Comoro kushirikiana na Tanzania katika sekta za kimkakati asema Rais Azali Anena

  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazumgumzo na Rai...

Latest Post

WAZIRI UMMY AKAGUA UTAYARI WA KUKABILIANA NA EBOLA AMESISITIZA MAFUNZO ZAIDI KWA WATUMISHI NA VIFAA KINGA

Written By CCMdijitali on Sunday, October 30, 2022 | October 30, 2022

Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu  ametembelea kituo cha kutibu magonjwa ya mlipuko na ambukizi cha Temeke {Temeke Isolation Center} pamoja na Kipawa kujionea utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola.

Waziri Ummy amesema kuwa Ugonjwa wa Ebola ni tishio huku hadi kufikia jana katika nchi ya Uganda ambapo kuna ugonjwa wa Ebola wamepata wagonjwa wapya 5 na kufanya idadi ya waliopata maambukizi hayo tangu mlipuko {Septemba, 2022} kufikia sasa ni jumla ya watu 126.

Amesema waliolazwa {Active Cases Admitted in hospital} 54 na vifo 32 vimethibitika. Uganda kufikia sasa wanafuatilia watu 2183 {contacts} ambao walikuwa karibu na watu waliothibitishwa kuwa na ebola.

"Wasiwasi wetu unazidi baada ya kuwa ugonjwa umeingia Kampala na Entebbe kwa hiyo ndege zinazokuja kutoka Kampala, kuja Dar es Salaam na mabasi "Kuibuka kwa Ebola Uganda kunaiweka Tanzania katika hatari ya kupata mlipuko huu Kutokana na mwingiliano mkubwa wa kiuchumi na kijamii na Uganda" amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha Waziri Ummy amesema timu ya wataalam ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko itapatiwa mafunzo ya namna ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola ili waweze kutoa huduma bora.




RAIS SAMIA ATOA FEDHA UJENZI WA NJIA NNE MBEYA TUNDUMA KUPUNGUZA FOLENI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema barabara kuu ya Kutoka Dar es salaam kuelekea Mpakani Tunduma imelemewa. 

 Akizungumza katika ziara yake Mkoa wa Songwe Mbarawa amesema ufinyu wa barabara hiyo unaweza kuwa chanzo cha Mlundikano wa magari katika mpaka wa Tunduma .

 "nimekuja kuangalia hali halisi ya mpaka kiufupi barabara hii ya mpaka imelewa, na tayari serikali imeshaandaa mkakati wa kutatua Changamoto hii tayari makampun nane yameshajitokeza kwaajili ya Ujenzi wa barabara hizi nne, Rais samia ameshaliona tatizo hili ndiyo maana ametoa fedha za Ujenzi wa barabara hizo nne" amesema Mbarawa.

 Aidha Mbarawa amezungumzia upungufu wa mashine ya scana katika upande wa nnchi jirani hali ambayo inachangia kuwepo kwa mlundikano wa magari mpakani hapo .

 Hata hivyo Mbarawa ametembelea mipaka yote miwili katika Mkoa wa Songwe ambapo amekagua daraja lililopo Mpaka wa Malawi,lakini pia Mbarawa ametembela Mpaka wa Tunduma na baadaye kuendelea Mkoani Rukwa .






VIJIJI 5 NA VITONGOJI 41 KUONDOLEWA HIFADHI YA USANGU

Written By CCMdijitali on Friday, October 28, 2022 | October 28, 2022


 

Na Munir Shemweta, WANMM MBARALI

 

Serikali imeamuru vijiji vitano na vitongoji 41 katika vijiji 14 pamoja na sehemu ndogo ya kitongoji cha magwalisi kilichopo mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa wilaya ya mbarali kuhamishwa ili kupisha hifadhi.

 

Pia vitongoji 3 katika kijiji cha Lualaje wilayani Chunya navyo vinatakiwa kuondoka kupisha hifadhi.

 

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 25, 2022 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula katika mkutano wa hadhara na wananchi wa eneo la Ubaruku Mbarali wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta walipofanya ziara kwenye eneo la mto ruaha na mnazi katika kijiji cha Mwanavala ambapo eneo lote liko katika hifadhi.

 

Uamuzi huo wa serikali unalenga kutunza na kulinda ardhi oevu pamoja na vyanzo vya kupokea na kutunza maji yanayotiririka kutoka mito mbalimbali.

 

Alivitaja vijiji vitakavyoondoka kwa asilimia mia moja kuwa ni Luhanga, Madundasi, Msanga, Iyala na kalambo vyenye idadi ya watu 21,252 na kusisitiza watu wa maeneo hayo wanatakiwa wasiwepo na usajili wa vijiji hivyo kufutwa.

 

‘’Katika zoezi hili wenye kulipwa fidia watalipwa na wale wasiostahili wataondoka kama walivyokuja na lengo la serikali ni kuwa na urithi wa watu wote’’ alisema Dkt Mabula.

 

Adha, Dkt Mabula alisema serikali imeridhia vijiji 15 vyenye ukubwa wa hekta 74, 324.12 na ranchi ya Usangu ya NARCO kuendelea kubaki huku vijiji vyote vinavyopakana na hifadhi ya Ruaha kufanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi.

 

Katika mapendekezo yake timu ya wataalamu ilipendekeza eneo la ranchi ya usangu linalopendekezwa kuondolewa ndani ya hifadhi litumiwe na wafugaji watakaohamishwa kutoka kwenye vijiji na vitongoji vinavyopisha hifadhi.

 

Aidha, Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya za Mbarali na Chunya pamoja na wadau wengine waandae mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji vyote vinavyopatikana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

 

Pia Ofisi Tamisemi iwe inashirikiana wadau wote muhimu katika suala la usajili wa vijiji na vitongoji ili kuepusha migogoro ya ardhi inayoweza kujitokeza miongoni mwa wadau ni wizara ya ardhi, wizara ya maji, maliasili na utalii, ofisi ya makamu wa rais mazingira.

 

Uhifadhi wa Bonde la Usangu ulianza mwaka 1953 wakati eneo likijulikana kama pori tengefu la utengule likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 500 kwa lengo la kuhifadhi bioanuwai katika ardhi oevu ya ihefu.

 

kutokana na uharibifu mkubwa wa  mazingira na vyanzo vya maji uliofanyika miaka ya 1990 serikali iliamua kupandisha hadhi pori tengefu la utengule na kuwa Pori la Akiba la Usangu likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 4148 kwa tangazo la serikali namba 436A la tarehe 24 julai 1998.

 

Hata hivyo, uharibifu ulisababisha serikali kuja na mkakati wa kitaifa wa hifadhi ya mazingira ya ardhi oevu na vyanzo vya maji mwaka 2006 na kutaka bonde la usangu kuwa kati ya maeneo ambayo wafugaji waliovamia mabonde na maeneo ya vyanzo vya maji waondolewe.

 

Bonde la usangu ni ardhi oevu ya usangu ni kitovu cha kupokea na kutunza maji yanayotiririka kutoka mito mbalimbali ikiwemo mto Mkoji , Chimala, Kimani, Mbarari , Ndembera na Mzombe inayoanzia katika wilaya ya Wanging'ombe , Makete, Mufindi, Mbeya vijijini na Chunya na kuchangia maji kwenye mto Ruaha. Pia ni makazi ya bioanuwai mbalimbali ikiwemo wanyamapori, ndege wakubwa kwa wadogo aina zaidi ya 300 , samaki na mimea ya aina mbalimbali.

 

‐----------MWISHO-----------

 

Published from Blogger Prime Android App
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisaidiwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (Kulia) kuteremka kutoka kuangalia ukingo wa kuzuia maji katika kijiji cha Mwanavala eneo la Mnazi Mbarari mkoani Mbeya leo.

Published from Blogger Prime Android App
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta ilipokwenda kuangalia uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji katika eneo la Usangu Mbararli Mbeya. Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja leo.

 
Published from Blogger Prime Android App
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakiangalia sehemu ya eneo lenye uharibifu wa mazingira na vanzo vya maji katika kijiji cha Mwanaval eneo la Mnazi Mbarali Mbeya.

 
Published from Blogger Prime Android App
Manaibu Mawaziri wa Wizara za Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, TAMISEMI David Silinde, Nishati Stephen Byabato na Kilimo Anthony Mavunde wakiangalia maji katika mto Ruaha wakati Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta walipotembelea eneo la Mnazi Mbarari Mbeya leo. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).

 

Show quoted text



Mama Mariam Mwinyi Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) akutana na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Rockefeller

Written By CCMdijitali on Tuesday, October 25, 2022 | October 25, 2022

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) amekutana na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Rockefeller Andrew Sweet kwa makubaliano ya kuisaidia kuwezesha mfumo wa chanjo ya Covid-19 kwa wilaya za Zanzibar zilizokuwa hazifanyi vizuri wilaya ya Magharibi "A" na wilaya ya Kaskazini "A".

Pia Taasisi ya Rockefeller imeonyesha nia   ya kushirikiana na  kuisaidiaTaasisi ya Zanzibar Maisha Bora(ZMBF)  kufikia malengo ya kuwawezesha  Vijana na Wanawake kupambana na unyanyasaji wa kijinsia, lishe,vifo vya Mama na mtoto. 

📆 25 Oktoba 2022 

📍Ikulu, Migombani,Zanzibar.




Waziri wa Afya Mhe. Ummy afanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Rocke Feller

Written By CCMdijitali on Monday, October 24, 2022 | October 24, 2022

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Rocke Feller katika Kukabiliana na UVIKO 19, Adrew Sweet na kujadili namna ya kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha huduma za kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo UVIKO 19 na Ebola pamoja na kuimarisha mifumo ya afya.

Mazungumzi hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya zilizopo Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 24, 2022.






@wizara_afyatz @ummymwalimu

TAHLISO Waionya Chadema.

Jumuiya ya Wanafunzi  Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO)  wamekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kutokana na tabia yake ya kupinga mambo mbali mbali yanayofanywa na Serikali hata kama yana manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Rais wa Jumuiya hiyo Ndg. Frank Nkinda amesema kwa kipindi kirefu, Chama hicho kimejijengea tabia  Mbaya_ya  kutafuta uungwaji mkono hata katika masuala yasiyo na maslahi kwa Taifa na kupinga mapendekezo yenye dhamira  ya kuwaweka watanzania pamoja.

Akitolea mfano wa baadhi ya mambo hayo ikiwemo ripoti ya kikosi kazi iliyokabidhiwa  juzi kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa imesheheni mapendekezo mbali mbali yenye tija kwa taifa letu. *Nkinda alisema wao kama wasomi wa Elimu ya juu hawaoni sababu yeyote ya Chadema kuipinga ripoti hiyo* 

“Sote tulisikia muhtasari wa kile kilichowasilishwa na Mwenyekiti wa Kikosi kazi, Prof. Rwekaza Mukandala kwa Mhe. Rais, kwakweli dhamira yake ni njema. Sasa tumeshangaa kakikundi kamoja kamekuja juu na kusema mapendekezo haya hayafai na kwamba ni matumizi mabaya ya fedha za umma, _lakini ikumbukwe kwamba watu hawa waliitwa kutoa maoni yao wakakataa, sasa wanataka hata yale yaliyotolewa na  watanzania wengine kwa uhuru na haki watu wayapinge_ ”alisema Nkinda

Aliongeza kuwa TAHLISO kama Taasisi inayolea nguvu kazi ya Taifa, kimsingi wana mamlaka ya Kuonya, kukemea na kushauri mambo mbalimbali katika Kuchochea maendeleo ya Taifa.

" Tumesikitishwa na kauli ya Katibu mkuu wa Chadema John Mnyika ya kuita ripoti hiyo kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuwa tu wao walikataa kuwasilisha maoni kwenye kikosi kazi cha Rais" alisema Nkinda

Alisema mtu au taasisi yoyote ya kiungwana ilipaswa kupongeza dhamira iliyoonyeshwa na Rais Samia Suluhu Hassan  ya kutafuta maridhiano ya kitaifa kwa kupata maoni ya wadau juu ya njia gani za kupita kabla ya kufikia hitimisho na siyo kulalamika mbele ya vyombo vya habari suala alilosema halina msingi wowote.

Aliongeza kuwa Watanzania wameipokea ripoti  hiyo kwa mikono miwili na wanawapongeza wadau wote walioshiriki kutoa maoni kwenye kikos...


BODI PSSSF YAKAGUA UKARABATI KIWANDA CHA CHAI MPONDE

Ukarabati umekamilika, kinazalisha
Kitasaidia zaidi ya wakulima 3500
Na Mwandishi Wetu, Lushoto

Mwenyeki wa Bodi ya PSSSF, Mha. Musa Iyombe (kulia) akipata maelezo juu ya aina mbalimbali za chai zinazozalishwa katika kiwanda cha Mponde kutoka kwa Menaja wa Kiwanda hicho, Bi.Sane Kwilabya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mhandisi Musa Iyombe ameridhishwa na ukarabati uliofanyika katika kiwanda cha Chai cha Mponde. Sasa kiwanda hicho kimenza uzalishaji.

Mhandisi Iyombe alisema hayo mwishoni mwa wiki, ambapo yeye, akiongozana na wajumbe wengine wa Bodi ya Wadhamini wa PSSSF walitembelea kiwanda hicho kilichopo katika kijiji cha Kweminyasa,wilayani Lushoto ili kukagua maendeleo ya ukarabati wa kiwanda hicho.

“Tumetembelea kiwanda hiki cha Mponde ambacho kinazalisha chai bora, chai nzuri ambayo inaweza ikatumika ndani na nje ya nchi. Kiwanda kipo vizuri baada ya ukarabati, tumeona kiwanda kimeanza kuchakata majani ya chai, naamini wakulima wenye mashamba kwenye wilaya ya Lushoto, hususan Bumbuli, Korogwe na maeneo jirani watanufaika sana na uwepo wa kiwanda hiki” alisema Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF.

Mhandisi Iyombe alisema kuanza uzalishaji kwa kiwanda cha Chai Mponde ni wazi kwamba vijana wengi watapata ajira na kwamba uchumi wa kata ya Mponde na wilaya ya Lushoto, ikiwemo Bumbuli na maeneo jrani utakuwa iwapo fursa ya kuwepo kwa kiwanda itatumiwa vyema.

Kwa upande wake, Meneja wa Kiwanda hicho, Bi.Sane Kwilabya alisema, “kwa upande wetu tumejipanga vyema kuzalisha chai bora katika kiwanda hiki, na tunaamini ardhi ya huku ni nzuri kwa kilimo cha majani ya chai yaliyo bora."

Msimamizi wa ukarabati wa mradi huo, Mhandisi Ally Shanjirwa alisema ukarabari wa kiwanda hicho umekamilika kwa asilimia mia moja (100%) na sasa kinachofanyika ni kujaribu mitambo ili kubaini dosari na kuzirekebisha.

Kiwanda cha Chai Mponde kinaendeshwa kwa pamoja kati ya PSSSF na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kupitia kampuni ya Mponde Holding Company Limited, ambapo kila Mfuko umewekeza asilimia 42 na Msajili wa hazina anamiliki hisa 16.

Kiwanda kinategemewa kuzalisha ajira za muda mrefu zisizopungua 79 na ajira za muda mfupi zinazokadiriwa kuwa kati ya 100 hadi 300 kutegemea na msimu wa mavuno ya majani ya chai.

Uwepo wa kiwanda cha Chai Mponde kitaongeza kipato kwa wakulima wa chai katika Halmashauri ya Bumbuli na maeneo jirani, kuongeza mapato kwa taifa kupitia kodi mbalimbali na kuongeza kipato cha fedha za kigeni kwa taifa kupita mauzo ya nje ya chai ya Mponde.


Mwenyeki wa Bodi ya PSSSF, Mha. Musa Iyombe (kulia) akipata maelezo juu ya aina mbalimbali za chai zinazozalishwa katika kiwanda cha Mponde kutoka kwa Menaja wa Kiwanda hicho, Bi.Sane
 Kwilabya.

Meneja wa Kiwanda cha Chai Mponde, Bi. Sane Kwilabya (kulia) akitoa maelezo juu ya uzalishaji wa chai kwa wajumbe wa Bodi ya PSSSF wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Musa Iyombe (kushoto)

Wajumbe wa Bodi ya PSSSF wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kiwanda cha Chai cha Mponde kilichokarabatiwa.

MKUU WA MKOA NA WAKUU WA WILAYA WASAINI MIKATABA YA LISHE

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, hivi karibuni amesaini mkataba wa utendaji kazi za lishe baina yake, Katibnu Tawala na wakuu wa Wilaya ambao unaratibiwa na kusimamiwa na idara ya afya Mkoa. Shughuli hiyo imefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Lengo kubwa la mkataba huu ni kufanikisha suala la kuboresha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo katika Halmasahauri, kuhakikisha Halmashauri inasimamia ipasavyo utekelezaji wa afua za lishe pamoja na kuchukua hatua madhubuti za kupunguza hali duni ya lishe katika halmashauri.

Akiongea, mara baada ya kusaini mkataba huo , Mhe.Senyamule amesema kuwa mkataba huo umepewa uzito wa pekee na Serikali ndio maana wamesaini na amewataka wakuu wa Wilaya kwenda kuutekeleza. 
“Twende tukaupe uzito mkataba huu na tukautekeleze, tuongeze ufanisi na ubora kwenye hili kwani Dodoma bado tuna tatizo la lishe kwani tunaambiwa udumavu upo kwa asilimia 37 hivyo tuna kazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya lishe”

Hata hivyo, Mhe. Senyamule ametoa maelekezo juu ya upandaji miti ya matunda kwani matunda yanasaidia katika kuboresha lishe hasa kwa Watoto.

“Tufanye vikao na tathmini za uhalisia juu ya tatizo la lishe na mukasimamie zoezi la upandaji miti ya matunda ili watoto wapate matunda kwa afya” Amesisitiza Mhe.Senyamule.

Utekelezaji wa mkataba wa utendaji kazi za lishe unasimamia pia utoaji wa taarifa kwani kila Wilaya itatakiwa kuwasilisha taarifa za utendaji kazi za kila robo mwaka kila ifikapo tarehe 07 ya mwezi unaofuata huku taarifa ya utendaji kazi ya mwaka ikitakiwa kuwasilishwa kabla ya tarehe 16 ya mwezi Julai ya kila mwaka.

Aidha, mkataba huu wa kiutendaji utakua wa muda wa miaka nane (8) na umeanza rasmi Julai Mosi, 2022 hadi Juni 30, mwaka 2030 na utakua ukipimwa kila mwisho wa mwaka husika. Iwapo utajitokeza mgogoro wowote katika utekelezaji wake, pande zote mbili zitakaa pamoja ili kutatua mgogoro huo.

MWISHO




TIC yanadi fursa za Uwekezaji za Tanzania Nchini Ureno.

Written By CCMdijitali on Sunday, October 23, 2022 | October 23, 2022

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeshiriki katika kunadi fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini kupitia kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ureno lilifanyika jijini Lisbon Ureno leo Alhamisi tarehe 20 Oktoba, 2022 .

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Nje ya Ureno, TIC na Taasisi inayohamasisha biashara na Uwekezaji ya Ureno (AICEP Portugal Global). 

Kongamano limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania na Ureno wakiongozwa na Mhe. Dkt. Stagomena Lawrence Tax, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Bernado Ivo Cruz, Waziri wa Nchi, Biashara za Kimataifa na Uwekezaji kutoka Nje. Kongamano hilo lilihudhuriwa na wawekezaji zaidi ya 50 chini ya mwavuli wa AICEP Portugal Global taasisi inayotekeleza majikumu kama ya TIC nchini Ureno.

Kongamano hilo ni mojawapo ya kazi katika ratiba ya ziara ya kikazi ya Mhe Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nchini Ureno katika mikakati na juhudi zinazoendelea za Wizara hiyo katika kuhamasisha Uwekezaji kupitia Diplomasia ya Uchumi. 

Katika ziara hiyo, TIC inawakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji Uwekezaji Bw, Revocatus Rasheli ambaye alitoa mada kuhusu mazingira ya uwekezaji na fursa zilizopo katika sekta za kimkakati hapa nchini pamoja na kuwasilisha “Offer” kwa wawekezaji wa Ureno ya miradi zaidi ya 130 ya uwekezaji iliyofungashwa na TIC kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta ya Umma na Binafsi inayotafuta mitaji, teknolojia, ujuzi nk ili kuitekeleza kwa ufanisi. 

Aidha, TIC imefanya mazungumzo na AICEP Portugal Global kwa lengo la kuwa na makubaliano ya mashirikiano yanayolenga katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na kuwasaidia wawekezaji wa Ureno wanaopanga kuwekeza Tanzania kupata taarifa na taratibu za uwekezaji nchini.

Lisboa, Portugal 20 Oktoba, 2022










WAZIRI JAFO ASHIRIKI ZOEZI LA KUPANDA MITI KATIKA WILAYA YA BAGAMOYO.

Written By CCMdijitali on Saturday, October 22, 2022 | October 22, 2022

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais( Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt Selemani Jafo ameshiriki katika zoezi la upandaji miti lililofanyika katika  shule ya Msingi Mtoni iliyopo katika Wilaya ya Bagamoyo.

Akiwa shuleni hapo amepongeza Benki ya Standard Chattered ambao ndiyo waandaaji na wasimamizi wakubwa wa tukio hilo la upandaji miti katika shule hiyo.

“Nawapongeza sana benki ya Standard Chattered kwa kunialika kuwa Mgeni Rasmi katika shughuli hii ya upandaji miti ambayo ni mwendellezo wa juhudi katika kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti”. Mhe Dkt Jafo

Aidha  ameziagiza Halmashauri zote Nchini ambazo hazijafikia malengo ya upandaji miti kama ilivyokua imeelekezwa awali  kuhakikisha wanapanda miti na kufanikisha azma hiyo ya Serikali ya ukupanda miti kwa wingi katika kila Halmashauri Nchini ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Naagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinafikia malengo ya kupanda miti ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa  inayoikabili dunia kwani husababisha, ukame, kuongezeka kwa kina cha bahari na maziwa”. Mhe Dkt Jafo

Naye Mkurugenzi wa Standard Chattered Bwana Herman Kasekende  amesema watendelea kuunga mkono juhudi za Serikali  kwa kusimamia zoezi la upandaji miti katika mashule mbalimbali  ili kusaidia kutunza na kuhifadhi mazingira.

#Kaziiendelee
#MheDktJafo
#Zoeziendelevulaupandajimiti 
#MitiRafikikwaMazingira 
#VivulinaMatundaMengineyo 
#KupambanaMabadilikoyaTabianchi 
#DktJafoktkMazingira 1
#Endeleakuupigamwingi 
#SSH2025🇹🇿
#MunguIbariki🇹🇿







WAZIRI DKT.PINDI CHANA ATEMBELEA ONESHO LA KIMATAIFA LA UTALII LA SWAHILI.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) ametembelea Onesho la Kimataifa la Utalii la Swahili lililoanza leo jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Naibu Waziri wake ,Mhe. Mary Masanja(Mb).

Lengo kuu la Onesho hilo ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania, na kukutanisha wanunuzi na wauzaji wa bidhaa za utalii wa Kitaifa na Kimataifa.

Onesho hilo litahudhuriwa na waoneshaji zaidi 200, wanunuzi wa Kimataifa takribani 100 kutoka masoko ya Kimakakati hususan nchi za Marekani, Uholanzi, Afrika Kusini, India, Urusi, Hispania, UAE, Poland, Finland, Japan, Oman na nyinginezo.

Onesho hilo litamalizika tarehe 23 Oktoba 2022.









 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link