Comoro kushirikiana na Tanzania katika sekta za kimkakati asema Rais Azali Anena
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazumgumzo na Rai...
Latest Post
November 30, 2022
Nape na vijana wadeki barabara kumpokea Rais
Written By CCMdijitali on Wednesday, November 30, 2022 | November 30, 2022
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, akideki barabara pamoja na vijana wa mkoa wa Lindi |
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, ameungana na vijana wa mkoa wa Lindi kufanya usafi maeneo mbalimbali ya mkoa huo ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye atawasili mkoani humo kesho Desemba Mosi, 2022.
Vijana hao walifanya zoezi hilo la kusafisha barabara baada ya kumaliza matembezi maalum katika maeneo mbalimbali ambapo walitumia fursa hiyo kufikisha salamu zao kwa Rais Samia kupitia kwa Waziri wa Habari Nape.
"Sisi Vijana wa Lindi ilifikia hatua baadhi ya wanasiasa walituita watoto tuliotengwa lakini walisahau licha ya mkoa wa Lindi kutotembelewa na Rais kwa muda mrefu Mama yetu Samia Suluhu akiwa Makamu wa Rais alitutembelea sana" Amesema Mustafa Dumbo kwa niaba ya vijana wa Lindi
Akiwajibu vijana hao Waziri Nape Nnauye amewataka vijana hao kutambua Rais Samia anaupenda sana mkoa wa Lindi na ndiyo maana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, anatokea huko.
November 30, 2022
7th SWAPO PARTY CONGRESS
7th SWAPO PARTY CONGRESS
24-28 NOVEMBER 2022
MBUNGE wa Jimbo la Mlalo, Rashid Abdallah Shangazi amewakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM)-katika Mkutano Mkuu wa Saba wa Chama cha Ukombozi wa Nchi ya Namibia -SWAPO(Southe West Africa Peoples Organization)
SWAPO kimeendelea kuwa Chama cha Siasa chenye Malengo Makuu ya Kushika Dola na kutengeneza umoja na Mshikamano kuelekea Maendeleo makubwa ya kijamii na kiuchumi (Socio-Economic Development )kwa wananchi wa Namibia.
Aidha Mheshimiwa Shangazi amefurahishwa kuona bado vyama vingi vya ukombozi wa eneo la kusini mwa Africa vipo imara sana na kukumbuka wema wa watanzania wakati wote wa harakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika kupitia Jukwaa la Nchi zilizo Mstari wa Mbele chini ya Utendaji mahiri wa aliyekuwa Katibu Mkuu wake Hayati Brigedier Hashim Mbita (RIP)
Aidha vita dhidi ya siasa za ubaguzi wa rangi yaani (Apartheid)katika Nchi ya Afrika ya Kusini vilihusisha pia vyama hivi vya ukombozi kwa nyakati tofauti.
Historia hii imevikutanisha vyama rafiki vya-
1- Chama Cha Mapinduzi -Tanzania
2- Zanupf-Zimbabwe
3- MPLA-Angola
4- Communist Party of Cuba
5- Communist Party of China
6- Communist Party of Russia
7- FRELIMO -Mozambique
8- ANC -South Africa
9- Palestine Liberation Movement
10- United Socialist Party of Venezuela (PSUV)
Shukrani za dhati kwa Mwenyekiti wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa uongozi bora na mahiri katika stratejia na mikakati madhubuti ya kukuza diplomasia na kuimarisha undugu kichama na kisiasa.
Ahsante comrade Daniel Chongolo kupitia idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kwa kuimarisha na Kuyaenzi Mahusiano Yetu na Vyama rafiki.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
November 26, 2022
Wafanyakazi KADCO watakiwa kuwa Wazalendo.
Written By CCMdijitali on Saturday, November 26, 2022 | November 26, 2022
Wafanyakazi KADCO watakiwa kuwa Wazalendo.
Na Jamal Zuberi, Tanga
Serikali mkoani Tanga imesema kuwa mikutano ya Baraza la Wafanyakazi itumike kujadili malengo na mipango ya Taasisi ikiwa ni pamoja na maslahi ya watumishi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba akifungua Mkutano wa kwanza 2022/2023 wa Baraza la Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KADCO) katika ukumbi wa Tanga Beach Hoteli, Jijini Tanga.
"Mabaraza haya ni jukwaa muhimu kujadili utendaji wa kazi wa kila siku na jinsi ya kuboresha utendaji huo zaidi" alisisitiza zaidi Mgumba.
Amesema kuwa ni muhimu tija na maslahi lazima yawe na uwiano ili kuwa na matokeo chanya ya utendaji bora, unaolenga kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi tunaowatumikia.
"Tuelewane utendaji bora zaidi unaongeza tija, tija ikiongezeka ni rahisi kuongeza maslahi ambayo hatimae yanawawezesha watumishi kuishi maisha bora zaidi.
" Naomba kama watumishi katika Sekta ya Usafirishaji wa Anga, lazima mfanye kazi kwa uzalendo, maadili na nidhamu ya juu muonyeshe mfano wakuigwa " alisisitiza Mkuu huyo
Mgumba amewapongeza Wafanyakazi hao wa KADCO kuwa kiwanja bora cha ndege Afirka na Duniani kwa jumla kwa kupewa Tunzo mbali mbali za kimataifa kwa huduma bora pamoja na kuwa na Hati Safi ya matumizi ya fedha.
November 25, 2022
PROFESA MBARAWA AWATAKA TRC KUTOA TAARIFA KWA WAKATI
Written By CCMdijitali on Friday, November 25, 2022 | November 25, 2022
PROFESA MBARAWA AWATAKA TRC KUTOA TAARIFA KWA WAKATI
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amelitaka Shirika la Reli nchini (TRC), kutoa taarifa kwa wakati kuhusu maendeleo ya reli ya kisasa ya sgr na mchakato wa ununuzi na mapokezi ya vifaa vyote vya reli hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya mabehewa 14 kati ya 59 ya awamu ya kwanza ya SGR yaliyowasili Prof. Mbarawa amesema zaidi ya shilingi bilioni 882 tayari zimetumika katika kununua vichwa vya treni, mabehewa na vifaa vingine muhimu vitakavyotumika katika uendeshaji wa reli hiyo na vitawasili kwa awamu.
“Waelezeni wananchi ukweli kuwa kuna mabehewa ya aina tatu yaliyoagizwa yaani daraja la kwanza, la juu na la tatu ili wasipotoshwe pindi yanapowasili”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa mabehewa 45 yaliyosalia ya daraja la tatu yatawasili mwezi mei mwakani.
Amezungumzia umuhimu wa wanahabari kufanya utafiti na kujiridhisha kwa vyanzo sahihi kabla ya kuandika na kutangaza taarifa za miradi mikubwa ya kitaifa ili kuondoa upotoshaji kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Bw. Masanja Kadogosa amesema wamejipanga kuongeza mabehewa katika reli ya kati na kaskazini katika kipindi cha mwisho wa mwaka ili kuondoa changamoto za usafiri.
“Tumejipanga kuhakikisha usafiri wetu unakuwa salama na safari zote zinafuata ratiba iliyopangwa ili kutoa huduma bora kwa wananchi’ amesisitiza Kadogosa.
Naye Balozi wa Korea Kusini, Kim Sun Pyo amesema nchi yake itaendeleza ushirikiano na Tanzania katika uimarishaji wa miundombinu nchini.
@tzrailways
November 25, 2022
MAJALIWA: MRADI WA SGR UTAKAMILIKA KAMA ULIVYOPANGWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kwamba Serikali itaendelea kuhakikisha mradi huo unajengwa kwa viwango na kukamilika kama ilivyobainishwa kwenye mkataba.
Amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo unaendelea vizuri katika vipande vyote na kwamba Serikali itahakikisha mradi huo haukwami na itakabiliana na viashiria vyote vinavyoweza kukwamisha utekelezaji wake.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 24, 2022) wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa stesheni kuu ya Dodoma katika eneo la Mkonze, jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa stesheni hiyo, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania wanaoshiriki katika ujenzi wa mradi huo wasimamie usalama wa mradi na wawe walinzi ili ukamilike kama ilivyokusudiwa.
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassam inaendelea kufanya maboresho kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya usafirishaji.
“Rais Samia anaendelea na mkakati wake wa ujenzi wa reli, endeleeni kuwa na imani na Serikali yenu, lengo lake ni kuhakikisha anainua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuwa na mkakati wa maeneo ya uwekezaji kutokana na fursa ya ujenzi wa reli hiyo ikiwemo ujenzi wa kituo cha mabasi jirani na stesheni hiyo.
Kwa upande wake, Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema kuwa Shirika hilo lipo kwenye mpango wa ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa ya mizigo. “Hadi sasa TRC imesaini mkataba wa ununuzi wa vichwa vya treni vya umeme 19, seti za treni 10 zenye uniti 80.”
Amesema pia shirika hilo itanunua mabehewa ya kawaida ya abiria 89, mabehewa ya ghorofa 30 ambayo yanakuja, mabehewa ya mizigo 1,430 na vifaa vya matengenezo 26.
November 25, 2022
MKUTANO MKUU WA KUMI WA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA 24 NOVEMBA 2022 DODOMA
UCHAGUZI MKUU JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA
MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU JUMUIA YA WAZAZI
MWENYEKITI
1.ALLY KHAMIS MASUDI-5
2.HASSAN HAJI ZAHARA-6
3.BAKARI NAMPENYA KALEMBO-21
4.SAID MOHAMED SAID-43
5.ALLY MAULID OTHMAN-57
6.MWANAMANGA JUMA MWADUGA-61
7.DR.EDMUND BENARD MNDOLWA-64
8.FADHIL RAJAB MAGANYA-578
MAKAMU MWENYEKITI
1.FATMA ABEID HAJI-25
2.AMEIR AHMED-44
3.HAIDARY HAJI ABDALLAH-48
4.ZAHORO SALEHE MOHAMED (MKULIMA)-56
5.SAID MOHAMED DIMWA-77
6.DOGO IDD MABROUK-530
NAFASI YA HALMASHAURI KUU YA CCM(NEC) TANZANIA BARA NAFASI TATU(3)
1.NYIRIZA MAKONGORO NYIRIZA-21
2.BUPE NELSON MWAKANG'ATA-26
3.MECKTRIDIS FRATERN MDAKU-27
4.DANIEL GEORGE SAYI-41
5.MOHAMED NASORO NGINGITE-46
6.MGORE MIRAJI KIGERA-58
7.ANGELA CHARLES KIZIGHA-163
8.KELVIN PASCHAL TEGWA-176
9.ADAMU KIGHOMA ALLY MALIMA-195
10.PAUL HERMAN KIRIGINI-215
11.DR.ANGELA LUBALA MABULA-234
12.GEORGE BRUNO GANDYE-238
13.DR.DOTO MASHAKA BITEKO-535
14.HAMOUD ABUU JUMA-569
NAFASI YA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC) TANZANIA VISIWANI NAFASI MBILI(2)
1.ZAWADI SULEIMAN ABDULA-21
2.SAID MUSA ZUBERI-26
3.SULEIMAN AME KHAMIS-32
4.SAID MUSA ZUBERY-41
5.DR.HAJI MWITA HAJI-65
6.KHAMIS JUMA MWALIM-86
7.RAMADHAN ISSA KIPAYA-160
8.SULEIMAN JUMA KIMEA-205
9.AMINA ALLY MOHAMED-266
10.HABIBA ALLY MOHAMED-335
11.KHADIJA SALUM ALLY-387
November 25, 2022
RAIS SAMIA AIPONGEZA CCM MANYARA KWA UCHAGUZI USIO NA PURUKUSHANI
November 24, 2022
MKUTANO MKUU WA KUMI WA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA 24 NOVEMBA 2022 DODOMA
Written By CCMdijitali on Thursday, November 24, 2022 | November 24, 2022
UCHAGUZI MKUU JUMUIA YA WAZAZI TAIFA
NAFASI YA HALMASHAURI KUU YA CCM(NEC) TANZANIA BARA NAFASI TATU(3)
1. NYIRIZA MAKONGORO NYIRIZA-21
2. BUPE NELSON MWAKANG'ATA-26
3. MECKTRIDIS FRATERN MDAKU-27
4. DANIEL GEORGE SAYI-41
5. MOHAMED NASORO NGINGITE-46
6. MGORE MIRAJI KIGERA-58
7. ANGELA CHARLES KIZIGHA-163
8. KELVIN PASCHAL TEGWA-176
9. ADAMU KIGHOMA ALLY MALIMA-195
10. PAUL HERMAN KIRIGINI-215
11. DR.ANGELA LUBALA MABULA-234
12. GEORGE BRUNO GANDYE-238
13. DR.DOTO MASHAKA BITEKO-535
14. HAMOUD ABUU JUMA-569
NAFASI YA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC) TANZANIA VISIWANI NAFASI MBILI(2)
1. ZAWADI SULEIMAN ABDULA-21
2. SAID MUSA ZUBERI-26
3. SULEIMAN AME KHAMIS-32
4. SAID MUSA ZUBERY-41
5. DR.HAJI MWITA HAJI-65
6. KHAMIS JUMA MWALIM-86
7. RAMADHAN ISSA KIPAYA-160
8. SULEIMAN JUMA KIMEA-205
9. AMINA ALLY MOHAMED-266
10. HABIBA ALLY MOHAMED-335
11. KHADIJA SALUM ALLY-387
November 24, 2022
DR JAFO APOKEA TUZO YA MWANAFUNZI BORA ALIYELETA MANUFAA KWA CHUO NA TAIFA MIAKA 40 YA SUA
DR JAFO APOKEA TUZO YA MWANAFUNZI BORA ALIYELETA MANUFAA KWA CHUO NA TAIFA MIAKA 40 YA SUA
Morogoro
Kuelekea miaka ya Arobaini tokea kuanzishwa na Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA kimetoa tuzo ya Kudhamini Mchango kwa Mwanafunzi Dr Selemani Said Jafo ambaye amefanya vizuri katika masomo na kuleta tija kwa Jamii hiyo Leo kwa miongoni mwa walisoma SUA,
Akizungumza wakati wa kupokea Tuzo hiyo Dr Jafo alisema kuwa ni heshima kwake binafsi na Taifa Kupokea Tuzo hiyo ya Udhamini Mchango mzuri kwa mwanafunzi aliyesoma SUA na kuleta tija kwa Jamii hasa katika Kilimo,Elimu na Mazingira ,
"Hii ni heshima Sana kwangu na taifa pia natoa Shukran za dhati kwa Uongozi Chuo kikuu cha Kilimo SUA Kwa kunipatia Tuzo maana nilipata kusoma hapa miaka iliyopita katika ngazi ya Shahada na Wanafunzi wapo wengi Sana ila waliona wanipatie mie hasa kwa Mchango mkubwa nilioutoa katika uhifadhi na utunzaji wa Mazingira alisema Dr Jafo"
Chuo kikuu cha Kilimo Sua leo 25.12.2022 kinahitisha Mahafali ya arobaini kwa kudahilisha wanafunzi katika kada mbalimbali ikiwemo ya Kilimo,Mifugo,Elimu na Afya.
November 24, 2022
Mheshimiwa Mgandilwa na Kamati ya Usalama Wilaya wafanya ziara ya kutembelea viwanda vya saruji Wilayani Tanga.
TANGA MJINI
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mheshimiwa Hashim Mgandilwa Novemba 24, 2022 akiambatana na Kamati ya Usalama Wilaya walifanya ziara ya kutembelea viwanda vya saruji kwa lengo la kukagua utekelezaji wa uthibiti uchafuzi wa mazingira hasa kutokana na uzalishaji wa saruji katika viwanda hivyo.
Mh Mgandilwa amewasisitizia wamiliki wa viwanda kuhakikisha wanaweka mifumo bora ya kuzuia kusambaa kwa vumbi,katika makazi ya Wananchi ili kupunguza athari za kiafya zitakazo jitokeza hapo baadaye kwa wale watako pata madhara kutokana na vumbi linalozalishwa katika viwanda hivyo ikiwa ni pamoja na kuandaa (Action plan) ya namna ya kutunza mazingira kwa kupanda miti mingi na mingine kugawa kwa wananchi.
@ofisi_ya_dc_tanga @ofisiyamkuuwamkoawatanga @hashimmgandilwa @dashian__
November 12, 2022
𝗠𝗔𝗩𝗨𝗡𝗗𝗘: 𝗨𝗧𝗘𝗞𝗘𝗟𝗘𝗭𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗜𝗥𝗔𝗗𝗜 𝗬𝗔 𝗨𝗝𝗘𝗡𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗕𝗪𝗔𝗪𝗔 𝗬𝗔 𝗨𝗠𝗪𝗔𝗚𝗜𝗟𝗜𝗔𝗝𝗜 𝗜𝗧𝗔𝗖𝗛𝗢𝗖𝗛𝗘𝗔 𝗞𝗨𝗞𝗨𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗘𝗞𝗧𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗟𝗜𝗠𝗢.
Written By CCMdijitali on Saturday, November 12, 2022 | November 12, 2022
𝗠𝗔𝗩𝗨𝗡𝗗𝗘: 𝗨𝗧𝗘𝗞𝗘𝗟𝗘𝗭𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗜𝗥𝗔𝗗𝗜 𝗬𝗔 𝗨𝗝𝗘𝗡𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗕𝗪𝗔𝗪𝗔 𝗬𝗔 𝗨𝗠𝗪𝗔𝗚𝗜𝗟𝗜𝗔𝗝𝗜 𝗜𝗧𝗔𝗖𝗛𝗢𝗖𝗛𝗘𝗔 𝗞𝗨𝗞𝗨𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗘𝗞𝗧𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗟𝗜𝗠𝗢.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde amesema utekelezaji wa miradi ya mabwawa unaoendelea nchini hivi sasa utasaidia sana kukuza sekta ya kilimo nchini Tanzania na kuongeza eneo kubwa zaidi linalofanya kilimo cha umwagiliaji.
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 12 Novemba, 2022 wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa bwawa la Membe linalojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.
"Katika bajeti ya mwaka 2022/2023 Serikali kupitia Tume ya Umwagiliaji imepanga kujenga jumla ya mabwawa 14 nchi nzima, likiwemo bwawa hili la Membe litakalo kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita Bilioni 12."
Pamoja na bwawa hili kutumika katika shughuli za umwagiliaji, pia litawekwa miundombinu ya kusaidia unyweshaji maji mifugo, kupeleka maji ya matumizi ya majumbani kwa vijiji vinavyozunguka na kuwa sehemu ya utalii kwa wananchi mbalimbali, hatua ambayo itaongeza mapato ya Halmashauri ya Chamwino.
"Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ametuongezea bajeti Wizara ya Kilimo ambapo fedha nyingi zimeelekezwa katika miradi ya umwagiliaji ili kuhakikisha tunakuwa na vyanzo vya uhakika vya maji na kuwezesha wakulima kufanya kilimo zaidi ya mara moja ndani ya mwaka”Alisema Mavunde
Vilevile, Mhe Mavunde alimpongeza Bw. Raymond Mndolwa, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kazi nzuri anayoifanyia ya usimamizi madhubuti wa mkakati wa Serikali wa kendeleza kilimi cha umwagiliaji, na kubainisha kuwa ni wazi kuwa ndoto ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kufikia eneo la umwagiliaji la hekta 1,200,000 ifikapo 2025 linaenda kufikiwa.
Naye Diwani wa Kata ya Membe Wilayani Chamwino, Mheshimiwa Simon Petro Machengu alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mradi huo mkubwa kwenye Kata yake, na kubainisha kuwa wananchi wa Membe hawana cha kumlipa zaidi ya kumwombea kwa Mungu ili azidi kumpa afya njema na utashi wa kuwatumikia watanzania.
@bashehussein @anthonymavunde
@nirc_tz
#SSH
#Agenda10/30
#KilimoNiBiashara
November 11, 2022
WAZIRI BASHUNGWA AMTEMBELEA RAIS MWINYI, IKULU ZANZIBAR
Written By CCMdijitali on Friday, November 11, 2022 | November 11, 2022
WAZIRI BASHUNGWA AMTEMBELEA RAIS MWINYI, IKULU ZANZIBAR
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Innocent Lugha Bashungwa(Mb) leo tarehe 11 Novemba 2022, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi. Ikulu, Zanzibar.
Hii ni ziara maalum ya Waziri Bashungwa kumtembelea na kufanya Mazungumzo na Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hussein Ali Mwinyi ambaye pia aliwahi kuiongoza Wizara ya Ulinzi na JKT kabla ya nafasi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Kadhalika, Waziri Bashungwa amemshukuru na kumpongeza Rais Mwinyi kwa kuhudumu wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa miaka 11 huku akiahidi kuendelea kusimamia misingi aliyoianzisha kwa manufaa ya ustawi wa nchi na ustawi wa Muungano.
MWISHO
November 10, 2022
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewataka wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanazingatia mkataba wa lishe ili kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Written By CCMdijitali on Thursday, November 10, 2022 | November 10, 2022
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewataka wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanazingatia mkataba wa lishe ili kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Ameyasema hayo Mjini Kibaha kwenye kikao cha kusaini mkataba wa lishe kwa kipindi cha miaka nane hadi Juni 30 mwaka 2030 baina yake na wakuu wa Wilaya za mkoa huo.
Kunenge asema kuwa mkataba huo una malengo ya kupunguza vifo vya watoto wachanga ambapo kupitia mkataba huo faida zitakazopatikana ni kupungua kwa vifo hivyo endapo suala la lishe litazingatiwa.
"Faida nyingine ya kusainiwa mkataba huu ni kuondoa kaya asilimia 1.8 ambazo zinatumia chumvi ambayo haina madini joto ya kutosha, kuhakikisha utapiamlo kwa watoto hauzidi asilimia tano ya viwango vinavyokubalika duniani,"amesema Kunenge.
Aidha amesema kuwa faida nyingine ni kuimarisha mkakati wa mwaka 1994 wa uwekaji madini joto kwenye chumvi kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto mwilini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Gunini Kamba amesema kuwa lishe duni ni hatari zaidi kwa wanawake wajawazito, watoto wachanga ambapo athari zake ni vifo kwa akina mama na watoto.
Kamba amesema kuwa lishe duni husababisha kinga ya mwili kushuka na mwili kushindwa kupambana na vimelea vya magonjwa hivyo ni muhimu lishe bora kuzingatiwa kuanzia ngazi ya Kijiji Mtaa na kata na hiyo itasaidia kupunguza gharama za matibabu ambapo watatoa elimu kuhusu lishe bora.