TANZANIA YAPONGEZWA KUWA KINARA WA MASUALA YA AMANI NA USALAMA UKANDA WA MAZIWA MAKUU
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa kwa kuwa kinara katika masuala mbalimbali yanayolenga kuleta amani na usalama katika Ukanda wa...
PINDA ATAKA MRADI UJENZI CHUO CHA ARDHI MOROGORO KUWEKEWA NGUVU
Written By CCMdijitali on Saturday, June 29, 2024 | June 29, 2024
Na Munir Shemweta, MOROGORO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ametaka mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ardhi Morogoro unaojumuisha eneo mahali chuo kilipo na eneo la mlima Kola kuwekewa nguvu ili uweze kukamilika kabla ya muda uliopangwa.
Mhe. Pinda ametoa kauli hiyo leo tarehe 29 Juni 2024 wakati alipokwenda kukagua eneo la ujenzi wa mradi huo katika eneo la mlima Kola mkoani Morogoro.
Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ardhi Morogoro unaojumisha mahali chuo kilipo pamoja na eneo la Mlima Kola umeelezwa kuchukua miaka 20 mpaka kukamilika kwake mwaka 2043 na utagharimu kiasi cga shilingi bilioni 70 ambapo bilioni 64 zitawekezwa eneo la mlima Kola na bil 6 kwenye kampasi ya chuo Kilakala.
Mradi huo unajumuisha Jengo la Utawala, Madarasa, Maktaba, Hosteli za Wanafunzi, Kumbi kubwa za kufundishia, Zahanati, Migahawa pamoja na maeneo ya kuabudia.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Idara ya Taaluma Pius Kafefa, vyanzo vya mapato kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo wa chuo cha ARIMO ni ada za wanafunzi, miradi mbalimbali ya chuo kama vile ushauri wa kitaaluma, fedha kutoka serikalini pamoja na maombi kutoka kwa wafadhili.
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Pinda amesema, ni vyema mradi huo ukawekewa nguvu ili uende kwa haraka kwa kuwa kuchukua muda mrefu kutafifisha uharaka wa maendeleo ya chuo.
"Kujipa muda mrefu kukamilisha mradi wa chuo chenu hakuko sawa kabisa na sisi tunataka mradi uishe haraka ili tuwe na matokeo ya muda mfupi sambamba na waanzishaji mradi kuushuhudia". amesema Mhe. Pinda.
Ameutaka uongozi wa chuo cha ARIMO kuandika mapendekezo ya namna ya kukamilisha ujenzi wa mradi huo kwa haraka ili wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ione namna ya kusaidia ili uishe kabla ya muda wa miaka 20 uliopangwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ardhi Morogoro Profesa Ernest Kahanga ameeleza kuwa, changamoto kubwa inayokikabili chuo ni upungufu wa walimu pamoja na miundombinu ambapo ameweka wazi kuwa, kama chuo hicho kingetatua changamoto hizo kingefanikiwa kudahili takriban wanafunzi 3000 na kukifanya chuo kusonga mbele kwa kasi na kuondokana na utegemezi.
WAZIRI MAKAMBA ASHIRIKI MKUTANO WA 45 WA KAWAIDA WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC
Written By CCMdijitali on Friday, June 28, 2024 | June 28, 2024
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ameongoza ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Kawaida wa 45 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika leo tarehe 28 Juni, 2024 jijini Arusha.
Mkutano huu pamoja na masuala mengine unapitia na kujadili masuala mbalimbali ya kipaumbele katika ukanda wa EAC ambayo ni, Maendeleo ya Miundombinu, forodha na biashara, masuala ya siasa na kijamii, taarifa ya kamati ya rasilimali watu pamoja na kupokea taarifa ya kamati ya ukaguzi na udhibiti wa hesabu za jumuiya kwa kipindi cha mwaka wa fedha unaoishia Juni 2023.
Masuala mengine ni pamoja na, jitihada za kubidhaisha Kiswahili kikanda na kimataifa sambamba na taarifa ya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani tarehe 7Julai ambayo kikanda yatafanyika nchini Kenya na kuhudhuriwa na Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kadhalika, mkutano huu pia umejadili na kusisitiza umuhimu wa kuwasilisha michango ya mwaka kwa wakati kutoka kwa nchi zote wanachama ili kuiwezesha Sekretarieti ya EAC kujiendesha na kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake ya kikanda.
Aidha, kupitia mkutano huo Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Veronica Mueni Nduva alijitambulisha kwa Baraza hilo na kueleza nia yake ya kusimamia ustawi wa kikanda katika kukuza uchumi, uvumbuzi, biashara, ajira na amani na usalama kwa maendeleo endelevu ya wananchi wa EAC.
Viongozi wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (Mb.), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.), Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali.
Mkutano huo umefanyika chini ya Uenyekiti wa Jamhuri ya Sudan Kusini na umehudhuriwa na Nchi zote Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, isipokuwa Somalia imeshiriki kwa njia ya mtandao.
RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA JOPO WAZEE WA JUMUIYA YA SADC NCHINI LESOTHO
Written By CCMdijitali on Thursday, June 27, 2024 | June 27, 2024
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tarehe 26 Juni, 2024, yuko katika Ufalme wa Lesotho kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Jopo la Wazee wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Jopo hili la Wazee wa SADC ambalo Makamu Mwenyekiti wake Mheshimiwa Paramasivum Pillay B. Vyapoory, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Mauritius, limekutana na Serikali na wadau mbalimbali ndani ya Ufalme wa Lesotho, kama mwendelezo wa juhudi ya kusaidia upatitanaji wa utulivu wa kisiasa katika Ufalme huo.
Jopo limekutana na Mhe. Ntsokoane Samuel Matekane, Waziri Mkuu wa Ufalme wa Lesotho; Mhe. Nthomeng Justina Majara, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Sheria na Masuala ya Bunge; Mhe. Mamonaheng Mokitimi, Mwenyekiti wa Seneti; Viongozi wa Vyama vya Upinzani; Mhe. Constance Seoposengwe, Balozi wa Afrika Kusini nchini Lesotho; na wadau mbalimbali.
DKT.DIMWA: AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA
Written By CCMdijitali on Tuesday, June 25, 2024 | June 25, 2024
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amesema Serikali inakopa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya Wananchi wote na sio kwa maslahi ya watu wachache.
Hayo ameyasema katika mwendelezo wa ziara yake wakati akizungumza na wanachama wa katika Tawi la CCM Mafufuni Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini "B" Kichama Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Dkt.Dimwa, alisema kauli za baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani kuilaumu Serikali juu ya masuala ya mikopo ya fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo inatakiwa kupuuzwa kwani fedha hizo ni kwa ajili ya kuimarisha miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami,maji safi na salama,ujenzi wa Skuli za kisasa,hospitali,viwanja vya ndege vya kisasa pamoja na bandari za kisasa.
Alifafanua kuwa katika bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 2024/2025 iliyopitishwa hivi karibuni, zaidi ya asilimia 63 ya fedha za bajeti hiyo zimeelekezwa katika uimarishaji wa miradi ya maendeleo kwa ajili ya kukabili changamoto za wananchi wote wa mijini na vijijini.
"suala la kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo sio la Zanzibar tu wala Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali nchi mbalimbali duniani zinakopa na kwa mujibu wa takwimu kutoka shirika la fedha duniani (IMF) nchi zilizoendelea kiuchumi mfano marekani,urusi,ufaransa na zingine ndio zenye madeni makubwa hivyo hao wanasiasa nawashauri wajiongeze kwa kufanya utafti wa kujua mwenendo wa uchumi wa dunia unaendaje.
Wito wangu kwenu tuendeleeni kuwaombea dua njema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi Mwenyezi Mungu awajaalie nguvu,busara na imani ili nchi iendelee kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika nyanja kiuchumi na kijamii",alisema Dkt.Dimwa.
Katika maelezo yake Dkt.Dimwa, aliwataka Wanachama wa CCM na Jumuiya zake kwa ngazi za Mashina na Matawi kufanya vikao vya mara kwa mara ili kujadili masuala ya maendeleo,changamoto na mikakati ya pamoja ya kuimarisha taasisi hiyo.
Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa, aliwasihi Viongozi,Watendaji na wanachama kwa ujumla kuhamasisha wananchi na wafuasi wa Vyama vya upinzani kujiunga na Chama ili kuongeza idadi ya wapiga kura wa Chama Cha Mapinduzi.
Mapema Dkt.Dimwa akizungumza na wanachama,viongozi na watendaji wa Chama na Jumuiya zake baada ya kuwasili katika Mkoa huo,aliwapongeza kwa kazi kubwa ya kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025 ndani ya Mkoa huo.
Naye Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Omar Ibrahim Kilupi, aliwasisitiza Wanachama hao kuhakikisha wanapata kadi za kupiga kura ili wawe na uhalali wa kukipigia kura nyingi Chama Cha Mapinduzi.
Alitoa shukrani Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa huo, Haji Juma Hajialiahidi kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha CCM inapata ushindi mkubwa wa majimbo yote ya Mkoa huo katika Uchaguzi Mkuu ujao.
DKT.DIMWA: AAGIZA WATENDAJI NA VIONGOZI KURATIBU KERO ZA WANANCHI.
Written By CCMdijitali on Monday, June 24, 2024 | June 24, 2024
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amewataka Viongozi na Watendaji wa CCM kuanzia ngazi za Mashina hadi Mikoa Kichama kuratibu na kufuatilia changamoto zinazowakabili Wananchi na kuziwasilisha katika ngazi za juu za kiutendaji zitafutiwe ufumbuzi wa kudumu.
Hayo ameyasema katika muendelezo wa ziara yake na Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar ya kuimaridha uhai wa Chama, katika Mkoa wa Magharib Wilaya ya Mfenesini Kichama wakati akizungumza na wanachama katika Tawi la CCM Mwanyanya Unguja.
Dkt.Dimwa, alisema kipaumbele cha CCM ni kuhakikisha kila mwananchi anaishi maisha bora na yenye hadhi yanayoendana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.
" Chama Cha Mapinduzi kinaamini kuwa Wanachama na Wapiga kura wapo katika ngazi za Matawi na Mashina yetu hivyo dhamira yetu ni kuwatumikia kwa uadilifu kwani mlituamini na kutupa ridhaa kubwa ya kuongoza nchi.
Kila mtu anaona kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi, kila sehemu ya Zanzibar kuna Hospitali za kisasa zenye vifaa tiba vyote,Skuli za ghorofa, barabara za lami, uwekezaji wananchi kiuchumi na maji safi na Salama yote haya yametekelezwa mijini na vijijini.",alisema Dkt.Dimwa.
Alieleza aliwataka Wanachama hao kuendelea kuhamasisha Wananchi wengine kujiunga na CCM ili kupata idadi kubwa ya wapiga kura wa uhakika.
Akizungumza na wanachama wa CCM katika Wadi ya Bububu shina namba 12, aliwataka wafanye kazi ya kuimarisha uhai wa Chama katika ngazi hiyo kwa kulipa ada kwa wakati.
Kupitia ziara hiyo aliwapongeza Viongozi wa majimbo yote ya Wilaya ya Mfenesini Kichama wakiwemo Wabunge,Wawakilishi na madiwa kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Pamoja na hayo aliwasisitiza Wanachama na Wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la Wapiga kura kwa awamu ya pili ili kupata takwimu sahihi.
Katika ziara hiyo Naibu Dkt.Dimwa, ameambatana na Wakuu wa Idara za CCM Zanzibar pamoja na Manaibu Makatibu wakuu wa Jumuiya zote.
CCM Z'BAR KUWASILISHA PENDEKEZO LA DK.MWINYI KUONGOZA NCHI KWA MIAKA 7.
NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, amesema Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar wamepitisha pendekezo la kuishauri Kamati Maalum ya NEC kuridhia kuongeza muda wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi kuongoza nchi katika muhula wake wa kwanza kwa kipindi cha miaka saba badala ya mitano.
Hayo ameyaeleza wakati akifunga Mkutano wa Baraza Kuu la UVCCM Wilaya Dimami kichama Zanzibar uliofanyika katika Ofisi za Wilaya hiyo Kiembesamaki.
Dkt.Dimwa,alieleza kuwa maamuzi hayo ya kumuongezea muda wa kuongoza nchi Dk.Mwinyi yanatokana na kuridhishwa na kasi yake ya kiutendaji katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa zaidi ya asilimia 100 ndani ya kipindi miaka mitatu na miezi kadhaa toka aingie madarakani.
Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa, alieleza kuwa CCM Zanzibar imeona Serikali kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwani wananchi wanahitaji maendeleo endelevu hivyo Rais Dk.Mwinyi anafaa kuongezewa muda ili Zanzibar iwe nchi ya visiwa iliyoendelea kiuchumi katika ukanda wa Afrika mashariki.
" Wajumbe wa Sektetarieti tumejadili na kutathimini kwa kina juu ya utendaji wa Rais Dk.Mwinyi, tukajiridhisha kuwa hakuna mbadala wake na anastahiki aongoze nchi kwa kipindi cha miaka saba ili apate muda mzuri wa kufanya Mapinduzi ya kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi na kijamii.
Maamuzi yetu yatafuata taratibu za kikatiba na kikanuni kwa kuyawasilisha katika vikao vya ngazi za juu ili vitoe baraka zake ili hoja hii ikapitishwe katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili yaendelee kufanyika mabadiliko ya baadhi ya vipengele vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kwa lengo kuhakikisha tunafanya Uchaguzi Mkuu wa dola kwa kila baada ya miaka saba.", alifafanua Dkt.Dimwa.
Alieleza kuwa Wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla visiwa vya Zanzibar wanampenda,kumthamini na kuridhishwa na utendaji wa Rais wa Zanzibar Dk.Mwinyi kwani amekuwa kiongozi bora katika kutatua kero za wananchi kupitia uimarisha wa sekta mbali mbali za umma na binafsi.
Pamoja na hayo Naibu huyo alisema kila mwananchi mwenye uzalendo na utimamu wa akili anajua maendeleo yaliyotekelezwa visiwani Zanzibar katika sekta ya afya,elimu,usafiri wa anga na majini,uwekezaji,barabara za kisasa,uwezeshaji wananchi kiuchumi,utalii,michezo na miundombinu bora ya biashara na ujasirimali.
Kupitia kikao hicho Dkt.Dimwa, alifafanua juu ya hoja ya ACT-Wazalendo kudai kuwa nchi ina deni kubwa ambapo alieleza kuwa suala la mikopo kwa ajili ya uimarishaji maendeleo ya nchi sio dhambi au uvunjaji wa sheria za nchi kwani hakuna nchi yoyote duniani inayojiendesha kiuchumi kwa fedha zake za ndani bila kukopa benki ya Dunia au nchi zilizoendelea kiuchumi.
Alisema CCM inafanya siasa za kisayansi kwa kusimamia utekelezaji wa sera na mikakati yake kwa vitendo vinavyoonekana na sio porojo na ahadi hewa.
MWISHO
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AONGOZA MATEMBEZI YA BUNGE BONANZA KWA NIABA YA RAIS WA ZANZIBAR
Written By CCMdijitali on Saturday, June 22, 2024 | June 22, 2024
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiongoza matembezi ya Grand Bunge Bonanza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi yaliyoanzia katika viwanja vya Bunge na kumalizia katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi amesema Serikali zote mbili zitaendelea kuweka mazingira bora ya miundombinu ya michezo nchini itakayowawezesha wanamichezo kufanya michezo yao katika mazingira rafiki ambayo yatapelekea kuibua vipaji vipya vya michezo hasa kwa vijana.
Ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika Tamasha la Grand Bunge Bonanza lililofanyika katika kiwanja cha Jamhuri Jijini Dodoma.
Rais Dk Mwinyi amesema kuwa Serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Sera na Mikakati mbali mbali zitaendelea kuboresha Sekta ya Michezo ikiwa ni pamoja na kujenga Uwanja wa kisasa wa michezo Dodoma Mjini ambao utajumuisha viwanja vya mpira wa mikono, pete na netiboli ambapo utakapo kamilika utachukua zaidi wa watazamaji elfu thelathini watakao kuwa wamekaa katika viti bila ya usumbufu wa aina yoyote.
Amesema kuwa Serikali inaendelea kujenga viwanja vya mazoezi na vya upumzikia katika Jiji la Dodoma utakao jumuisha viwanja vya kisasa vya mpira wa miguu, viwanja vya mpira wa wavu, kikapu, pete, tenis na miundombinu mengine ambapo kwa sasa ujenzi huo umefikia asilimia 41.
Aidha amesema kuwa mazoezi yana umuhimu mkubwa katika kuimarisha afya, kujenga umoja na upendo, udugu, nidhamu, ukakamavu na kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kila siku hivyo amewataka Wabunge kuendelea kufanya Tamasha hilo la michozo ambalo linapaswa kuigwa na Taasisi nyengine hapa nchini.
Rais Dkt Mwinyi amesema Grand Bunge Bonanza limekuwa likiwahamasisha Wabunge na watumishi wa Ofisi ya Bunge kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya na kuboresha ufanisi wao kiutendaji sambamba na kuendeleza umoja baina ya Muhimili wa Bunge na Baraza la Wawakilishi pamoja na kudumisha na kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao umeshatimia miaka 60 tokea kuasisiswa kwake.
Nae Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa umoja wa Mabunge Duniani Mhe. Dkt Tulia Ackson amesema Tamasha la Grand Bunge Bonanza linatoa fursa ya kufanya mazoezi pamoja na kuifanya miili iwe na Afya na Utayari wa kufanya kazi kwa uweledi na umakini wa hali ya juu.
Dkt. Tulia amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga kuboresha na kuimarisha Sekta ya Michezo nchini kwa kutenga bajeti ya zaidi ya shilingi Bilioni mia mbili na themanini (280) ambazo zitatumika katika maboresho hayo.
Aidha Mhe. Spika ameipongeza na kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kushirikiana na Bunge katika kufadhili program mbali mbali za Kimichezo zinazoendeshwa na Bunge jambo ambalo linazidisha umoja, upendo na ushirikiano baina ya Bunge na Taasi mbali mbali nchini.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu ABDULMAJID NSEKELA ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha hilo amesema CRDB imekuwa ikifanya kazi kwa karibu sana na Bunge katika shuhuli mbali mbali ikiwemo michezo ambapo wanajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya Grand Bunge Bonanza ambalo limekuwa likitoa hamasa kubwa kwa wananchi kufanya mazoezi.
Nsekela amesema CRDB Benki itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake na kuwa mstari wa mbele katika kutoa ushirikiano na kudhamini program mbali mbali za kimichezo ili kuhakikisha ustawi wa jamii unaimarika na Sekta ya Michezo inaimarika zaidi siku hadi siku.
🗓 22.06.2024
DKT.DIMWA: ASEMA DK.MWINYI AMEWASHIKA PABAYA ACT-WAZALENDO
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amesema viongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo wamekuwa wakitoa kauli za kumtukana Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kutokana na kuwashika pabaya kwa kumaliza ajenda zao kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na Wanachama wa CCM wa Tawi la Fuoni Kiembeni katika ziara ya Wajumbe wa Sektetarieti ya Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar iliyoanza leo katika Mkoa wa Magharibi katika Wilaya ya Dimani Kichama Zanzibar.
Dkt.Dimwa, alisema kasi hiyo ya Dk.Mwinyi ya kutekeleza ahadi alizoa katika kampeni za uchaguzi mkuu wa dola uliopita umekuwa ni pigo kubwa kwa Chama ACT-Wazalendo kwani wamekosa ajenda na hoja za kuwaaminisha wafuasi wao na badala yake wameanzisha mtindo wa upotoshaji na porojo zisizokuwa na muelekeo kisiasa.
Katika maelezo yake Dkt.Dimwa, amewambia wanachama hao kuwa CCM ipo imara na kelele na porojo za wapinzani haziwezi kuitoa Katika malengo yake ya msingi ya kutatua kwa wakati changamoto zinazowakabili wananchi mijini na vijijini.
Aliwasihi Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi kwa ujumla kuendelea kukiamini Chama kwa kukipigia kura nyingi katika Uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025 ili kiendelee kuongoza dola na kufanya mambo mengi ya maendeleo yenye tija kwa vizazi vya Sasa na vijavyo.
" Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi kwa maneno ya siku hizi ameupiga mwingi tena tunasema tatu bila kwa upinzani amekuwa ni mwiba ndio maana wanatapa tapa hawana ajenda wala hoja hivyo wanaamua kupotosha na kubeza kila jambo jema linalofanywa na Serikali zetu.
Wito wangu kwenu endeleeni kutuamini na kutuunga mkono kuna mengi mazuri ya nakuja kwani CCM ni Chama chenye Viongozi wangwana na wenye utu, tumejipanga vizuri kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na maisha bora.",alisema Dkt.Dimwa.
Alisema CCM ina dhamira ya kuimarisha Ofisi zake kuwa za kisasa ili ziendane na hadhi ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
Alifafanua kuwa Chama hicho kitaendelea kufanya siasa za kistaarabu sambamba na kuheshimu misingi ya demokrasia ndani na nje ya taasisi hiyo kisiasa.
Kupitia ziara hiyo awasisitiza Wanachama hao kuendelea kulipa ada ili Chama kipate mapato yatakayosaidia katika kutekeleza shughuli mbalimbali za kisiasa.
Pamoja na hayo aliwataka Wanachama na Wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya pili ili wapate uhalali wa kukipigia kura katika Uchaguzi mkuu ujao.
Dkt.Dimwa akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Jumbi, alisema Serikali imejenga masoko hayo ya kisasa ili kuwawekea Wananchi mazingira bora ya kufanya biashara kwa ajili ya kuongeza vipato vyao.
Alisema baada ya masoko hayo kuanza kufanya kazi Serikali imejipanga kusimamia zoezi la utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ili kuhakikisha wanaendelea kuimarika kiuchumi.
Kupitia ziara hiyo Dkt.Dimwa,aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi kwa utekelezaji mzuri na wenye viwango wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Wananchi katika ziara hiyo wamepongeza kazi kubwa ya utatuzi wa changamoto za wananchi mijini na vijijini.
Akizungumza Mkaazi wa Fuoni Kiembeni Kassim Juma Bakari,alisema Serikali imeweka miundombinu bora ya maji na barabara za ndani zenye lami jambo ambalo ni kielelezo cha utekelezaji wa sera zake kwa vitendo.
Naye Khadija Abdi Kombo mkaazi wa Kisakasa, alisema maendeleo yaliyotekelezwa na Dkt.Mwinyi kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita ndio kibali cha Wananchi kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi.
CAPTION
Picha no.111-NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akivishwa sikafu na Vijana wa Hamasa baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Mkoa wa Magharibi iliyopo Mwera kwa ajili ya ziara ya Wajumbe wa Sektetarieti ya Kamati Maalum ya NEC ya CCM Taifa Zanzibar iliyoanza leo katika Wilaya ya Dimani Kichama.
Picha no.222- NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akisalimiana na Wafanyabiashara mbalimbali katika Soko la Jumbi katika ziara yake ya Wajumbe wa Sektetarieti.
Picha no.333-NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Jumbi katika ziara ya Wajumbe wa Sektetarieti ya Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.
Picha no.444-NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akishiriki ujenzi wa Tawi la CCM Kisakasaka Wilaya ya Dimani Kichama.
MWISHO
NAIBU WAZIRI PINDA ATAKA MABORESHO SEHEMU YA UCHAPISHAJI CHUO CHA ARDHI TABORA
Written By CCMdijitali on Monday, June 17, 2024 | June 17, 2024
Na Munir Shemweta, TABORA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amekitaka Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) kufanya maboresho kwenye sehemu yake ya uchapishaji ili kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia.
Mhe Pinda ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika chuo hicho ikiwa ni jihudi zake za kuhakikisha chuo cha ARITA kinafanya kazi kwa ifanisi na kutoa huduma bora za uchapishaji.
Amesema, uboreshaji sehemu ya uchapishaji ndani ya chuo hicho kutakiwezesha chuo kupata kazi nyingi za uchapishaji na hivyo kukiingiza pesa.
" Hivi vifaa mlivyokuwa navyo ni vya kizamani sana na haviendani na teknolojia ya sasa labda kama vitaendelea kubaki kwa ajili ya kufundishia wanafunzi ili kujua tulikotoka lakini kwa kipindi hiki mnahitaji kuboresha ili muende sambamba na tekonolojia ya sasa" alisema Mhe. Pinda.
Naibu Waziri ameutaka uongozi wa chuo hicho cha Ardhi Tabora kuandika gharama za vifaa vya kisasa ili aoene namna ya kukisaidia kupata vifaa vya kisasa vitakavyokiwezesha chuo kuingia kwenye ushindani wa kibiashara.
Aidha, ameutaka uongozi wa chuo cha ARITA kwenda kuiifunza kwa taasisi nyingine kama vile Taasisi ya Uchapishaji ya Serikali (Government Printers) ili kuona namna bora ya kuimarisha sehemu hiyo ili kiweze kufanya vizuri kwenye utendaji kazi wake.
‘’Chuo hakina Afisa Miradi na lazima chuo kiwe na watu wanaohitajika kama wataalamu wa usimamizi wa miradi hivyo lazima ‘to change direction’ hii ni biashara. Lazima kuwa na mtazamo mpya kuhakikisha mamlaka ya chuo inatoa matokeo. Mnaweza kuona kama mnakwenda lakini mko katika mark time’’. Alisema Mhe. Pinda
Awali Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Juma Mkuki amemueleza Naibu Waziri Mhe. Pinda kuwa, chuo chake kinaendesha mafunzo pamoja na shughuli za uchapishaji kwa kushirikiana na wizara pamoja na wadau wegine ambapo chuo hicho kinazalisha machapisho mbalimbali kwa idara za serikali, taasisi na mashirika mbalimbali kama sehemu ya kujiongezea kipato.
Kwa mujibu wa Mkuki, kuanzia mwaka 2019/2020 hadi sasa chuo kinazlisha machapisho ya nyaraka mbalimbali zinazotumiwa na wizara ya ardhi kwa ajili ya kumilikisha ardhi na usajili kwa ujumla.
‘’Chuo kinatoa huduma kwa taasisi zingine ambazo zinatumia baadhi ya machapisho yetu ikiwa ni pamoja na vitabu mbalimbali na nyaraka zisizo za kiserikali’’. Alisema Mkuki.
Kaimu Mkuu huyo wa chuo cha Ardhi Tabora, amesema, sehemu ya uchapishaji inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maabara kwa ajili ya uchapishaji,
Hata hivyo, ameeleza kuwa, pamoja na chuo kujitahidi kutafuta mitambo na vifaa vya uchapishaji lakini jengo linalotumika ni dogo hivyo chuo hicho cha ARITA kiko kwenye hatua za kuhakikisha jengo hilo linajengwa kwa kushirkiana na wadau nje ya chuo.
-----------------------------------MWISHO--------------------------------------
CCM TANGA YATAJA VIGEZO VITAKAVYOTUMIKA KUWAPATA WAGOMBEA WA UDIWANI, UBUNGE TANGA 2025
Na Oscar Assenga, PANGANI
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimesema kuwa vigezo ambavyo vitatumika kuwapata wagombea kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka huu na ule Mkuu wa Wabunge na Madiwani wa mwakani 2025 kwamba ni wale ambao wanashiriki kwenye vikao kuanzia ngazi ya mashina.
Vigezo hivyo vilitangazwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman wakati aliposhiriki kwenye mkutano wa Shina namba 5 Mtaa wa Majengo Kata ya Pangani Mashariki ambapo pamoja na mambo mengine alihamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wakati utakapofika.
Katika mkutano huo wa Shina namba 5 Mwenyekiti huyo aligawa viti 100 ikiwa ni kuhakikisha wanakuwa na uchumi imara ambao utawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika shina hilo
Alisema kwamba wanahitaji wapate viongozi ngazi ya serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wa Ubunge na Madiwani ambao wanakiheshimu chama cha Mapinduzi.
Alisema kwamba tafsiri ya kukiheshimu chama hicho ni kuhudhuria mikutano ya mashina yako na waanapokuwa hawaudhurii maanake bado haujaonyesha kukithamini na kukipenda chama cha mapinduzi.
“Niwaambie kwamba sio hiari ni suala la lazima viongozi wa ngazi za mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa wilaya, Kata na Mitaa na Vitongoji kuhudhuria kwenye mikutano ya mashina na kwa sasa atakayechukua fomu na kujaza na kueleza mikutano ya shina amehudhuria mara tano wakati hajafanya hivyo tutafuatulia maana mikutasari ipo”Alisema
“Sio suala la Hiari ni lazima kuhakikisha viongozi wa ngazi za wilaya wahudhurie mikutano ya shine lake ,Mwenyekiti wa Kata, Mbunge,Diwani hilo ni jambo la msingi linahimizwa kwenye chama chetu lazima wahudhurie kufanya hivyo ndio kukitendea haki chama chetu ujumbe huo ni kwa viongozi wote wa mkoa wa Tanga kwa sababu ndi anadhama nao na wote”Alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha alisema kwamba suala la viongozi hao kuhudhuria kwenye mikutano hiyo ya mashina yao sio suala la hiari ni suala la lazima na mtakumbuka wakati najaza fomu kwenye uchaguzi wa chama 2022 ile fomu inavipengelea vingi miongoni mwao ilitaka ueleza vikao ambavyo ulivyoshiriki vya CCM kwa nafasi yako.
“Kwa maana lazima ueleze mikutano ya shina umehudhuria mara ngani kwa maana vikao vya matawi na mikutano mashina umehudhuria mara ngapi hilo ni suala la lazima na mara nyingi tumekuwa tukifanya mazoea kuona jambo la kawaida kawaida”Alisema
“Niwahakikishie uchaguzi unaokuja wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji na Mkuu wa Mwakani 2025 wa uchaguzi wa kumchagua Rais, Ubunge na Madiwani kipaumbele cha kwanza cha watakaopewa kwenye kugombea ni wale wote ambao wanashiriki vikao na mikutano ya matawi na mashina ya CCM”Alisema
Aidha alisema kwamba atakayejaza fomu na kueleza mikutano ya shina amehudhuria mara tano na hajawahi kufanya hivyo watafuatilia maana mikutasari ipo kwa nafasi hiyo nyeti wanayotaka kumpa huyo mtu wanajua lazima akakiheshimu chama hivyo lazima wapate kumbukumbu zake kwa usahihi na kwa uhakika.
“Kwa hivyo wale wote wanaotarajia kugombea nafasi kwenye chama chao kwenye kura za maoni wajue kama kwenye mashina yao hawakuheshimu vikao vya mashina waliviona havina maana yoyote balozi balozi maana balozi kazi tuliomuachia ni kusuluhusha ndoa za watu”Alisema Mwenyekiti.
MAMA MARIAM MWINYI ASHIRIKI HAFLA YA UGAWAJI WA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WASICHANA
Written By CCMdijitali on Sunday, June 16, 2024 | June 16, 2024
Mama Mariam Mwinyi, alisema, zoezi la ugawaji wa taulo hizo kwa wasichana wa Zanzibar ni endelevu wa kuwafikia wasichana wote nchi nzima ili kuondosha changamooto inayowakumba wengi wanaoshindwa kuhudhuria masomo yao wakiwa kwenye ada zao za mwezi.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Salama Mbarouk Khatibu pia aliipongeza taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation kwa jitihada zake na kuendelea kutoa huduma bora za jamii ikiwemo elimu na afya hasa kwa watu wa mkoa huo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Taasisi ya “Zanzibar Maisha Bora Foundation”, Gulam Abdul Karim, alisema lengo la mradi wa “Tumaini Initiative” wa taasisi hiyo ni kutatua changamoto za hedhi kwa wanafunzi wote wa kike wa Zanzibar.
DKT.DIMWA : AMTEMBELEA SHEIKH MSABAHA. Inbox
NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, amesema Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kutekeleza wajibu wake wa kusimamia Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 kwa kasi na kwa ufanisi kama kilivyoahidi katika kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na Mtumishi wa Chama hicho Sheikh Salum Msabaha huko nyumbani kwake Fuoni, Wilaya ya Magharibi ‘’A’’ Unguja.
Alisema wananchi wanahitaji maendeleo endelevu ili wapate unafuu wa maisha katika masuala mbali mbali ya kiuchumi na kijamii.
Dkt.Dimwa, alieleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kumfariji mtumishi huyo wa Chama Cha Mapinduzi anayeumwa kwa muda mrefu ili awe na matumaini ya kuamini kuwa bado viongozi na watendaji wa Chama wanathamini mchango wake mkubwa wa kiutendaji katika ngazi mbali mbali za Chama.
“Chama Cha Mapinduzi kinathamini sana mchango wako katika utekelezaji wa majukumu na tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuafu na kukujaalia afya njema ili upone na kurudi kazini ili tuendelee kushirikiana katika kuimarisha Chama chetu.”, alisema Dkt.Dimwa.
Alifafanua kuwa Chama kitaendelea kutoa mchango wake katika kusimamia masuala ya matibabu ili kuhakikisha mtumishi huyo anapona ili aendelee na majukumu yake.
Kupitia ziara hiyo Dkt.Dimwa, alisema CCM ni daraja baina ya wananchi na Serikali katika kusimamia masuala mbalimbali ya maendeleo yanayotoa fursa pana ya kunufaika kiuchumi kwa wananchi wote bila ubaguzi.
Naye Mtumishi huyo Salum Msabaha, amempongeza Naibu Katibu Mkuu Dkt.Dimwa kwa kazi kubwa anayofanya katika kuimarisha Chama Cha Mapinduzi nchini katika nyanja za kisiasa,kiitikadi,kiutendaji na kiungozi.
MWISHO
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI TAMASHA LA JOGGING LA KM 5
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 16, 2024 ameshiriki katika Tamasha la Jogging lililoandaliwa na kituo cha Televisheni na Radio cha EFM.
Jogging hiyo la Kilomita tano imeanzia katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe hadi Tangi Bovu mbezi na kurejea viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pia ameshiriki katika jogging hiyo.
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- AFUNGUA KITUO CHA UFUNDI
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema ujenzi wa kituo cha Karakana ya Uchongaji kilichopo Mwera PONGWE ni hatua muhimu ya utekelezaji wa miradi jumuishi ya elimu itakayowawezesha vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu kupata ujuzi utakaowasaidia katika maisha yao.
Ameyasema hayo katika hafla ya Uzinduzi wa kituo cha ujuzi kwa vijana cha utekelezaji wa mpango changmani wa kuwawezesha vijana rika wenye umri wa miaka 15- 19 iliyofanyika katika viwanja vya skuli ya Mwera Pongwe, Wilaya ya Kati Unguja.
Amesema utekelezaji wa mradi huo unatoa fursa kwa vijana kujifunza kwa vitendo na kuweza kuwa mafundi mahiri wa kuchonga aina mbali mbali za samani pamoja na kupatiwa ujuzi wa kutengeneza vifaa vya aluminium ili kuwajengea uwezo zaidi katika kukabiliana na harakati za kimaisha.
Mhe. Hemed amesema kituo hicho pamoja na kutoa ujuzi kwa vijana pia kitatoa msaada mkubwa wa kufanya ukarabati wa vifaa mbali mbali kama vile meza, viti na madawati yatakayo haribika katika Maskuli sambamba na kuwataka walimu wakuu kuitumia fursa hio kwa kwa kufanya marekebisho ya samani zilizoharibika katika maskuli yao ili ziendelee kutumika kwa muda mrefu.
Aidha Mhe. Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imeongezwa na kufikia Bilioni 830 lengo ikiwa ni kuiwezesha wizara hio kufikia mageuzi ya elimu ya juu na kuimarisha miundombinu ya elimu kwa kujenga madarasa 1500 ilj kufikia azma ya Serikali ya kuingia mkondo mmoja wa asubihi kwa idadi ya wanafunzk 45 kwa kila darasa.
Sambamba na hayo amesema katika kuimarisha mafunzo ya Ufundi na Amali Serikali imejipanga kujenga vituo viatano vya Mafunzo ya amali vitakavyojengwa Unguja na Pemba pamoja na kujenga vituo vya ujuzi bunifu katika skuli 33 za Sekondari kwa Unguja na Pemba ambapo kwa sasa zitajengwa katika skuli tatu (3 ) kila Wilaya lengo ikiwa ni kuwatayarisha vijana kupata ujuzi ambao utawasaidia katika kujiajiri baada ya kumaliza masomo yao.
Mhe. Hemed amewashukuru washirika wa maendelo Serikali ya Canada na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Duniani (UNICEF) Kwa kufadhili mradi huu wenye lengo la kuwasaidia vijana kupata ujizi utakaowadaidia katika kupata ajira na kujikwamua kiuchumi.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesisitiza suala la kutunza Amani iliyopo ndani ya nchi na kuvitaka vyombo husika kutumia zaidi busara wakati wa kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa amani kwa bila ya amani hakuna maendeleo nchini.
Kwa upande wake Kaimu Waziri wa elimu Zanzibar Ali Abulghulam Hussein amesema Serikali ya Awamu ya Nane(8) imeazimia kufanya mabadiliko makubwa katika Sekta ya Elimu kwa kusomesha Mafunzo ya Amali na ubunifu kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuoni.
Amesema Wizara itahakikisha wanafunzi wanaomaliza katika vyuo hivyo wanapata ujuzi ambao utawasaidia katika kujiajiri na kuajiriwa katika mashirika na Taasisi mbali mbali ndani na nje ya nchi sambamba na kujenga vituo vya elimu amali kila wilaya kwa unguja na pemba.
Akitoka maelezo ya Kitaalamu kuhusu program ya ZIPOSA Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdulla Said amesema uwepo wa mradi huo utawasezesha watoto wa kike na kiume katika kumaliza elimu yao ya lazima ambayo waliikosa kutokana na chamgoto mabali mbali za kimaisha.
Amesema kuwa jumla ya vijana 150 wapo katika vituo vya elimu mbadala Unguja na Pemba wakijifunza fani mbali mbali za ufundi pamoja na kujiongezea ujuzi na maarifa unaoendana na soko la ajira nchini.
Mapema Mwakilishi Mkaazi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Duniani UNICEF nchini Tanzania Bibi Elke Wisch ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kuboresha Sekta ya Elimu nchini na kutoa kipaombele kwa vijana hasa wale walioacha skuli kwa sababu mbali mbali na kuhakikisha wanawarudisha skuli na kuendelea na masomo yao.
Imetolewa na kitengo cha Habari (OMPR)
Tarehe 15.06.2024
..................................................................................
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa kituo cha ujuzi kwa vijana kilichopo Mwera Pongwe Wilaya ya Kati Unguja. |
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akiweka jiwe la zinduzi wa kituo cha ujuzi kwa vijana kilichopo Mwera Pongwe Wilaya ya Kati Unguja. |