWAKITA) lililolenga kumuombea na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt: Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuyagusa Moja kwa Moja Maisha ya Makundi maalumu hasa Wanawake na Watoto (Walemavu,Yatima na Wajane) katika nyanja mbali mbali.
Katika Kongamano hilo imesomwa Dua maalumu ya Kumuombea Dkt: Samia na Taifa kwa Ujumla ambapo mbali na Dua hiyo Kiasi Cha zaidi ya Shilingi Milioni 31 zimechangwa kwaajiri ya kuyasiadia Makundi hayo maalumu ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuunga Mkono Jitihada za Rais Dkt: Samia.
Ushiriki Wa RC Homera umewaibua pia Waziri wa Fedha pia Dkt: Mwigulu Nchemba ambaye ameshiriki kwa Njia ya Simu kadharika Naibu Waziri wa Maji Eng: Maryprisca Mahundi.
Katika hotuba yake fupi aliyoitoa baada ya Harambee RC Homera amewaasa Waislamu wote(Wanawake) kuendelea kudumisha Moyo wa kujitoa kwa kuwasaidia wasiojiweza na kuepuka Tabia ya kuyatenga na kuyanyanyapaa Makundi ya wasiojiweza na kuiga mfano kwa Rais wa Taifa hili.
Homera amesema mara zote Dkt: Samia amekuwa akiasa kuwa Kila binadamu anastahili kupendwa na kuthaminiwa hivyo jambo walililolifanya ni Ibada tosha na wamejitwalia thawabu Kutoka kwa Mwenyezi MUNGU kama ambavyo Mtume S.W.A anavyowaagiza katika Quran tukufu.
Labels:
MIKOANI
October 29, 2023
WATUMISHI WA AFYA 10,305 KUAJIRIWA MWAKA WA FEDHA 2023/24
MHE.MCHENGERWA: WATUMISHI WA AFYA 10,305 KUAJIRIWA MWAKA WA FEDHA 2023/24
OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa amemshukuru Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali ombi la kuajiri watumishi wengine wa afya 10,305 kwa mwaka wa fedha 2023/24 ambao watapangwa kwenye Vituo vipya vya kutolea huduma za Afya ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Akizungumza Oktoba 28, 2023 jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa ripoti ya Afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya Maralia kwa Mwaka 2022, Mhe.Mchengerwa amesema maboresho ya miundombinu yanayofanyika yanakwenda sambamba na upatikanaji wa rasilimali watu ambapo OR-TASMISEMI imeajiri watumishi wa kada za Afya 17,950 katika kipindi cha miaka miwili na wengine 10,305 wanatarajiwa kuajiriwa kwa Mwaka wa fedha 2023/24.
“Vituo vya kutolea huduma za Afya vilivyokuwa vimekamilika sasa vinaenda kuanza kutoa huduma kwa wananchi, Aidha, nichukue nafasi hii kuwasisitiza sana Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa Vituo vya kutolea huduma za Afya ambavyo vimeishakamilika vinaanza kutoa huduma za Afya kwani watumishi na vifaa tiba kwa kiasi kikubwa vimetolewa.”
“Serikali imejenga miundombinu bora ya Vituo vya kutolea huduma za Afya nchini kwa gharama kubwa na kuweka Vifaa na vifaa tiba, hivyo nawataka watumishi waliopewa dhamana ya kuwahudumia wananchi katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini, kuhakikisha wanatoa huduma bora na kuwa na kauli nzuri kwa wateja,”amesema.
Amesisitiza kuwa atahakikisha anawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wataokaobainika kuzembea katika kuwahudumia wananchi.
“Natumia fursa hii pia kutoa wito kwa wananchi wanaofuata huduma katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya kutosita kutoa tarifa za watumishi wasio waadilifu, wazembe na wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili niweze kuchukua hatua stahiki kwa wakati kupitia kituo cha huduma kwa mteja kupitia namba 0735-160210 na 0262 – 160210,” amesema.
Labels:
KITAIFA
October 28, 2023
DR. TULIA ACKSON TRIUMPHS AS IPU PRESIDENT - A RESOUNDING VICTORY FOR AFRICAN LEADERSHIP.
Written By CCMdijitali on Saturday, October 28, 2023 | October 28, 2023
----‐----‐---------------------------------------------
Friday, 27th October 2023
Christopher Makwaia
Tel: +255 789 242 396
1. Introduction.
In a watershed moment for African leadership, Dr. Tulia Ackson has clinched victory as the President of the Inter-Parliamentary Union (IPU). This remarkable win not only crowns her distinguished career but stands as a testament to the strength, resilience, and visionary leadership she brings to the global stage. I take pride in noting that I have previously predicted her triumph in this election, and today, that prediction has come true. This article extends heartfelt congratulations to Dr. Ackson, celebrating her historic achievement and highlighting the profound impact her presidency will have on Tanzania, Africa, and the international community.
2. A Trailblazer's Victory.
Dr. Ackson's journey to the IPU Presidency has been characterized by tireless dedication, unparalleled expertise, and a resolute commitment to democratic values. From her academic triumphs to her distinguished career in parliamentary affairs, she has consistently demonstrated the qualities of a trailblazer. Today, I proudly note that my previous prediction of her triumph in this election has come to fruition.
Dr. Ackson's election as the first woman from Africa to hold the esteemed IPU Presidency is a historic breakthrough. Beyond individual achievement, this victory signifies Africa's increasing influence and its amplified voice in shaping global governance and diplomacy.
With Dr. Ackson at the helm, we anticipate a transformative era in global parliamentary diplomacy. Her exceptional leadership, diplomatic finesse, and commitment to collaboration are poised to elevate the IPU's role in shaping legislative agendas, fostering dialogue, and championing democratic principles on a global scale.
Dr. Ackson's presidency is anticipated to prioritize inclusivity, gender equality, and sustainable development. By amplifying African voices and advocating for policies that prioritize marginalized populations, she is set to make significant contributions to global discussions on pressing issues.
Dr. Ackson's victory serves as an inspiration for aspiring leaders, particularly women, across the globe. Her success reinforces the transformative power of education, determination, and a steadfast dedication to public service. Dr. Ackson's journey will undoubtedly inspire future generations to aspire to leadership positions and contribute to positive change.
3. Conclusion.
As Dr. Tulia Ackson commences her tenure as IPU President, we commend her on this historic achievement. Her victory is not merely a personal triumph but signals the dawn of a new era in global governance. I extend my sincere congratulations to Dr. Ackson, proud that my prediction of her triumph in this election has been realized. We eagerly anticipate the positive transformations her visionary leadership will bring to the world stage.
Dr. Ackson's success breathes life into the very essence of inspiration, embodying the transformative power that arises from resilience, dedication, and an enduring devotion to public service. As her story evolves, it transforms into a guiding force, shedding light on the path for aspiring leaders, particularly women, globally.
Stepping into the role of IPU President, Dr. Ackson's journey assumes a broader significance. It becomes a pledge to elevate the discourse of global diplomacy, ensuring that African voices resonate prominently in international conversations. Her presidency emerges as a catalyst for the advancement of democratic principles, heralding an era of inclusivity and collaboration on a truly global scale.
As we bear witness to the unfolding chapters of Dr. Tulia Ackson's leadership, it's impossible not to recognize the profound impact she is poised to have. Her ascendancy is not just a moment; it's a narrative that will echo through generations. Dr. Ackson becomes a lodestar, guiding future leaders toward a future characterized by positive change in global governance, diplomatic dialogue, and visionary leadership.
In extending heartfelt congratulations to Dr. Tulia Ackson, we celebrate more than a victory; we celebrate the promise of a brighter, more inclusive future entwined in the nuanced network of global leadership.
Thank you.
Written by Christopher Makwaia
Tel: +255 789 242 396
- The writer, is a University of West London graduate (formerly Thames Valley University) and an expert in Management, Leadership, International Business, Foreign Affairs, Global Marketing, Diplomacy, International Relations, Conflict Resolution, Negotiations, Security, Arms Control, Political Scientist, and a self-taught Computer Programmer and Web Developer.
October 27, 2023
AL HAJJ DK. HUSSEIN ALI MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA KIISLAMU KWENYE IBADA YA SALA YA IJUMAA.
Written By CCMdijitali on Friday, October 27, 2023 | October 27, 2023
RAIS WA ZANZIBAR AL HAJJ DK. HUSSEIN ALI MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA KIISLAMU KWENYE IBADA YA SALA YA IJUMAA.
Zanzibar,
27 Oktoba, 2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa Kiislamu kwenye Ibada ya Sala ya Ijumaa, viwanja vya Markas Bungi, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Alhaj Dk. Mwinyi aliendelea kuikumbusha jamii juu ya kuamrishana mema na kukatazana maovu ili kuendelea kupata radhi za Mwenyezi Mungu (S.W) na taifa lenye maadili na kumcha Mungu.
Alisema, viongozi wa dini wananafasi kubwa kwa jamii kuwaelekeza mambo ya heri ili kupata jamii yenye busara, upendo, amani, umoja na mshikamano na kuongeza kuwa kupitia utengamano huo hata Serikali inapata fursa nzuri ya kuwaletea maendelo ya watu wake kwa ufanisi wa hali ya juu.
Alhaj Dk. Mwinyi aliwaeleza waumini hao kwamba, bado jamii inahitaji msaada mkubwa wa viongozi wa dini ili kurekebisha mitazamo ya waovu wachache, kwa kuyakataza na kuyakemea maovu yanayotendeka kupitia kundi la vijana ambao ni waathirika wakubwa kwenye suala la mporomoko wa maadili.
Alisema, viongozi hao wanamchango mkubwa kwa Serikali hususani kwenye suala zima la kujenga maadili ya umoja wa watu, suala ambalo linaleta mazingira mazuri ya maendeleo.
Sambamba na kuwaomba viongozi wa dini na waumini hao kuendelea kuliombea dua taifa na viongozi wake kupitia kazi kubwa wanayoifanya ya kulitumikia taifa.
“Sisi viongozi tunahitaji dua zenu kuombewa ili kutimiza majukumu yetu kwa ufanisi mkubwa” Alisisitiza Alhaj Dk. Mwinyi.
Naye, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume, alipongeza juhudi za masheikh wa tablikh kwa kufanikisha majukumu yao kwa uadilifu mkubwa bila kuchanganya siasa na mikinzano isiyofaa kwa jamii, pia aliwaomba mashekh hao kuendelea kuwaombea Rais Alhaj Dk. Mwinyi na viongozi wa nchi kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kulitumikia taifa.
Akizungumzia umuhimu wa darsa za kufundishana mambo mema ya heri, Khatib wa sala ya Ijumaa viwanjani hapo Sheikh, Abubakar Mubarak, aliwaeleza waumini kwenye mkusanyiko huo na jamii kwa ujumla kwamba darsa za kiislamu hukusanya waumini wa chache kwenye eneo moja lakini kwenye mkusanyiko mkubwa kama huo uliokusanya miji, nchi na makabila tofauti yasiyojuana kukaa pamoja na kumtaja Allah (S.W) hupatikana zaidi radhi za Mwenyezi Mungu.
IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR.
Labels:
ZANZIBAR
October 27, 2023
RAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEIN MWINYI AISHUKURU BENKI YA DUNIA
Zanzibar,
27 Oktoba, 2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Benki ya dunia kwa jitidaha zake za kuendelea kuziunga mkono nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Rais Dk. Mwinyi ametoa shukurani hizo, Ikulu, Zanznibar alipozungumza na Mwakilishi Mkazi wa benki hiyo, Nathan Balete na ujumbe wake.
Dk. Mwinyi alimueleza mgeni wake huyo juu ya Zanzibar inavyonufaika na fursa na misaada na mikopo ya gharama nafuu kutoka kwa benki hiyo kupitia mirandi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo zikiwemo sekta za afya, elimu, miundombinu, uchumi wa buluu, uwezeshaji wa Wanawake na mahakama.
Alisema, Zanzibar imekua na miradi mingi ya maendeleo inayoungwa mkono na benki ya dunia kupitia ushirikiano mzuri uliopo baina ya benki hiyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi alieleza fursa nyingine ambapo Zanzibar inanufaika kutoka Benki ya dunia ni pamoja na kuwajengea uwezo Wanzania kupitia mikutano ya kimataifa, warsha, makongamano pamoja na misaada ya kiufundi.
Akizungumzia sekta ya nishati hususani umeme wa jua, upepo na suala la gesi asilia, Rais Dk. Mwinyi aliieleza Benki ya dunia kuangalia namna bora ya kuiungamkono Zanzibar kujitegemea kwenye suala zima la kuzalisha umeme wake mwenyewe ili kuwafikishia huduma bora wananchi wake kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo gesi asilia na hewa ukaa.
Dk. Mwinyi alisema, ni jambo la faraja endapo Zanzibar ikipata kujitegemea kuzalisha nishati ya umeme, kwani kwa miaka mingi imekua ikitegemea umeme kutoka Tanzania bara, hivyo alimueleza mgeni huyo nia ya Zanzibar kujitegemee kupata umeme wake.
Pia, Rais Dk. Mwinyi alisifu wazo la Benki ya dunia kuanzisha ofisi zake Zanzibar, litaimarisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo baina ya pande mbili hizo mbali na kuungamkono sekta za maendeleo Tanzania ikiwemo Zanzibar.
Naye, Mwakilishi huyo Mkazi wa benki ya dunia Tanzania, Nathan Balete alisifu juhudi za Rais Dk. Mwinyi kwa kuimarisha maendeleo na huboresha huduma bora za jamii kwa wananchi wake ambazo zimeijengea sifa Zanzibar kimataifa.
Nathan Balete, pia anaziwakilisha nchi nyengine tatu za Afrika mbali na Tanzania zikiwemo Malawi, Zambia na Zimbawe, alimweleza Rais Dk. Mwinyi nia ya benki hiyo kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo wanayoiungwa mkono pamoja na wazo lao la kufungua ofisi zao hapa Zanzibar.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum alieleza, Zanzibar inatajia kupata heshima kubwa ya kimataifa kwa kutembelewa na viongozi wakubwa duniani akiwemo Rais wa Benki ya dunia, Ajay Singh Banga anaetarajiwa kuhudhuria mkutano wa 20 wa Mapitio ya benki hiyo, unaotoa misaada ya kiufundi na maendeleo kwa miaka mitatu mitatu kwa mataifa yanayoendelea duniani.
Alisema, mkutano huo pia utahudhuriwa na mawaziri wengine akiwemo wazairi wa masuala ya Afrika kutoka Uingereza.
Dk. Mkuya aliitaja Zanzibar kwa mara ya kwanza itakuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa duniani utakaohudhuriwa na wageni mashuhuri mwezi Disemba mwaka huu ambao unaotarajiwa kuhudhuriwa kati ya wageni 300 hadi 350 wenye lengo la kufanya mapitio ya miadi inayoungwa mkono na benki ya dunia pia kuangalia namna bora ya utekelezwaji wa miradi hiyo na namna ya kuongezwa fedha na ruzuku kwa miradi itakayofanya vizuri zaidi na mataifa wanufaika.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi |
IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR.
October 27, 2023
(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
DKT MPANGO AKABIDHI HATIMILIKI ZA KIMILA MAKETE
Na Munir Shemweta, WANMM MAKETE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Philip Isdori Mpango amekabithi Hati ya Hakimiliki za Kimila kwa wananchi wa Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe.
Dkt. Mpango amekabidhi hati saba za mfano kati ya Hatimiliki za Kimila 6,883 zilizoandaliwa tarehe 27 Oktoba 2023 katika halfa iliyofanyika Kijiji cha Tandala Wilayani humo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoa wa Njombe.
Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amesema, utolewaji Hati za Kimila wilayani Makete unafuatia uwezeshwaji uandaaji mipango ya matumizi bora ya ardhi uliofanywa na wizara yake kupitia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi katika vijiji.
Kwa mujibu wa Mhe. Pinda mkoa wa Njombe una jumla ya vijiji 323 ambapo vijiji 264 kati ya hivyo tayari vimewezeshwa kuandaliwa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
"Mhe Makamu wa Rais mkoa wa Njombe tunavyo vijiji 323 na kati ya hivyo vijiji 295 tayari vimewezeshwa na sasa tuko katika wilaya ya Makete kama taarifa ilivyoeleza" alisema Mhe. Pinda.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bw. William Makufwe amesema kuwa, upatikanaji wa Hatimiliki hizo ni jitihada za Wilaya kukuza zao la ngano àlilolieleza kuwa linazalishwa kwa wingi katika Wilaya hiyo.
Aidha, Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa, Wilaya yake imeamua kuendesha kilimo cha zao hilo Kimkakati kwa kupima na kumilisha mashamba kupitia Hatimiliki za Kimila ili ziwape fursa wakulima ya kuongeza mitaji itakayoinua wigo wa uzalishaji zao hilo.
Ugawaji wa Hatimiliki hizo unafuatia kazi iliyofanywa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi iliyowezesha uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 64 katika wilaya ya Makete na kutoa jumla ya Hatimiliki za Kimila 6,889.
Kazi hiyo imetekelezwa katika awamu mbili ambapo, wamu ya kwanza, ilihusisha uandaaji mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji 44 na upimaji wa vipande vya ardhi katika vijiji 17 ambapo jumla ya hati 6,594 ziliandaliwa.
Aidha, katika awamu ya pili uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 20 kwenye Tarafa ya Ukwama na Lupalilo ulifanyika ambapo Vijiji 20 viliwezeshwa kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi na hati miliki za kimila 287.
----------MWISHO----------
Labels:
KITAIFA
October 26, 2023
TAARIFA KWA UMMA: WATANZANIA WAWILI HAWAJULIKANI WALIPO NCHINI ISRAEL
Written By CCMdijitali on Thursday, October 26, 2023 | October 26, 2023
October 26, 2023
TANZIA - ARUSHA
MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA ZELOTE STEPHEN AFARIKI DUNIA
-Alhamisi, October 26, 2023
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Zelote Stephen amefariki dunia jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katibu wa CCM mkoa Arusha, Mussa Matoroka amesema wamepata taarifa za kifo hicho leo jioni Alhamis Oktoba 26,2023.
"Ni kweli Mwenyekiti amefariki jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amekwenda kupatiwa matibabu...huu ni msiba mkubwa kwetu CCM, familia ndugu na jamii," amesema Matoroka.
Katika ukurasa wake wa Instagram, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameweka picha ya Marehemu Stephen huku akiandika maneno yanayoonyesha kuumizwa na kifo hicho.
“Taarifa za kuondokewa na Zelote Stephen, Mwenyekiti wetu wa CCM mkoa wa Arusha ni taarifa za kusikitisha sana. Kwani kwa hakika kifo chake kimetunyima fursa muhimu ya kuendelea kujifunza mengi na kuuishi uongozi wake"
“Mungu ameendelea kutufunza. Mipango yetu imekwama. Nenda Laigwanan. Nenda mzee wangu. Nilipokutembelea siku chache zilizopita hospitali ulinipa matumaini. Kumbe mipango ya Mungu ikabaki. Wewe ni shujaa, Nenda Kamanda", imesomeka sehemu ya taarifa hiyo.
@ccmtanzania @musamatoroka @rc_mkoa_arusha @felicianmtahengerwa @arusha_district_council @arusha_city_council_ @arusha_city_council @uvccm_arusha_jiji @wilaya_ya_arushaa @uvccmkimandolu @uvccm_kaloleni @seneti_arusha @auwsatz @uwt_m_arusha @wilaya_ya_arusha @ccmarusha
Labels:
ARUSHA
October 26, 2023
WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA ATUA MKOANI ARUSHA.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) amewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K.Mongella na viongozi wengine wa Chama na Serikali pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Arusha, kwenye Uwanja wa Ndege Arusha kwa Ndege ya Air Tanzania.
Mhe. Waziri Mkuu yuko mkoani Arusha kwa ajili ya kufungua mkutano mkuu wa 9 wa Wadau wa Lishe, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha 26.10.2023.
Mkutano wa 9 wa Wadau wa Lishe 2023 umebeba Kauli mbiu ya "Kuimarisha Mifumo Endelevu ya Chakula kwa Maendeleo Bora ya Lishe na Maendeleo ya Rasilimali Watu"
#ArushaFursaLukuki🇹🇿
#kaziinaendelea✍️
October 25, 2023
BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA ATEMBELEA MKOANI NJOMBE
Written By CCMdijitali on Wednesday, October 25, 2023 | October 25, 2023
BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA ATEMBELEA MKOANI NJOMBE NA KUTAMBULISHWA FURSA ZINAZOPATIKANA NDANI YA MKOA
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa |
Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka ofisini kwake leo Oktoba 26, 2023 na kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
Moja ya sekta zilizoguswa kwenye mazungumzo ya viongozi hao wawili ni pamoja na kilimo, uwekezaji na utunzaji wa mazingira na uboresheji wa miundombinu ya zahanati za Mkoa wa Njombe.
Katika mazungumzo yao balozi huyo amesema serikali ya Japan imekuwa ikiendelea kuisaidia Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Itambo Wilayani Wanging'ombe,Ujenzi wa hostel na vyoo kwenye shule mbalimbali na wataendelea kusaidia katika nyanja nyingine.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka pamoja na katibu tawala Mkoa Bi.Judica Omary wameshukuru Kwa jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya Japan katika kutekeleza miradi hiyo huku wakiomba kuendelea kwa mashirikiano katika fursa zilizopo mkoani Njombe.
Aidha, Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa amepata nafasi ya kutembelea mabanda mbalimbali ya wajasiliamari katika maonesho ya SIDO Kitaifa yanayoendelea mkoani Njombe.
Pia viongozi wa Mkoa wa Njombe akiwemo Katibu Tawala Bi. Judica Omari, Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Kissa Gwakisa, Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda pamoja na Katibu Tawala Wilaya ya Njombe Bi. Agatha Mhahiki wameshiki mapokezi ya kiongozi huyo.
Labels:
MIKOANI